Sitasahau Special Thread

sintosahau siku niliyomtia jirani yetu mimba nikiwa na umri wa miaka 12,aisee lilikuwa bonge la zengwe uswahilini kwetu.Nalog off
 
Sintoweza kusahau siku mtoto wangu wa kwanza my lovely doughter alipofariki. Dah! Ee Mwenyez mungu mpumzishe kwa amani!
 
siku baba yangu mzazi alipofariki. Ilikuwa tar 5 january 2006. Alituita watoto wake wote ktk xmas tukasherehekea, baada ya new year akatwambia kila mtu arudi kwake. Nilibaki. Tar 5 saa moja usiku nilishuhudia akiwa ktk comma, miguu yake ilikuwa ya baridi. Kufika hospt hali ilizidi kuwa mbaya, hadi anakata roho nashuhudia. Kila nionapo msiba popote, scene yote ya kifo cha baba inanijia.r.i.p baba.
pole saana mpendwa,mungu ampumzishe baba yetu kwa amani
 
mie nilifurahi sana nillipoona matokeo yangu ya form 6,coz wakati nasubiri pepa ya mwisho nililala nikawaomba wenzangu waniamshe mda ukufika wakanisahau,niliposhtuka ilikuwa saa nane na nusu na mtihani ulianza saa nane kamili,nilikurupuka na shimizi na sketi na soksi miguun bila viatu wala,shati nikiwa nalia kwa sauti huku nikielekea chumba cha mtihani nikikimbia,dah namshukuru mungu nikaruhusiwa kufanya mtihani na nikafaulu vizuri sana.
ahhh! Mdada ulikua unaota nn!!!
 
siwezi sahau darasa la tatu, imla ya sadiki na sikiri, kalamu yangu ikagoma kuandika halafu mwalimu alikuwa mkali kama simba.bahati nilikuwa mwembamba ingekuwa watoto hawa wa sasa wanaojua stress siku hiyo wangeita ambulensi maana hiyo presha haikiwa ya kawaida.thank god akamwambia monita akusanye madaftari, nikapata muda wa kukopi.
eeh!! Siku yangu umeifanya iwe nzuri kongosho!!!
 
Siku nilipouliza kitendawili shuleni mbele ya mwalimu mdomo wa chupa umefanana na nini then nikatoa jibu aliendani nilikula mboko sana.
 
siku JJ anatangazwa mbunge wa ubungo, nilikuwa miongoni mwa walinda kura wake.
 
Nikiwa darasa la saba mwalimu akawa anafundisha nishati. Akasema mwanga ni nishati inayotuwezesha kuona, nikamuuliza giza ni nini? Nilikula fimbo za kutosha.
Nikiwa sekondari nilimuuliza mwalimu mkuu, dagaa kwa kiingereza anaitwaje, nikapewa suspension ya mwezi mzima.
Walimu wa shule za upe na za kata hatari kabisa

Most of them wamekuwa promoted sasa hivi ni wanasiasa na wabunge, lol!!
 
sintosahau siku niliyomtia jirani yetu mimba nikiwa na umri wa miaka 12,aisee lilikuwa bonge la zengwe uswahilini kwetu.Nalog off
Washawasha umeniacha hoi 12 years ushaanza kujingonolaizi haroooooooooooooooo.!!!!
 
Sintoweza kusahau siku mtoto wangu wa kwanza my lovely doughter alipofariki. Dah! Ee Mwenyez mungu mpumzishe kwa amani!

Pole sana mpenzi mungu aendelee kukupa nguvu na ujasiri kwa hili ,ni zito sana ktk hali ya kibinadamu.lakini katika ulimwengu wa roho tunasema mshukuru mungu kwa kila jambo.
 
Nikiwa darasa la saba mwalimu akawa anafundisha nishati. Akasema mwanga ni nishati inayotuwezesha kuona, nikamuuliza giza ni nini? Nilikula fimbo za kutosha.
Nikiwa sekondari nilimuuliza mwalimu mkuu, dagaa kwa kiingereza anaitwaje, nikapewa suspension ya mwezi mzima.
Walimu wa shule za upe na za kata hatari kabisa

Dah!hii umenitengenezea vema siku yangu,dagaa kwa kimombo wanaitwa sardines or sardine.
 
Similar Discussions

3 Reactions
Reply
Back
Top Bottom