Siri za Uchunguzi wa Tukio la Dkt. Ulimboka zaanza Kuvuja

Kama kweli serikali haihusiki, kwanini hadi sasa hivi takribani mwezi mmoja hajashikwa hata mtuhumiwa mmoja??
 
ninachoona gazeti la jamhuri huwa wanatumia maoni ya humu jf kuandika habari zao....
 
Siri za uchunguzi wa awali wa tukio la kutekwa na kujeruhiwa kwa Dkt. Stephen Ulimboka zimeanza kuvunja, lakini kwa mshangao wa wanaojua kilichotokea, uchunguzi huo unatoa majibu yenye tata.

Habari za kutoka ndani ya vyombo vinavyochunguza tukio hilo, zinasema katika hatua ya awali zimeibuka na nadharia tatu juu ya kwa nini na nani aliyemteka Dkt. Ulimboka.

Nadharia hizo zinazozua utata wa hali ya juu, zinaonyesha na kutoa maelezo ya hatari, ambayo madaktari hawakubaliani nayo hata kidogo, ingawa wamekiri kuwa nao wameyasikia maelezo hayo waliyoyaita ya ‘kipuuzi’.
1. Nadharia ya kwanza inaelezwa kuwa Dk. Ulimboka alipigwa na madaktari wenzake wanaoamini kuwa alikuwa ‘amepotea njia’ na kuanza kuwauza kwa Serikali na taasisi zinazotoa fedha kufanikisha mgomo huo, “Kuna viashiria kuwa alikuwa anachukua fedha kutoka kwenye baadhi ya mashirika yasiyo ya kiserikali (NGOs) na chama fulani, ambao lengo lao ni kutaka vurugu ziendelee kuwapo na nchi isitawalike. Lakini kilichotokea wanasema zile fedha alizokuwa anapewa alikuwa anawapiga panga njiani, hivyo wenzake wakaona wamshughulikie,” kilisema chanzo chetu kwa siri kubwa.
2. Nadharia nyingine ni ikle inayoelezwa kuwa wapo wagonjwa waliofiwa na ndugu yao mbele ya Dkt. Ulimboka hapo Muhimbili, na waliahidi kulipiza kisasi, hivyo hii nayo inafanyiwa uchunguzi na vyombo vya dola kubaini ukweli wake.
3. Nadharia ya tatu na ya mwisho ni ile iliyogusiwa hadi bungeni na wabunge wa CCM - akina Mwigulu Nchemba na Injinia Stella Manyanya - kuwa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kinahusika na utekaji wa Dk. Ulimboka kwa nia ya kuwafanya wananchi waichukie Serikali. CHADEMA kupitia Mkurugenzi wake wa Mawasiliano, John Mnyika, imekanusha mara moja na vikali kuhusika na unyama huu, na baada ya kubainika kuwa hoja hii ingeleta machafuko katika ukumbi wa Bunge, Spika wa Bunge Anne Makinda ameamua kuipiga marufuku isizungumzwe bungeni.

Dkt. Ulimboka, ambaye si mwajiriwa wa Serikali, anadaiwa kutekwa usiku wa kuamkia Juni 26, mwaka huu Dar es Salaam. Baada ya kupigwa na kujeruhiwa, inadaiwa kwamba alitelekezwa katika msitu wa Pande, wilayani Kinondoni jijini humo.
• Wakati utata wa tukio hilo ukiendelea kutanda, kumekuwa na taarifa nyingi, lakini zinazotajwa zaidi ni ile ya kwamba Dk. Ulimboka alifanyiwa kitendo hicho na marafiki zake wa karibu. Taarifa kutoka kwa baadhi ya vyombo vya usalama zimedokeza kuwa chanzo cha kadhia hiyo ni kujitokeza kwa mgongano wa maslahi kati yake na wenzake.
• Inaelezwa kwamba wenzake hawakufurahishwa na matumizi ya fedha na misaada mingine iliyokuwa ikitolewa na asasi zisizo za kiserikali, ambazo zimekuwa mstari wa mbele kuunga mkono mgomo wa madaktari nchini, “Jambo hili hatujalithibitisha moja kwa moja, lakini tumepata taarifa kuwa baadhi ya rafiki zake ndiyo walioshiriki kumteka kwa sababu za kimaslahi. Tunaendelea kuchunguza kujua ni maslahi gani ingawa kuna taarifa zinazodai kwamba wenzake walianza kumtilia shaka juu ya mwenendo wake na dhima aliyopewa ya kuwatetea madaktari. “Inasemekana walianza kumtilia shaka kwa ukwasi alioupata ndani ya kipindi kifupi, wenzake wakawa na imani kuwa huenda anajinufaisha na uenyekiti,” kimesema chanzo kingine.
• Kuna madai mengine kwamba tukio la kutekwa na kupigwa kwa Dkt. Ulimboka lilitokana na ndugu wa mgonjwa mmoja aliyefariki dunia kwa kukosa matibabu, bado nayo ni ya kutia shaka kubwa. Hata hivyo, daktari huyo hakuwa mwajiriwa wa serikali, ingawa inadaiwa kuwa kwa nyakati kadhaa alikuwa amepewa nafasi ya kuwahudumia wagonjwa katika Taasisi ya Mifupa (MOI). Mmoja wa wafanyakazi wa MOI aliyezungumza kwa masharti ya kutotajwa jina amesema; “Kuna ndugu walikasirika baada ya mgonjwa wao kufariki dunia. Hawakufurahishwa na majibu waliyopewa na mmoja wa madaktari (Ulimboka). Walionekana kuchukia. Siku chache baadaye ndipo ukatokea huo utekaji. Baadhi yetu tumelihusisha na kifo cha yule mgonjwa.”

Dkt. Ulimboka kwa sasa anatibiwa nje ya nchi. Taarifa za awali zilisema alipelekwa Afrika Kusini, ingawa kumekuwapo na taarifa nyingine kwamba anatibiwa katika moja ya nchi barani Ulaya.

Madaktari wenzake walikataa msaada wa Serikali wa kumpeleka nchini India kwa matibabu, jambo ambalo Msemaji wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Nsachris Mwamaja, amenukuliwa akisema limeisikitisha Wizara na Serikali kwa jumla.

Pamoja na kukataa ofa ya matibabu, madaktari hao walizuia viongozi wa Serikali kwenda kumjulia hali Dk. Ulimboka alipokuwa amelezwa MOI.
• Serikali ndiyo mtuhumkiwa mkuu katika sakata la kutekwa na hatimaye kujeruhiwa kwa Dkt. Ulimboka. Maelezo yake ya awali, ya kwamba alitekwa na watu wenye silaha, yamewafanya baadhi ya watu waamini kuwa alitekwa na polisi.
• Aidha, maelezo yake mengine ya kwamba alipotekwa aliwekwa katika gari lililoelekea Barabara ya Bagamoyo, na kwamba walipofika eneo la Victoria alifunikwa uso kwa kitambaa cheusi, yameibua hisia za kuihusisha Idara ya Usalama wa Taifa. Ofisi za Usalama wa Taifa zipo jirani na eneo la Victoria, ingawa mmoja wa viongozi wao alipowasiliana na JAMHURI mwishoni mwa wiki alikanusha vikali wao kuhusika, “Wasihamishie matatizo yao kwetu. Sisi hatupo kwenye siasa zao. Hiki ni chombo huru na wala hatutaki kazi zetu kuingiziwa siasa. Na wala hatutaki kutoa jibu lolote kwenye vyombo vya habari,” alisema Afisa wa Usalama wa Taifa kwa ukali.

Viongozi wengi wa Serikali akiwamo Waziri Mkuu Mizengo Pinda, wameshatoa taarifa za kukanusha madai hayo.

Rais Jakaya Kikwete, katika hotuba yake ya kila mwezi kwa wananchi, alikanusha madai hayo na kuahidi kuwa vyombo vya ulinzi na usalama vitafanya kila linalowezekana ili ukweli wa jambo hilo uweze kujulikana kwa uwazi.

Katika hotiba hiyo, Rais Kikwete alisema; “Napenda kuungana na Watanzania wenzangu wote kuelezea masikitiko yangu makubwa na kuhuzunishwa kwangu na kitendo cha kinyama alichofanyiwa Dkt. Stephen Ulimboka usiku wa Juni 26, 2012.

“Kitendo hicho ni kinyume kabisa na mila na desturi zetu. Watanzania hatujayazoea mambo hayo. Nimeelekeza vyombo vyetu vya ulinzi na usalama kufanya uchunguzi wa kina ili ukweli ujulikane. Nimesema kuwa ningependa ukweli huo ujulikane mapema ili tuondoe wingu baya la kutiliana shaka na kulaumiana kunakoendelea hivi sasa.

“Natambua kuwa Serikali nayo inatajwa katika orodha ya wanaotiliwa shaka. Mimi nimeshangazwa sana na hisia hizo kwani siioni sababu ya Serikali kufanya hivyo. Dkt. Ulimboka alikuwa mmoja wa viungo muhimu katika mazungumzo baina ya Serikali na madaktari. Ni kweli kwamba yeye si mtumishi wa Serikali, hivyo hakustahili kuwa sehemu ya majadiliano haya.

“Kulikuwa na rai ya kutaka asiwepo, lakini nilisema wamuache maadamu madaktari wanamwamini kuwa anaweza kuwasemea vizuri zaidi kuliko wao wenyewe walioajiriwa na Serikali.”

Madaktari wasisitiza Serikali haijinasui

Katibu wa Jumuiya ya Madaktari Tanzania, Dk. Edwin Chitage, aliiambia JAMHURI kuwa hata yeye ameyasikia maelezo hayo kwamba madaktari ndiyo waliomteka au wanatumiwa na vyama.

“Ukweli utabaki kuwa ukweli. Tunajua waliohusika wanajitahidi kweli kweli kujiondoa katika hili, ila itakuwa ngumu. Katika hili Serikali ina kazi ya ziada kujitoa. Tangu mwanzo tumeikataa Tume iliyoundwa na tunasema tunataka uchunguzi huru,” alisema Dk. Chitage.

Alisema wao wanahitaji uchunguzi huru unaopaswa kuwahusisha majaji na kada ya watu wanaoheshimika katika jamii, kitu anachosema kitasaidia kwa kiasi kikubwa kuimarisha imani ya wananchi katika taifa.

Dkt. Ulimboka alindwa na Interpol

Habari zilizolifikia Gazeti la JAMHURI muda mfupi kabla ya kwenda mitamboni, zilieleza kuwa Dkt. Ulimboka alikuwa akilindwa kwa karibu na polisi wa kimataifa (Interpol) kutokana na maombi yaliyofikishwa kwao na wanaharakati.

Hata hivyo, habari hizi hazikuweza kuthibitishwa mara moja, kwani waliotajwa kufanya kazi hiyo ambao ni Mkurugenzi wa Haki za Binadamu, Helen Kijo-Bisimba na Mkurugenzi wa Chama cha Wanahabari Wanawake Tanzania (TAMWA), Ananilea Nkya, hawakuweza kupatikana mara moja.
Chanzo: http://www.wavuti.com
Uongo, uzushi, utapeli wa serikali. Lakini hao waongo watambue kuwa mwisho ulishafika, kila taarifa wananchi tunazo. Hata vyombo vya habari vimekuwa viongo, waandishi wakila rushwa au kushinikizwa wapo tayari kudanganya umma.
 
Mwisho wa Ubaya aibu.....Story za kupika utazijua tu yaan tume wamejifungia sehemu cooking and Doctoring Ripoti?Shame on you. Hata mwandishi sentensi za kuunga unga ........BOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOO:A S 465:
 
Mwaka huu mtafukunyuka sana. Ila UKWELI utajulikana tu. Get well soon Dr Ulimboka, kwa kuwa wewe ndio Mwenye UKWELI tunaousubiri. Halafu UMMA utajua hatua gani za kuchukua.
 
Waandishi wa aina aliyeandaa hii habari ni wa kuogwa sana, hakuna uweledi uliotumika kutafuta zaidi ya hizo nadharia. Bahati mbaya sana, hata vyombo vya dola vinatuhumiwa kwa kiasi kikubwa 'huku mtaani' lakini JAMHURI wameamua kuja na hii 'nadharia' mara 'NGO zilizokuwa zinawapa fedha madokta, na chama cha siasa, halafu ndugu wa marehemu!

LHRC na SIKIKA hawajitokezi kwenye nadharia hizi kwa bahati mbaya na kwa mkusudi mwandishi anajifanya kufanya juhudi za kutowapata.
Rubbish!!!!!!!!!!!
 
These speculations are boring, should have at least very less weighted evidence supported by facts.
Inasikitisha mpaka leo watu wanakuja na nadharia bila proof, we need indications or any sort of clarification.
These theories should be substantiated otherwise ni upuuzi tu!
 
Ukweli tunaujua manake hii serikali inatumia mbinu chafu sana ili ijipendeze kwa watu lakini pasipo yenyewe kujua kuwa inajichimbia kaburi na Mr DHAIFU LAZIMA AJE APELEKWE THE HEAGUE.
 
michael scofied, angeweza kutengeneza series nzuri sana hapa! nways siku zote ukweli hujulikana na uongo kujitenga, ipo siku wahusika watajulikana.
 
Wizi wa nyama buchani upelelezi kumwachia fisi ni kutegemea kudanganywa...! Zumbe atogolwe.

Kwenye Tukio la wazi kabisa ambalo halihitaji msaada wa nje juu ya kuzisajili Meli za Iran wameshindwa na kuomba msaada wa Wamerekani, leo hii issue inayohitaji uchunguzi wa kitaalam, wanalazimisha wafanye wao uchunguzi. Jiulize, kuna nini hapo!
 
Nilicho gundua kwenye uzi huu mtoa maada ni muhusika wa upotoshaji, harafu ndio wale TISS wa drs la saba au div 0 form4
 
Mwache MUNGU aitwe MUNGU. Unajua Wana JF watapinda na kukata lakini ukweli will remains the truth. It is God's Grace that save Dr. Ulimboka and the purpose of God is to reveal all the dirty filty game that this Serikali does to INNOCENT TANZANIANS. The will be stripped naked this time. Neno la MIZENGO PINDA holds something Strange. He would deny the truth but the reason of saying that in PUBLIC tena BUNGENI sio masiara ETI. Na JK kutoa speach ya ongo to cover up he knows and it was planned. KAZI KWAO JK, PINDA NA SERIKALI YAKE LAZIMA IJULIKANE ATUKUPALI KAMWE
 
WATAEMEZA TUU hata kama inawakaba. WASHENJI SANA KAWA USALAMA WA TAIFA. Time will tell
 
Njia ya muongo ni fupi, Ulimboka alishaongopa Mwenyewe, kusema aliyemteka katoka ikulu bila kumtaja jina nin dhahiri anahisi tu na hakuna ukweli wowote na hata akija leo hana la kusema.

Hapo kwenye red naona umeamua kuwa mtabiri, mbona unamsemea mtu mawazo yako binafsi kiasi hichi??
 
Serikali ikiweza kusema alipo Dr. Bilali basi itaweza kusema na wapi watekaji wa Dr. Ulimboka!!!!!

Mengine ni sanaa tu ya kutaka kujinasua na tope na kutafuta nafuu ya kuonewa huruma na wananchi baada ya kushindwa kupata suluhu ya kudumu ya mgogoro huo.

mkuu hapo kwenye nyekundu unamaanisha huyuhuyu makamu wa raisi!?
sijakuelewa kwani haijulikani alipo??
 
Siri za uchunguzi wa awali wa tukio la kutekwa na kujeruhiwa kwa Dkt. Stephen Ulimboka zimeanza kuvunja, lakini kwa mshangao wa wanaojua kilichotokea, uchunguzi huo unatoa majibu yenye tata.

Habari za kutoka ndani ya vyombo vinavyochunguza tukio hilo, zinasema katika hatua ya awali zimeibuka na nadharia tatu juu ya kwa nini na nani aliyemteka Dkt. Ulimboka.

Nadharia hizo zinazozua utata wa hali ya juu, zinaonyesha na kutoa maelezo ya hatari, ambayo madaktari hawakubaliani nayo hata kidogo, ingawa wamekiri kuwa nao wameyasikia maelezo hayo waliyoyaita ya ‘kipuuzi’.
1. Nadharia ya kwanza inaelezwa kuwa Dk. Ulimboka alipigwa na madaktari wenzake wanaoamini kuwa alikuwa ‘amepotea njia’ na kuanza kuwauza kwa Serikali na taasisi zinazotoa fedha kufanikisha mgomo huo, “Kuna viashiria kuwa alikuwa anachukua fedha kutoka kwenye baadhi ya mashirika yasiyo ya kiserikali (NGOs) na chama fulani, ambao lengo lao ni kutaka vurugu ziendelee kuwapo na nchi isitawalike. Lakini kilichotokea wanasema zile fedha alizokuwa anapewa alikuwa anawapiga panga njiani, hivyo wenzake wakaona wamshughulikie,” kilisema chanzo chetu kwa siri kubwa.
2. Nadharia nyingine ni ikle inayoelezwa kuwa wapo wagonjwa waliofiwa na ndugu yao mbele ya Dkt. Ulimboka hapo Muhimbili, na waliahidi kulipiza kisasi, hivyo hii nayo inafanyiwa uchunguzi na vyombo vya dola kubaini ukweli wake.
3. Nadharia ya tatu na ya mwisho ni ile iliyogusiwa hadi bungeni na wabunge wa CCM - akina Mwigulu Nchemba na Injinia Stella Manyanya - kuwa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kinahusika na utekaji wa Dk. Ulimboka kwa nia ya kuwafanya wananchi waichukie Serikali. CHADEMA kupitia Mkurugenzi wake wa Mawasiliano, John Mnyika, imekanusha mara moja na vikali kuhusika na unyama huu, na baada ya kubainika kuwa hoja hii ingeleta machafuko katika ukumbi wa Bunge, Spika wa Bunge Anne Makinda ameamua kuipiga marufuku isizungumzwe bungeni.

Dkt. Ulimboka, ambaye si mwajiriwa wa Serikali, anadaiwa kutekwa usiku wa kuamkia Juni 26, mwaka huu Dar es Salaam. Baada ya kupigwa na kujeruhiwa, inadaiwa kwamba alitelekezwa katika msitu wa Pande, wilayani Kinondoni jijini humo.
• Wakati utata wa tukio hilo ukiendelea kutanda, kumekuwa na taarifa nyingi, lakini zinazotajwa zaidi ni ile ya kwamba Dk. Ulimboka alifanyiwa kitendo hicho na marafiki zake wa karibu. Taarifa kutoka kwa baadhi ya vyombo vya usalama zimedokeza kuwa chanzo cha kadhia hiyo ni kujitokeza kwa mgongano wa maslahi kati yake na wenzake.
• Inaelezwa kwamba wenzake hawakufurahishwa na matumizi ya fedha na misaada mingine iliyokuwa ikitolewa na asasi zisizo za kiserikali, ambazo zimekuwa mstari wa mbele kuunga mkono mgomo wa madaktari nchini, “Jambo hili hatujalithibitisha moja kwa moja, lakini tumepata taarifa kuwa baadhi ya rafiki zake ndiyo walioshiriki kumteka kwa sababu za kimaslahi. Tunaendelea kuchunguza kujua ni maslahi gani ingawa kuna taarifa zinazodai kwamba wenzake walianza kumtilia shaka juu ya mwenendo wake na dhima aliyopewa ya kuwatetea madaktari. “Inasemekana walianza kumtilia shaka kwa ukwasi alioupata ndani ya kipindi kifupi, wenzake wakawa na imani kuwa huenda anajinufaisha na uenyekiti,” kimesema chanzo kingine.
• Kuna madai mengine kwamba tukio la kutekwa na kupigwa kwa Dkt. Ulimboka lilitokana na ndugu wa mgonjwa mmoja aliyefariki dunia kwa kukosa matibabu, bado nayo ni ya kutia shaka kubwa. Hata hivyo, daktari huyo hakuwa mwajiriwa wa serikali, ingawa inadaiwa kuwa kwa nyakati kadhaa alikuwa amepewa nafasi ya kuwahudumia wagonjwa katika Taasisi ya Mifupa (MOI). Mmoja wa wafanyakazi wa MOI aliyezungumza kwa masharti ya kutotajwa jina amesema; “Kuna ndugu walikasirika baada ya mgonjwa wao kufariki dunia. Hawakufurahishwa na majibu waliyopewa na mmoja wa madaktari (Ulimboka). Walionekana kuchukia. Siku chache baadaye ndipo ukatokea huo utekaji. Baadhi yetu tumelihusisha na kifo cha yule mgonjwa.”

Dkt. Ulimboka kwa sasa anatibiwa nje ya nchi. Taarifa za awali zilisema alipelekwa Afrika Kusini, ingawa kumekuwapo na taarifa nyingine kwamba anatibiwa katika moja ya nchi barani Ulaya.

Madaktari wenzake walikataa msaada wa Serikali wa kumpeleka nchini India kwa matibabu, jambo ambalo Msemaji wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Nsachris Mwamaja, amenukuliwa akisema limeisikitisha Wizara na Serikali kwa jumla.

Pamoja na kukataa ofa ya matibabu, madaktari hao walizuia viongozi wa Serikali kwenda kumjulia hali Dk. Ulimboka alipokuwa amelezwa MOI.
• Serikali ndiyo mtuhumkiwa mkuu katika sakata la kutekwa na hatimaye kujeruhiwa kwa Dkt. Ulimboka. Maelezo yake ya awali, ya kwamba alitekwa na watu wenye silaha, yamewafanya baadhi ya watu waamini kuwa alitekwa na polisi.
• Aidha, maelezo yake mengine ya kwamba alipotekwa aliwekwa katika gari lililoelekea Barabara ya Bagamoyo, na kwamba walipofika eneo la Victoria alifunikwa uso kwa kitambaa cheusi, yameibua hisia za kuihusisha Idara ya Usalama wa Taifa. Ofisi za Usalama wa Taifa zipo jirani na eneo la Victoria, ingawa mmoja wa viongozi wao alipowasiliana na JAMHURI mwishoni mwa wiki alikanusha vikali wao kuhusika, “Wasihamishie matatizo yao kwetu. Sisi hatupo kwenye siasa zao. Hiki ni chombo huru na wala hatutaki kazi zetu kuingiziwa siasa. Na wala hatutaki kutoa jibu lolote kwenye vyombo vya habari,” alisema Afisa wa Usalama wa Taifa kwa ukali.

Viongozi wengi wa Serikali akiwamo Waziri Mkuu Mizengo Pinda, wameshatoa taarifa za kukanusha madai hayo.

Rais Jakaya Kikwete, katika hotuba yake ya kila mwezi kwa wananchi, alikanusha madai hayo na kuahidi kuwa vyombo vya ulinzi na usalama vitafanya kila linalowezekana ili ukweli wa jambo hilo uweze kujulikana kwa uwazi.

Katika hotiba hiyo, Rais Kikwete alisema; “Napenda kuungana na Watanzania wenzangu wote kuelezea masikitiko yangu makubwa na kuhuzunishwa kwangu na kitendo cha kinyama alichofanyiwa Dkt. Stephen Ulimboka usiku wa Juni 26, 2012.

“Kitendo hicho ni kinyume kabisa na mila na desturi zetu. Watanzania hatujayazoea mambo hayo. Nimeelekeza vyombo vyetu vya ulinzi na usalama kufanya uchunguzi wa kina ili ukweli ujulikane. Nimesema kuwa ningependa ukweli huo ujulikane mapema ili tuondoe wingu baya la kutiliana shaka na kulaumiana kunakoendelea hivi sasa.

“Natambua kuwa Serikali nayo inatajwa katika orodha ya wanaotiliwa shaka. Mimi nimeshangazwa sana na hisia hizo kwani siioni sababu ya Serikali kufanya hivyo. Dkt. Ulimboka alikuwa mmoja wa viungo muhimu katika mazungumzo baina ya Serikali na madaktari. Ni kweli kwamba yeye si mtumishi wa Serikali, hivyo hakustahili kuwa sehemu ya majadiliano haya.

“Kulikuwa na rai ya kutaka asiwepo, lakini nilisema wamuache maadamu madaktari wanamwamini kuwa anaweza kuwasemea vizuri zaidi kuliko wao wenyewe walioajiriwa na Serikali.”

Madaktari wasisitiza Serikali haijinasui

Katibu wa Jumuiya ya Madaktari Tanzania, Dk. Edwin Chitage, aliiambia JAMHURI kuwa hata yeye ameyasikia maelezo hayo kwamba madaktari ndiyo waliomteka au wanatumiwa na vyama.

“Ukweli utabaki kuwa ukweli. Tunajua waliohusika wanajitahidi kweli kweli kujiondoa katika hili, ila itakuwa ngumu. Katika hili Serikali ina kazi ya ziada kujitoa. Tangu mwanzo tumeikataa Tume iliyoundwa na tunasema tunataka uchunguzi huru,” alisema Dk. Chitage.

Alisema wao wanahitaji uchunguzi huru unaopaswa kuwahusisha majaji na kada ya watu wanaoheshimika katika jamii, kitu anachosema kitasaidia kwa kiasi kikubwa kuimarisha imani ya wananchi katika taifa.

Dkt. Ulimboka alindwa na Interpol

Habari zilizolifikia Gazeti la JAMHURI muda mfupi kabla ya kwenda mitamboni, zilieleza kuwa Dkt. Ulimboka alikuwa akilindwa kwa karibu na polisi wa kimataifa (Interpol) kutokana na maombi yaliyofikishwa kwao na wanaharakati.

Hata hivyo, habari hizi hazikuweza kuthibitishwa mara moja, kwani waliotajwa kufanya kazi hiyo ambao ni Mkurugenzi wa Haki za Binadamu, Helen Kijo-Bisimba na Mkurugenzi wa Chama cha Wanahabari Wanawake Tanzania (TAMWA), Ananilea Nkya, hawakuweza kupatikana mara moja.
Chanzo: http://www.wavuti.com
[/QUOT

Tunatatizo katika fikra zetu ndiyo maana tumejikita katika kudhani na hisia kujibu kadhia hii,Uoga wa kifkra utaangamiza Taifa hili
 
Kwani hamjui Usalama wa Taifa ni Wauaji. Ni kikosi maalum cha kuua watu kwa maelekeezo ya Viongozi kulinda viongozi wabovu. They ARE KILLERS . msituletee theories zenu za kipuuzi
 
Back
Top Bottom