Elections 2010 Sitomtambua Kikwete kuwa ni rais wa nchi yangu

Ameshakubalika TZ hata mbinguni pia kwani mamlaka hutoka kwa mungu haukuona wazee walimpa mkuki na ngao? ile ni ya kipiga na kukinga angalia isikupige hiyo
 
Hata mimi rais wagu siyo kikwete huyo ni rais wa ccm na rais wa familly yake
 
Ameshakubalika TZ hata mbinguni pia kwani mamlaka hutoka kwa mungu haukuona wazee walimpa mkuki na ngao? ile ni ya kipiga na kukinga angalia isikupige hiyo

Usitumie neno la Mungu kuhalalisha uovu! Mamlaka inayokubalika mbele za Mungu lazima iwe imepatikana kwa njia ya haki sio wizi! Usipokuwa makini utaanza kuruhusu kila uchafu kwa kigezo hichohicho, hata mtu akikupora mke na kummiliki utasema amepewa mamlaka na Mungu! Halafu unachanganya vitu viwili tofauti: wazee na Mungu, hakuna uhusiano hapo ni kama giza na nuru! Take care
 
True!
\
Kikwete siyo rais halali wa jamhuri ya muungano wa Tanzania. Matokeo ya uchaguzi yanakuwa halali yakikubaliwa na kusainiwa na pande zote zilizoshiriki uchaguzi. matokeo yaliyomsimika Kikwete hayakukubaliwa na Slaa, kwa hiyo usimikwaji wa Kikwete haukuwa halali.
 
tatizo kubwa bado itabidi awalipe mafisadi ahsante kwa ajili ya kumrudisha tena,kwa hiyo miaka mingine 5 hatuna maendeleo maana analipa deni la waliomrudisha ikulu,wewe subiri uone mawaziri wake maana tayari wamesema wataponyeshana madonda ya kampeni
 
Ameshakubalika TZ hata mbinguni pia kwani mamlaka hutoka kwa mungu haukuona wazee walimpa mkuki na ngao? ile ni ya kipiga na kukinga angalia isikupige hiyo

Mamlaka sio mtu. Mungu ameweka mamlaka (sio mtu) ila katupa free will kuamua mamlaka hiyo aiongoze nani. Kama sisi tukiamua kumuweka mwizi kwenye mamlaka hiyo its up to us, ila katika kila uamuzi kuna consequences.
 
Hata Kikwete mwenyewe anajua kuwa watanzania hawamtaki. Kutokana na alivyoingia madarakani hata yeye imeuathiri - hata ukimtazama amepoteza confidence kabisaaa. Hivi taratibu za kwenda THE HAGUE Ziko je?
 
Ushauri kwa serikali? Serikalo gani? Ya JK? Je, ni lini waliwasikiliza watu? That is pure joke, actually intentional comic to incite anger from those that are being robbed of their rights
 
Ameshakubalika TZ hata mbinguni pia kwani mamlaka hutoka kwa mungu haukuona wazee walimpa mkuki na ngao? ile ni ya kipiga na kukinga angalia isikupige hiyo
ni kweli kakubalika kwa huyo wako wa helufi ndogo but Mungu wangu hapana!kaulize unakoabudu tofauti ya hizo mbili!
 
Usipokuwa makini utaanza kuruhusu kila uchafu kwa kigezo hichohicho, hata mtu akikupora mke na kummiliki utasema amepewa mamlaka na Mungu!

HIVI HUYU JAMAA ALIYEPORA MKE WA MTU ANAFAA KUWA RAIS? JE, NAYE NI CHAGUO LA MUNGU????????
 
unashangaa nini matokeo kupinduliwa?

Mosi, Chama chenyewe ni cha MAPINDUZI, kwa hiyo kupindua matokeo si jambo la ajabu.
Pili, Viongozi wake wote wa juu ni Wanajeshi

Mwenyekiti: Luteni Kanali Jakaya Kikwete
Katibu Mkuu: Luteni Yusuf Makamba
Naibu Katibu Mkuu: Kapteni George Mkuchika
Katibu wa Itikadi/Uenezi: Kapteni john Chiligati
Meneja Kampeni: Kanali Abdulrahaman Kinana

Tatu, Gazeti la Serikali, Daily News ambalo editor in Chief ni Rais, limeshasema: Dk. Slaa hatakuwa rais wa tano wa Tanzania

Nne: Tamko la Luteni Jenerali Shimbo linajieleza: "Wagombea wakubali matokeo, la sivyo..."

Tano: Katiba ya nchi/ sheria ya uchaguzi iko wazi: Matokeo ya urais yakishatangazwa, hakuna chombo chochote kinachoweza kuyapinga.


Sasa mnashangaa nini eti mnajidanganya bila kujua kuwa nchi hii ni ya utawala wa kijeshi.

Kumbuka mlienda kupiga kura ili kutimiza haki yenu ya kikatiba, narudia tena kutimiza haki yenu ya kikatiba.
Haya kazi kwenu
 
Back
Top Bottom