Sitta atakumbukwa kwa lipi Urambo?

Kaka mwisho

JF-Expert Member
Dec 19, 2011
402
166
Ndugu zangu wa URAMBO ni mambo gani Mh SAMWEL SITTA amewafanyiwa katika vipindi vyake vyote vya ubunge ambayo kamwe hamtayasahau? je hapo mlipo kimaendeleo mnastahili?
 
Mkuu, Samwel Sitta amefanikiwa kujenga ofisi ya Spika huko Urambo. Hii ni kumbukumbu kubwa sana kwa watu wa Urambo kwa kuwa hata Spika Makinda nadhani atakuwa akiitumia hiyo ofisi ya Urambo, bila shaka.
 
Samweli Sitta anajifanya mpambanaji wakati jimbo lake liko hoi bin taaban hakuna barabara, shule ziko hoi, eti akajenga ofisi ya spika kama vile atakuwa spika wa maisha, yani hamna chochote cha maana alichofanya zaidi ya fitina, majungu na roho mbaya, la ajabu hata wanyamwezi wenyeji wala hawashituki, wakipewa pilau wanampa kura, kwa kweli watani zangu wanyamwezi msipobadirika maendeleo mtabaki kuyasoma kwenye magazeti. Badilikeni acheni ujinga.
 
mi namchukia kwenye ufisadi wa richmond, alinizuia mimi nisijue ukweli kwa kulinda chama. Upuuzi
 
Huyo nae ni fisadi, anakwenda kujenga ofisi ya Spika jimboni kwake? mliisikia wapi hii duniani? au sijamuelewa mleta mada?
 
Hata kama Lowassa kakutuma umwage hii haja kubwa jamvini kamwambie kuwa Lowassa hatumtaki kwa sababu ya UBAGUZI wake wa kidini. Atafanya taifa hili tuliloishi kwa upendo tugawanyike kwa misingi ya kidini. Mwambie hatumtaki
 
Kwa kujenga Ofisi ya Mbunge kubwa kuliko zote Nchini; hadi Rais Mwenyewe alishtuka alipoliona hilo jengo

Pesa, ni za walala hoi Urambo sio wote wana nyumba za bati na Umeme...

Lakini Wanamchagua Samwel Sitta bita tatizo; kosa ni CCM au Wananchi?
 
Wala hakuna alietumwa na Lowassa humu, isipokuwa ukweli ni kwamba Sitta ni mzigo kwa watu wa Urambo. Hakuna alilofanya zaidi ya kujenga ofisi ya gharama kwa matumizi yake. Hata mke wake ni yaleyale, amekuwa waziri wa elimu lakini hakufanya la maana Urambo ambapo ni kwao pia. Wote ni mizigo. Wanasafiria ujinga wa wapiga kura wa Urambo.
 
Ofisi ya bunge kujengwa Urambo,
Chuki dhidi ya kambi ya akina Kapuya,
Kugawia wanachama majoti ya kushona sare za chama,
Nguvu nyingi kulalamika nje ya mkoa dhidi ya wimbo wa taifa 'ufisadi' badala ya kuwapatia unafuu wa bei za pembejeo kwa wananchi na hususan zao la Tumbaku,
 
Atakumbukwa kwa kujenga ofisi kubwa sana ya spika huko kwao ambayo hata sijui inawasaidia vp wananchi wake!
 
Hata kama Lowassa kakutuma umwage hii haja kubwa jamvini kamwambie kuwa Lowassa hatumtaki kwa sababu ya UBAGUZI wake wa kidini. Atafanya taifa hili tuliloishi kwa upendo tugawanyike kwa misingi ya kidini. Mwambie hatumtaki

huo ubaguzi wa Kidini umetokea wapi wakati Lowasa na Sitta ni dini moja?
 
kwa kweli ile wilaya hipo mahututi wakuu! nimetembelea pale mwaka jana watu wapo hoi bin taabani! Hakuna access yoyote na barabara nzuri,huyo mzee aachie watu wengine wajaribu,...
 
Haya ndio matatizo ya ufahamu wa siasa zetu za kibongo, eti unakuta mgombea ubunge anasimama kwa wapigakura wake anajinadi eti nitawajengea barabara,nitaleta umeme,hospitali,visima nk nk utadhani yeye ndio anafungu lote la serikali na anapanga yeye bajeti na mke wake Kazi ya mbunge ni ile inayofanywa na akina Januari makamba, Tundu Lisu, Ziito, Kigwangala, Mdee, Kafulila, Myika, Mbowe nk nk pindi wanapokuwa mjengoni na si kama wanavyofanya akina Azim Dewji,Lowasa,Abood nk ya kutoa pesa mfukoni na kusaidia baadhi ya mambo
 
Kwa kujenga ofisi ya spika jimboni kwake! akafikili uspika ni wa milele kumbe CCM wana mpango wa kumuweka mbeijing!
 
Back
Top Bottom