Sitaichukia nchi yangu tanzania,lkn kwa haya nitasema tu

cheusimangala

JF-Expert Member
Feb 27, 2010
2,585
497
DSC00085.JPG


From michuzi jr!
 
Yap..mwendo wa shule hiyo ni huo...kama usipoleta dawati unakaa chini!
Lakini wazazi wa watoto hawa ni aina gani, maana watoto wamevaa vizuri sana, wanashindwa nini kuchangia madawati?
 
Hizi skuli zetu jamani

Pakajimmy hivi kuchangia madawati ni kazi ya wazazi au?
 
Cheusi hata ukisema, utaumiza koo lako bure.
Mi huwa nikiona hali kama hiyo najifungia ndani alafu nafanya ibada baalum ya kuwalaani viongozi wabinafsi na mafisadi.
 
Ndio maaaanake serikali ilisema tugawane umaskini kwa kila upande kuchangia hadi universities!!!
Wakuu hilo tatizo basi serikali yetu inashindwa kwanini? wakati watoto wao wanasoma shule nzuri kuliko hiyo shule wanayo kaa chini hao wanafunzi?hayo ni matatizo ya Viongozi wetu waache mambo ya ufisadi nchi yetu itaendelea ni kitendo cha aibu kwa serikali kushindwa hata madawati kuwapatia watoto wa shule Ehhh tutafika kweli jamani tuendako?
 
Wengi wa viongozi wetu walisoma kwa shida,wanapenda watoto wa wengine nao waonje joto ya jiwe,ila inasikitisha sana kwamba huu ni ulimwengu mwingine,kizazi kingine!!
Ipo siku bubu watasema kama sisi hatusema haya na kuyakemea!!
 
kwani hiyo shule ni ya wapi? isije aibu za Malawi unapazia Tz, oooh!
 
Kimsingi ni kazi ya serikali, lakini wakati tunaisubiri serikali(sijui kwa muda gani!) ni lazima wazazi wajishughulishe!

Kama ndo hivyo kila mtoto anapoanza skuli lazima aende na dawati lake ..
inakuwaje kwa sisi tusio na kipato cha kueleweka
 
Yap..mwendo wa shule hiyo ni huo...kama usipoleta dawati unakaa chini!
Lakini wazazi wa watoto hawa ni aina gani, maana watoto wamevaa vizuri sana, wanashindwa nini kuchangia madawati?

Na mtoto akimaliza shule anarudi na dawati lake nyumbani ama vipi?Si mali yake ati?
 
kwani hiyo shule ni ya wapi? isije aibu za Malawi unapazia Tz, oooh!
Hiyo shule itakuwa ni ya Tanzania, kwani mpiga picha anatupatia shule ya Malawi (ambayo ni mbaya) ili tujifunze nini, anataka tujifunze UBAYA?

Swali hapo ni, je,tutafika? Ukitilia maanani Muungano wa Nchi za Afrika Mashariki!!!!!!!!!
 
Does it make any sense kununua dawati?

Kwangu mimi gharama ya elimu ni kubwa kuliko dawati. Kama mwanafunzi hapati dawati, hiyo elimu anaweza kuipata? Sio ajabu majibu yakawa mepesi tu kuwa matokeo mabaya ya kidato cha nne na huko tuendako cha sita siyo sababu ya shule za voda faster kama alivyosema waziri.

Hebu Tanzania tuwe na vipaombele vitatuwezesha kusonga mbele kwa kasi ya ajabu tofauti na hii itizamo ya kisiasa zaidi.

Mfano: 1. Sikuridhika na stimulas package- Ile hela (zaidi ya Trilioni) italiwa na wachache, ingeweza kuondoa tatizo hili
2. Mabilioni ya JK yangeweza kupunguza kwa kiasi kikubwa tatizo hili, kuliko kwenda kuwekeza sehemu ambazo hazina maandalizi kwa sababu za kisiasai zaidi. Elimu ndio itakayomkomboa Mtanzania na sio kumnunulia Tshirt na Kofia zenye picha nzuri za wagombea walionenepeana kwa rushwa!
 
Kimsingi ni kazi ya serikali, lakini wakati tunaisubiri serikali(sijui kwa muda gani!) ni lazima wazazi wajishughulishe!

PakaJimmy tupo pamoja mkuu nadhani kuna haja ya wazazi kujishughulisha katika hili maana wanaoteseka ni watoto na sio serikali. Jana JK amefungua utaratibu wa kuchangia chama kwa njia ya simu kwa ajili ya uchaguzi! Huku vijana na watoto wa Taifa hili wanakaa chini? Hey tubadilike ndugu zangu tumelala sana kiasi kwamba ila kitu ni serikali? Shule twazijenga wenyewe iweje madawati ni serikali ndo ichangie? Hapana me siungi mkono katika hili kwamba serikali ndo ihusike katika kila kitu!
 
Cheusi hata ukisema, utaumiza koo lako bure.
Mi huwa nikiona hali kama hiyo najifungia ndani alafu nafanya ibada baalum ya kuwalaani viongozi wabinafsi na mafisadi.

Gud idea mkuu!! nilikuwa nafikiri la kufanya!!!
 
kwani hiyo shule ni ya wapi? isije aibu za Malawi unapazia Tz, oooh!

Hiyo ni TZ tu, huna haja hata ya kufikiri na hao ni watoto Waalimu ndio wale wanaofundisha Square root. (miaka 5 Mjengoni 46m) unaondoka nazo na kama mko mume na mke 92m zinaingia ndani. Mungu awape nini viongozi wetu. Tunafahamu mambo mengi mengine unamezea
 
Yamekwenda wapi masomo ya kiufundi shule za msingi?
Watoto wapewe fursa ya kujifunza taaluma ya useremala ili kuwawezesha kujichongeshea madawati yao chini ya uangalizi wa mwalimu husika.
Hii mambo ya kusubiria msaada wa serikali,unawaumiza watoto wetu.
 
Kinachonishangaza zaidi ni huyo mwanafunzi wa kwanza kushoto, kalaza dawati moja akalikalia. Is it my eyes? really hii shule inaelekea haina uzio kama kawaida ya shule nyingi. Viti utakuta vinatumika kukaliwa na walevi wa lubisi mahali hapo jirani jirani!
 
Back
Top Bottom