Siri ya wizara ya nishati na madini kushambuliwa hii hapa

kumusoma

JF-Expert Member
Feb 3, 2014
566
889
Watanzania walio wengi wataendelea kujiuliza na kushangaa wakati wote pale ambapo wanapoona Wizara ya Nishati na Madini inashambuliwa na kutuhumiwa wakati wote kwa "Scandal" kila mwaka na kusababisha hata viongozi wake kujiuzulu au kuondolewa katika Wizara hiyo.

Kila mwaka Wizara hiyo kama haijaondoa Waziri basi Katibu Mkuu anaondolewa na Wizara hii ndiyo kila inapotokea baraza la mawaziri kuvunjwa basi Wizara ya Nishati na Madini ndiyo sababu. Kama mtakumbuka Wizara hii ndiyo pia iliyosababisha aliyekuwa waziri Mkuu wakati ule, Edward Lowassa kujiuzulu kutokana na sakata la RICHMOND.

Hebu sisi Watanzania tutafakari na kujiuliza kwa kina hivi kuna nini Wizara hii ndiyo inayokodolewa macho na hata Wabunge kuongea bungeni na hata kwenye vyombo vya habari hadi mapovu yanawatoka juu ya Wizara hii na kwa nini Wizara nyingine hazilalamikiwi wala hazina mikiki mikiki kama ilivyo Nishati na Madini.

Kuna Wizara kama za Afya ambazo zinagusa maisha ya wanadamu ambao ni Watanzania moja kwa moja kama vile gharama za madawa, uhaba wa vituo vya afya, vifo vya watoto walio chini ya miaka mitano, vifo vya akina mama wajawazito n.k.

Ukiachilia mbali Wizara ya Afya kuna Wizara kama za elimu, Mambo ya Ndani n.k. zote hazipigiwi kelele ambazo zinazopigwa kwa Wizara ya Nishati na Madini, hebu tutafakari na tujue tatizo nini?

Tumesahau tulikotoka katika Wizara hii kwani sasa lile suala la mgawo halipo tena kama ilivyokuwa huko nyuma, miaka ya nyuma umeme ulikuwa haujawahi kwenda vijijini sasa hivi umeme unakwenda vijijini na kufanya kila jimbo hapa nchini kwetu basi lazima utakuta vijiji kadhaa vimepatiwa umeme.

Kwa akili ya haraka haraka ukitafakari Wizara hii imebeba maliasili na "madeal" ambayo kila mtu anayokodolea mimacho kwamba anajua akipiga tu atapata fedha hebu tuangalie kama ifutavyo kwenye sekta zilizo chini ya Wizara hii – NISHATI & MADINI

IDARA YA NISHATI:
Katika eneo hili kila mfanyabishara, mbunge (mwanasiasa) anataka kufanya bishara na TANESCO ambapo utasikia mara wamekuja na wawekezaji wanataka kuwekeza katika umeme ili wakiuzia umeme TANESCO kama wanavyofanya SYMBION, SONGAS, PAN AFRICA, AGRRECO wakiuzia umeme TANESCO wanapata faida kwani mashirika hayo yote niliyoyataja wanasiasa wamo ndani yake na wanavuna fedha ndefu pale TANESCO ndiyo maana wanayapigia chepuo.

Ukiachilia mbali umeme hebu fikiria ukiwa mwanasheria wa TANESCO kama alivyokuwa NIMROD MKONO ujue utavuna fedha kama alivyokuwa akizipata MKONO ambazo ni Sh. Bilioni kumi kila mwezi.

Ukiiuzia mafuta TANESCO bado utavuna hela nyingi sana TANESCO na kuna wabunge ambao wanayapigia chepuo ili yapate zabuni ya kuuza mafuta TANESCO ili wabunge hao nao wapate fedha lukuki.

Hiyo ni mifano michache kwa shirika moja tu la TANESCO lakini zipo biashara nyingi na hata nyingine za kipumbavu wanasiasa wanalazimisha wapewe ili wafaidike.

Usisahau mashirika mengine kwenye Idara ya Nishati kama TPDC ambayo nayo wanasiasa wana deal zao humo, REA n.k

IDARA YA MADINI
Huku nako usiseme wabunge kibao wanapigania kunufaika kwa kupata vitalu vya madini ambapo wabunge wengi wana vitalu vya kufa mtu yaani ni kufuru na wanalazimisha hata Serikali kupitia Wizara ya Nishati na Madini ivunje sheria na Wizara ikibaki na msimamo kwa kuwataka wanasiasa hawa wafuate sheria wanatia kuwalipua bungeni. Na haya yanayotokea sasa ni kutokana na MUHONGO NA MASWI kugangamala kuwataka wabunge wengi wenye vitalu vya madini katika maeneo mbalimbali nchini kufuata sheria.

Mbaya zaidi nay a kusikitisha kuna wabunge ambao wamefikia hatua hata ya kuwataka maofisa wa madini katika mikoa mbalimbali nchini wakiwalazimisha wawape maeneo ya wachimbaji wadogo kwa kweli inauma sana ambapo wabunge wetu ambao eti wanasema wao ni wawakilishi wa wananchi lakini kwa mlango wa nyuma ndiyo wanaowadhulumu haki zao.

Wabunge hawa hawa ndiyo madalali wa makampuni mbalimbali ya nje ya nchi wanawaleta na wanalazimisha wapewe vitalu popote wanapotaka hata kama maeneo hayo tayari wachimbaji wadogo wanamiliki kwani wanajua mwisho wa siku wakifanikiwa kuwa wanapata hela kwa wawekezaji. Wiki ijayo tunawataja wabunge wote wenye vitalu vya madini.

Kwa kweli kelele zote zinazopigwa kwa Wizara ya Nishati na Madini wakati kila wakati zinatokana na "CONFLICT OF INTEREST" yote ni ulaji katika Wizara hiyo. ZITTO mwenyewe amechukua fedha kibao kwa yule Mhindi Seth kwa kwa kuwatuma yule mwanasheria wake, Filikunjombe, Vivian na wengine tunawatumia document za fedha alizochukua.

Kelele hizi ni ulaji tu hakuna kingine wakiminywa na Serikali wasitafute fedha kama alivyofanya Maswi na Muhongo kuwakomalia hakuna fedha za bure Nishati na Madini wanatafuta wapi nao walipize kisasi na hata ikiwezekana wawaondoe ili viongozi legelege na goigoi ambao wabunge wataweza kuwayumbisha waingie pale Wizara na wabunge kama akina Zitto wapenyeze ‘madeal' yao ya ulaji.
Mathalan wakati ule wa MHANDO wa TANESCO wabunge waliigeuza TANESCO kama shamba la bibi na kijiwe cha kuchota fedha na hata kufikia akina Sarah Msafiri na akina Munde Tambwe kupanda zabuni ilivyo halali ambapo wakaleta matairi substandard na kusababisha ajali kibao uliza madereva wa TANESCO watakwambia ajali zilizovyokuwa nyingi kwa matairi kupasuka. Jamani inauma na kusikitisha tunaipeleka nchi hii wapi.

Leo hii tumewapata akina MUHONGO NA MASWI ambao si wanasiasa na wanapigana kuleta mabadiliko kwenye sekta husika hizo mbili midomo mirefu ya kina Zitto na tumbili Kafulila inachongoka hatutaki tumewachoka mkope mkafie mbele nyamafu nyie!!!!!!!!!
Mhe. Rais Kikwete umefika wakati sasa Serikali yako iamke iachwe kuchezewa na hawa wanasiasa uchwara kama kweli wao wanataka haki juu ya IPTL waihoji MAHAKAMA mbona wanagwaya wanabaki kuionea Serikali mara wawakamate viongozi wa TPDC utadhani wao ni mahakama.

inayoonekana reporti ya CAG haijawagusa akina MASWI NA MUHONGO na wala hawahusiki ila kinachotafutwa hapa ni kuwachinjia baharini ili wale wenye 'madeal' Wizara ya Nishati na Madini waendelee kuchuma maana kwa sasa wana hasira wanashindwa pa kupita MASWI NA MUHONGO wamefunga mianya yote na ukifanya mzaha wanakumbua ndiyo maana wanachukiwa.

Magazeti ya Mtanzania, RAI na Macheo nayo yanatumika kummaliza Mizengo Pinda ili ajiuzulu kama alivyojiuzulu LOWASSA mwaka 2008 na huyu Pinda kinachompoza ni pale alipotangaza kugombea urais. kazi kwenu Watanzania pimeni maji sio kila mnachoambiwa na wanasiasa mnaamini!!!!
 
Back
Top Bottom