BAK
JF-Expert Member
- Feb 11, 2007
- 124,789
- 288,011
Sitta amcharukia Jaji Mkuu
Stella Nyemenohi, Dodoma
Daily News; Monday,February 09, 2009 @20:04
Wakati Bunge likitarajiwa leo kujibu kauli ya Jaji Mkuu Augustino Ramadhan aliyoitoa wiki iliyopita kuwa chombo hicho kimekuwa kikiingilia mahakama, Spika Samuel Sitta amesema malalamiko yaliyotolewa na jaji hayawezi kunyamaziwa. Amesema Bunge kama taasisi, haliwezi kukaa kimya kwa kuwa suala hilo ni la kikatiba. Stella Nyemenohi, Dodoma
Daily News; Monday,February 09, 2009 @20:04
Akitoa taarifa hiyo bungeni leo mjini hapa, Sitta alionyesha kulaumu baadhi ya uamuzi ambao umekuwa ukitolewa na mahakama na kusema kwamba unatoa fursa kwa mtu mmoja kuliko jamii nzima, jambo linaloumiza. Alisema wao kama wabunge hawana nia mbaya na mahakama, lakini akatahadharisha kwamba chombo hicho cha sheria, hakina budi kuzingatia kwamba jamii inakiangalia.
"Hapa watasema pia naingilia mahakama…potelea mbali," alisema Sitta bungeni hapo. Kwa mujibu wa kiongozi huyo wa Bunge, tamko la Bunge litatolewa kesho baada ya kipindi cha maswali na majibu. Akifafanua juu ya kile alichosema baadhi ya uamuzi kuegemea kwa mtu mmoja badala ya jamii, Sitta alitoa mfano kuwa Mamlaka ya Udhibiti wa Nishati na Maji (EWURA) iliwahi kukifungia kituo kimoja cha mafuta kwa kuzingatia kanuni zake.
Kwa mujibu wake, matajiri walikwenda mahakamani kupinga uamuzi huo ambao ulikubalika mahakamani na ikaamriwa kifunguliwe. Wiki iliyopita, katika maadhimisho ya Siku ya Sheria, Dar es Salaam, Jaji Mkuu licha ya kutaja Bunge kuingilia mahakama, vile vile alivionya vyombo vya habari kwa kile alichosema kwamba vimeshindwa kutofautisha kati ya maoni na ukweli.
Katika hatua nyingine, Bunge leo jioni liliahirisha kikao chake baada ya Naibu Spika Anne Makinda kugundua kuwa hakuna mtu hata mmoja wa serikali.
Last edited: