Sisi wa form 4 ndo hakuna kazi

Eddy Love

JF-Expert Member
Jul 25, 2011
13,652
8,542
Daah maisha yamekuwa magumu tupeane ishu za kufanya jameni tunaogopa kuwa wezi
 
Mimi nina degree naanza uza chips, we nakushauri uuze karanga au mayai ya kuchemsha,hahahaha

Wazo zuri na ushauri mzuri kwa vijana wetu umewapa wa kufikiria kuuza karanga, ifike mahali mawazo yetu yasiishie tu kwenye kazi za kuajiriwa bali yafikirie upande mwingine wa shilingi. Najua kuna ambao watakaosema mtaji ni shida lakini hata ukiwa na business idea ni mtaji tosha kabla ya kuanza kuangalia kupata pesa. (kuna wengine unakuta anakwambia natafuta kazi ukimwambia kazi gani anakwambia yoyote na mwingine atakuambia anatafuta mtaji wa kufanya biashara ukimwambia biashara gani atakuambia bado hajapata idea, sasa mtu kama huyu ukimpa mtaji hata business idea hana atasaidiwaje). Serikali yetu wengi wasanii lakini hata sie wananchi inabidi tujiandae kiaina kwani ipo siku watatokea watu makini watatukuta tayari tupo katika mchakato wa awali). Kwa alieko form 4 atatufute ajira (naposema ajira ni pamoja na ya kuajiriwa na kujiajiri pia) huku anaangalia uwezekano wa kusoma kidato cha sita kwa mwaka mmoja ili in future aweze kwenda elimu ya juu zaidi.
 
JoDOKI ur very right..inabid m2 kujitosa, unatafuta idea ya biashara then unakopa mtaji cz 2kiendelea kusubir mitaj mikubwa itakula kwe2 mana nchi ipo ktk chaos..NDO IVO WAJAMEN NIMESOTA CHUO 3 YEARS NAUZA CHIPS KARIBUN MBEZI BEACH, MAKONDE AREA FRM NEXT WEEK..bado nasaka ajira pia..alunta kontinua.
 
rudi kijijini kwenu, nenda kajifunze namna vijana wa huko ambao hata hiyo form four hawajaiona wanawezaje kumudu maisha yao....jifunze kutoka kwao na kisha anzia hapo.

shida yenu vijana ni kufikiri kwa muelekeo mmoja tu...soma mpaka utakapokuta ubao umeandikwa no class ahead na kisha uajiriwe.
 
Daah maisha yamekuwa magumu tupeane ishu za kufanya jameni tunaogopa kuwa wezi

mbona sekretarieti ya ajira walitoa hadi form 4 kufanya usafi maofisi kutuandalia chai,kuonyesha vyombo,hata jkt pia walitoa ungeomba then ungepata ajira huko coz ukishamaliza depo lao la jkt polisi,magereza na jwtz wanaenda kuchukua huko wenye form 4 wanapewa kipaumbele hawarudi mtaani ukiona mtu alikua jkt halafu karudi mtaani ujue huyo la 7 cku nyngine jaribu kabla umri haujakuacha nao ni muhimu wanaangalia.
 
Alafu asikudanganye mtu Kilahunja hata kama una degree kama ukiwa serious na kazi yako utatoka tu kikubwa kujiamini, mfano mtu anaweza kuwa mama/baba lishe kama amepata sehemu nzuri anaweza kuingiza ela sawa na mtu mwenye daladala na wakati huohuo baba/mama lishe hana pressure ya service maana masufuria service yake ni kuyaosha tu. alafu hakuna PAYE. hivyo unakuwa unapiga business unapata hela ya kununua magazeti mwisho wa siku unapata kazi na bado unakuwa na vyanzo viwili vya mapato
 
Last edited by a moderator:
ukiwa huna kazi kila tusi utalipata toka kwa wafanyakazi

Sio wafanyakazi ni watumishi kwa kuwa wanafanya kazi ambazo sio zao hivyo wanatumwa kutekeleza majukumu ya ofisi iliyomwajiri, in this case ni watumishi, wafanyakazi ni kama wamilki wa makampuni hayo, wakulima pia na wafanyabiashara
 
mbona sekretarieti ya ajira walitoa hadi form 4 kufanya usafi maofisi kutuandalia chai,kuonyesha vyombo,hata jkt pia walitoa ungeomba then ungepata ajira huko coz ukishamaliza depo lao la jkt polisi,magereza na jwtz wanaenda kuchukua huko wenye form 4 wanapewa kipaumbele hawarudi mtaani ukiona mtu alikua jkt halafu karudi mtaani ujue huyo la 7 cku nyngine jaribu kabla umri haujakuacha nao ni muhimu wanaangalia.

Ubwege huu ndio unawafanyaga mnajinyonga siku mkiambiwa kazi imefika tamati. Kuna ***** mmoja ambaye ni derava wa wizara ya kazi alikuwa anamtukana mfanyakazi wa kampuni fulani ya kufanya usafi maofisini kwa kumdharau na kumwita mwosha choo. Siku moja huyu bwana mwosha choo aliumwa tukaenda kumuona nyumbani kwake, balaa! Bonge la jumba kitunda. Kumbe huyu bwana anapomaliza kuosha choo huanza kuosha magari likiwamo la yule dereva *****. Kwa siku hujitengenezea karibu elfu 8 - 10 wakati huyu ***** anayejiona wa maana (kama ulivyo wewe) analipwa 186,000 (by then) na anaishi Mburahati kwenye nyumba ya kupanga
 
Alafu asikudanganye mtu Kilahunja hata kama una degree kama ukiwa serious na kazi yako utatoka tu kikubwa kujiamini, mfano mtu anaweza kuwa mama/baba lishe kama amepata sehemu nzuri anaweza kuingiza ela sawa na mtu mwenye daladala na wakati huohuo baba/mama lishe hana pressure ya service maana masufuria service yake ni kuyaosha tu. alafu hakuna PAYE. hivyo unakuwa unapiga business unapata hela ya kununua magazeti mwisho wa siku unapata kazi na bado unakuwa na vyanzo viwili vya mapato

dah, umeoona eeh, ndo napokupendea mimi hapo, great thinker..much respect!
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom