Sitaki kutukanwa, nataka nishauriwe

Je mkeo akikuomba kupata mme wa pili utakubali? maana mapenzi yanauma sana hasa unapofahamu kwamba muda huu yupo kwa naniii.
 
Heheheee nilijua tu huwezi.



Kwamba kuna baadhi ya mambo ambayo watu wengi huwawia vigumu, hiyo ni kweli. Kwa hiyo nimekuelewa.




I say hi too. Nataka nimnunulie personalized sipper cup ya Disney ila nataka kujua favorite Disney character wake...

huyu bado sijajua atapenda character gani maana bado kila kitu kwake ni mshangao.
Tumwache ushamba umtoke ndo nitakwambia favorite wake ili hata ukimnunulia aweze kukithamini.
 
kwani akioa kuna shida gani jamani?
Mbona mwajijaza taabu za bure?

Aoe tu mtu mwenye quality za kuosha, sio alete Asha Ngedere nyumbani.
 
Naam! Kwani nina wivu kukaa nyumba za kupanga ni hatari na humu ndani ya madaladala michezo ya kupeana namba za simu hupendwa sana!

Na hata namba ya simu ya huyo mwandani wako, hakikisha inasajiliwa kwa jina lako...laini ikipata matatizo unaenda ku-renew mwenyewe; otherwise, ukiogopa namba yake kuitoa kwenye daladala, lazima akaiache kwa brazamen wa customer care pale tigo!!
 
USIOE kisa dini,hio dini ambayo inaruhusu mwanaume kuwa na wake wengi na si mwanamke kuwa na waume wengi HUONI KAMA HAISMAMII HAKI???? ingekuwa inasimamia haki ingeruhusu pia na mwanamke kuwa na waume wengi!

Haki kwako wewe ni ipi kwani pale wanawake wanapopewa viti vya upendeleo ndio wewe unaita haki? Haki na upendeleo ni vitu viwili tofauti. Kama wewe uliona ni sawa kpendelewa kwanini useme kupendelewa kwa dini hakuzingatii haki. Halafu bibi yangu kwani wewe ulijiamulia kuwa mwanamke? Kwanini hupeleki malalamiko kwanini wewe tu ubebe tumbo la mimba na mwanamme asibebe. Tafadhali nishauri yenye kuwa ndani ya uwezo wetu na tuache kulaumu amri za Mungu!
 
Upuuzi, haya ni maamuzi yako binafsi ambayo hayatuhusu!

Nahisi wewe ni mpuuzi iwapo unahangaika muda wako kujali mambo ya kipuuzi! Ulimwengu ni mkubwa na hii siyo thread pekee iliyomo humu. tafuta yanayokuhusu na tuwachie upuuzi wetu la ni mwanachama endelea!
 
ujue mkuu wangu,kitabu kitakatifu cha Mungu Quran kiliporuhusu ndoa za mke hadi wanne kilikua na malengo mazuri tu mf.kama kuwajali yatima na wajane.Lakini wengi wa kaka zetu mnatumia hii ruhusa kinyume kabisa na mapenzi ya Mungu,mfano mzuri ni wewe hapo kwenye dhambarau,wewe unaoa sbb tamaa zako za kimwili zinakutuma kuona kuwa wako wazuri zaidi ya mkeo wa kwanza.Ni kweli wazuri wako wengi na mzuri kuliko wote bado hajazaliwa,lkn sasa kama wewe unaoa sbb unataka ujijazie wanawake wazuri nyumbani kwako mbona sasa dini inakubana maana mwisho ni wa nne,sasa inaonesha utakapofikia kiwango cha mwisho na wewe ni mwenye uroho kila mwanamke mzuri unamtaka,utaanza kuwa asherati sbb nina hata ukioa wanne bado kuna utakayemuona amewazidi hao wanne.

Sasa je sisi hapa tukikushauri uoe sbb dini anakuruhusu halafu mkeo akakataa kata kata sbb na yeye dini inasema ni lazima aridhie ndio uoe,wakati huo huo wewe ndio umeona kabinti kazuriiiii na kamekubali ukaoa itakuaje hapo na macho yako yanakuonesha kabisa kuwa ni kazuri kumshinda mkeo wa sasa,ukikatizama kana miaka 22 na mkeo ana 44,kana ziwa saa 6 na ya mkeo yamezimia kwa usingizi,uso wa mkeo umejaa wrinkles wa kabinti umenyooka na wenye kuteleza mithili ya hariri,ni kazuri mkeo anaonekana kinyago akisimama mbele yake lkn ndo wife anasema no sitaki mke mwenza,kama watoto naweza kukuzalia idai utakayo,penzi hujawahi kuomba nikakunyima labda nikiwa mgonjwa maana hata ww ukiumwa nakuvumilia,sijawahi kulalamika kuwa kuna kinachonishinda sasa kwanini wataka kuniletea mwenzangu,sitaki.Utafanyaje.Sidhani kama utakaacha kabinti,utaoa kinguvu huku ukipita kifua mbele kuwa dini imeniruhusu kumbe huna hata moja ulilofanya linalikubaliana na dini itakavyo.

Cheusi mbona unanifanya kama hao wanaume wenye roho mbaya? Nimesema ndowa inatufunga kuamua kubadilisha wanawake hata kama kila siku wanazaliwa wazuri basi na sio naowa kwasababu natafuta wazuri(nitapata tabu kama nina lengo hilo).
Hili la kuongeza mwengine huwezi kunizuia kwani mimi sitegemei kitendo cha ndowa (Kuingiliana) kuwa ndio kila kitu kwangu. Inawezekana kuna mengine na wewe mwenyewe umekiri kuwa kuna sababu zilizowekewa kuowa wake hadi wanne. Unataka kuamini kuwa mimi simo katika hao waliopewa ruhusa?
Kwenye dini kisisitizo ni kuowa wake wawili, watatu au wanne na ikiwa huwezi uadilifu basi owa mke mmoja. Sasa wapi palipotowa masharti hayo unayoyasema wewe? Iwapo ndowa ni mfumo mzima wa mahusiano katika jamii kwanini hili la mie kuowa ulielekeze kwenye hamu ya mwili?
Usiwe na waswasi iwapo wewe bado hujaolewa unaweza kuwa candidate kwani nitakapoamuwa kuowa nitafuata maagizo yote na kitoka nyumba nitatowa! Mke wangu hana sababu ya kunizuia nisiowe mwengine kwani haki aliyonayo inaishia pale anapokosa sababu ya kunizuia nisiowe.
 
hakuna mwanamke anayependa,wanaridhia baada ya kuona hamna jinsi,kwa mwanaume hamna u turn ndio afanyeje in short wanakubali shingo upande....mtu uliyempenda huwezi kumruhusu awe na mtu mwingine period.
Usifikiri watu wote wako sawa na wewe amabe hata maagizo ya Mungu unayatia dosari. Sasa kuna haja gani ya kuolewa si utowe tu kwa unaempenda kwani pana haja ya mkataba maalum kwenye aina ya mapenzi unayotaka wewe?
 
Ushauri wangu wa bure, ndoa ya pili au ya tatu ni ndoa ya utapeli au uwizi, keep in mind love is not enough to convince someone lazima kutakuwa kuna maslahi fulani yanatarajiwa from both side.

Hakuna mwanamke anayekubali kushare mume if there is nothing in return apart from love thats the fact.
 
NN mfano dini ingekua inaruhusu na wanawake tuolewe na wanaume wengi.
Mkeo anakujia,"mume wangu Ngabu unajua kiasi gani nakupenda,mpenzi wangu naomba unipe ridhaa yako niongeze mume mwingine,muwe wawili,hana shida ni mtulivu cha msingi umheshimu tu na kumpenda,utapata rafiki wa kushangilia naye mechi za MAN U pia atakusaidia mambo mengi si unajua tena we umeshaanza kuwa mtu mzima na yeye bado ni kijana."
Kama kweli utaridhia kwa moyo wako bila kushurutishwa basi ujue kuna wake wa kwanza wanaoridhia ila kama moyo wako utakataa basi ujue hakuna mwanamke anayeridhia hii kitu.

Cheusi, haya ni malezi na mila tulizozooleshwa. Kwa mfano si kuna makabila ambayo wanawake wanaowa wanawake wenzao na kuwapagaza wanaume ili wapate watoto? Si kuna makabila kwanza unapiga ngwala na kubikiri ndio unapeleka posa? Si wazungu mwanamke anaweza akakukataa na kuondoka na mwanamme mwengine nawe ukabaki solemba usimfanye kitu?(Fanya Bongo uone).
Mimi naowa mke wa pili kwa vile dini yangu imenipa ruhusa na mke wangu kwa kufahamu hilo atakubaliana nalo huku akisisitiza haki zake zilizowekwa.Inashangaza kuwa unakubali sheria mama ya kuishi na mwenzio baada ya kuowana lakini unakataa kifungu kinachofuata na kudai kuwa sheria ni batili.
Cheusi unakumbuka Marehemu sofia Kawaw alifanyiwa maandamano kwa hili na wanawake walishiriki?
 
NN mim nilikuomba wewe ujibu kama wewe.UNGEMKUBALIA?

Ha Ha Ha! Hivyo hujaona wanaume wakawapeleka wake zao kwa mabosi? Hujaona wanaume hawaendi nyumbani kwanza kabla hawajawapigia simu wake zao ilikupewa ruhusa? Hujasikia wanaume wanaondoka nyumbani kutwa hawajaacha kitu nyumbani wakirudi wakafakamia pilau wala wasiulize kitu? Hebu kamuulize Busheke!
Hii si sawa na kuruhusu mume wapili?
 
Ngabu nilijua huwezi kukubali,hata ungesema ungekubali bado ningejua unadanganya,sbb najua haiwezekani.
Nakuomba utuambie kwanini wewe moyo wako umeona kwamba usingemkubalia.

Cheusi hata mimi ninaetaka kowa wa pili nisingemkubalia.Kwasababu hii ni out of context katika jamii yetu

 
Ukioa nakushauri wasikae mbali,manake kuna Mdingi namfahamu anao watatu,mmoja anakaa Tanga,mwingineKibaha,mwingine Dar.
Kwa hiyo inabidi karibu kila wiki adrive kutoka Tanga kuja either Dar au Kibaha,ili kuhakikisha anawapa haki yao sa si shughuli hiyo?

Nitazingatia,tena ahsante kwa kunikumbusha hilo!
 
Kwani mmoja hakutoshi???? Au keshachuja kwani miaka 20 mingi ati!

Hanitoshi! Napenda mambo mengine yeye hayawezi au bora azidishe muda wake kunifanyia hayo ninayompendea yeye badala ya kugawa muda kwa mambo ambayo hayaniridhishi!
 
Siwezi kutoka na mandingo hata kama akinambia aliaacha hiyo kazi miaka kumi ilopita.

NN mim pia sipendi generalisation,lkn ukiwa kama binadamu unaweza kujua kitu ambacho ni kigumu binadamu mwingine kufanya,au ukiwa kama mwanamke unaweza kujua ni nini mwanamke mwenzio anaweza kufanya au kutofanya sbb na wewe unafanana nao,japo kila mmoja ana tabia zisizofanana na mwenzie.

Mfano binadamu yeyote wa kawaida anajua kuua binadamu mwingine ni kitu kigumu sana,hata kama sisi sio every human being lkn tunajua kuua binadamu mwingine ni kitu kigumu sana na wengi hatuwezi lkn wapo wachache wetu wanaweza kufanya,na wanapofanya tunawashangaa kuwa wana mioyo ya aina gani mpaka wameweza kufanya hivyo.

hivyo sihitaji kuwa every woman kujua kuwa haiwezekani kwa mwanamke aridhie mpenzi wake ampende mwanamke mwingine.


btw uncle wako anasema hi.

Cheusi sikulaumu lakini ulipaswa kwanza kuona huo uchungu wa kuolewa matara ndio ungeweza kujuwa kweli hilo jambo ni baya au vipi. Bado nakupa nafasi unifanyie majaribio mimi (kama hujaolewa) na baadae utajuwa kwanini wanawake wenzio wanaweza kukubali kile unachoona wewe huwezi. Jaribu kidogo haiumi, ukiona mambo magumu utaondoka!
 
Kwangu mimi kuniongezea mke mwingine au kufanywa mke wa pili ni tusi wala sio mapenzi (samahani kwa wale mtakaokerwa/kukwazwa na maneno yangu)! Siamini katika kupendwa sawa kwa sawa hasa kwa pendo kama hili linalohitaji attention, care na hisia za dhati toka moyoni. Na pia sipendi kupangishwa foleni kwenye penzi langu.....so nikitoa ruhusa basi itakuwa kwa mimi kuachia ngazi coz najua siwezi kuridhia kabisa!!

Nauheshimu msimamo wako lakini nini tusi katika ulimwengu wetu wa sasa? Samahani, lakini kama kivazi chenyewe ni kuvionyesha hivyo vinavyoitwa matusi unafikiri dunia yetu ni ya kujali nani kasema nini? Angalia maslaha dada angu after all hakuna uhakika wa mtu chake peke yake dunia yetu ya leo. Tukiowana angalau tutakuwa tumehalalisha huo usasa wa leo.
 
hata mim mtu kunijia eti ananiomba aongeze mwenzangu nitaona kanitukana na nitamkubalia kisha natimua zangu nimuache na ampendae.

Wanawake wanaokubali kuna sababu nyingi zinazofanya wakubali ikiwa ni uoga wa kwenda kupata shida,hawa ni wale wanawake wavivu wasiojiamini wanaoishi hapa duniani kwa support ya mwanaume,bila mwanaume kanga nzuri hawezi kuvaa au bila mwanaume watoto wake watapata shida eti anabaki kwa faida ya watoto wake,au wengine ushirikina unafanya abaki huku akihangaika kwa waganga akidhani iko siku penzi lililohamishiwa kwa bi mdogo litarudi kwake.
Kubaki ktk ndoa ya hivi ni kutojua thamani yako,hata kama sizai siwezi kukuruhusu uoe mke mwingine eti ili upate watoto,je ingekua ni yeye mwanaume ndo hana uzazi angeniruhusu nikazae nje ili aitwe baba.
Omba Mungu yasikukute! Unaonaje wale wanaojitundika?
 
Back
Top Bottom