Sitta aliondolewa uspika ili mafisadi wa Dowans wapone

Watanzania

JF-Expert Member
Jul 7, 2009
727
42
Picha sasa inaonyesha wazi kuwa Spika mstaafu Mh. Sitta aliondolewa uspika na CCM ili kujaribu kuruhusu ulipwaji wa Dowans ambayo ilirithi mkataba wa kampuni feki ya Richmond. Kwa vyovyote vile Serikali ya kifisadi ya CCM ilimwona Sitta kama kikwazo kwa sababu angeruhusu bunge kuhoji nyendo zozote za Serikali kujaribu kuwatwisha mzigo wananchi wa Tanzania kuwalipa mafisadi wa Dowans. Kwa vile Richmond ilipata mkataba wa rushwa na kampuni yenyewe kuwa feki, bunge la Sitta lingeshainyoshea kidole Serikali na kuikumbusha kuwa Lowasa, Karamagi na Msabaha walijiuzuru kwa kashfa ya Richmond ambayo imerithiwa na Dowans.

Sasa CCM isuburi tu kuona kwa vitendo jinsi watanzania walivyochoka na utawala mbovu wa CCM Mafisadi maana Spika wa sasa yuko usingizini. Hasemi chochote kupinga mafisadi wa CCM kupitia Dowans wanaotaka kuendeleza utumwa wa watanzania. Sitta endeleza mapambano na mafisadi wa Dowans, sisi watanzania tuko tayari kwa lolote, tumechoka kubeba mizigo ya mafisadi wa CCM.
 
Ni kweli usemalo, fuatilia kesi na hukumu yake chini ya REX ATTORNEYS na utajua yaliyomo,
Ila majina yamo ya wabongo wetu, ukibahatika kuisoma...utajua madudu yalivyo
 
nakubali picha hii sasa yaanza kuonekana laivu bila chenga> shame on our leaders

picha sasa inaonyesha wazi kuwa spika mstaafu mh. Sitta aliondolewa uspika na ccm ili kujaribu kuruhusu ulipwaji wa dowans ambayo ilirithi mkataba wa kampuni feki ya richmond. Kwa vyovyote vile serikali ya kifisadi ya ccm ilimwona sitta kama kikwazo kwa sababu angeruhusu bunge kuhoji nyendo zozote za serikali kujaribu kuwatwisha mzigo wananchi wa tanzania kuwalipa mafisadi wa dowans. Kwa vile richmond ilipata mkataba wa rushwa na kampuni yenyewe kuwa feki, bunge la sitta lingeshainyoshea kidole serikali na kuikumbusha kuwa lowasa, karamagi na msabaha walijiuzuru kwa kashfa ya richmond ambayo imerithiwa na dowans.

sasa ccm isuburi tu kuona kwa vitendo jinsi watanzania walivyochoka na utawala mbovu wa ccm mafisadi maana spika wa sasa yuko usingizini. Hasemi chochote kupinga mafisadi wa ccm kupitia dowans wanaotaka kuendeleza utumwa wa watanzania. Sitta endeleza mapambano na mafisadi wa dowans, sisi watanzania yuko tayari kwa lolote, tumechoka kubeba mizigo ya mafisadi wa ccm.
 
Ni kweli usemalo, fuatilia kesi na hukumu yake chini ya REX ATTORNEYS na utajua yaliyomo,
Ila majina yamo ya wabongo wetu, ukibahatika kuisoma...utajua madudu yalivyo

Hebu ibandike hapa tuone hiyo hukumu ya Rex. Halafu huyu Makinda amekaa kimya kama picha tu hivi haoni wananchi anaowawakilisha wanaelekea kubeba mizigo ya ufisadi wa Dowans?
 
The game was technically played, and now is over.
Tanzania under ccm will never make it.
 
Jamani Makinda ni chombo kiteule cha mafisadi ili kukamilisha pigo la mwisho kwa watz kabla ya ujio wa katiba mpya ambayo dhahiri ndiyo kaburi la CHAMA CHA MAFISADI
 
Jamani Makinda ni chombo kiteule cha mafisadi ili kukamilisha pigo la mwisho kwa watz kabla ya ujio wa katiba mpya ambayo dhahiri ndiyo kaburi la CHAMA CHA MAFISADI

Kambi ya wapiganaji dhidi ya mafisadi wa CCM wa Richmond na Dowans mko wapi? Mwakyembe, Shellukindo, Kilango Malecela mko wapi? Msisubiri hadi watanzania tumezikwa na mizigo ya kifisadi ya Mzimu wa Dowans. Watanzania tuko hoi tumepigika bado mafisadi wa Dowans wanatunyemelea watuzike kabisa. Hivi mnasubiri wananchi wafanye maasi? Wapiganaji wanasheria unganeni na wananchi haraka kupinga makaburu hawa wa CCM Dowans.
 
Labda tumpe mama yetu makinda muda wa kutafakari na kuamua, may be anasubiri bunge lijalo la Feb 11 aweze kumwaga cheche zake.
Harakati ambazo tayari zimeshaanza ziendelee kwa kasi zaidi ikiwa ni pamoja na kuunganisha nguvu kutoka makundi mbalimbali kupinga UNYAMA UNAOFANYWA NA CCM.
 
walijua sana kuwa ni lazima walipane hizo pesa, ndio maan waliona wamtimue mapema ili asiwazibie
 
Kambi ya wapiganaji dhidi ya mafisadi wa CCM wa Richmond na Dowans mko wapi? Mwakyembe, Shellukindo, Kilango Malecela mko wapi? Msisubiri hadi watanzania tumezikwa na mizigo ya kifisadi ya Mzimu wa Dowans. Watanzania tuko hoi tumepigika bado mafisadi wa Dowans wanatunyemelea watuzike kabisa. Hivi mnasubiri wananchi wafanye maasi? Wapiganaji wanasheria unganeni na wananchi haraka kupinga makaburu hawa wa CCM Dowans.

akina Mwakyembe wameshakatiwa na kufungwa midomo. They do not care about wananchi anymore:whoo:
 
Back
Top Bottom