Elections 2010 Siri za CCM, CUF zavuja.

Indume Yene

Platinum Member
Mar 17, 2008
2,948
710
Jamani hii stori nimeikuta kwenye gazeti la Mwanahalisi. Hii habari ni ya kweli kutokana na interviews za wahusika. Kweli hii ni fedheha, sasa ndo nimeona ni kwa nini CHADEMA hawakutaka muungano wa vyama katika chaguzi. Habari ndiyo hiyo hapo chini. Na Fisadi RA kishawaingilia CUF......Toba.


cuf_211.jpg



MAKUBALIANO kati ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Chama cha Wananchi (CUF) kuhusiana na mwendo kuelekea uchaguzi mkuu yamevuja, MwanaHALISI linaweza kuripoti.
Taarifa zilizofikia gazeti hili zinasema kumekuwa na maelewano juu ya tabia na mwenendo wa viongozi wa vyama hivyo viwili ili kuzuia kuumbuana hadharani.
Lakini gazeti limeelezwa kuwa kinachoitwa makubaliano hakikuandaliwa na ngazi ya juu ya uongozi, kiasi kwamba mgombea urais wa CUF, Profesa Ibrahim Lipumba anadaiwa "kuharibu dili."
Wakati imeelezwa kuwa CCM na CUF walikubaliana kutoshambuliana hadharani, na hasa kutoshambulia wagombea urais binafsi, Prof. Lipumba tayari amemkwaruza Jakaya Mrisho Kikwete.
Kwenye mkutano wa kampeni wilayani Mbalizi, mkoa wa Mbeya, tarehe 19 mwezi uliopita, Profesa Lipumba alinukuliwa akisema, Kikwete hafai kuwa kiongozi kwa kuwa ameshindwa kuendesha nchi.
Taarifa hizo zilizochapishwa katika gazeti la Tanzania Daima chini ya Kichwa "Lipumba, Slaa wamshambulia Kikwete," zilimkariri Lipumba akisema, "…matumizi makubwa ya familia yake (Kikwete), yamesababisha ashindwe kuendesha nchi."
"Tangu ameingia madarakani, amekuwa na matumizi mabaya, hasa ya familia yake kufanya ziara ambazo si za lazima, akiwamo mke wake Mama Salma na mwanawe Ridhiwani wanaozunguka nchi mzima kumpigia kampeni," ananukuliwa Lipumba akisema.
Aliwataka wananchi kutomchagua tena katika nafasi hiyo.
Kuvuja kwa siri hii kumetokana na mawasiliano kati ya Msaidizi wa Rais, January Makamba na Mkurugenzi wa mambo ya Nje wa CUF, Ismail Jussa Ladhu.
Katika mawasiliano yao kati ya Januari na Oktoba mwaka huu, Makamba analalamikia CUF kuvunja makubaliano kutokana na Lipumba kumshambulia Kikwete.
Makamba anamwandikia imeili Jussa kwa kusema, "Utakumbuka yale makubaliano yetu; imekuwaje muafaka wa kutoenda personal?" (kushambulia mtu binafsi). Imeili hiyo iliandikwa saa nane na nusu usiku wa 22 Septemba 2010.
Akiandika kwa msisitizo, Makamba ananukuu taarifa ya gazeti na kumpelekea Jussa.
Naye Jussa akijibu Makamba aliandika, "January, maelewano yetu yako palepale. Kosa lilikuwa langu kumsubiri (Lipumba) hadi tuonane uso kwa uso ili nimpe briefing – taarifa. Bahati leo amekuja Zanzibar na tumeelewana. Nitakupigia tuzungumze zaidi. Jussa"
Maelezo haya ya Jussa ni ya tarehe 22 Septemba 2010 saa 11:05 alfajiri. Gazeti hili limethibitisha kuwa Profesa Lipumba alikuwa Zanzibar siku inayotajwa na Jussa.
MwanaHALISI lilipomuuliza Jussa kwa simu, juu ya mawasiliano hayo ambayo yanaweza kutibua chama chake, haraka aling'aka na kusema, "Naomba nikuulize, wewe imeili yangu umeipataje?"
Akiongea kwa sauti ya kufoka, Jussa aliuliza, "Umewezaje kufungua imeili yangu? Hiyo haiwezi kuwa imeili yangu. Umepata wapi kifungulio?"
Alipoambiwa kwamba gazeti lina uhakika kuwa mawasiliano liliyonayo ni yake, Jussa alisema, "Najua nyie waandishi wa Tanzania mmezoea kutunga taarifa. Huo ni utungaji na hauwezi kuisaidia nchi hii."
Kwa upande wake, Makamba alikiri kumuandikia Jussa ujumbe huo, lakini akasema aliandika "kama rafiki tu."
"Kama ujuavyo, mimi sina wadhifa wowote ndani ya CCM. Kwa hiyo, kwa namna yoyote ile, siwezi kuwa msemaji wa chama katika mambo kama hayo.
"Kilichopo ni kuwa Jussa ni rafiki yangu. Kwenye mazungumzo yetu mara nyingi nimekuwa nikimwambia kuhusu umuhimu wa kuzingatia siasa zenye kuleta maendeleo na si zile za mambo binafsi," anaeleza.
Lakini kauli ya Makamba inaonyesha ama amesahau, anaficha ukweli au anasema uwongo, kwani mawasiliano ya awali tayari yanaonyesha Jussa akikiri kuchelewa "kumwambia" Lipumba juu ya mpango wao huo.
Ni Jussa anayesema, "Kosa lilikuwa langu kumsubiri (Lipumba) hadi tuonane uso kwa uso ili nimpe briefing…"
Bali Makamba anaendelea kudai kuwa, "Yale ni mawasiliano kati ya marafiki na si vinginevyo."
Prof. Lipumba hakuweza kupatikana kutolea maelezo sakata hilo. Alipoitwa kwa simu, alijibu mara moja kuwa yuko njiani akienda Sumve, mkoani Mwanza. Simu ilikatika na hakuweza kupatikana tena.
Naye Hamad Rashid Mohammed, mwanzilishi wa CUF na kiongozi mwandamizi, amesema hajui lolote kuhusu kile kinachoitwa makubaliano kati ya chama chake na CCM.
"Kama Lipumba alizungumza kuhusu matumizi ya familia ya rais, hilo haliwezi kuwa jambo la kibinafsi. Hilo linahusu matumizi ya fedha za walipa kodi na hata kama hayo makubaliano yangekuwapo, kwenye hili yasingeingia," amesema Hamad Rashid.
Alimwambia mwandiki kuwa kama "…umeona barua ya mwenzetu (Jussa) ikizungumzia mambo hayo, naomba umuulize yeye, maana ndiye mhusika."
Kumekuwa na uvumi kuwa makubaliano kati ya vyama hivi viwili yametokana na msaada wa fedha ambazo Rostam Aziz, mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM aliipa CUF kuendeshea shughuli zake.
Hata hivyo, Hamad alipoulizwa juu ya hilo alisema fedha zote wanazotumia ni kutoka kwenye mfuko wao wa ruzuku na michango ya wanachama.
Amesema, "Mara ya mwisho nilionana na Rostam wakati tukiwa wabunge bado na sijaonana naye tangu bunge lilipovunjwa."
Taarifa za kuaminika zinasema Rostam Makamba na Jussa ni "pete na kidole."
Aidha, kupatikana kwa taarifa juu ya "mpango wa kutoshambuliana" kati ya CCN na CUF, kumeelezwa na wachunguzi wa mambo kuwa usaliti uliofanywa na mmoja wao kwa makusudi.
Chanzo kingine cha habari hii kinasema, siyo tu taarifa juu ya makubaliano ambazo "ziko njenje," bali kila taarifa inayotolewa na CUF inatinga ofisini na nyumbani kwa baadhi ya viongozi wa CCM.
Kwa mfano, barua ya Naibu Katibu Mkuu CUF (Bara), Joran Bashange ya tarehe 15 Oktoba, Ijumaa iliyopita, inadaiwa kukutwa pamoja na nyaraka zinazoonyesha mawasiliano ya Makamba na Jussa.
Katika barua hiyo, Kumb. Na. CUF/AK/DSM/NKM/B/002/A2/2010/83
Bashange anaandika, "Chama chetu kina matarajio ya kuibuka na ushindi mkubwa katika uchaguzi mkuu huu."
Bashange amelaumu "…taasisi mbalimbali za kitafiti ambazo hutoa matokeo (kura za maoni) yaliyopikwa kwa minajili ya kuwakatisha tamaa wananchi."
Jingine ambalo analalamikia katika barua ambayo tayari imevuja hadi ikulu, ni "mkakati wa kuzuia wagombea wa CUF kufanya kampeni kikamilifu kwa kuingilia ratiba zao za kampeni."
Alipoulizwa mgombea wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dk. Willibrod Slaa kwamba naye ana mpango kama vyama hivi viwili alisema, "Hatuna mpago huo. Hatufikirii kuwa nao."
 
Back
Top Bottom