Sitaki tena, sipendi wampime Rais akili!?

Nadhani angekuwa anatuambia kabla ya kupima chochote kuwa anatarajia kupimwa a,b,c etc, ili tusubiri majibu ya kila kipimo. Hii ya kuja kutushtukiza na majibu ya vipimo wakati hatukuambiwa kwamba atapimwa, naona haijakaa vizuri. Mtu unaweza kuanza kufikiria kwamba yapo majibu yanayokuja mabaya na hayatangazwi.
 
Mheshiwa M.K, huwezi kupimwa malaria ukifika kwa daktari kama ukueleza maelezo ambayo yanaonyesha dalili zote za malaria au ukanda wenu au mahali ukaapo pana tatizo la watu kuugua malaria.

Sasa hapa ni mawili aidha Muheshimiwa historia yake inaonyesha kuwa na matatitizo ya akili au eneo analotoka kuna matatizo mengi ya akili.

Kwa hiyo kama sampo kutoka kwenye population hiyo akapimwa au historia yake inamashaka.

Halafu huu ujiko wa kuwa ulienda kupima na afya, kwani lazima tufahamu kuwa umepima.

Kuna watu hawafanyi kazi yao Rais ajibu majibu hovyo hovyo namna hii, au ndio matatizo ya akili?

Na kama ni kweli akili sio sawa utampa majibu gani asiyakosee.

Poleni wafanyakazi wa ikulu kwa kazi ngumu, tupo nyuma yenu kwa maombi. Mungu atawavusha katika hili pia kama alivyowavusha mara nyingi ambazo Muheshimiwa amekuwa akilipuka. Uwezo mnao, shule ya kutosha mnayo, nia njema mnayo, fanyeni kazi.
 
Rais wa JMT ni mtu kama walivyo watu wengine,ana matatizo ya afya kama ilivyo kwa watu wengineingawa tatizo lake ni kubwa hasa kwa nafasi ya Rais.Aina ya ugonjwa alionao Rais wetu mpendwa chaguo la Mungu ndiyo kikwazo kikubwa katika kutekeleza majukumu yake.

Unapokuwa na Rais mwenye matatizo ya akili anayeongoza watu milioni 40 na ushee na katiba inayompa madaraka makubwa yanakaribina na yale ya mwenyezi mungu bila shaka mwenye matatizo ya akili ni wananchi milioni 40 tuliokubali kumpeleka magogoni kwa kura za kishindo.

Wenye matatizo ya akili ni CC,NEC na mkutano mkuu wa CCM waliowakataa watu ambao kwa fikra zangu wasingetufikisha hapa tulipo sasa.Wenye matatizo ya akili ni vyombo vya habari vilivyowaaminisha watanzania kwamba Tanzania ni lazima iongozwe na Kikwete na genge lake la wasanii.

Wenye matatizo ya akili ni mimi na wewe tunayemjadili mtu ambaye kwa vigezo vyote hakustahili kuwa Rais wa Tanzania.
 
HIV umepimwa na uko okay, akili umepimwa na uko okay.....mbona unapimwa sana baba? Kuna issue? Na kwa nini uliondoka Cuba last week ukafika Dar jana, kwani umerudi na meli?

Na ndege yetu umeiacha wapi, maana kwenye gazeti umeonekana unashuka kutoka kwenye Emirates, wakati hapa tulikuona ukikwea Tanzania One. Ni hayo tu, labda niongezee kidogo, baba nilivokuona kwenye bembea na huku mama yuko kwenye vitenge, niijua hapa kuna issue..sasa nimeelewa.
 
Mwanakijiji,

Jamani si alikuwa anapima ubongo kama check up ili kujua afya yake? Wabongo bwana. tatizo hamjazoea kufanya check up, mnataka mpaka muugue.

Rais amekumbana na mambo mengi kulikuwa kuna haja ya kupima ubongo wake ili kuoona kama kunas msongo wa mawazo na isitoshe amekuwa akianguka mara kadhaa, nadhani tatizo ltakuwa kwenye ubongo.
 
Mimi sioni cha ajabu.

Kwani alipopimwa ngoma ili maanisha kuwa ana ngoma? Ni suala la kujiridhisha tu.

Wapo wanaosema kuwa kila mtu ni chizi ila tu kiwango cha uchizi ndiyo kinatofautiana hadi ikafika hadi kila mtu akaanza kushuku ( kama ilivyotokea kwa mheshimiwa mmoja aliyeshauriwa apitie hospitali moja ya machizi Dodoma akapime kiwango cha uchizi). Kama kweli kaamua kupima akili ni wazo zuri.

Lakini kwani nini kimetokea hadi ajishuku na kuamua kupima akili? n ka je itakuwa ni kwa hiariyake au shinikizo la wafadhili?
 
Hao waliompima akili wanafuatilia siasa za Tanzania na jinsi nchi inavyoendelea kuyumba hivyo wakajiuliza inawezekanaje raisi akaacha hali tete kiasi hichi nchini kwake na kuja kubembea na kutazama kaburi la Cheguivara kama hana shida kwenye ubongo.
 
kama inawezekana bora awe anapimwa kila baada miezi sita.

Nadhani miezi sita itakua mbali sana maana kama raisi ataenjoy hiyo benefit angalao mara mbili tu kwa kipindi kilichosalia maana sidhani kama watanzania na akili zetu tutamchagua tena mtu mwenye matatizo ya akili.

Aidha kwakua sisi ndo tuliomuingiza kwenye haya matatizo makubwa ya akili kwa kumpa majukumu yanayozidi uwezo wa ubongo wake, naomba uwepo utaratibu wa akili yake kuchekiwa japo kila baada ya miezi miwili na tuombe bunge limuondolee sifa za kufanya maamuzi makubwa ktk taifa hili mpaka ugonjwa wake utapothibitishwa umepona na haupo kabisa. Hii ni kuondoa uwezekano wa mkuu wa nchi kufanya maamuzi makubwa kwa mamlaka aliyopewa huku tukijua fika anamatatizo ya akili
 
Labda alikuwa ana maanisha kupimwa afya ya ubongo wake na siyo akili!

Ukiwa wamaanisha kuwa ndio huwa inachangia kuanguka anguka kwake au?

Obvious rais akiwa nje ya nchi ni lazima apimwe afya yake kama muda utakuwa unamruhusu na sioni kama ni jambo la ajabu, ila hiyo kupimwa akili mmmh lets be serious with some other issues and not bring jock za kuzusha manenno hapa

 
mzee mwanakijiji mi nakuamini sana, ila sasa sikuelewi what u mean, tupe hizo data, ila kama Rais wetu amepimwa but it concerns with health not mental. tafadhalini sana msimfachafue mzee wetu, hajaonyesha kitu kibaya alichofanya kumfanya ashukiwe akili.
 
Mwalimu wangu alinambia hivi; "SHOW ME YOUR FACE, I WILL KNOW YOUR NAME". Hiyo ndiyo sura ya Rais wako. Unaweza kuunganisha nukta mwenyewe!
 
au hawakumwelewa Malecela aliposema anayetakiwa kupimwa akili ni Sofia Simba? Mi hata sijui bwana! I need to have my akili checked too maana ...
Chonde Chonde mzee wa kijiji! Mpaka wafikie hatua ya kuchanganya kama wale wagonjwa waliobadilishwa mguu na kichwa katika upasuaji wa muhimbili basi tujue ndo kwishnei
 
Nadhani hapa ni tatizo la msamiati. Nijuavyo mimi, katika viungo vya binaadamu hakuna kiungo kinachoitwa akili. Kujua mtu ana akili au hana utamjua kwa matendo yake. Na moja ya kujua uwezo, kiakili, wa mtu ni kumpima kwa kumuhoji na kuangalia majibu yake yanaingia akilini au la.

Baada ya kuona kuwa mtu huyo akili zake ni pungwani ndipo sasa madaktari hutafuta chanzo cha upungwani huo kwa kupima UBONGO sio AKILI.

Sasa matatizo yanayotokana na ubongo, si tu kuwa pungwani. Inawezekana pia ukawa na akili timamu lakini bado uakwa na athari katika ubongo wako, kama vile cancer, mishipa kuziba n.k. na kufanya kuwe na mulfunction katika ubongo. Pia ubongo unaweza kutetereka kutokana na mstuko kati ajali n.k. Hapa hujitokeza pia dalili nyingine, kama vile kutokwa na damu puani, kuanguka anguka n.k. kujitokeza kwa hali hizo nako pia kunaweza kusababisha kupimwa kwa ubongo.

Baada ya kusema hayo, sasa tukiangalia hali ya Rais wetu mpendwa tangu kabla hajingia madarakani, amepata midhoruba ya kuanguka hadharani mara mbili, jambo ambalo si la kawaida. Na sisi wa nje hatujui amekwisha naguka mara ngapi katika hali ambayo si ya hadharani.

Matokeo hayo kwa mtu yeyote yule, yatawajibisha apimmwe ubongo na vioungo vingine ili kujua hali ya afya yake ilivyo hususan kwa matokeo hayo ya kuanguka anguka na sio tu kuridhika na assessment ya local doctors wetu kuwa hali hiyo imejitokeza kutokana na uchovu na kazi nyingi. Hili ni jambo la kawaida.

Kutokana na scenareo hiyo, ni wazi kuwa Rais wetu mpendwa alipimwa UBONGO na sio AKILI. Huenda alikosea tu katika maelezo yake kutokana na kuzongwa sana na mapaparazi.

Nachukua nafasi hii kumpongeza sana Rais wetu mpendwa kwa kuwa muwazi kwa wananchi wake. Kwa tabia ya sisi Waafrika, hasa Watanzania, huwa ni aibu sana kukubali kupimwa ubongo au tu kuhojiwa na Daktari wa Akili mtu hakubali kwa hofu tu kuwa jamii itakuoan kuwa ni mwendawazimu. Kumbe kule nchi zilizoendelea ukipata depression kidogo tu hata kugombana na mkeo mnashauriwa kumuona Daktari huyo. Hapa kwetu tunaishia kumaliza matatizo yetu kwa kudundana mpaka kieleweke.
 
HIV umepimwa na uko okay, akili umepimwa na uko okay.....mbona unapimwa sana baba? Kuna issue? Na kwa nini uliondoka Cuba last week ukafika Dar jana, kwani umerudi na meli?
Na ndege yetu umeiacha wapi, maana kwenye gazeti umeonekana unashuka kutoka kwenye Emirates, wakati hapa tulikuona ukikwea Tanzania One. Ni hayo tu, labda niongezee kidogo, baba nilivokuona kwenye bembea na huku mama yuko kwenye vitenge, niijua hapa kuna issue..sasa nimeelewa.

zanaki umepiga magogoni....!!! ...ime click..pia kwangu ..aliondoka na gulf stream akiwa na mama ...amerudi na emirates akiwa peke yake...!! ....au ndege walipotoka jamaica au trinad ilimpeleka mama kutembelea ma shost zake...??
na ni kweli aliondoka ijumaa cuba....amefika jana ...kweli atakuwa amechoka sana kwa sana kwa safari ya masaa72..toka cuba....badala ya masaa 18!!......si aseme tu alimrudisha mama nyumbani akaendelea na bi mdogo....its time sasa wananchi wajuwe status .....mbona we were okay with MWINYI polygamous status...si dhambi!!..ila ukificha ni dhambi!!!

amezidi kupiga miayo!!
 
Kulikoni,Rais wetu kwenda kupimwa akili ughaibuni? kuna lipi wanatuficha jamani katika nchi hii yenye siri kuanzia mikataba mpk afya ya Rais? au ndo ashapigwa kipapai! na ripoti ya daktari iko wapi kutuonyesha yu mzima? Hii nchi ina hatari! Jamani Mr 6, we ndo tunaekuaminia u kiongozi uliyebakia fanya ze manouvres kuokoa jahazi! Huyu Mr Da Gama kesha pata kizunguzungu!

Mafuta ya generator za IPTL yameisha generator 6 kati ya 7 zimezimwa! Sasa tujiulize hata kununua mafuta serikali hii kunashindikana ama tenda lazma ipite kwa Mr RA? Hivi do they really know a word PLAN????????
 
Raisi kubembea ilhali asilimia 38 ya wananchi wake wanaishi chini ya mlo mmoja ni mzima kweli???????? huko ku-vascodagama kulikopitiiza kwaweza kuwa ndo dalili za matatizo ya akili.


ouch.. inanikumbusha vichaa fulani waliodaiwa kupigwa albadir pale Tanga miaka ya themanini. Mmoja alikuwa anapenda kuvaa vizuri sana lakini kila wakati ameshikilia steering ya gari akitembea nayo huku akijaribu kufuata sheria zote za barabarani.
 
Back
Top Bottom