Sitaki kuidhulumu nchi yangu, kamwe sitojiunga na CHADEMA chini ya uongozi huu

Siami Chadema kuwakumbatia mafisadi na ikitokea hivyo watajizika wenyewe.Chadema msije mkawakumbatia mafisadi au makapi ya CCM.
 
HUKU MWANAKIJIJI,KUBENEA na wanaharakati wengine wakijitahidi kuhakikisha ufisadi unapungua, kumbe mambo tofauti kabisa
gazeti la Chama cha CDM kilichoapa kumbana na mafisadi linakuwa mstari wa mbele kuwatetea? lipo tayari kuangamiza familia ya rais lkn wakiwatetea wanaoujulikana na watz wengi. msimamo huu unanifanya nikichukie Chadema huku viongozi wake wakikaa kimya
linakuwa mstari wa mbele kumchafua rais wa nchi ilimradi muhariri anafanikisha malengo yake binafsi ya kuwatetea akina EL,RA na wengine ambao tayari CDM wanaona ni hatari kwa taifa letu.
Watz wengi wanaamini vyombo vya habari, ndio maana wengi tunaamini msimamo wa CDM kuhusu ufiadi ni kiini macho tu. sina haja ya kujiuna na CDM Hii chini ya mwenyekiti mbowe, katibu slaa, naibu Zito.
SITOJIUNGA NA CHADEMA NA KUINGAMIZA NCHI YANGU

hapo kwenye red, walau MzeeWaHoja umetaja majina maana ccm wamekuwa wanaimba kuwa mafasadi wanatakiwa waondoke ndani ya siku 90 lakini hakuna mwana ccm aliyetaja kwa majina. Vipi mmeshawapelekea barua hao unaowaita mafisadi?
 
Haya wazee na mzee wa hoja,ni aibu sana kuona nchi inatafunwa na wachache,ila pia sio vizuri kutumiwa na wachache ili wao wanufaike
Mimi naamini tunatakiwa tushiriki wote kwa dhamira ya kweli kuokoa haka ka'nchi jamani.
MIMI NAAMINI TUSIKAE TUKISUBIRI WATU FULANI WALETE MABADILIKO NDO NASI TUJIUNGE,NAKUOMBA WEWE MZEE WA HOJA UJE CDM UFANYE MABADILIKO KWA HOJA NA KUKEMEA MAOVU UNAYOYAONA,ILA KAMA UNAONA HUTAPEWA NAFASI YA KUSIKILIZWA KAMA TUNAVYOWASIKIA WANACHADEMA WENGI WAKINUNGUNIKA,BASI KATIBA INAKURUSU KUANZISHA CHAMA CHAKO ILI UIBADILISHE NCHI.
 
Cha kushangaza Gazeti tukufu la Chadema, Tanzania Daima linanatetea mafisadi wa CCM

unajua umiliki wa gazeti la tzdaima au unaongea tu! Ni kama vilaza wa ccm wanahisi kila mpiga ufisadi ni cdm.
 
hii ni hatari ikiwa kibanda anatumia kalamu yake vibaya huku cdm ya mbowe ikikenga meno na kucheklea, sitaki kuona tz ikikkupmbwa na vita kwa sababu ya wachache

MzeeWaHoja,

Huna hoja mzee! Maneno yako yanaonyesha kuwa wewe ndiye unayetetea UFISADI. Kila mtz mwenye akili timamu anajua kabisa kuwa Lowassa,Chenge na Rostam ni MAFISADI waliokubuhu ndani ya Chama Cha Magamba-CCM na Serikali yake. Hilo halina ubishi.EL,RA na AC wako kwenye LIST OF SHAME YA WATU 11 iliyoibuliwa na Dr. Slaa wa CDM.

Rais wako na M/kiti wako wa CCM wakti wa Kampeni za mwaka jana alizunguka kwenye MAJIMBO ya EL,RA na AC akiwanadi kuwa ni WATU SAFI na ndiyo maana mkawachagua kuwa wawakilishi wenu Bungeni! Je, huoni kwamba Kiwete wako yuko pamoja na hawa MAFISADI??? Watu wanaposema kuwa Kiwete na Riz 1 wote ni MAFISADI hawajakosea.!

Wazungu husema,nanukuu,''Birds of the same feather flock together". Kiswahili chake ni kwamba Ndege wa manyoya aina moja huruka pamoja. Kwa hiyo Mzee ni kwamba JK,EL,RA,AC,RIZ1 wote ni ndege wa aina moja. LAZIMA WARUKE PAMOJA!

Wewe ni CCM damudamu kwa hiyo hatukuhitaji CDM. Tunakutakia kila rakheri katika mkakati wenu wa kujivua magamba.

CDM iko IMARA.
 
kwani ni nani amekuita chadema? chadema haihitaji watu wanafiki kama wewe. unaonekana umetumwa na ccm kukichafua chama chetu cha wanyonge. endelea kubaki kwenye hicho chama cha mabepari (ccm).
 
unajua umiliki wa gazeti la tzdaima au unaongea tu! Ni kama vilaza wa ccm wanahisi kila mpiga ufisadi ni cdm.

Sasa wewe ndio kilaza kabisa hivi kuna mtu ambae hajui kuwa Tanzania Daima ni gazeti la Mbowe na Mbowe ni Mwenyekiti wa CDM! Acheni propaganda za kichadema chadema hapa!
 
Hoja ya kinafiki toka kwa mnafiki!!!!!!! Umepata majibu yako siku nyingine fikiria kwanza kabla ya kumwaga pumba hapa, Mwone!
 
HUKU MWANAKIJIJI, KUBENEA na wanaharakati wengine wakijitahidi kuhakikisha ufisadi unapungua, kumbe mambo tofauti kabisa.
Gazeti la Chama cha CDM kilichoapa kupambana na mafisadi linakuwa mstari wa mbele kuwatetea?

Lipo tayari kuangamiza familia ya rais lkn wakiwatetea wanaoujulikana na watz wengi. Msimamo huu unanifanya nikichukie Chadema huku viongozi wake wakikaa kimya.

Linakuwa mstari wa mbele kumchafua rais wa nchi ilimradi muhariri anafanikisha malengo yake binafsi ya kuwatetea akina EL,RA na wengine ambao tayari CDM wanaona ni hatari kwa taifa letu.

Watz wengi wanaamini vyombo vya habari, ndio maana wengi tunaamini msimamo wa CDM kuhusu ufisadi ni kiini macho tu. Sina haja ya kujiunga na CDM hii chini ya mwenyekiti Mbowe, katibu Slaa, naibu Zitto.

SITOJIUNGA NA CHADEMA NA KUINGAMIZA NCHI YANGU

Mkuu, bora ukae mbali maana hata uongozi huu wa CDM usipokuwepo halafu ukajiunga na uanfiki wako wa ki-CCM kamanda Godbless Lema lazima atakubomoa makonde tuu ... kaa huko huko usije umizwa kaka
 
Back
Top Bottom