Sisi wa vijijini, Tanzania kama sio yetu vile

kiLimIlire

JF-Expert Member
Apr 8, 2012
311
639
Matukio ya mjini yameteka uTanzania wetu tuishio vijijini, mara Ponda,mara Fareed, mara Ulimboka, mara JWTZ k/koo, mara soja kampiga polisii Ubungo mataa... yaan nchi inaendeshwa na matukio yaliyoko sehmu ndogo tu ya nchi! what the hell!!!sisi huku vijini,elimu ya kata haitupi matumaini,wajawazito hawaishi kuombwa hela ya kujifungulia,maji tunayafuata mbali kwa punda... "nyie" mpo bize na vijimatukio vyenu vya kulealea...tujuavyo sisi wa vijijin,nchi ina mbuga,misitu,maziwa,madini,ges i nk. mnatusahulisha yote hayo tukiwa katika hali duni na kushadadia vijimatukio vyenu huko mjini...

U Wapi UTANZANIA WETU SISI WA VIJIJINI
 
mkuu

Umesahau kauli ya mwalimu?

Pengo kati ya walionacho na wasionacho likiongezeka hatutakuwa salama - JK Nyerere.

Kinachofanyika mijini Pengo limekuwa kubwa mno sio pengo tena ni Bonde la ufa. kwahiyo sisi maskini huku mjini tumeachwa na watu tunaoshinao, hivyo ni kujenga chuki za kila aina Udin, ukabila, ukanda, nk- mtafaruku anakuwa mjukuu.

Huko vijijin mmesahaulika na pengine uchochezi haujakomaa kwasabab wengi wenu maisha na vipato vyenu vinalingana.

Lakini Mwanga wa matumaini unawakaribia, nuru yake itaangaza Inchi nzima na kuwakombowa wanyonge na masikini wa taifa - Tanzania mwanga huo ni CHADEMA (chama cha democrasia na maendeleo) Tunahitaji uongozi utakaowaunganisha watanzania wote bila kujali itikadi za dini zao, kabila zao au wanatoka kanda gani bali ticketi ya kujiunga chadema ni UTANZANIA wa kila mmoja wetu.

Tunahitaji Elimu Bora, Afya bora, Miundombinu bora na siasa safi maeneo yote ya tanzania, Kwenu huko VIJIJINI na pia MIJIN sio hivi sasa mjini tena kwa waheshimewa wachache tu wa vijisenti
 
njoo mjini nina chumba kikubwa na sebule hakina mtu
hahaha nimecheka sana! obviously utakuwa na upeo mdogo. status yangu ipo general kwa maana ya kuwakilisha kundi la wanajamii! its not about me, ts about ppo...
 
Ndo maana kila mtu anajilundika mijini, tena mostly Dar kwenye Dickensian squalor.
 
Dickensian wat??! Mind digesting it for us with delicate stomachs??!

Google is your friend, you learn more by the participatory process rather than by being spoonfed. In this case the participation is a simple google search.

You might even find an interesting site.

You are supposed to be a Mentor after all.
 
hahaha nimecheka sana! obviously utakuwa na upeo mdogo. status yangu ipo general kwa maana ya kuwakilisha kundi la wanajamii! its not about me, ts about ppo...
Usijali mambo ya upeo dogo, Njoooni wote mjini kama mnaona huko bush serikali inawapotezea . Halafu nataka uniambie pamoja na upeo wako mkubwa , umefanya nini cha maana kujisaidia wewe na nchi yako.
 
Matukio ya mjini yameteka uTanzania wetu tuishio vijijini, mara Ponda,mara Fareed, mara Ulimboka, mara JWTZ k/koo, mara soja kampiga polisii Ubungo mataa... yaan nchi inaendeshwa na matukio yaliyoko sehmu ndogo tu ya nchi! what the hell!!!sisi huku vijini,elimu ya kata haitupi matumaini,wajawazito hawaishi kuombwa hela ya kujifungulia,maji tunayafuata mbali kwa punda... "nyie" mpo bize na vijimatukio vyenu vya kulealea...tujuavyo sisi wa vijijin,nchi ina mbuga,misitu,maziwa,madini,ges i nk. mnatusahulisha yote hayo tukiwa katika hali duni na kushadadia vijimatukio vyenu huko mjini...

U Wapi UTANZANIA WETU SISI WA VIJIJINI
Mkuu umenichekesha kwa kichwa cha habari ...'kama si yetu vile!' lakini umeongea ukweli mtupu..Vyombo vya habari vipo kwa ajili ya Dar na si sehemu nyingine yoyote ya nchi kwani vyombo vya habari wakati mwingine ni sumu...wanasema MEDIA CAN DESTROY OR MAKE YOU!
 
Mkuu umenichekesha kwa kichwa cha habari ...'oh! umenishtua ulvyoniita "Mkuu", sijawah kuitwa hivyo! huku vijijini wote tunajiona sawa... "wa mjini" bhana!! Terible kie kie kie kie anyway asante kwa mawazo mazuri
 
Google is your friend, you learn more by the participatory process rather than by being spoonfed. In this case the participation is a simple google search.

You might even find an interesting site.

You are supposed to be a Mentor after all.

Dat last sentence isnt fair.
I got t though Charles dickens.
 
wanaodhani kuwa lazma tujazane mjini wanataka tuje vipi? Reli ya kati ilokuwa muhimiri wetu wa usafiri kwa nauli nzuri hatuioni tena ikikatiza vijijin mwetu, "wa mjini" mmekuwaje na ubinafsi! Hata sisi ni watanzania,mtuletee maendeleo.
 
Halafu nataka uniambie pamoja na upeo wako mkubwa , umefanya nini cha maana kujisaidia wewe na nchi yako.
nchi hii haisaidiki iwapo itaendelea kuwa mikononi mwa viongoz tulionao... hata hivyo nakumbushia, matukio "hovyo" ya mjini yasitufanye watanzania wenzenu tulio vijijini kusahaulika kimaendeleo,huo mchango wangu kwa jamii yangu
 
njoo mjini nina chumba kikubwa na sebule hakina mtu

ah mkuu umenifuraisha sana, kaka mjini kuna masaibu, jitulilie kijijini pazur pia pametulia na umewai kumwagiwa moshi na polisi wenye radha ya pilipili? Zaid je mnadai barabara na matibabu mnakusanya sh. Ngap km kodi?
 
Dar haina sifa yakuitwa jiji wale waliotembea watakubaliana nami,its just a big village as well
 
ukiona wamekuja huko vijijini ujue wamekuja kuwanyang'anya mashamba, nyumba, machimbo ya madini na rasilimali zingine so msiombee waelekeze mashambulio huko vijijini waache wababuane huko mijini
 
Dar haina sifa yakuitwa jiji wale waliotembea watakubaliana nami,its just a big village as well
kie kie kie kie ni kweli ndugu, wengi wao "wa mjini" wakiishi Dar wanaona wameyapatia maisha! vp wakifika J'burg? Tunis? San Fransisco? NY? etc watasemaje?Fareed na comrades ndani ya nyumba but still "wa mjini" mtatafuta vijimatukio vipya vitakavyo wasahaulisha ahadi hewa za daraja la Kigamboni, barabara za juu, mabasi ya mwendokasi... Miundombinu mibovu yawafanya kudamka usiku kama walozi kuwahi foleni... NI YAPI YA MSINGI KATIKA TAIFA HILI KIMAENDELEO
 
Back
Top Bottom