Sitta awasha moto mpya DOWANS

Hana lolote! Hawa ndio magamba walopangiwa kuja na vijihoja vya kutetea maslhi ya taifa ili ccm ionekane bado ina watu! Tumeshakujua bora ukae kimya ule upacho gamba mkubwa!
 
Mhe. Sitta kwa kweli umeongea mengi, je unatushauri watanzania tufanye nini katika hili au tu unaongea sana ili tukuone kama nawe ni mmoja wetu sisi mnaotuibia????Ningekuelewa sana kama ungeamua kuonesha ni jinsi gani hili suala linakukera kwa kujiuzuru ktk nafasi yako mana kwa maneno yako ni kama ushaishauri serikali sana tu ndani ya vikao vyenu ila serikali inaonyesha kutokukuelewa na ndo mana umeamua kufunguka kwa wananchi. Bila kufanya hivyo mzee unaqualify kuitwa Mnafki.
 
Mi nawashangaa sana ninyi watu, sasa mnataka akae ili kimya hela zilipwe kwa hao dowans? at least yeye anajitokeza hadharani kupinga hayo malipo, ninyi mnaosema hajafanya kitu mmefanya nini, au mmeshakubali deni lilipwe? Mtu akisema kitu chenye manufaa, hata kama ni kwa kutafuta popularity anapaswa kuungwa mkono, maana mwisho wa siku tunachotaka ni maendeleo katika taifa letu.

Na ni nani kawaambia kwamba ukiwa CCM ni marafuku kukosoa makosa ya CCM? Ili tuendelee tupaswa kuondokana na hizi itikadi za kung'ang'ania vyama na tuangalie zaidi jititihada katika kuleta maendeleo, maanake sasa naona watu wanasahau udui yetu ni nani, siyo Sita mnaemshambulia, ni DOWANS wanaotaka kuiba pesa zetu.

Nakuunga mkono. Pamoja na usanii na unafiki wa Sitta hastahili kushambuliwa katika kutetea Tanzania katika malipo haya (Shilingi bilioni 113) yaliyojaa ufisadi wa hali ya juu yanayotaka kufanywa dhidi ya kampuni hewa ya Dowans. Wako wapi hao Watanzania ndani ya chama ambao si wanafiki au wasanii wasimame hadharani kama alivyofanya Sitta kutoa kauli za kupinga malipo haya ya wizi wa mchana kweupe.

Watu hawajui kwamba kwa kumshambulia Sitta basi wananyamazisha sauti moja ya Mtanzania mwenzetu katika kutetea maslahi ya nchi. Inawezekana kabisa Sitta ni mwizi, msanii, mnafiki n.k. lakini katika hili la kupinga malipo yanayotaka kufanywa dhidi ya Dowans, Sitta hajakosea lolote na anastahili kuungwa mkono na Watanzania wote ambao ni wapenda haki na wako mstari wa mbele katika kutetea maslahi ya nchi.

Sioni sababu yoyote ili ya kumnyamazisha Sitta na kuwarahisishia mafisadi kulipana shilingi 113 bilioni pesa ambayo hawakuitolea jasho kabisa, ikumbukwe mitambo ile inadaiwa imeshauzwa kwa Symbion kwa shilingi bilioni 120.

Kuikosoa CCM/Serikali si lazima uwe nje ya CCM, wako wanachama chungu nzima ndani ya CCM ambao wanaikosoa CCM/serikali na wengineo kati ya hao waliwahi kushika nyadhifa za juu ndani ya CCM na Serikali.
 
Sitta - hicho ni kilo cha mamba. Ulipokuwa na rungu la kumaliza tatizo hili, hukulitumia au uliiogopa kulitumia. Wenzako walikujua wakakunyima hilo rungu, sasa unatuambia nini?
Katika watu wa kubeba lawama na wewe umo. Mwakyembe alipokuletea ripoti ulipaswa kuiweka wazi yote na hili lingesababisha serikali yote kujiuzulu na kufanyika uchaguzi mpya - uliogopa hilo. Umemlea nyoka sasa amekuwa mkubwa - atakumeza wewe na sisi pia.
 
Huwezi kupambana na wezi walioko ndani ya chama chako!!
Huu ni usanii waTZ wanataka kuonyeshwa ili imani yao na chama isipotee...

Pambana na adui ukiwa upande wake wa pili!!!
Pesa walizokopa kuendeshea uchaguzi wa 2005 kwa (DOWANS)-Mbunge Mstaafu wa Igunga kama wanavyomwita(Rostam) hazijarudi, sasa watanzania wote tunawajibika kulipa mikopo ya chama kimoja ambacho kimetuletea hasara ya kuendelea kwa miaka yote kilipokuwa madarakani tangu utaifishaji wa mali, vita vya Nyerere na Uganda, sasa mafuta na gas kupanda bei huku tukihimizwa kuhifadhi misitu etc...
 
Huyu Sitta kweli msanii amesahau kama ni yeye aliumaliza mjadala wa Rich Monduri pale bungeni yy akiwa ni spika au anataka kufanya na ss wananchi tunatumia MASABURI kufikiria.Mzee uonage na kaaibu kidogo basi washauri na wenzako nchi imeamuka mda huu tuna Library zetu mzee tunatunza tu kuna mda wa kukamatana utafika ss kuingia road tunajua tutaanza na nani na kumaliza na nani!
 
Mi nawashangaa sana ninyi watu, sasa mnataka akae ili kimya hela zilipwe kwa hao dowans? at least yeye anajitokeza hadharani kupinga hayo malipo, ninyi mnaosema hajafanya kitu mmefanya nini, au mmeshakubali deni lilipwe? Mtu akisema kitu chenye manufaa, hata kama ni kwa kutafuta popularity anapaswa kuungwa mkono, maana mwisho wa siku tunachotaka ni maendeleo katika taifa letu.

Na ni nani kawaambia kwamba ukiwa CCM ni marafuku kukosoa makosa ya CCM? Ili tuendelee tupaswa kuondokana na hizi itikadi za kung'ang'ania vyama na tuangalie zaidi jititihada katika kuleta maendeleo, maanake sasa naona watu wanasahau udui yetu ni nani, siyo Sita mnaemshambulia, ni DOWANS wanaotaka kuiba pesa zetu.
tulichogundua ni kwamba Sitta hachukii ufisadi bali anawachukia Mapacha watatu kwa sababu za 2015
Sitta ni mnafiki na kwa sasa akawaeleze wajinga kuwa yeye ni mzalendo
 
Mhe. Sitta kwa kweli umeongea mengi, je unatushauri watanzania tufanye nini katika hili au tu unaongea sana ili tukuone kama nawe ni mmoja wetu sisi mnaotuibia????

Ningekuelewa sana kama ungeamua kuonesha ni jinsi gani hili suala linakukera kwa kujiuzuru ktk nafasi yako mana kwa maneno yako ni kama ushaishauri serikali sana tu ndani ya vikao vyenu ila serikali inaonyesha kutokukuelewa na ndo mana umeamua kufunguka kwa wananchi. Bila kufanya hivyo mzee unaqualify kuitwa Mnafki.

Ajiuzulu! Wajua action speaks louder than words! akiweza kuonyesha huo mfano tutamtetea asiuawe na magamba, kwanza kesha kula sana yeye na mkewe aliyekamatwa akitoa rushwa na kuachiwa!

Akijiuzulu na kuomba ulinzi against magamba atawaincourage wengine wote akina Ngereja wamfuate wanatamani lakini wanatishiwa kuuawa, wote hawa kina Pinda, wanadhalilishwa wanakomaa tu unafikiri wana namna ingine hao wamebanwa na uzalendo hawana! sasa mtu kama Mangula naye alienda Igunga kufanya nini?

Njaa pevu hiyo inawaua walizoea kusomeshewa watoto nje sasa wamekwama kabisa tunapanga wote foleni za mafuta yaliyochakachuliwa filling stations! teh teh teh, nacheka kwa hasira na machungu!
 
@Mzee kipara, tafakari hii; Sita na akina mwakyembe wanajua walimuokoa nani kwa kuficha mambo muhimu ktk issue ya richmond, sita anawajua wenye dowans watakaolipwa hela hizo, sita anajua kuwa kama wakati ule wangelipasua jipu lote la richmond na kulitoa tusingeona huu utumbo wa sasa... Leo hii bila aibu anasema kila mzalendo 'alaani' tukishalaani ndo iweje???? Sita na wenzake wana deni kubwa kwa Taifa hili.. Atuwekee wazi siri walizotuficha wakati ule.

Sikatai kwamba labda Sita na wenzake wana personal interest katika hili, lakini akikaa kimya halafu hizo hela zikalipwa tutakuwa tumemkomoa nani, wala siyo Sita, bali kila mtanzania atasugua meno maana katika kuzilipa. Mimi nawahakikishia wenye DOWANS wanafurahi sana wakiona argument zenu, maana wanajua kumbe sasa tuna support.

Cha muhimu deni lisilipwe kwa sababu ni wazi hizo pesa tunatapeliwa, hata kichaa analijua hilo, na tusitegemee judicial system yetu itatusaidia katika hilo, tunachotakiwa ni kukomaa tu katika kukataa deni lisilipwe.
 
“Nakwambia wazi labda kama na wewe gazeti lako hilo ni la kifisadi…lakini sisi Dowans hatukuwapa mkataba bali walirithi wizi wa kampuni hewa, hivyo hatuwezi kubebesha wananchi matatizo ya majizi halafu tukashangilia kuibiwa,” alisema Sitta kwa hasira.

Sitta, maarufu kama Spika wa Kasi na Viwango, katika Bunge lililopita alisimama imara pamoja na baadhi ya wabunge waliojipambanua kama wapambanaji wa ufisadi kupinga Kampuni hewa ya Richmond (sasa Dowans) na kuishinikiza serikali ivunje mkataba huo.

Akifafanua zaidi, alisema kuwa Watanzania wanapaswa kuwa na uzalendo wa kulipigania taifa lao badala ya kukatishwa tamaa kwa kutishwa kuwa Dowans lazima ilipwe. Hivyo, alidai kuwa mapambano ya kupinga malipo hayo yasifanyike bado yanaendelea.

“Kwanza nikuhakikishie huu si mwisho wa mapambano…Dowans kulipwa ni sawa na kuhalalisha ushenzi wa majizi hayo…hatuwezi kushangilia, nitapinga hadi mwisho…unanielewa, hatuwezi kulipa wezi,” alisisitiza Sitta na kukata simu.ICC iliitia hatiani Tanesco kwa kosa la kuvunja mkataba na Dowans iliyokuwa ikitetewa na wakili wa kimataifa Kennedy Fungamtama na ikaiamuru iilipe tuzo hiyo na riba ya asilimia 7.5.


Kwa hili nakuunga mkono Mheshimiwa 6,
Huu ndo uzalendo tunaoutaka sio tukubali tuu kila kitu kisa eti waziri husika ni wa CCM.
Kwenye suala linalohusu maslahi ya nchi lazima tuache kiuanachama na ushabiki wa chama na tutetee maslahi ya nnchi kwanza (huu ndo ujasiri tunaoutaka).
Sio kuteteana/kulindana tuu huku tukizidi kuangamiza uchumi wetu na kunufaisha matumbo wachache.

Kaza msuli mkuu...Mwenyezi Mungu akubariki na aendelee kukupa ujasiri na uzalendo wa dhati kama huo.
 
Kwa hili nakuunga mkono Mheshimiwa 6,
Huu ndo uzalendo tunaoutaka sio tukubali tuu kila kitu kisa eti waziri husika ni wa CCM.
Kwenye suala linalohusu maslahi ya nchi lazima tuache kiuanachama na ushabiki wa chama na tutetee maslahi ya nnchi kwanza (huu ndo ujasiri tunaoutaka).
Sio kuteteana/kulindana tuu huku tukizidi kuangamiza uchumi wetu na kunufaisha matumbo wachache.

Kaza msuli mkuu...Mwenyezi Mungu akubariki na aendelee kukupa ujasiri na uzalendo wa dhati kama huo.[/COLOR][/COLOR]
it seems humfaham SITA
huyu ndiye aliye yeyusha hii saga bungeni sasa leo anadai nini???
SITA ni mpuuzi sana hana uzalendo
 
Maria we hujaelewa nini? Anachokataa ni malipo kwani yanaenda kwa wezi, richmond ilishasemwa ni kampuni feki, sasa ufeki unaondoka kurithisha mkataba kwa dowans? Mapacha watatu wapi na kama wanahusika basi, kinachopiganiwa hapa ni hoja na si ushabiki, ka una hoja yenye mashiko then poa, lakini kuja na post zako za ushabiki hapa si mahala pake dada, hawa niwezi na haya yalisemwa na ucgunguzi ulifanywa, sasa tunamlipa nani?

Nadhani kwenye ujenzi wa nchi lazima tuwe kitu kimoja, tujibizane kwa hoja zenye mantiki na si ushabiki!sitta ni speaker ambaye kwenye kizazi chetu bado sijamuona kama yeye, tanzania ukiwa muwazi na kutaka mambo yajadiliwe kwa uwazi basi unakuwa adui wa watu, na hiyo lazima itokee kwa sababu sisi wote si watu safi, na sita ni nani afanya kazi apendwe na kila mtu? Wazalendo tu ndo wanaweza kusema mazuri aliyoyafanya.

Kila mtu ana mazuri na mabaya yake, katika hili mhe, sita nakupongeza na usife moyo!kuwa speaker uanyajua mengi ambayao sisi hatuyajui, unaposema hivyo mimi nakiri kuwa richmond ni kampuni tapeli!
 
Huwezi kupambana na wezi walioko ndani ya chama chako!!
Huu ni usanii waTZ wanataka kuonyeshwa ili imani yao na chama isipotee...

Pambana na adui ukiwa upande wake wa pili!!!

Kwenye BOLD, it is neither the principle nor the rule. Trojan were fighting from in within.

Let him fight from within this will weaken the stronghold of the enemy and fight from outside that wili assure total destruction.
 
Maria we hujaelewa nini?anachokaa ni malipo kwani yanaenda kwa wezi, richmond ilishasemwa ni kampuni feki, sasa ufeki unaondoka kurithisha mkataba kwa dowans?

Mapacha watatu wapi na kama wanahusika basi, kinachopiganiwa hapa ni hoja na si ushabiki, ka una hoja yenye mashiko then poa, lakini kuja na post zako za ushabiki hapa si mahala pake dada, hawa niwezi na haya yalisemwa na ucgunguzi ulifanywa, sasa tunamlipa nani?nadhani kwenye ujenzi wa nchi lazima tuwe kitu kimoja, tujibizane kwa hoja zenye mantiki na si ushabiki!

Sitta ni speaker ambaye kwenye kizazi chetu bado sijamuona kama yeye, Tanzania ukiwa muwazi na kutaka mambo yajadiliwe kwa uwazi basi unakuwa adui wa watu, na hiyo lazima itokee kwa sababu sisi wote si watu safi, na sita ni nani afanya kazi apendwe na kila mtu?

Wazalendo tu ndo wanaweza kusema mazuri aliyoyafanya!kila mtu ana mazuri na mabaya yake, katika hili mhe, sita nakupongeza na usife moyo!kuwa speaker uanyajua mengi ambayao sisi hatuyajui, unaposema hivyo mimi nakiri kuwa richmond ni kampuni tapeli!

Mimi sileti ushabiki na kama ni ushabiki mimi nilikuwa kundi la SITTA. kinachoniudhi ni namna alivyolimaliza swala hili bungeni kiujanjaujanja (sio kwamba naunga mkono malipo ila siamin katika uzalendo wa SITA). Pia awali nilidhani SITA ni mzalendo lakini kwa mambo aliyoyafanya mwishoni wa 2010 mpaka leo SITA anastahili adhabu kutoka kwa WATANZANIA

Nikuulize kidogo...hivu unadhani SITA anaongozwa na uzalendo au ni kuzidiwa mgao/harakati 2015 na sasa anataka watu tumwonee huruma kwa kujifanya anatutetea?? yeye alikuwa spika kwa nini hakutumia rungu kipindi kile kuuwa dowans?
 
Siku zote mie usema "Ukiona kitu chochote chenye kujali masilahi ya taifa kimeongelewa na mtu kutoka CCM basi ujue ni kwasababu kakosa mgao au aliyepiga deal ni adui wake kisiasa (wanagombea madaraka)" na bado naendelea kaamini hivyo mpaka pale itakapodhirika vinginevyo!

Sitta ayasemayo ni kweli lakini unaona hapa hata jamii badala ya kuangali ukweli wa kauli zake inabaki kushangaa kwanini anasema hivyo. Inaonekana jamii yetu imekata tamaa mpaka mwisho na kuanza kuhalalisha uharifu!

Najiuliza maswali haya mara nyingi:

1. Hivi huyu 6 akienda kwenye vikao vya baraza la mawaziri usema haya maneno anayoyasema kwenye magazeti au ubakia ndiyo mzee?

2. Hivi aliyemteua akisikia waziri anatamka maneno haya na mengine mengi aliyoyasema huko nyuma anaogopa nini kumpumzisha?

Sitaki majibu kwa sasa ila wote tutafakari!

For the record:
Nakubaliana na 6 mia kwa mia kuwa hatupaswi kuilipa DOWANS japo nahoji kinachomsukuma kusema hivyo kama ni huruma kwa watz manake mbali na Dowans yapo mengi sana (ufisadi) ambayo hata siku moja hawayasemei. Sioni kwa mtindo huu ambako watu wanaliibia taifa wazi wazi na wanalindwa kwa visingizio vya sheria huko tuendako umma ukiamka kama Misri na Tunisia sitashanga!

Mungu ibariki Tanzania!
 
mimi sileti ushabiki na kama ni ushabiki mimi nilikuwa kundi la SITTA
kinachoniudhi ni namna alivyolimaliza swala hili bungeni kiujanjaujanja (sio kwamba naunga mkono malipo ila siamin katika uzalendo wa SITA)
pia awali nilidhani SITA ni mzalendo lakini kwa mambo aliyoyafanya mwishoni wa 2010 mpaka leo SITA anastahili adhabu kutoka kwa WATANZANIA

nikuulize kidogo...hivu unadhani SITA anaongozwa na uzalendo au ni kuzidiwa mgao/harakati 2015 na sasa anataka watu tumwonee huruma kwa kujifanya anatutetea?? yeye alikuwa spika kwa nini hakutumia rungu kipindi kile kuuwa dowans?????

Lugha gani mtaelewa wana Jf?SITTA SAMWEL MH (MB)Huyu bwana ni Mnafiki sana tena sana.
 
Huwezi kupambana na wezi walioko ndani ya chama chako!!
Huu ni usanii waTZ wanataka kuonyeshwa ili imani yao na chama isipotee...

Pambana na adui ukiwa upande wake wa pili!!!

Kwenye BOLD, it is neither the principle nor the rule. Trojan were fighting from in within.

Let him fight from within this will weaken the stronghold of the enemy and fight from outside that wili assure total destruction.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom