Siri ya waraka wa Mwakyembe yafichuka; Kisa ni kifo cha ghafla cha mhudumu ofisini kwake

Ni sawa mdau,lakini kwanini iwe ni Dr.Mwakyembe pekee wakati yeye alichofanya ni kusoma ripoti ya kamati teule ya Bunge iliyokuwa na wajumbe wengi? Hawa wajumbe wengine wa kamti ile mbona hatusikii wakiwindwa? au kuwa mwenyekiti wa tume ndio ilikuwa nongwa?

Unaijua ile list ya watu wanaowindwa kuwekea sumu au kuuwawa kwa njia yoyote ile?
 
Jinsi anavyougua Dr. kuna ndugu yangu pia alishawahi kuugua hivyo hivyo lakini haikutokana na kulishwa au kunawia sumu.
Inabidi uchunguzi wa kina ufanyike kujua ni ugongwa gani hasa badala ya kuendelea kuhisi tu kwasababu ya hofu aliyokuwa nayo ya kulipiziwa kisasi kutokana na aliyowatendea wenzake kihalali au pengine sio kihalali mimi sijui. Sisi ndugu yetu Dokta alitupa ripoti kwamba ugonjwa ni kansa iliyosababishwa kwa kiasi kikubwa na madawa ya kuulia wadudu mashambani aliyokuwa anapulizia, pamoja na dawa za kuulia magugu.

Ni more likely kuwa huo ugonjwa wa ndugu yako sio sawa na ule wa Dr. Mwakyembe kwa sababu huo wa ndugu yako madaktari wa hapa bongo waliweza kuestablish kilichomsibu lakini wa Dr. Mwakyembe madaktari wa bongo wameshindwa kuestablish ni ugonjwa gani na nini kimecause.

Na hata huko India for months madaktari wanahangaika kufanya uchunguzi. Hicho ni kielelezo kuwa ndugu yako aliugua ugonjwa tofauti na wa Dr. Mwakyembe.
 
Sijui mjadala huu ni wa Kizalendo ama wa wale wenye mapenzi mema kwa Mwakyembe au ni wa aina gani. Napata taabu manake Mwakyembe alipokwenda India kwa mara ya kwanza kuna maneno yaliandikwa kwenye vyombo mbali mbali vya habari na kwenye mitandao kubwa likiwa tamko la Mwakyembe kuwa atakaporudi Nchini ataweka mambo hadharani; unfortunately mzee amerudi hilo halijafanyika worse enough karudi tena India katoa kitu wanachokiita "waraka wa siri" (nachukia sana hayo maneno) leo hii inakuaje kuitwa waraka wa siri ati kwa Familia, jamaa, ndugu, marafiki na watu wa karibu. Kwani yeye Mwakyembe hajui kwamba wakati huu Watanzania karibu wote wameshakuwa jamaa zake ama ndugu zake??

Kidogo hili kuingia akilini ni ngumu manake inawezekanaje watu waamue kukuvua nguo hadharani ila wewe nawe unapopata nafasi ya kuwavua nguo ati unaenda wavulia SIRINI kuna kitu hakijakaa sawa somewhere. Jambo hili limeshakuwa la Watanzania si la NYARAKA wala WARAKA wa SIRI. Watu wanaumiza kichwa kujadili sintofahamu yote hii na kweli wanaelekea kutofahamu chochote. Kila kukicha linaletwa jambo moja kati ya mambo maelfu yanayohitajika. Tatizo ni nini?? Anachoogopa ama anachokionea haya Mwakyembe ni nini?? Kama asipofanya yeye sasa hivi ili hatua zichukuliwe anategemea Familia yake itafanya lipi pasipo yeye kama atatangulia mbele za haki??

Mwakyembe azinduke upya na abatilishe ule waraka wake na auandike upya uwe ni "Waraka wa Mwakyembe kwa Watanzania wenzangu juu ya lile linalonisibu."

Ila katika haya yote nami pia nishawishika kusimamia yale ya Manumba mpaka hapo APOLLO watakapothibitisha vinginevyo manake nashawishika kuamini kuwa hata Mwakyembe mwenyewe hawezi ama ameshindwa kuwa reliable source of his own......
 
habari za kuamika kuwa huyo muhudumu alikufa kutokana na ugonjwa unaoua watu sasa na kwamba huyo binti alikuwa ni mwenza wake wa siku nyingi .imekuwaje?

The most flippant remark in this thread (in my book) it tops Pasco's and Sweety Radhia's.
 
Kifo cha muhudumu kinaweza kuhusika au kutokuhusika na ugonjwa wa Dr, ni lazima uchunguzi wa kina ufanyike ila kama serikali ni wahusika wakuu Dr atakuwa ameshashindwa kesi sikunyingi. Na inavyoonyesha serikali wanapotezea kwa kumtuma Manumba kutoa ripoti wakijua itapingwa na Dr na wao wasapoti kupoteza muda. Na serikali itawafungulia kesi wale waliosema kalishwa sumu ili watoe uthibitisho wa kujitosheleza mahakamani wa kumtaja mpaka aliyeweka sumu na akiri, wakishindwa kufanya kuthibitisha, wataadhibiwa mchezo unakwisha. Ni vigumu sana kushindana na serikali kama imeamua kukumaliza.

Mkuu uko sahihi kiasi fulani,ila pia ni vigumu serikali kushindana na umma utakapo amua
 
mkuu kuna mahali umeona report ya kifo cha huyo sekretary?......
Hapana Mkuu, ndio maana nimesema nashindwa kuimagine wakati ninaanza hiyo aya. Nipo makini kuchagua maneno ninayoyatumia. Hata hivyo nimeweka hivyo kama uchokozi ili wenye taarifa watupe, kwan wengine kwa Dr. Massawe hatuwezi kupata
 
habishani anachosema yeye si polisi na hafanyi uchunguzi na hawezi kuingilia uchunguzi wa polisi hivyo hawezi jua wamepata wapi hizo data,pili wanobishana kuhusu ugojwa wa mwakyembe sijui sumu,ripoti,sijui sabuni kwenye vyombo vya habari wanakosea sasa unataka rais naye aingie kwenye uchemfu huu,no research no right to speak sasa hao wanaosema lbd wanareseach zao
Nchi hii inafanya maamuzi based on research???toka lini???huko acha tu tusipaguse, kama tungekuwa tunafanya maamuzi based on the research results tusingekuwa hapa. Kimsingi sio sahihi watu mnatoka nyumba moja kuja kushangaana barabarani, kwani c mpo pamoja kwann hamkushangaana huko ndani ili huku nje mtoe kauli moja????Msemaji wa Wizara ni Manumba au Vuai???Iweje msemaji mkuu ashangae vitu vinavyofanywa chini yake???Vuai ndo alipaswa kuliongelea hili suala kwa marefu na mapana mana yeye ndo msemaji mkuu wa Serikali katika Wizara hiyo. Kimsingi anataka kusema kiti alichonacho hakimtoshi.
 
Kama kweli huyo binti alikufa katika mazingira ya kutatanisha mwili wake ulifanyiwa uchunguzi baada ya kufariki? Kama mwili haukufanyiwa uchunguzi polisi katika kulifanyia kazi jambo hili (kuugua kwa Dr.) walichukua hatua gani kwani naamini pamoja na mambo mengine naamini walipata taarifa hizi mapema sana. Kama itaamuliwa kuwa mwili wa huyo dada ufukuliwe na kufanyiwa uchunguzi wa kina hilo haliwezekani kufanyika kwa sasa?. Mambo mengine ya kuangalia kwa undani ni mazingira ya huyo dada kuhamishiwa kwenye ofisi ya Dr. Harrison na namna jambo hilo lilivyofanyika, waliohusika katika kufanikisha uhamisho huo ni watu gani ama ulikuwa ni utaratibu wa kawaida.

"UKIONA GIZA NENE FAHAMU KUWA MAPAMBAZUKO YANAKARIBIA"

mawazo yako ni mazuri sana lakini kwa tanzania hii hata 1 haliwezi kukupa jibu sahihi.Kwani wote wanaotakiwa kuchunguza na kufuatilia ishu hii wapo chini ya hao mapapa/vifaru ambao ndiyo wahusika wakuu.
Na mbaya zaidi ni kwaheshima na nidham ya ndiyo afande,mkuu kwa polisi.

Hapa mwenye siri na ukweli wa kifo chake ni MUNGU, waliopanga na waliofanikisha kifo na mwisho ni mwakyembe mwenyewe.
 
Sijui mjadala huu ni wa Kizalendo ama wa wale wenye mapenzi mema kwa Mwakyembe au ni wa aina gani. Napata taabu manake Mwakyembe alipokwenda India kwa mara ya kwanza kuna maneno yaliandikwa kwenye vyombo mbali mbali vya habari na kwenye mitandao kubwa likiwa tamko la Mwakyembe kuwa atakaporudi Nchini ataweka mambo hadharani; unfortunately mzee amerudi hilo halijafanyika worse enough karudi tena India katoa kitu wanachokiita "waraka wa siri" (nachukia sana hayo maneno) leo hii inakuaje kuitwa waraka wa siri ati kwa Familia, jamaa, ndugu, marafiki na watu wa karibu. Kwani yeye Mwakyembe hajui kwamba wakati huu Watanzania karibu wote wameshakuwa jamaa zake ama ndugu zake??

Kidogo hili kuingia akilini ni ngumu manake inawezekanaje watu waamue kukuvua nguo hadharani ila wewe nawe unapopata nafasi ya kuwavua nguo ati unaenda wavulia SIRINI kuna kitu hakijakaa sawa somewhere. Jambo hili limeshakuwa la Watanzania si la NYARAKA wala WARAKA wa SIRI. Watu wanaumiza kichwa kujadili sintofahamu yote hii na kweli wanaelekea kutofahamu chochote. Kila kukicha linaletwa jambo moja kati ya mambo maelfu yanayohitajika. Tatizo ni nini?? Anachoogopa ama anachokionea haya Mwakyembe ni nini?? Kama asipofanya yeye sasa hivi ili hatua zichukuliwe anategemea Familia yake itafanya lipi pasipo yeye kama atatangulia mbele za haki??

Mwakyembe azinduke upya na abatilishe ule waraka wake na auandike upya uwe ni "Waraka wa Mwakyembe kwa Watanzania wenzangu juu ya lile linalonisibu."

Ila katika haya yote nami pia nishawishika kusimamia yale ya Manumba mpaka hapo APOLLO watakapothibitisha vinginevyo manake nashawishika kuamini kuwa hata Mwakyembe mwenyewe hawezi ama ameshindwa kuwa reliable source of his own......
Kumbuka waliomfkisha Mwakyembe hapa alipo ni watanzania hao hao unaosema karibu wote wamekuwa jamaa zake. Mimi nadhan bado anawajibu wa kuwa makini mana leongo la waliofanya hivyo lilikuwa ni kumpoteza mazima, hivyo wanapoona anatoa kauli ni dhahiri wanajipanga kummalizia au wanajiskia vbaya sana. So mimi binafsi siishangai hatua yake ya kubana some info after all aliyemfikisha hapo bado hatujamjua so kujihami ni muhimu. Wananchi tumepotezewa sifa ya kuaminiwa na familia ya Mwakyembe kwa yaliyomtokea ndg yao, so tukubaliane na hali halisi.
 
Unasimama na taarifa inayosema hajalishwa sumu?hiyo tu inatosha kukamilisha uchunguzi makini? na wewe unasimama nao,duh!
 
Hamjamwelewa pasco? Anakusanya taarifa kutoka upande wa pili, maana yupo upande wa wasumishaji. Anakusanya info ili kuboresha mikakati yao
Nimeshazoea. Tutukanane, tudharauliane, tuhisiane mabaya, tunyoosheane vidole kuwa sisi ndio wahusika!. At the end of the day, ukweli utasimama!, na ndipo tutaheshimiana zaidi humu humu jukwaani!.

Kwa waliobobea kwenye practice ya saokolojia, kuna kitu kinaitwa "high state of mind sugestibility", ukiamini sana jambo fulani, linageuka ni ugojwa "pychosamatic desease" na symptoms of the real desease zinajitokeza!.

Nikiweka pure purified water kwenye glass, nikaiweka mezani, wewe akaja na kiu ukanywa hayo maji, baadae mimi nikazungumza na mtu pembeni kwa saiti ya chini, ili na wewe uwe una overhear kama namnong'oneza kitu kuwa
Yale maji pale mezani ni mkojo, ile nimeutia sumu ya kuondoa chumvi chumvi ili akinywa, ajisikie ni kama maji!.

Kama will power ya mwili wako iko juu, baada ya kuisikia kauli yangu, mwili wako utaingia kwenye hali ya "high state of mind suggestibility" na mwili wako utareact instanly kwa kutapika na kuishiwa nguvu as symptoms zote za sumu!, utakimbizwa hospitali, utapimwa, watakuta hakuna kitu!.

Kwa nini tunashadadia sana speculations wakati uchunguzi unaendelea Apollo na huku nyumbani waziri Nahodha ameinitiate forensic?!.

Mimi ni muumini wa kutafuta ukweli, wale waumimi wa kutafuta kweli, ni kweli tuu ndio itawaweka huru! "Seek the truth, and the truth will set you free".
 
Naikumbuka sana ile thread iliyoandika barua ya dr mwakyembe kwa IGP.
Kuna mahali alisema kuwa mpango wa kuwaua viongozi huhusisha na iman za kishirikina kwani wauaji hao huenda kwa sangoma kuwapumbaza watanzania ili mauaji yakitokea asipati kane wakuyashikia bango na tuwe kama wendawazim aonapo uchafu /takataka.

Tunaomba masangoma wenye ujuzi na wazalendo waipendayo tz waungane na kutegua bom hili lililotegwa na sangoma mwenzao

pia viongozi wote wadin mbalimbali waitishe mkesha mkubwa watu tufunge na kuomba mpaka tego/bom na mapepo yote machafu yatoke na kufungua fikra na akili za watz.

MUNGU IBARIKI TZ MUNGU TUBARIKI WATANZANIA
 
Tuondolee umalaya wako...

QUOTE=Radhia Sweety;3404613]Afrika ndivyo ilivyo, hata akifa Mandela watasema eti na yeye kawekewa sumu na Frederick de Clerk.[/QUOTE]
 
Bongo bana!!!

Yani Mwakembe anawekewa sumu, yeye analalamika kwenye magazeti tu!!!
sasa atalalamika huku ananyonyoka kama kuku....kama una hard evidence, kwa nini huendi mahakamani?!!
mwakembe, mwanasheria, ina maana ukitaka kukomaa na hii issue hutaweza kwenda mahakani?
kwa nn unataka huruma ya jeshi la polisi?
unafahamu jeshi la polisi ni hewa, kwa nini unakimbizana na hewa?

Hapa sasa, hii ni siasa tu!!!
 
The most flippant remark in this thread (in my book) it tops Pasco's and Sweety Radhia's.
Mkuu Mwendakulima, jf ni ukumbi wa mijadala, humu tuna ma great thinkers ambao huchambua ideas za watu, tuna ma ordinary thinkers ambao wao huzungumzia matukio, events na tuna ma simple minds ambao wao hukesha kuzungumzia watu!.

Badala ya kuchambua Pasco kasema nini, mtu anabaki kumzungumzia Pasco!. Wote wako right, ma great thinkers kwenye horizon zao, na ma simple mind pia kivyao, ila mwisho wa siku tutafika kwenye kweli isiyo na ubishi, simple na great alike!.
 
There were persons, I think they felt a burden of being blackmailed for their past wrong doings. Thats why even the government is silent !
 
wana jf

waziri wa mambo ya ndani NAHODHA hawezi kuja na report inayoeleweka...si yeye , si manumba wala wakiongozi yeyote anaweza kusema ukweli..mkakati wa kummaliza mwakyembe umesimamiwa na watu wakubwa serikalini.kwa sasa kinachofanyika ni kupindisha kila aina ya ukweli na kila mmoja kuongea la kwake hasa wanapoombwa kuongea juu ya ugonjwa mwakyembe.kikosi maalum kipo na kinahakikisha ukweli unapindishwa.
tanzania sasa hivi hakuna usalama wa taifa.usalamawa wa taifa umegawanyika katika makundi saba na kila moja linamtumika mtu flani.nchi haina salama wa taifa.mwaka jana wakati yuko india ilikuwa apelekewe sumu aina nyingine ikiwa ndani ya tube ya kuhifadhia dawa ya meno.hii ingemmaliza haraka sana.zoezi hili halikufanikiwa baada tube hiyo kuangukia mikononi wanausalama waliokuwa hawakubaliani na kitendo hiki cha kumpa sumu mwakyembe katika hatua za mwisho za maandalizi .

huo mwili wa huyo dada wakiufukua leo na wakapima watajua yeye aliuawa kwa sumu gani lakini kuufuka mwili wa huyu dada ni ngumu maana kuna kila aina ya hila inafanyika ili kuzima juhudi za kuujua ukweli mzima.si kwamba rais wa nchi hajui mchezo huu juu ya mwakymbe anajua sana na ni mhusika pia.hivyo msitarajie mapya.mwakyembe anaweza kusema yote lakini wahusika hawawezi kuchukuliwa hatua yoyote. the whole system is corrupt.totaly corrupt.nimefanya kazi kuanzia awamu ya mzee mwinyi lakini sijawahi ona mtu mkorofi na mlipa visasi kama kikwete, msitarajie atasema lolote maana na yeye ni sehemu ya maandalizi.

Taifa kama taifa hasa wananchi wa kyela wana haki ya kuujua ukweli juu ya mwakyembe lakini ukweli huo hauwezi kutolewa na serikali hii iliyoko madarakani.hata mwakyembe akisema na kuwataja hao wuhisika msitegemee lolote kufanyika dhidi yao.cha msingi na la muhimu ni watanznai kwa ujumla kupinga na kuikataa serikali hii.
 
Back
Top Bottom