Sisi watanzania, mapinduzi ya umma na CHADEMA (ni mapinduzi gani tutarajie toka kwa sisi watz?)

jouneGwalu

JF-Expert Member
Apr 11, 2011
2,687
1,780
Ipo wazi sana sasa kuwa hali ni mbaya!
Kwa yanayoshuhudiwa kutokea katika medani ya siasa zetu,
Hali mbaya hii imefasiliwa na kila msoma alama za nyakati,
Wadau mbalimbali kutoka kila kada wametoa onyo juu ya hili.

Ni muda sana toka tuasisi mizaha, uongo, unafiki, kulindana,
na ubabaishaji katika siasa za nchi yetu,
Kinachoendelea kwenye serikali ya Rais Mh Kikwete,
Ni muendelezo tu wa vituko visivyo na jipya toka awamu za nyuma,

Tofauti kubwa inayoleta mshindo zaidi ni kusambaa sana kwa habari,
Na mabadiliko makubwa katika siasa za upinzani, zikiratibiwa vyema na watu
Wanaojua wanachokifanya…….CHADEMA!

Hali hii katika nchi yetu imefanya watu makini wote washike midomo mithiri ya
Watu wanaosubiri kushudia janga kutokea… ndio, "MAPINDUZI YA UMMA"
Dunia ikiwa kwenye mpito wa kushuhudia UMMA ukitwaa mamlaka yake na kubadili mustakabali wao,
Hicho ndicho kinachoaminiwa kitatokea hapa kwetu, tena mda si mrefu.

Na hii imeshaonywa na watu makini wote kwenye nchi yetu kwa nyakati tofauti.
Binafsi, bado napata shida sehemu moja!

Kwa uelewa wangu wa dhana hii ya "MAPINDUZI YA UMMA"
Na nikilinganisha na sisi waTZ kwa ujumla wetu. Bado ninashaka sana.
Na ujasiri wetu na fikra zetu kuelekea kufanya "MAPINDUZI YA UMMA YA WATZ"

Pamoja na ujasiri unaoonekana kutokea kwa baadhi ya watu wetu, lakini bado tunahitaji kujichambua zaidi kabla ya kuweka hofu/shauku katika kutarajia kitu ambacho kiuhalisia kinaweza kisiwepo au hata kama kitatokea kitakuwa sio katika sura yake halisi.
Kwa mpaka sasa ukichambua matukio ambayo kwayo watu wamepelekea kuonya, utagundua kuwa karibia matukio yote ni yanaratibiwa na aidha chama cha siasa chenye nguvu au dhehebu la dini!

Rejea matukio ya CUF (enzi hizo ngangari) na ya sasa ya CHADEMA. Pia rejea matukio ya "vurugu za mwembe chai" na "Kakobe na TANESCO".

Ninachotaka kusema hapo ni kwamba bado hatujakuwa na UMMA wenye uwezo wa kuhoji na bado ionekane kuwa "UMMA WAZT UMEAMUA"
UMMA wa waTZ bado unataka kusukumwa na kuendeshwa kuelekea kuzitambua na kuzihoji haki zake.
Kitu pekee kinachotosha na bado kikabaki katika MAPINDUZI YA UMMA ni AJENDA, inayojenga uhalali wa UMMA kuhoji mfumo uliopo kwamba "Mnayotenda ni kinyume na tulivyokubaliana" (KATIBA).

Si sahihi kwa MAPINDUZI YA UMMA, kuongozwa na kusimamiwa na vyama vya siasa au jeshi.
Ndio maana Wamisri na Watunisia walisikika wakisema kuwa "HAYA NI MAPINDUZI YETU"… Hakuna chama cha siasa kilichojipa kuhodhi mapinduzi yale japo vyama hivyo vilishiriki na kuunga mkono lakini havikuongoza.

Ndio maana kamwe kinachoendelea Libya hakitakuja kuitwa "MAPINDUZI YA UMMA"..Kamwe!

Kutoka kwenye ukweli huo, hali hapa kwetu kiukweli haipo hivyo.
Kinachoonekana kinaweza kutokea ni kuwa WATZ kwa sasa wapo tayari kuongozwa na CHADEMA kuelekea kufanya MAPINDUZI ambayo ntasita kuyaita ya UMMA.

Na sidhani kama CHADEMA wapotayari kulifanya hilo, sababu sio nia yao (labda)……
Kama hiyo ni nia yao, sioni sababu za wao kushindwa kila kitu ni dhahiri sasa.
UMMA usio jitambua kama wetu hauwezi kufanya MAPINDUZI ambayo wengi tuyatamani.
 
Back
Top Bottom