Siri za Uchunguzi wa Tukio la Dkt. Ulimboka zaanza Kuvuja

Siri za uchunguzi wa awali wa tukio la kutekwa na kujeruhiwa kwa Dkt. Stephen Ulimboka zimeanza kuvunja, lakini kwa mshangao wa wanaojua kilichotokea, uchunguzi huo unatoa majibu yenye tata.

Habari za kutoka ndani ya vyombo vinavyochunguza tukio hilo, zinasema katika hatua ya awali zimeibuka na nadharia tatu juu ya kwa nini na nani aliyemteka Dkt. Ulimboka.......​

Daktari kwa vile hakufa basi yeye anao ukweli woote, kuanzia kuitwa na watekaji wake hadi yule bwana mwenye pochi lake Insp Msangi ambaye alihamishwa Morogoro na IGP kwa makosa ya kuwatesa watu na kuwauwa!!!

Purukushani hizi zote zitapata majibu live wakati ukifika!!!

 
Wananchi wanataka samaki lakini JK na ccm wanawapa nyoka.

Tunajua kwa kitambo sasa pumba na mchele ktk hili; ni hivi serikali hii hii ya JK ndio mtuhumiwa mkuu kwa vile ndio mwandaaji na mtekelezaji pekee wa mpango mzima wa njama za kumtesa/kumuua Dr. Ulimboka.

Hamwezi kutupotosha, toeni majibu ni kwanini mlifanya hayo? Mengine yote ni makapi na uzushi mnapojaribu kutafuta exit doors za suala hilo.
 
Njia ya muongo ni fupi, Ulimboka alishaongopa Mwenyewe, kusema aliyemteka katoka ikulu bila kumtaja jina nin dhahiri anahisi tu na hakuna ukweli wowote na hata akija leo hana la kusema.
Wacha wasi wasi enginia wa mpango mzima ni Bwana Jack Zoka, Bwana Msangi hao ni baadhi ya wahusika waletwe mahakamani ili wakanushe kuhusika wenyewe!!!!!

 
Chadema wenye wasiwasi wa kuuwawa na magamba leo wanashukiwa kuweza kuteka mtu na mavifaa ya kipolisi labda wangetuambia na hivyo vifaa walitoa wapi uupuuzi mtupu.

Dr balali walidai amekufa mtu wa watu maskini aliebahatika kumuona wakamuua na kutufanya tuamini aliuawa na majambazi hata huyu yangemfika mabaya tungeambiwa majambazi walitaka kumuibia simu ya blakiberi upuuzi mtupu hizo dhana zao ni ngumu kumeza wakaandae nyingine
 
Utajikunja kuandika hizi hadithi zako na wengine watakuja na theories zao lakini ukweli upo na utajulikana na ngoja Ulimboka mwenyewe apone na hata kama watamhujumu usisahau kuna Mungu na kwa uweza wake anaweza kuyafunua yote. Ushauri wangu kwako usiwaze sana wala usipoteze mda na jambo hili subiri mda wa kuujua ukweli ni waja.
Mkuu hata kama watamhujumu Dr ameisha record kanda na imeseviwa kwenye sehemu nyeti na inazidi kusambazwa ili ukweli ujulikane!!!!

 
Ina maana wale polisi kweli hapa ndiyo mwisho wako wa kufikiri!!!

Yaani na usomi wao woooote ndo theories walizoona zitawafanya wadanganyika wadanganyike eeh!!! Sasa naazna kukubali kuwa NIDA walipaswa kufanya uhakiki wa kina vyeti feki vitakuwa vingi sana!!
 
"Nature abhors vacuum"
hawakuongopa waliosema hivyo, katika mazingira tulionayo, kigugumizi cha kufanya maamuzi ata kwa mambo madogo, serikali isiyo na kauli moja, yaani kila mtu asema lake, huku kuna walionyanganya tonge kinywani na wengine kuisi kuonewa ama kutolewa kafara ktk ufisadi ama kuvua magamba katikati ya wanaotaka kutawala lije jua ije mvua, hapo theory ama lolote laweza tokea.

Yawezekana kabisa ikawa serikali haikuhusika moja kwa moja lakini kwa kuwa asili inachukia ombwe, ikajikuta yahusika
News Alert: Siri Za Uchunguzi Wa Tukio La Dkt. Ulimboka Zaanza Kuvuja
 
Kweli yale maeno ya Dr. Mwakyembe kwamba Polisi wetu wanafanya kazi kama waganga wa kienyeji yamekuwa VINDICATED.

hivi kuunda tume huru inahitaji mtu ushauriwe na rocket scientist?
.

Ndiyo!. Mimi naona ni zaidi ya Rocket Scientist wanahitajika kulazimisha sio kushauri! sababu tume huru ikiundwa itathibitisha haya uliyosema mwenyewe!

Theory MOJA ambayo hamtaki kuisema na mnajaribu kui cover up ni kwamba Dr. Ulimboka alitewkwa na kuteswa na USALAMA wa TAIFA. Hii ndiyo theory ita stand hayo matundu yote.
 
Kwa kuwa yeye mwenyewe anawajua waliomteka tumsubiri aje kutegua kitendawili hiki.
 
toka lini serikali ya ccm ikaionea chadema huruma?
kama kuna viashiria vya chadema kuhusika na inajulikana na imeshatangaza kuwa haina imani na polisi kwa nini serikali inakataa kuunda tumehuru ili chadema waaibike?
Hii huruma inaanzia wapi?
 
Kumbe kama Dr Ulimboka angekufa ndio tungeambiwa hizi ngonjera kwamba ni madaktari wenziwe, mara ndugu wa wagonjwa au CHADEMA?

Well, he lived to tell.

Na huyu mwanandishi aliyeandika hii habari anapataje usingizi?? Hawakutaka hata kusikiliza masimulizi ya Dr Ulimboka mwenyewe badala ya kuandika huu wakara?
 
Uongo wa Jackton Manyerere huo, anakaa chumbani, kusoma JF na kutunga uongo.na sasa yupo dodoma bungeni, kama amefanya uchunguzi kwa nini hata dr mmoja amtaje.

Uandishi wa kutumia makalio kama siyo masaburi ndio huu. Kama yeye kafanya investigative journalism ni rahis kufanya na kupata uhakika kama je Dr. Ulimboka alikuwa anapewa fedha na wanaharakati ilikuwa ni cash money au cheque?

Fanya lobbying na watu wa benki na kuona cash flow ya account ya Dr. Ulimboka ilikuwaje na utaweza kuona credits zilitoka wapi?.kwa taarifa hii kuanzia leo gazeti ili la jamhuri nitaliona tu kama lilivyo la uhuru.ni kama vile lina ajenda maalum kwa watu na maslahi binafsi.
 
Tuseme yote lakini pia tukumbuke matukio ya vifo vya akina CHACHA WANGWE, kifo cha mtu alisemwa kuwa mfuasi wa CDM wakati uchaguzi mdogo kule Igunga. Tamko la Ulimboka kuwa mmoja wa watekaji wake alikuwa amevaa magwanda.
Hakina matukio hayo yanaweza kubadili kabisa mtazamo wa watanzania walio wengi wa nani anahusika hasa na tukio hili la utekwaji Ulimboka. Kwanini tukio lolote ambalo CDM wanatuhumiwa, wanaharakati nao wanakuwa nyuma kwa karibu sana?

Nina uhakika wewe ni kinyago mkuu wa vinyago huko kwenu hii si akili ya mtu Wa kawaida
 
Waje na nyingine!
Ile ya kuwaua wafungwa au mahabusu wa ujambazi imeishia wapi?
 
Siri za uchunguzi wa awali wa tukio la kutekwa na kujeruhiwa kwa Dkt. Stephen Ulimboka zimeanza kuvunja, lakini kwa mshangao wa wanaojua kilichotokea, uchunguzi huo unatoa majibu yenye tata.

Habari za kutoka ndani ya vyombo vinavyochunguza tukio hilo, zinasema katika hatua ya awali zimeibuka na nadharia tatu juu ya kwa nini na nani aliyemteka Dkt. Ulimboka.

Nadharia hizo zinazozua utata wa hali ya juu, zinaonyesha na kutoa maelezo ya hatari, ambayo madaktari hawakubaliani nayo hata kidogo, ingawa wamekiri kuwa nao wameyasikia maelezo hayo waliyoyaita ya ‘kipuuzi'....​


Hiyo tume imeishashindwa kabla ya kuanza. Mungu si binadamu wala hadhihakiwi.
NGOs gani hutoa pesa mkononi kama sadaka?

Huo ni uongo uliokithiri. NGOs zote zina systems hivyo kama fedha inakwenda kwenye chama cha madaktari, haiwezi kwenda kwa dr. Ulimboka!

ndugu za waginjwa kumteka: Hilo haliwezekani kwa sababu ushahidi unaonesha kuwa mtu wa Ikulu ndiye waliyekuwa wanawasiliana tangu mgomo wa mwanzo.

Itaichukua serikali zaidi ya miaka 20 kujiosha katika uchafu huu ilioutenda kama njia ya kulazimisha madaktari warudi kazini kwa mabavu. CCM na serikali yake inataka kuigeuza Tanzania kuwa kama Sudani na somalia
 
Back
Top Bottom