Sitasahau!!!

Wakumwitu

Naufahamu vizuri huo wimbo, natena juzi kaka alikuja kwangu akaniambia dada kwenye harusi yako wimbo huo lazima tutaupiga!! ili wajue kuwa tunawaombea, nilibaki kucheka tu!
 
Susy pole sana tena yaani inauma!!! Jamani watu wengine roho zao za kinyama? hivi yeye angependa kesho na kesho kutwa akiwa hayupo hapa duniani mtoto wake afanyiwe hivyo?????
 
Wakumwitu

Naufahamu vizuri huo wimbo, natena juzi kaka alikuja kwangu akaniambia dada kwenye harusi yako wimbo huo lazima tutaupiga!! ili wajue kuwa tunawaombea, nilibaki kucheka tu!


Japo najua ni ngumu lakini Biblia inatufundisha kusamehe na kusahau. Kwa msaada wa Mungu tutashinda tuu

 
Strategizt

Tena watoto wake ninawapenda kuliko maaelezo!!!

Basi tu hiyo ni roho mbaya!!
 
Binadamu huwa wanasahau kwamba aliyemdogo leo kesho atakuwa mtu mzima na ataweza kujihudumia mwenyewe, ubinafsi na umaskini ni chanzo cha dhuluma kwa watoto yatima na wajane, lakini pia shida hizo huwa zinajenga immunity hakuna litakalokubabaisha ukubwani. pole sana
 
Asalam aleikum!!!

Bwana Yesu asifiwe!!

Nimesoma thread ya Lizy kuhusu unyanyasaji wa watoto ikanikumbusha mbali sana, hakika imenitoa machozi!!

Nakumbuka miaka ya nyuma sana wakati nikiwa na miaka 4 tu, mama yangu alifariki kwa ugonjwa wa cancer, hatukukaa hata mwaka baba naye alifariki na ugonjwa wa figo, hapo ndipo nilipotamani dunia igeuke chini juu.

Nakumbuka dada yangu mkubwa alikuwa ndio kwanza yupo 4m3 na kaka yangu ambaye nafatana naye alikua yupo darasa la pili, tulinyang'anywa mali zote za baba yetu, tena tukarudishwa kijijini kabisa ambapo baba aliweka mifugo yake, baada ya muda bb mdg akaja akachukua ngombe wote wakagawana na watoto wa mama mkubwa.

Hakuna aliyetujali, tuliachiwa mbuzi tu pale kijijini, nakumbuka kaka yangu ilibidi aache shule aanze kuchunga hao mbuzi kwa taabu, mimi nilikua nachota maji na kufagia, hakuna aliyejua tunakula nini, tunavaa nini wala tunalala vipi. Dada yangu alichukuliwa na dada mtoto wa mm mkubwa na kugeuzwa house girl.

Nakumbuka wale rafikize baba walipoona hivyo, wakamlipia dada yangu ada tena kwa kuchangiwa na kijiji dada akarudi shule, jirani yetu mmoja akasema tuchanganye mbuzi zetu na zake ili kaka asiende kuchunga tena awe anaenda shule.

kutokana na baridi ya mkoa ambao tulikuwepo, na hatukuwa na blanket siku moja nilishikwa na naimonia ikiambatana na homa kali, yule bb mkubwa rafikiye baba akamtuma kaka yangu aende kwa ba-mdogo akamweleze, kaka yangu akapanda gari kwenda mjini kumwambia baba mdogo, baba mdogo akamwambia kama baba yake na mama yake wamekufa yeye anafaida gani, mwache afe akupunguzieni taabu!! kaka alirudi kijijini na kuomba msaada kwa yule rafiki yake na baba (ba-mkubwa) ndipo nikapelekwa hospitali na kulazwa, ikimlazimu kufanya vibarua vya kulima wakati akiwa mdogo ili kutupatia fedha za matumizi na kuniuguza.

kaka yangu mtoto wa m.mkubwa akaoa kule kijijini akatuchukua lakini niliona bora tulivyokuwa tunakaa wenyewe maana wifi alitunyanyasa sana, jina langu lilibadilika ghafla, nikawa naitwa mbwa, nakumbuka alikua ananiita hivi, "we mbwa mkubwa njoo hapa" ukifika tu unakutana na kibao kizito alafu ndio maagizo mengine yanafuatia!!!

Baada ya muda, wale wote waliotudhulumu alikufa mmoja baada ya mwingine, wale waliotunyanyasa kwa chakula leo ndio wanatuomba chakula, waliotulaza chini leo wanatembea wameinamisha vichwa vyao!!

"usimnyanyase yatima wala kumuonea mjane, mkono wa Mungu utakuwa juu yako"


lakini bado mnasema akina mama ni watu wenye huruma. Ukweli ni kwamba akina mama wengi wapo kama huyo wifi yako
 
dunia ina majaribu ya kutosha, kila mtu akitoa lake humu patakuwa hapatoshi,mie ndio ctakagi kabisa kukumbuka past yangu na nilivyo na kinyongo najish2kiziaga nimeanza kuwachukia upya upya...Mungu huyu mwache aitwe Mungu....pole sana susy wengi tumeyapitia hayo majaribu...
 
lakini bado mnasema akina mama ni watu wenye huruma. Ukweli ni kwamba akina mama wengi wapo kama huyo wifi yako

kwakweli siwezi kulisemea hilo, ila wifi yangu alikuwa funga kazi!!! alikuwa na roho zite zinazotekea kwa shetani!!!!
 
dunia ina majaribu ya kutosha, kila mtu akitoa lake humu patakuwa hapatoshi,mie ndio ctakagi kabisa kukumbuka past yangu na nilivyo na kinyongo najish2kiziaga nimeanza kuwachukia upya upya...Mungu huyu mwache aitwe Mungu....pole sana susy wengi tumeyapitia hayo majaribu...

thanks my dia
 
Pole sana Suzy,
Mungu siku zote anakuletea majaribu ili apime imani yako, na hawezi kukuacha mpweke hata siku moja
Nina imani kwamba imani yako sasa hivi juu ya uwezo wa mungu iko juu sana
ingekuwa tofauti pale ambapo wazazi wako (RIP) wangekuwepo
Na nina imani kwamba Mungu ana makusudi makubwa juu yako na anataka kukutumia
 
Askofu

Nimekusoma!! nimekuelewa

nashukuru kwa kunitia moyo
 
Mpaka mwili wangu umekuwa wa baridi kuna wakati najiuliza hivi m2 anapataje ujasiri wa kuwanyanyasa watoto wa mtu mwingine tena ndugu yake zaidi sana yatima na hata kumpora mali alizoachiwa na wazazi wake!?

Pole sana dada Susy Mungu yupo na yeye ni mfariji wa wote na atakufuta kila chozi lako weka imani yako kwake zaidi sana usilipize walivyotendea waombee na uwasaidie ili wafe kwa aibu zao wenyewe

ONCE AGAIN POLE SANA INAUMA KULIKO UNAVYOSIMULIA
 
Duh, pole sana dada, usisahau "If God is for us who is against us"???? Mshukuru kila wakati.
 
13 Reactions
Reply
Back
Top Bottom