TRIPLE H
JF-Expert Member
- Feb 18, 2013
- 651
- 349
Wadau salaam,
Nataka kushirikisha uzoefu wangu kidogo kuhusu haya masuala ya kupaa angani usiku na hata mchana. Faida na hata hasara zake!
Nilibahatika kuishi na mjapani mmoja jina lake Yokho Zim nchini Canada. Huyu mtu alikuwa mpole na mstaarabu sana. Alipendwa na kila mtu miaka hiyo ya '90 wakati tunasoma chuo kimoja jijini Ontario. Kwa kuwa nilikuwa mtu ninayejiweza kimasomo alishawishika kuambatana nami kila mahali na hapo ndipo nilipoanza kuichunguza mienendo yake.
Kama angeamua kukaa kimya hata iweje asemi na mtu. Aidha kama ingetokea nikamwacha mji mwingine kama Saskatchewan au Fort hills nilikuwa nashangaa kukuta ashanitangulia kufika chuoni. Angelala kumuamsha haikuwa rahisi labda aamke mwenyewe. Ungemwazia vibaya angekuuliza "kwa nini unaniwazia hivyo?" au "kwani nimekukosea nini hadi utake kuni...." tabia hiyo ilishangaza wengi.
Hayo na mengine mengi yalinipelekea kumchunguza ndipo nilipomgundua hakuwa mtu wa kawaida!
Alipogundua kuwa nishamgundua aliniambia mambo mengi sana ya ajabu na ya kutisha kwa angalizo nisimwambie mtu yoyote, la sivyo ningekutwa ya kunikuta!
Niliamua kukaa kimya, hatimaye nikamsihi anifundishe 'manjonjo' yake, akakubali kwa sharti lilelile la kumsetiri. Tulianza kufanya mazoezi kila siku za j.4 na alhamis mida ya saa 2 - 5 na kuanzia saa 5 - 9 usiku tulikuwa tunaenda 'field'!
Tulipomaliza chuo kila mmoja akashika njia yake, akarudi kwao Japan nikaenda kufanya kazi Colombia. Hata hivyo tulikuwa tukiwasiliana mara kwa mara, mara mie nimfuate Japan au yeye anifuate Colombia. Tulikuwa tunapaa zetu kila tulipotaka kutembeleana.
Niliporudi Tanzania mwaka 2010 niliishi maisha hayo hayo ya kupaa, kupotea ghafla (disappear), kusense mind za watu, kujihudhurisha katikati ya watu bila wao kunitambua, kulala na wanawake ofsn bila wao kujua iwe ucku au mchana, kusema mawazo ya mke wangu nk.
Maisha haya yamenikosesha raha sana kwa sababu nakosa kampani ya watu, ndg na jamaa wananiogopa, nikifika mahali watu wanakaa kimya au wanatawanyika, mke wangu wa kwanza amenikimbia, Wateja kwenye biashara zangu wanapungua kila mara, sipati kabisa ucngz kwa sababu nikipanda tu kitandani nasafiri angani kwenda nchi mbalimbali na wakati mwingine napambana na nguvu pinzani au wachawi, sina hamu ya mambo ya Mungu. Na kadhalika!
Sasa nimeamua kuacha rasmi mambo haya ili nami niishi kama binadamu wa kawaida, nimjue Mungu na niendelee na ishu zangu. Pia kwa wenzangu na mie hususani mliosomea far east haya mambo si ishu kabisa, yanakosesha raha, twawezayaacha.
Nasisitiza,
SITAKI TENA KUPAA!!!!!!