SIRI YAFICHUKA: Deni la 2 billion/- latua Ikulu!

Tatizo ni kuwa nchi hii imajaa viongozi wasiotumia akili hata siku moja.

Tatizo sio viongozi tu. Ni mijitu yenyewe maana hata hao viongozi wanatoka miongoni mwetu.

Ni ukweli unaouma kuwa Miafrika Ndivyo Tulivyo na mpaka sasa hakuna mtu aliyenithibitishia vinginevyo.

Kazi kunyoosheana vidole tu...oooh ni viongozi...oooh wasomi vile...oooh wananchi vile...SMH
 
Yaani haka kama wewe ndiwe ungalikuwa kiongozi wa TFF ungefanya upuuzi huo huo?
 
nakumbuka kuwa kuna wakati fulani alikuja Beyonce na mme wake pale Mwananyamala, ahalafu akaja msanii mwingine sikumbuki jina lake. Kilichoonekana kwenye TV ni upuuzi mtupu pamoja na watu wengine kupiga picha za MIKONOOZ badala ya kutumia nafasi ile kutangaza mambo ya muhimu kuhusu nchi.

Siku nyingine alikuwa Wil Smith, akaishia kuonyeshwa akiwa na Karume badala ya kutumia mwanya ule pia kutangaza mambo ya maana. ujinga kabisa umetujaa waswahili.
 
Yaani haka kama wewe ndiwe ungalikuwa kiongozi wa TFF ungefanya upuuzi huo huo?

Kuna lawama za kutosha kuwapatia wengi na si kiongozi wa TFF peke yake.

Mimi ningekuwa kiongozi wa aina yoyote ile mambo mengi sana yangekuwa tofauti. Mtu kama wewe kwa mfano ungekuwa jela....lol
 
Mimi sikubaliani hata kidogo kwamba ni kosa kuileta Brazil kucheza Tanzania. Suala la msingi ni kama pesa ilikuwapo ya kuwalipa basi lakini isitumike kodi ya mlala hoi kuwalipia deni TFF kwa hesabu zao mbovu.
 
Asalaam Aleykum,

Taarifa nilizonazo ni kuwa TFF walienda benki ya NMB kuomba mkopo kwa njia ya overdraft ili waweze kuwalipa Brazil appearance fees za kuja Tanzania. Sina uhakika na exact figure ya mkopo ila taarifa ni kuwa it was $2.5 million (kama shilingi bilioni 3 hivi). NMB wakijua fika kama sponsors wa TFF kuwa shirikisho hilo halina uwezo wa kulipa mkopo huo, walikataa kutoa fedha hizo. Waziri wa Michezo, George Mkuchika, akaiandikia barua NMB kuunga mkono ombi la mkopo huo. Baada ya ku-assess risk za mkopo huo kwa TFF ambao NMB inawajua fika kuwa hawana pesa na kila siku wanatembeza bakuli la kuomba msaada, walimgomea Waziri Mkuchika na kusema hawamtambui. Uongozi wa NMB ukasimama kidete na kusisitiza kuwa kamwe hautatoa mkopo kwa TFF kuwalipa Brazil waje Tanzania mpaka Rais Kikwete au Waziri Mkuu Pinda aandike barua ya serikali kutoa guarantee kwa mkopo huo. Hapo ndipo baada ya kupata baraka zote za Ikulu, Waziri wa Fedha, Mustafa Mkulo, akaiandikia barua NMB kuwa serikali inaweka commitment ya kubeba deni lote iwapo TFF watashindwa kulipa deni hilo. Baada ya kupata guarantee hiyo kutoka kwa Waziri wa Fedha, NMB wakakubali kutoa overdraft kwa TFF.

Business plan ya TFF ilikuwa kwamba kwa wastani wa bei ya ticket ya 50,000/- x watu 60,000 = shilingi bilioni 3. Matokeo yake ni kuwa tiketi za VIP tu ndiyo zilikuwa sold out huku zile za walala hoi ambao ndiyo walitarajiwa kujaa uwanjani zikabaki wazi. Sijasikia TFF ikitangaza mapato, lakini sidhani kama itafika hata shilingi bilioni 1. Hii ina maana kuwa serikali italazimika kubeba deni la zaidi ya shilingi bilioni 2 kutokana na guarantee iliyoiwekea TFF.

It seemed like a good idea at that time. Ujio wa Brazil unge raise profile ya soka la Tanzania, ungeutangaza Uwanja wa Taifa duniani, ungevutia watalii na wawekezaji Tanzania na ungemjengea sifa JK kwa umma wa Watanzania kama "Mpenzi mahiri wa michezo" kama mabango makubwa yenye picha ya Rais akibusu Kombe la Dunia yalivyopambwa uwanjani siku ya mechi. Ninaambiwa kuwa Rais Kikwete alifurahia sana mpango wa kuileta Brazil nchini na kuamuru serikali itoe kila ushirikiano kwa TFF kufanikisha jambo hili.
Matokeo yake ni kuwa kulikuwa na maelfu ya viti vitupu uwanjani baada ya wananchi kushindwa kulipa kiingilio.

Hii ni ishara tosha ya kuwa serikali hii iliyo ahidi kuleta Maisha Bora kwa kila Mtanzania kumbe wala haijui umasikini halisi wa wananchi wake yenyewe! Hicho kiingilio cha chini cha elfu 30 ni mapato ya mwezi mzima ya Watanzania walio wengi ingawa its just pocket change kwa viongozi wetu.

HII NDIYO NCHI YETU NA HAWA NDIYO VIONGOZI WAKE.

Mkuu uko biased mno...... na maelezo yako hayana tija kwa sababu unailaumu Ikulu direct as if wewe ulihusishwa ktk makubaliano. Pamoja na mabaya mengi ya serikali ya CCM ktk awamu ya nne lakini kuileta Brazil Ikacheza hapa nchini ni vyema tu. Hata kama deni lipo serikali imedhamini tu TFF na watalipa with time.
 
Watanzania wangapi walienda uwanjani? Watanzania wangapi walifaidika na mechi hiyo? Halafu wote tutachangia kulipa deni hilo + interest!

Amandla.......
 
Unambiwa tangu enzi za huyo Mansa Musa Mfalme wa Mali, waafrika tunajulikana kwa kujitutumua kutoa mapesa wakati tu masikini.

Unaambiwa huyo Mansa Musa alivyokuwa anaenda kuhiji hapo Mecca, alipitia Cairo, basi alimwaga midhahabu hapo ndani ya Cairo mwaka 1324 mpaka thamani ya dhahabu ikashuka kwa mlongo mzima, Cairo ikapata bonge la inflation kutokana na Mansa Musa alivyo "make it rain" kujitutumua kuwaonyesha waarabu kwamba mtu mweusi na mimi nimo dunia hii.

Sasa upuuzi kama huu wa kutumia mamilioni ya madola kuwaleta Brazil wakati tuna matatizo kibao mimi hata sishangai, ni jadi yetu, tunafanya miharusi mikubwa tusiyoweza kuimudu, tunavaa mi suti ambayo hata kuifua hatuwezi kumudu, tunanunua migari ya anasa wakati hata barabara za kuiendeshea hatuna etc etc.

Mansa Musa mentality.

Mkuu hii ni kweli kabisa waafrika lazima mtu atutambue kwamba tuko matawi ya juu, lakini mimi sijui chanzo cha haya ni nini. Mfano mimi mwenyewe nilipata taabu sana wakati nipo nchi za asia kupanda vibaiskeli vya mikuu 3 eti ndo taksi basi watu wakaniona najikweza sana lakini ukweli ni kwamba roho yangu haikupenda vile vibaiskeli.
 
Kabla wote hatujawa PC palikuwa na usemi " nigg*r rich" !

Amandla......
 
Inaonyesha pia kulikuwa na mgomo baridi wa tff dhidi ya ujio mzima wa brazil. Wadau walioenda tff kununua tiketi wanasema palikuwa na umati nje ya ofisi lakini tff walikuwa hawatoi tiketi zilizokuwa ndani kibao. Waliopata kwa urahisi ni wale 'waliofahamika'. Tena waliambiwa wafiche tiketi zao wakati wakitoka!
 
Si mgomo baridi. Walitegemea kuzilangua baadae! Acalping ni time honoured tradition hapa kwetu. Another tradition ni kuzihifadhi, in case mkubwa atazihitaji! Matokeo ndio hayo tuliyoyaona. Uwanja mtupuuuuuuuu.

Amandla........
 
Unambiwa tangu enzi za huyo Mansa Musa Mfalme wa Mali, waafrika tunajulikana kwa kujitutumua kutoa mapesa wakati tu masikini.

Unaambiwa huyo Mansa Musa alivyokuwa anaenda kuhiji hapo Mecca, alipitia Cairo, basi alimwaga midhahabu hapo ndani ya Cairo mwaka 1324 mpaka thamani ya dhahabu ikashuka kwa mlongo mzima, Cairo ikapata bonge la inflation kutokana na Mansa Musa alivyo "make it rain" kujitutumua kuwaonyesha waarabu kwamba mtu mweusi na mimi nimo dunia hii.

Sasa upuuzi kama huu wa kutumia mamilioni ya madola kuwaleta Brazil wakati tuna matatizo kibao mimi hata sishangai, ni jadi yetu, tunafanya miharusi mikubwa tusiyoweza kuimudu, tunavaa mi suti ambayo hata kuifua hatuwezi kumudu, tunanunua migari ya anasa wakati hata barabara za kuiendeshea hatuna etc etc.

Mansa Musa mentality.

Umenifurahisha sana kunikumbusha historia ya Mansa Musa na safari yake ya Hijja. In fact baada ya ibada ya Hijja, jamaa huyu alikuwa kaishiwa kabisa kiasi kuwa ilibidi akope kutoka kwa mfanya biashara mmoja hapo Cairo ili aweze kupata nauli ya kurudia nyumbani.
 
Waungwana kabla hatujahukumu tujue kiasi gani kimepatikana katika mechi. Tusubirini hesabu za TFF ndio tuhukumu.
 
Siku nyingine TFF fahamu haya.
1.Kipato cha mtu hakiwezi kubadilika eti kwasababu ya brazil. Yaani kutoka 3000 hadi 30000.
2.Wanaingia mpirani wengi ni watu wa kipato cha chini na kati kidogo. Hivyo wakati wa kupanga viingiliao ni muhimu kuzingatia hilo.
3.Ninyi TFF soi wafanya biashara, ndiyo maana kila wakati ninyi mnakula shoti. Kazi kama hizo wanapewa watu wenyefani zao kutoa yushauri na kupanga muundo wote wa mchezo. Nyinyi(TFF) ni wasimamizi wa mpira tuu-Zingatieni sana hilo.
 
all in all, kuleta brazil kwa kuwalipa pesa zote zile was a lunacy! whats the point? utalii upi tunasingizia uongo, kenya hawajawaleta brazil wala nani mbona utalii wao unatangazika kuliko wetu, je wataalam wa utalii walitoa ushauri uo? mbona tunapenda kuhusisha vitu visivyohusiana ili tu tutimize lengo letu! tuongee ukweli, kuwaleta brazil au man u ipi ingekua bora? nchi hii wengi tunashabikia ligi ya uingereza, ingekuja man u au arsenal i am sure uwanja ungejaa na watalii wa kweli wangeijua tz, mechi ya tz na brazil hata kwenye vyombo vya habari vya ulkaya ilikua hata aiwi advertised ambako ndio kuna watalii wa kweli, brazil wala si matajiri adi tuwategemee kwa utalii!
 
Ama kweli sikio la kufa halisikii dawa, kwani haya ya kipato si yalisemwa toka mapema lakini wakasema NO Problem. haya subirini sas tushirikiane kulipa tusichotumia.!!!
 
Kawaida ya serikali hailipi madeni haraka, hivyo hilo deni NMB wategemee ku write off, make litaongezeka na interest mpaka litafika awamu ya sita. Tuwe pamoja.
 
Guys nimesoma kwa Mr Michuzi kuwa tff wamekula hasara kwenye mechi kati ya TZ na Brazil.
Tff wamepata tsh 1.6bn wakati walitegemea kupata tsh4bn,katibu mkuu wa tff ndg Mwakalebela kasema haya hivi punde tu.
 
Safi sana....nimeipenda hii
 
Back
Top Bottom