SIRI YAFICHUKA: Deni la 2 billion/- latua Ikulu!

Sijasikia TFF ikitangaza mapato, lakini sidhani kama itafika hata shilingi bilioni 1. Hii ina maana kuwa serikali italazimika kubeba deni la zaidi ya shilingi bilioni 2 kutokana na guarantee iliyoiwekea TFF.

Kuna tatizo gani ukisubiri kusikia wamekusanya kiasi gani?

omarilyas
 
Waswahili walisema Kukopa harusi, kulipa matanga.

Msiseme hatukusema. Mara ooh utalii -hamna utalii wowote tulioona. Mara ooh hela zitarudi -kimerudi deni tu.Kwa mwoga huenda kicheko na kwa shujaa huenda kilio.

Wakuu katika decision making system bongo wangekuwa na moyo sikivu na kuingia hapa JF wangetuepusha na mengi.Kuambizana kuko kusikizana hapana.

Sasa imebakia majuto mjukuu, ama kweli chamlevi huliwa na mgema na chombo cha kuzama hakina usukani au kama wanavyosema wengine, sikio la kufa halisikii dawa.

Na bado, hii chovya chovya itamaliza buyu la asali
 
Uongozi wa NMB ulijua kuwa TFF hawawezi kurudisha deni hilo. Kodi zetu ndo zitafidia deni hilo, mnaotaka maisha bora mlie tu.

CHANGANYENI AKIRI ZA KIKWETE NA TENGA ILI MUWE MBAYUWAYU
 
By Emmanuel Muga
BBC Sport, Dar es Salaam
Source: BBC Sport - Football - World Cup 2010: Tanzania count cost of Brazil friendly


The Tanzanian Football Federation are facing a big financial loss after a poor turnout to see Brazil beat Tanzania 5-1 in a friendly on Monday.
Fans were put off by record entrance fees ranging from 25-180 US dollars to see the world's best team.

The Tanzanian Football Federation (TFF) hoped to raise about US$3m and cushion an estimated US$2.5m used to secure a friendly against the Brazilians. But the 60,000-seater stadium was only half-full for the evening game. The match fee paid to Brazil triggered a debate in Tanzania with some people questioning the rationale behind a poor country spending massively on a single match.


This forced the government to come clean on the matter, saying it had contributed nothing to the costs.


"Inviting Brazil was the TFF's responsibility," the minister of sports George Mkuchika said.

"They have taken a bank loan, which they will repay through gate collections, so the government should not be accused of anything."

Away from the costs, the game was excitement-filled, especially after the host team managed to grab a goal against the five-time world champions in the 5-1 loss.


The stadium erupted with joy after Jabir Aziz's goal in the dying minutes of the game, while Brazil coach Carlos Dunga praised his hosts for 'a good test'. Robinho and Ramirez scored two goals each and Kaka was also on target as Brazil wrapped up their preparation before starting their World Cup Group G campaign against North Korea on 15 June.


"It was a good test for Brazil because Tanzania is a good team, very well organised," Dunga said afterward.


"The idea was to play teams with high speed, physically strong, so it was good for us to play Tanzania and Zimbabwe.


"My target is the same as all Brazilian people, to win the World Cup."


Dunga used his full-strength squad and all his players came through the match unscathed.
 
Tulisema hili si deal hapa, watu oooh, eeeh, sasa mnaleta majuto mjukuu.
 
Ilionyeshwa na TV nyingi tu za nje. Kwa UK, walionyesha ESPN ambayo ni TV ya kulipia ya michezo na inaonyesha michezo kwenye nchi mbalimbali za Europe na Amerika ya Kusini.

Kuwaleta Brazili ilikuwa lazima uwalipe vinginevyo wasingelikuja. Siku hizi michezo ni biashara. Rais wetu si anasema ukitaka kula lazima uliwe kwanza?

Kwa watu ninaowafahamu mimi, walishangaa kuona Tanzania tuna uwanja mzuri hivyo na pia kushangaa kuona timu ambayo iko kwenye sijui 108 kumbe inaweza kuwa na wachezaji wazuri tu.

Huwezi kujua matokeo ya hiyo ziara mpaka baada ya muda. Kikubwa ni kwamba huku Ulaya zaidi ya nusu ya watu hawajui Tanzania iko wapi, ingawaje wanajua Kenya iko wapi. Juhudi yeyote ya kuitangaza nchi lazima ipongezwe lakini pia lazima tuangalie je hiyo njia tuliyotumia ndio ilikuwa bora zaidi katika kutumia hizo pesa zote?

Mleta maada naona kaongeza na chumvi kwenye hilo la bill kwenda Ikulu maana kaangalia pesa za viingilio tu na ku ignore pesa za TV mbalimbali kuonyesha hiyo match pamoja na matangazo kibao.

Wacha tusubiri Tenga atupatie mahesabu kamili.

Mkulima... wacha mawazo ya kikulima kulima. Upumbavu wa aina hii ndio unaididmiza Tanzania
 
Siri kali inawasukumia bomu hili TFF na Viongozi wa TFF hawatakuwa tayari kujibizana na Serikali. Kutokana na mapato kiduchu ya mchezo huo TFF hawataweza kulipa hata 20% ya deni lao hivyo kutokana na deni kubwa kutokuwa na uwezo wa kuiweka timu ya Taifa kwamuda mrefu. Kwa mara nyingine kichwa cha mwendawazimu kimefanya madudu.
 
Ilionyeshwa na TV nyingi tu za nje. Kwa UK, walionyesha ESPN ambayo ni TV ya kulipia ya michezo na inaonyesha michezo kwenye nchi mbalimbali za Europe na Amerika ya Kusini.

Kuwaleta Brazili ilikuwa lazima uwalipe vinginevyo wasingelikuja. Siku hizi michezo ni biashara. Rais wetu si anasema ukitaka kula lazima uliwe kwanza?

Kwa watu ninaowafahamu mimi, walishangaa kuona Tanzania tuna uwanja mzuri hivyo na pia kushangaa kuona timu ambayo iko kwenye sijui 108 kumbe inaweza kuwa na wachezaji wazuri tu.

Huwezi kujua matokeo ya hiyo ziara mpaka baada ya muda. Kikubwa ni kwamba huku Ulaya zaidi ya nusu ya watu hawajui Tanzania iko wapi, ingawaje wanajua Kenya iko wapi. Juhudi yeyote ya kuitangaza nchi lazima ipongezwe lakini pia lazima tuangalie je hiyo njia tuliyotumia ndio ilikuwa bora zaidi katika kutumia hizo pesa zote?

Mleta maada naona kaongeza na chumvi kwenye hilo la bill kwenda Ikulu maana kaangalia pesa za viingilio tu na ku ignore pesa za TV mbalimbali kuonyesha hiyo match pamoja na matangazo kibao.

Wacha tusubiri Tenga atupatie mahesabu kamili.

Kazi ipo! Kulikuwa na ulazima gani kuliingiza taifa kwa jambo la kijinga kama hili? Mawazo yako ni mfu. Unategemea kwa mechi kama hiyo wachezaji wa Tanzania wauzike ? wanashindwa hata na Rwanda hapo....mawazo wa kijima na kikulima haya
 
Unambiwa tangu enzi za huyo Mansa Musa Mfalme wa Mali, waafrika tunajulikana kwa kujitutumua kutoa mapesa wakati tu masikini.

Unaambiwa huyo Mansa Musa alivyokuwa anaenda kuhiji hapo Mecca, alipitia Cairo, basi alimwaga midhahabu hapo ndani ya Cairo mwaka 1324 mpaka thamani ya dhahabu ikashuka kwa mlongo mzima, Cairo ikapata bonge la inflation kutokana na Mansa Musa alivyo "make it rain" kujitutumua kuwaonyesha waarabu kwamba mtu mweusi na mimi nimo dunia hii.

Sasa upuuzi kama huu wa kutumia mamilioni ya madola kuwaleta Brazil wakati tuna matatizo kibao mimi hata sishangai, ni jadi yetu, tunafanya miharusi mikubwa tusiyoweza kuimudu, tunavaa mi suti ambayo hata kuifua hatuwezi kumudu, tunanunua migari ya anasa wakati hata barabara za kuiendeshea hatuna etc etc.

Mansa Musa mentality.
 
Teh teh teh teh waungwana wanajua kugawana kodi zetu? hivi Brazil wametoa risiti ya hiyo billion $2.5?

Mkuu usiwe na wasi baada ya kuiweka wazi hii kitu na vyombo vya kimataifa kushikia bango Brasil watarudisha change tu, si unakumbuka ya Radar!
 
tatizo kubwa la watanzania na hasa watendaji wa serikali yetu ni kukosa business and entrepreneurial minds... na kibaya zaidi hawaheshimu wenye weledi huo!!!

wanasahau kwamba biashara si sawa ba blah--blahh

THE PROBLEM IS COMMON KILA SEHEMU NA MBAYA ZAIDI NOBODY HAS BEEN MADE TO PAY DESPITE ALL THE LOSSES WE INCUR IN ALMOST EVERY DECISION

HASARA ZA TFF HAZIJAANZA LEO
 
Mfanyabiashara huyo anaeleza kwamba kwa hali halisi iliyopo kwenye mfumo wa ukusanyaji kodi, ni vugumu kukwepa ushuru kwa kudanganya kiasi (idadi) cha mali kilichomo kwenye kontena (false declaration) au kuweka bei ndogo au ya chini ya ile bei halisi (under invoicing), lakini kwa kampuni hiyo hilo linawezekana kwa kuwa mfumo mzima tangu serikalini, Tiscan na TRA umekuwa nyuma yao kutokana na nguvu kubwa waliyonayo vijana hao.
Imeelezwa kwmaba kwenye kampeni za mwaka 2005 kampuni hiyo ilichangia chama tawala Sh. Milioni 200 na kwamba katika mwaka huu wameahidi kuchangia milioni 500 huku ofisini kwao zikiwa zimejaa picha walizopata kupiga na viongozi wa juu wa chama tawala na Serikali katika hafla za uchangiaji kampeni.

From: Ufisadi wa kutisha ushuru wa forodha

hawa ni vijana wa home shopping centre
wanaweza wakaingia na documents za $5,000 bandarini zenye thamani ya 500,000,000 tsh kila siku
 
Well hii hoja nitaijibu tukipata kwanza details za kilichopatikana katika mechi ya Tanzania na Brazil. TFF tunasubiria hesabu zenu!!!! kuhusu deni ikiwa litaweza kulipwa guarantee ni kana kwamba TFF wameshindwa is not an issue wakiwa wameweza kurecover pesa.
 
NINCOMPOOPS! Nani atataka kuangalia mpira kati ya Brazil na Tanzania ukituondoa sisi wenyewe?

Amandla..........
 
Taztizo ni kwamba hela ya walipa kodi ndio inaenda kulipa deni kwa vile viongozi wetu wanapenda hanasa za kijinga jinga bila kutumia akili.toka lini utalii ukatangazwa kwa njia hii waliotumia? kuna wasomi kweli ikulu au mijitu inajikusanya tu kwa vile marafiki?


kama wanataka kuleta urafiki waachie ngazi wakatafute biashara za kufanya za kuendeleza urafiki,sio kuleta mzaa na maisha ya watu mil 40 ambao wote kwa njia moja au nyingine wanategemea mali za taifa.
 
Mkuu usiwe na wasi baada ya kuiweka wazi hii kitu na vyombo vya kimataifa kushikia bango Brasil watarudisha change tu, si unakumbuka ya Radar!

Mkuu Hofstede,

Hakuna chenji hapo! Ndiyo tumeishaliwa, maana ni ujinga wetu. Chenji ilirudi kwenye radar kwa kuwa kulikuwa na element ya corruption, lakini hapa sioni kama kuna element ya corruption, ila ni ulimbukeni wa viongozi wetu ambao hawajui priorities za taifa.

Viongozi wetu wanaongoza kwa matumizi yasiyo ya lazima, na ndiyo maana mambo ya maana huwa hayatekelezwi, ukiuliza utaambiwa serikali haina fedha, lakini hela za kuwahonga Brazil ili wakubali kuja kucheza na Taifa Stars zipo.
 
Grim reality was, in the end, majority of dirt-poor, ordinary football crazy folk just couldn't afford paying top-dollar to watch a failed asylum-seeker (who used to be a 5th-division league star in some obscure North-European country) score only goal for Tz against Brazil...
 
Jana tuliambiwa serikali isilaumiwe ni TFF tu! Leo haya! Ya kesho nayaogopa sasa!
 
Tatizo ni kuwa nchi hii imajaa viongozi wasiotumia akili hata siku moja. Kuileta Brazil nchini lilikuwa ni jambo jema, ila wazo hilo walilletewa na Maximo aliproudi kutoka likizo mwaka jana na wala hakuna kiongozi aliyekaa kitako kulifanyia uchambuzi wa kutosha kupanga litekelezwe vipi. Wamekurupuka mwishoni bila kuwa na mkakati wowote, na hata hivyo viingilio vilipangwa bila kufanyiwa uchambuzi wa kitaalamu (break-even analysis). Tukio hili lingefanyiwa uchambuzi wa kutosha na kupangiwa mkakati mzuri, siku hiyo kiwanja kingejaa watazamaji na bado TFF ingepata faida bila hata kugusa shilingi za kodi zetu, huku ikiwaacha wapenzi wa mchezo ule wakiwa wamefurahi.

Initiative moja rahisi sana ambayo TFF walishindwa kuitumia ni pamoja na kuuza nguo zinazofanana na jezi za wacheazji wa timu ya Brazili, na ikiwezekana kuwaomba wachezaji hao waziasaini; hatua ndogo kama hii ingeweza kupunguza gharama zile kwa zaidi ya robo. Kupanga viingilio vinavyo vuta watazamaji wengi ilikuwa ni njia ambayo mfanyabisahara yeyote angetumia kwa makini sana. Ujio wa Brazil ulikuwa unatoa mianya mingi ya kutengeza pesa ila viongozi wetu waliangalia sehemu moja tu. Ni vivyo hivyo ndivyo walivyo hata viongozi wa serikali, wanategemea mapato kutokana na misaada na mikopo tu; akili ya kujipatia pesa kulingana na opportunity zilizopo ni sifuri kabisa.
 
Back
Top Bottom