Sirudi nyuma

Sina fedha,sina Godfather wala hati ya nyumba/shamba ila nina kitu kimoja tu kinachonitia moyo,yaani ki-saikolojia ninaamini kuwa nitakuwa settler hata kama si wa kiwango cha kutisha.Kuna members humu wana michango ya maarifa please nipeni na mimi nitawarudishia feedback hapahapa jamvini.

Mtu mwema huacha urithi kwa wana wa wanawe.

Hii signature yako ndo imekutia hasira au? ulikuwa unataka uachiwe urithi??!!!
 
Hapana mkuu,naziona fursa nyingi mbele yangu,labda pengine ujasiri wa kuthubutu kufanya. Ukipita mitaani wimbo ni hali mbaya kila mahali,mimi nimeona nijaribu kuthubutu nione matokeo,ndio maana nikaomba mchango wa mawazo toka jamvini.
 
Nimerudi toka safari ya Moro vijijini, huko nimeona naweza kutimiza ndoto za kuja kuwa settler fulani hivi hasa ktk kilimo, kama uko nasi njoo tuunganishe miguvu tukafanye mambo huko.

E bana eee unagusa mulemule yaani na mimi nina kaugonjwa hako muda mlefu sana ila nimekuwa nikikwamishwa na vitendea kazi mkuu. kuivamia ardhi bila vitendea kazi inaweza kukukatisha tamaa na kuiona siyo dili, maana kuclear land tu ni mtulinga wa nguvu.sasa basi tusaidiane mawazo namna ya kuanza kwa kutumia mitaji yetu midogo na kushauriana ili kutiana moyo ,pengine tutatoka!

kwa upande wangu mimi ningependa kuanza walau na kishamba cha ekari 30, power tiller 1,farm house 1 na vimifugo vichache kama eneo linaruhusu.
mpango wa baadae ni kuchimba kisima kwa ajili ya kupata / kuvuna maji kwa ajili ya kilimo cha mbogamboga na matunda kama watermelon.tangos n.k wakati nikiendelea kusitawisha mazao ya kudumu na ya msimu.

Ingawa kwa sasa ni mfanyakazi na kipato si haba lakini akili yote ipo huko wakuu, nahisi maisha yangu yatakuwa ya furaha nikifanikisha hayo.

..............................

Amani yetu inatumiwa vibaya.
 
TUPO wengi ktk hii safari ya Malila.
imagine kijiji kina wakulima wenye upeo wa kutumia internet,research on market and prices via intaneti :)
Malila haya lete feedbak ya mradi wa kilimo,tayari nimeshatenga vijisenti vyangu for kilimo project,nimeskia kuwa Tracktors in Malawi bei iko poa around mil3- 4 hivi

Hiyo kitu niliyobold hapo juu hata mi nilisikia hivyo zamani kidogo ila sikuweza kufatilia kwa kukosa mtu anayejua undani wake, labda kama kuna mtu mwenye jamaa kule amwombe atupe data kamili.

................................

Amani yetu inatumiwa vibaya.
 
Hongera sana Malila... Mwaka 2005 nilichukua ardhi Eka 10 huko Mlandizi mimi na wenzangu watano kila mmoja na eka 10... Lakini tulikatishwa tamaa baada ya kugundua ardhi tuliyouziwa ilikuwa imeuzwa kwa watu zaidi ya wanane tena wengine vigogo... Tukapania kuwafikisha kwenye vyombo vya sheria wakatuonyesha nyingine... Mwaka jana tukaisafisha...wakati wamemaliza kusafisha tukakuta Mitiki Midogo midogo... Kumbe na lenyewe lilishachukuliwa... Tumepanga na wenzangu tuvipeleke Vigagula (Vizee) Polisi kwani kila wakati tunatumia pesa nyingi sana ukizingatia kusafisha shamba la eka 1 ni shilingi Elfu Hamsini... inasemekana vina nguvu za giza... Mfano unapanga kwenda kesho... Jioni hiyo hiyo mmoja wenu mwenye 4WD anapata Brakedown... Wiki Ijayo Mnasema Mtaenda Mpaka Mlandizi kisha muache Magari pale mchukue Pikipiki Inajitokeza dharura nyingine,Mara misiba,Ugomvi kati ya Patners...Mara unaenda kwa kustukiza unakuta Vizee vimetoka vipo Mlandizi ukirudi Mlandizi vinadai tumepishana...mara vipo Dar... Lakini hatujakata tamaa...
 
Tafsiri ya settler ni mpishano wa lugha tu, ila kadri mimi niilivyomuelewa nia yake ni nzuri tu, kuwa mkulima au mzalishaji mkubwa sana kama wale wazungu wa zimbabwe, nandi hills kule kenya, au hata metl hapa Tanzania.
Tatizo kubwa linalotukumba sisi watanzania si rasilimali, bali ni kutothubutu. Amini nawaambieni, kuna mashamba ya bure kabisa hapa Tanzania, unaenda kwa mwenyekiti wa kijiji, unaomba ukazi, unalipa elfu 30tu unapatiwa kiwanja nusu eka kijijini kisha unapelekwa shambani, shamba lenye virgin land na miti ya miwanga kibao, unajipimia mwenyewe na kudiklea umiliki wa ardhi-kinachofuata KAZI KWAKO. pesa za vibarua hazina mbele jamani, wastani wa mshahara wa juu wa mfanyakazi ni mil3, ukitoa matumizi ya mil1 unabakiwa na mil2*12 ni mil24 tu kwa mwaka!!!!! kalaghabaho!
 
E bana eee unagusa mulemule yaani na mimi nina kaugonjwa hako muda mlefu sana ila nimekuwa nikikwamishwa na vitendea kazi mkuu. kuivamia ardhi bila vitendea kazi inaweza kukukatisha tamaa na kuiona siyo dili, maana kuclear land tu ni mtulinga wa nguvu.sasa basi tusaidiane mawazo namna ya kuanza kwa kutumia mitaji yetu midogo na kushauriana ili kutiana moyo ,pengine tutatoka!

kwa upande wangu mimi ningependa kuanza walau na kishamba cha ekari 30, power tiller 1,farm house 1 na vimifugo vichache kama eneo linaruhusu.
mpango wa baadae ni kuchimba kisima kwa ajili ya kupata / kuvuna maji kwa ajili ya kilimo cha mbogamboga na matunda kama watermelon.tangos n.k wakati nikiendelea kusitawisha mazao ya kudumu na ya msimu.

Ingawa kwa sasa ni mfanyakazi na kipato si haba lakini akili yote ipo huko wakuu, nahisi maisha yangu yatakuwa ya furaha nikifanikisha hayo.

..............................

Amani yetu inatumiwa vibaya.

ndugu yangu haujaamua tu, kama kuna land ya kuclear basi ni pesa hiyo, hiyo miti unayokata we geuza pesa kisha rudisha shambani. kidogokidogo mkuu shamba linaanza, usianzie pakubwa utaumia na kukata tamaa
 
Kwa kugeuza maliasili nilizozikuta pale shambani( kijiji fulani) hasa miti,nilipata mtaji na nikapiga goli kiulaini sana,tena kwa hela kidogo tu. Mimi nilimpa wazo dada mmoja,yeye akanipa hela za kugeuzia ile miti mtaji. Nikasimama ktk uaminifu,kilichotoka hapo na kinachoendelea leo ni heshima kwa Mungu tu.
 
Hongera sana Malila... Mwaka 2005 nilichukua ardhi Eka 10 huko Mlandizi mimi na wenzangu watano kila mmoja na eka 10... Lakini tulikatishwa tamaa baada ya kugundua ardhi tuliyouziwa ilikuwa imeuzwa kwa watu zaidi ya wanane tena wengine vigogo... Tukapania kuwafikisha kwenye vyombo vya sheria wakatuonyesha nyingine... Mwaka jana tukaisafisha...wakati wamemaliza kusafisha tukakuta Mitiki Midogo midogo... Kumbe na lenyewe lilishachukuliwa... Tumepanga na wenzangu tuvipeleke Vigagula (Vizee) Polisi kwani kila wakati tunatumia pesa nyingi sana ukizingatia kusafisha shamba la eka 1 ni shilingi Elfu Hamsini... inasemekana vina nguvu za giza... Mfano unapanga kwenda kesho... Jioni hiyo hiyo mmoja wenu mwenye 4WD anapata Brakedown... Wiki Ijayo Mnasema Mtaenda Mpaka Mlandizi kisha muache Magari pale mchukue Pikipiki Inajitokeza dharura nyingine,Mara misiba,Ugomvi kati ya Patners...Mara unaenda kwa kustukiza unakuta Vizee vimetoka vipo Mlandizi ukirudi Mlandizi vinadai tumepishana...mara vipo Dar... Lakini hatujakata tamaa...

Maeneo ya Mlandizi, Ruvu,Vigwaza mpaka wami inabidi uwe makini sana,vigogo wengi wamenunua huko,vile vizee vimegeuza ndio njia rahisi ya kupatia pesa. Nimeshaambiwa mara nyingi tu kwenda huko,lakini machale yananicheza. Nilikwenda talawanda hadi magurumatari nikakuta mafisadi wamenunua mwanzo na mwisho haujulikani, kwa sasa nimeanzisha zone yangu mwenyewe najimegea kiulaini tu bila taabu. Watakaposhituka nimeshafika niendako.
 
Mie nakuombea mafanikio katika mipangilio yako

Dada asante,ila siko peke yangu,nina wadada kama sita hivi,kwa hiyo utuombee,na kutoka kwao mimi nimefanikiwa sana,kwa sehemu wadada ni wakweli na waaminifu ktk dili nyingi ninazopiga nao. Pia nalishukuru jamvi letu.
 
Kwa kugeuza maliasili nilizozikuta pale shambani( kijiji fulani) hasa miti,nilipata mtaji na nikapiga goli kiulaini sana,tena kwa hela kidogo tu. Mimi nilimpa wazo dada mmoja,yeye akanipa hela za kugeuzia ile miti mtaji. Nikasimama ktk uaminifu,kilichotoka hapo na kinachoendelea leo ni heshima kwa Mungu tu.

Hiyo miradi yenu angalieni tu sustainability kila mtu akifanya kama mnavyoelezea basi jueni kuwa in a short term taifa litaingia katika janga lingine la environmental degradation..kuweni wa ungwana kwa kufanya EIAs....Angalizo la pili tamaa ya kila mtanzania elite ku-occupy land bila kufikiria implication yake kwenye rural livelihoods ni hatari vile vile amani unayo iona ni kwasababu tu in rural areas land is not a problem (sehemu kubwa ya nchi) to access na ndiyo inayowapa families nyingi once a day meal changanya na matunda pori, wanyama mwitu so a peasant economy ambayo ina lubricate hali ngumu ya maisha. Juhudi zenu za ku occupy large pieces of land matokeo yake ni mabaya kuliko siasa ya CCM tunayoshinda tunailalamikia hapa jf....Ninachoona ni kwamba kumbe wengine wetu kwavile hatuna nafasi ya kuvuna ndiyo maana twa lalamika lakini as a matter of the fact we are the very same people ...selfishness as usual....
 
Ni kweli usemacho,ila idadi ya Watz wanaofanya kilimo cha maana ni ndogo sana,wengi ni paperwork na maneno tu. La pili ni hili, lipi jema kwako,ardhi tuwaachie majirani zetu wachukue kila bonde/mlima halafu wakajenge kwao au na sisi tufurukute pamoja nao?

Angalia mashamba yote makubwa kwa sasa yana milikiwa nani? Ukijua wamiliki wa mashamba hayo sisi itabidi utupe hongera kwa kuanza kuunganisha nguvu kwa pamoja.
 
Sasa ndugu mwizi akiiba na wewe kwavile umeibiwa unaamua kuiba? Cha msingi ni tupigane kufa na kupona kuinfluence change to the direction we want. That the land should remain accessible to all and for the benefit of majority siyo na sisi tuanze ku extend muscles zetu kuwa marginalise the majority unimformed rural communities whose time preference is very high and so would want immediate returns; to them it matters a bread of the day so are able to give all their possession to quench hunger of a day!!! Badala ya kuungana kuwa nyang'anya ardhi ndugu zetu basi tuungane kuilinda haki yao ambayo waliachiwa urithi na baba wa taifa lao.
 
Bado hujanipata, sisi/mimi nazungumzia small scale ya eka 30 mpaka 50,ambazo kwa mishahara yetu bado hata kuziendeleza ni kazi ngumu,kama umepitia post zote utaona wengi wanalalamikia ugumu wa kilimo. Sasa hawa wachache wanaojitahidi ni sehemu ndogo sana ktk mamilioni ya Watz wanaotaka kuingia ktk kilimo cha Kisasa. Ukisoma sera za kilimo kwanza utaona kabisa,lengo ni kuwa na wakulima wenye tija ili taifa liweze kujitosheleza kwa chakula na hatimaye ziada iuzwe.

Ukitoka Mkuranga mpaka Lindi ni pori tupu,ukitoka Mikumi mpaka Ilula ni pori tupu,ukipita na Reli ya Tzr kuna mapori kibao yenye mito. Hoja yako inakosa nguvu kwa sababu,kilimo chetu hakitoshelezi mahitaji yetu. Hakuna aliye nyimwa ardhi ya kilimo. Watz tunapenda vitu laini kama DECI hivi,juzi kiongozi kawapa wawekezaji shamba la umma pale Usangu Chimala,badala ya kulima mpunga wao wanalima mibono,mbona hiyo husemi,bado sisi/mimi nasisitiza tukiweza kulima,basi tulime kilimo chenye tija cha mashamba makubwa,tuache paper work.

Leo pale Dar tunakula mpunga toka Thailand/India nk lakini mabonde yetu yenye maji yapo yapo pale Moro na Rufiji,na kesho jamaa toka middle east wanakuja kumegewa hekta 5000 walime.
 
Malila,
umemjibu vizuri felister,inatosha,hajui hali halisi ya mkulima wa kitanzania,na pia inaonyesha kutokuwa na dhamira ya kilimo kwanza.
Je umefikia wapi na kilimo chako na ufugaji wa samaki?ningependa kukutembelea siku unaenda kuvuna ,ili nione your progress na itanitia moyo kuanza kulima,maybe be ur neighbour ktk kilimo kwanza.
mimi nazichanga ili niweze kununu Massery Tractor kwa ajili ya kukodisha na kulima,shamba bado sijapata nahisi kama hecta 100 zitatosha kwa kuanza na tractor moja,
 
Kwa sasa mimi nimebobea sana ktk uoteshaji wa misitu ya miti ya mbao,nimeanza kufuga wanyama (sio ng`ombe) kama pilot ya animal husbandry,na mwezi
may naanza kitalu cha sato, nimeangalia kwa umakini mkubwa kilimo cha nafaka,bado muda na hali ya hewa ya sasa haitabiriki kwa kutegemea mvua,ila naingia jumla ktk matunda( ndizi,tikiti na parachichi). Nimekwenda Moro,nimeona naweza kulima kwa uhakika mara nitakapokamilisha kupata shamba linaloweza kupanuka,vishamba nilivyopata ni vidogo na mimi nataka shamba kwa maana ya shamba hasa,yaani liweze ku-accomodate vitu vingi ndani yake.

Matarajio ni makubwa,yaani mwaka huu nitakuwa na shamba hilo huko Moro,next itakuwa ni trector,itabidi turafikiane mapema ili tractor lako liwe useful siku za mwanzo mkuu. Karibu tuchape kazi.
 
All the best Malila, nifikishie best wishes zangu pia kwa wenzako. songeni mbele MSIRUDI NYUMA
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom