Siri yafichuka: CCM, Serikali na Bunge katika hali tete

Paparazi Muwazi

JF-Expert Member
Dec 23, 2007
310
79
Siri yafichuka: CCM, Serikali na Bunge katika hali teteIkiwa zimebaki siku mbili wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kuadhimisha sherehe za miaka 35 tangu kuzaliwa kwake hali katika chama hicho ni tete.Mivutano ya wazi na ishara za kushindwa zinazidi kujidhihirisha huku uwajibikaji wa pamoja ukipotea katika miongoni mwa chama hicho, serikali na wabunge wake inazidi kuongezeka.Kukataliwa kwa hoja mbili za serikali jana kwa wabunge wa chama hicho kuunga mkono hoja za kambi rasmi ya upinzani inayoongozwa na CHADEMA ni kati ya matukio ya wazi.Vyanzo toka ndani ya CCM vinaaleza kuwa uamuzi wa wabunge wa chama hicho ‘kuasi’ unatokana na kauli za Rais Kikwete kupitia kwa ikulu na kupitia CCM kuwageuka wabunge hao katika makubaliano waliyofikia katika kikao kati ya mwenyekiti huyo CCM kilichofanyika Dodoma mwishoni mwa mwaka jana.Katika mkutano huo Rais Kikwete aliwapongeza wabunge kwa kupitisha muswada wa sheria ya mabadiliko ya katiba na kuwapa kazi ya kwenda kutoa elimu juu ya sheria hiyo kwa wananchi, sambamba na kukubali uamuzi wa Spika wa kuongeza posho za vikao kwa wabunge.“Tumeamua kuionyesha serikali kwamba bunge ni chombo chenye nguvu, Rais Kikwete ametegeuka katika suala la posho na kufanya wabunge ndio tuonekane tumepandisha wenyewe posho bila ridhaa yake. Tutakaa mambo yao wajue kwamba tumeshikilia mpini, na tuweze kurejesha imani kwa wananchi”, alisema mbunge mmoja machachari ambaye hakutaka kutaja jina lake kuhofia mikakati yao kukwama.Kwa mujibu wa mbunge mwingine amesema kwamba wabunge wa chama hicho katika kikao chao cha kamati ya wabunge cha jana walimbana Waziri Mkuu Mizengo Pinda kuhusu mgomo wa madaktari wakieleza kwamba hali imekuwa mbaya kutokana na udhaifu wake wa kiutendaji. Hata hivyo, baadhi ya wabunge wamemlaumu Naibu Spika wa Bunge Job Ndugai kwa kuungana na wabunge wa upinzani katika kuibana serikali. Awali katika kikao cha jana wabunge hao walikubaliana kwa Spika atumie kila mbinu kauli ya mawaziri isijadiliwe ili kuweza kuilinda serikali. Hata hivyo kufuatia muongozo ulioombwa na John Mnyika akitaka bunge litimize wajibu wa katiba wa kuisimamia serikali na kueleza kwamba serikali ni watuhumiwa ikiwemo waziri ambaye anapaswa kuwajibishwa hivyo wabunge wachukue nafasi yao, Ndugai aliungana naye na kuagiza Kamati ya Bunge ya Huduma za Jamii ichukue hatua kwa haraka.Katika mkutano wa leo unaoendelea hivi sasa mvutano mkubwa umetawala huku wabunge walio wengi wakitaka maelezo toka kwa serikali kwa kuleta hoja zenye kasoro katika bunge na hivyo kufanya wabunge washindwe kutetea hoja za serikali. Wabunge hao wametaja mifano ya hoja hizo kuwa ni Azimio kuhusu Muswada wa ushuru wa Bidhaa liliwasilishwa na Waziri wa Fedha Mustapha Mkullo na Muswada wa Sheria ya Marekebisho ya Sheria mbalimbali yote ikiwa imewasilishwa na serikali jana. Huku wengine wakitaja muswada wa marekebisho ya sheria ya udhibiti wa fedha haramu uliojadiliwa leo ambao umeliingiza bunge katika kashfa ya kupitisha kifungu cha sheria kilichowasilishwa na Mbunge wa Ubungo cha kuongeza ukubwa wa adhabu kwa watakaobainika kufanya makosa yahusuyo fedha haramu kwa sheria kusomwa kwa mara zake zote tatu, halafu baadaye Mwenyekiti wa Bunge kutangaza kwamba ilipitishwa kimakosa na hivyo kusema anafuta maneno yake kwenye hansard aliyoyasema wakati bunge lilipokaa kama kamati.Katika suala hilo Serikali imejitetea kuwa siyo makosa yake bali ya Mwenyekiti wa Bunge aliyetajwa kwa jina moja la Mabumba kushindwa kuwaongoza wabunge. Hata hivyo mwenyekiti ametetewa na wabunge kutoka Zanzibar ambao wamesema kosa ni la wabunge wa CCM kwa kuitikia ndio bila kujua athari za kifungu ambacho walikipitisha. Kikao hicho kinatarajiwa kuendelea mpaka usiku zaidi kwa kuwa mvutano mkali zaidi unatarajiwa wakati wa kujadili msimamo wa chama hicho kuhusu muswada wa marekebisho ya sheria ya mabadiliko ya katiba.Mivutano hiyo miongoni mwa wabunge wa CCM vinara wakiwa ni viongozi waandamizi katika chama hicho, bunge na serikali kunadhihirisha hali tete huku turufu ikiwa kwa Rais Kikwete ambaye anatarajiwa kuzungumza na wabunge hao na pia kufanya mabadiliko katika baraza mawaziri hivi karibuni. PM
 
Niliwakumbusha watu siku chache zilizopita kuwa utawala ukifitinika hauwezi kusimama!CCM hawawezi tena kutawala kinachosubiriwa ni muda tu ufike yatimie. Watatoka hata kwa kuanzisha wao wenyewe. Tusubiri tuone.
 
Naona Shehe Yahya Husein,yule mtabiri wa nyota Afrika mashariki na kati amefufuka
 
Naskia wabunge wamepania kukwamisha hoja binafsi za January na Zitto wanazotarajia kuziwasilisha bungeni kisa wamepinga posho. Wabunge wanawasubiri kwa hamu ili wawakomoe.
Nashindwa kuelewa tuna wawakilishi wa aina gani wanaojali pesa kuliko maendeleo ya taifa!ikiwa kweli nitawashangaa sana
 
Karne ya thred za madudu ndio hii.hakuna hoja apa.lakini utapata wajinga wenzako watakuunga mkono ambao wana comment bila kusoma
 
Siri yafichuka: CCM, Serikali na Bunge katika hali teteIkiwa zimebaki siku mbili wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kuadhimisha sherehe za miaka 35 tangu kuzaliwa kwake hali katika chama hicho ni tete.Mivutano ya wazi na ishara za kushindwa zinazidi kujidhihirisha huku uwajibikaji wa pamoja ukipotea katika miongoni mwa chama hicho, serikali na wabunge wake inazidi kuongezeka.Kukataliwa kwa hoja mbili za serikali jana kwa wabunge wa chama hicho kuunga mkono hoja za kambi rasmi ya upinzani inayoongozwa na CHADEMA ni kati ya matukio ya wazi.Vyanzo toka ndani ya CCM vinaaleza kuwa uamuzi wa wabunge wa chama hicho ‘kuasi' unatokana na kauli za Rais Kikwete kupitia kwa ikulu na kupitia CCM kuwageuka wabunge hao katika makubaliano waliyofikia katika kikao kati ya mwenyekiti huyo CCM kilichofanyika Dodoma mwishoni mwa mwaka jana.Katika mkutano huo Rais Kikwete aliwapongeza wabunge kwa kupitisha muswada wa sheria ya mabadiliko ya katiba na kuwapa kazi ya kwenda kutoa elimu juu ya sheria hiyo kwa wananchi, sambamba na kukubali uamuzi wa Spika wa kuongeza posho za vikao kwa wabunge."Tumeamua kuionyesha serikali kwamba bunge ni chombo chenye nguvu, Rais Kikwete ametegeuka katika suala la posho na kufanya wabunge ndio tuonekane tumepandisha wenyewe posho bila ridhaa yake. Tutakaa mambo yao wajue kwamba tumeshikilia mpini, na tuweze kurejesha imani kwa wananchi", alisema mbunge mmoja machachari ambaye hakutaka kutaja jina lake kuhofia mikakati yao kukwama.Kwa mujibu wa mbunge mwingine amesema kwamba wabunge wa chama hicho katika kikao chao cha kamati ya wabunge cha jana walimbana Waziri Mkuu Mizengo Pinda kuhusu mgomo wa madaktari wakieleza kwamba hali imekuwa mbaya kutokana na udhaifu wake wa kiutendaji. Hata hivyo, baadhi ya wabunge wamemlaumu Naibu Spika wa Bunge Job Ndugai kwa kuungana na wabunge wa upinzani katika kuibana serikali. Awali katika kikao cha jana wabunge hao walikubaliana kwa Spika atumie kila mbinu kauli ya mawaziri isijadiliwe ili kuweza kuilinda serikali. Hata hivyo kufuatia muongozo ulioombwa na John Mnyika akitaka bunge litimize wajibu wa katiba wa kuisimamia serikali na kueleza kwamba serikali ni watuhumiwa ikiwemo waziri ambaye anapaswa kuwajibishwa hivyo wabunge wachukue nafasi yao, Ndugai aliungana naye na kuagiza Kamati ya Bunge ya Huduma za Jamii ichukue hatua kwa haraka.Katika mkutano wa leo unaoendelea hivi sasa mvutano mkubwa umetawala huku wabunge walio wengi wakitaka maelezo toka kwa serikali kwa kuleta hoja zenye kasoro katika bunge na hivyo kufanya wabunge washindwe kutetea hoja za serikali. Wabunge hao wametaja mifano ya hoja hizo kuwa ni Azimio kuhusu Muswada wa ushuru wa Bidhaa liliwasilishwa na Waziri wa Fedha Mustapha Mkullo na Muswada wa Sheria ya Marekebisho ya Sheria mbalimbali yote ikiwa imewasilishwa na serikali jana. Huku wengine wakitaja muswada wa marekebisho ya sheria ya udhibiti wa fedha haramu uliojadiliwa leo ambao umeliingiza bunge katika kashfa ya kupitisha kifungu cha sheria kilichowasilishwa na Mbunge wa Ubungo cha kuongeza ukubwa wa adhabu kwa watakaobainika kufanya makosa yahusuyo fedha haramu kwa sheria kusomwa kwa mara zake zote tatu, halafu baadaye Mwenyekiti wa Bunge kutangaza kwamba ilipitishwa kimakosa na hivyo kusema anafuta maneno yake kwenye hansard aliyoyasema wakati bunge lilipokaa kama kamati.Katika suala hilo Serikali imejitetea kuwa siyo makosa yake bali ya Mwenyekiti wa Bunge aliyetajwa kwa jina moja la Mabumba kushindwa kuwaongoza wabunge. Hata hivyo mwenyekiti ametetewa na wabunge kutoka Zanzibar ambao wamesema kosa ni la wabunge wa CCM kwa kuitikia ndio bila kujua athari za kifungu ambacho walikipitisha. Kikao hicho kinatarajiwa kuendelea mpaka usiku zaidi kwa kuwa mvutano mkali zaidi unatarajiwa wakati wa kujadili msimamo wa chama hicho kuhusu muswada wa marekebisho ya sheria ya mabadiliko ya katiba.Mivutano hiyo miongoni mwa wabunge wa CCM vinara wakiwa ni viongozi waandamizi katika chama hicho, bunge na serikali kunadhihirisha hali tete huku turufu ikiwa kwa Rais Kikwete ambaye anatarajiwa kuzungumza na wabunge hao na pia kufanya mabadiliko katika baraza mawaziri hivi karibuni.PM

Mkuu, ungefanya editing kidogo kwenye MS Word na kuweka paragraphs na spacing ingetusaidia sana.
 
Siri yafichuka: CCM, Serikali na Bunge katika hali teteIkiwa zimebaki siku mbili wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kuadhimisha sherehe za miaka 35 tangu kuzaliwa kwake hali katika chama hicho ni tete.Mivutano ya wazi na ishara za kushindwa zinazidi kujidhihirisha huku uwajibikaji wa pamoja ukipotea katika miongoni mwa chama hicho, serikali na wabunge wake inazidi kuongezeka.Kukataliwa kwa hoja mbili za serikali jana kwa wabunge wa chama hicho kuunga mkono hoja za kambi rasmi ya upinzani inayoongozwa na CHADEMA ni kati ya matukio ya wazi.


















Vyanzo toka ndani ya CCM vinaaleza kuwa uamuzi wa wabunge wa chama hicho ‘kuasi' unatokana na kauli za Rais Kikwete kupitia kwa ikulu na kupitia CCM kuwageuka wabunge hao katika makubaliano waliyofikia katika kikao kati ya mwenyekiti huyo CCM kilichofanyika Dodoma mwishoni mwa mwaka jana.

sasa wewe ndugu unafikiria kutumia kiungo gani cha mwili wako???????????kwa nini USIMPONGEZE RAIS KWA KUKATAA KUSAINI UFISADI WA POSHO KWA WABUNGE BADALA YAKE UNAMLAUMU?????????
 
kwanza una mwandiko mbaya sijui mwalimu wako alipata shida kiasi gani kukufundisha
 
Back
Top Bottom