Siri ya spika makinda kukwepa kugombea ubunge yaanikwa

2015 wanajua kunamziki,hata pinda muongo, hata gombea watuachie 2 cdm tuchukue nchi ili tuwatapishe vyooote walivyo iba.mungu niongeze uhai nijekushuhudia
 
Sisi tunaotoka ludewa tunamkubali deo filikunjombe japokuwa ni jamii ya magamba kwani ktk kipindi cha mwaka mmoja kafanya kazi ya miaka mitano ludewa, filikunjombe ni jamaa fresh.
 
"Tunamshangaa sana mbunge wetu Makinda kwa uamuzi wake wa kutangaza kutogombea .... kiukweli hata asingetangaza msimamo wetu wapiga kura wa jimbo la Njombe kusini japo hatukuweka wazi ila ilikuwa ni kumpiga chini katika kura za maoni sisi kwa sasa mbunge wetu ni kamanda wa umoja wa vijana wa chama cha mapinduzi (UVCCM) wilaya ya Njombe Deo Mwanyika ambaye amekuwa akiendelea kuhamasisha maendeleo jimboni "

Kuna mtu kanitonya kuwa, kule UVCCM, Deo Mwanyika anazuga tu, ila ukweli ni kwamba Deo Mwanyika naye kishasoma upepo kwamba CCM haikubaliki Njombe, kwa hiyo atagombea kupitia Chama Cha Magwanda. Welcome in board, Mwanyika.
 
kinachomuondoa ubunge sio tishio la cdm kukubalikajimboni kwake bali kazi aliyopewa na mafisadi inafikia ukomo na mafisadi wataangalia upepo ili kuona nani awe spika kwenye bunge lijalo. kipimo kilichotumika kumpimia sita ndio hicho hicho kitakachotumika kumuondoa makinda. nadhani atakuwa amesoma vizuri alama za nyakati na aina za siasa za chama chake. nimpongeze tu kuuona mwanzo wa mwisho wake katika nafasi yake ya uspika mapema!
 
hivi huyu bibi kaolewa naomba anaemjua vizuri anipe details zake...
Vipi mkuu unataka kutangaza uchumba ili uvifaidi vijisenti vya bajeti ya bunge? Huyu mama navyomjua hana mme wala mchumba na enzi zake wakati anasoma UD alikuwa kicheche wa kutupwa.
 
Maza hatogombea kwakuwa atakuwa mgombea mwenza wa urais c zamu ya zanzibar so bado ni chaguo la ccm kwa nafasi hy!
 
Nakumbuka kipindi Deo Mwanyika anatangaza nia ya kugombea, Makinda alimfuata na kulalamika , na hapa namnukuu " Mwanangu, mbona wewe huko unakofanyia unalipwa mahela mengi tu, sasa unakuja huku naju utachaguliwa, mimi sna kazi nyingine zaidi ya hii naomba basi unichie nimalizie" mwisho wa kumnukuu.
Ilibidi mzee Mwanyika aingilie na kumtaka kijana wake akae kando na kusubiri awamu ijayo.
Hivyo anachokifanya Makinda ni kutimiza ahadi aliyoitoa ya kumpisha Deo.
 
[h=3][/h]
Spika Anne Makinda
ZIKIWA zimepita siku chache toka mbunge wa jimbo la Njombe kusini Anne Makinda ambaye ni spika wa bunge kutangaza kutogombea ubunge tena katika uchaguzi mkuu mwaka 2015,mtandao huu wa Francis Godwin Mzee Wa Matukio Daima waibuka na siri nzito za mbunge huyo kuiogopa nafasi hiyo tena.

Baadhi ya wana CCM na mbunge wa jimbo la Iringa mjini Mchungaji Peter Msigwa(Chadema) wameanika siri hiyo ya Makinda kutangazwa kuto gombea kuwa ni kutokana na kuogopa kuja kung'olewa kwa aibu katika nafasi hiyo kutokana na uwezo wake mdogo wa kuwatumikia wapiga kura wake .

Huku wana chama wa CCM wa jimbo la Njombe kusini wakidai kuwa Makinda walianza kumchoka kutokana na kushindwa kufanya mambo ya kimaendeleo katika jimbo hilo na hivyo kusababisha jimbo hilo kuwa ngome ya chama cha Demokrasia na maendeleo (CHADEMA).

Kwani wamedai kuwa pamoja na jimbo hilo kuongozwa na mbunge Makinda ambaye pia ni spika wa bunge ila kasi ya maendeleo katika jimbo hilo haipo na kama jimbo halina mbunge kutokana na mbunge wao huyo kuonekana kuegemea mambo ya kitaifa zaidi huku jimboni kwake mambo yanakwenda kombo .

"Hatukutegemea jimbo la Ludewa ambalo mbunge wake Deo Filikunjombe ni kijana mchanga katika siasa kufanya mambo makubwa katika jimbo hilo kwa kipindi kifupi toka alipoingia madarakani uchaguzi wa mwaka 2010 .....huku mbunge wetu spika Makinda akishindwa hata kutengeneza barabara za jimboni kwake na kuwa barabara mbovu kuliko hata za wilaya ya Ludewa na zile za wilaya ya Makete" alisema John Sanga mkazi wa Njombe mjini

Alisema kuwa zamani jimbo la hilo la Njombe kusini bendera za vyama vya upinzani zilikuwa za kutafuta ila ukipita leo katika jimbo hilo la Makinda utitiri wa benderea za Chadema vijijini na mjini unaweza kufikiri ni ngome ya Chadema.

Sanga alisema kuwa hatua ya mbunge wao huyo kuwa mbunge wa kwanza wa CCM kutangaza kutogombea ni baada ya kuona hali ya upepo wa kisiasa kwake kuwa mbaya zaidi na hata akiwa katika ziara zake jimboni wananchi wamekuwa hawamkubali kivile.

Hata hivyo alisema jimbo la Njombe kusini ambalo mbunge wake Makinda limeendelea kuwa nyuma kimaendeleo na kupitwa na jimbo la Ludewa ambalo mbunge wake Fikunjombe ameendelea kufanya mambo makubwa katika jimbo hilo ukilinganisha na mbunge wao Makinda ambaye amekuwa ni mtalii katika jimbo hilo .

"Tunamshangaa sana mbunge wetu Makinda kwa uamuzi wake wa kutangaza kutogombea .... kiukweli hata asingetangaza msimamo wetu wapiga kura wa jimbo la Njombe kusini japo hatukuweka wazi ila ilikuwa ni kumpiga chini katika kura za maoni sisi kwa sasa mbunge wetu ni kamanda wa umoja wa vijana wa chama cha mapinduzi (UVCCM) wilaya ya Njombe Deo Mwanyika ambaye amekuwa akiendelea kuhamasisha maendeleo jimboni "

Kwa upande wake mbunge wa jimbo la Iringa mjini mchugaji Msigwa alisema kuwa Makinda ni sawa na mfa maji ambaye kimsingi haishi kutapa tapa kwani kauli yake ya kuwa wabunge nusu walitaka kujiuzulu kwa sakata la posho ni uongo mtupu na kuwa yeye ametumia kisingizio cha posho kuweza kueleza nia yake ya kutogombea ubunge ila ukweli Makinda amebanwa sana na Chadema katika jimbo lake.

Mbunge Msigwa alisema moja kati ya mikakati ya Chadema ni kuhakikisha inachukua majimbo mengi zaidi katika mkoa wa Iringa na moja kati ya majimbo ambayo ni rahisi zaidi kwa Chadema kushinda ni pamoja na jimbo hilo la Makinda ambalo wapiga kura wa jimbo hilo hawataki kabisa kusikia Makinda wala CCM.

"Makinda asijitetee kuwa anajiuzulu kwa ajili ya kupisha wanachama wengine kuongoza ama kwa ajili ya posho ya wabunge ....anapaswa kusema wazi kuwa jimbo hilo limemshinda kutokana na kushindwa kutimiza ahadi zake kwa wapiga kura wake"

Chanzo: Francis Godwin wa Iringa na matukio

Hapo ni kuruka mkojo na kukanyaga mavi wanakataa gamba kike na kukumbatia gamba dume cjui watakuwa wamefanya nini hivyo
 
Kwa hapa kwetu naona nafasi ya mbunge kuleta maendeleo ndogo sana wataishia kuikumbusha tu serikali lakini hawataweza kufanya mambo makubwa.

Ukitaka kujua kuna wabunge wanaofanya mambo makubwa nenda jimbo la babu ndesamburo pale Moshi ndo utaamini magamba wanatuhadaa tu
 
hivi huyu bibi kaolewa naomba anaemjua vizuri anipe details zake...

Kwa ninavyomwona anavyoliongoza bunge na kuzuia hoja za msingi ambazo ni faida kwa vizazi vijavyo sidhani kama ana mtoto na sidhani kama anaweza kuishi na mwanaume na kama anaishi nae basi atakuwa amemfanya mume *****
 
Kwa hulka ya Wanawake wa kabila la wabena ni kashfa mtoto wa kike kzalia nyumbani bila kuolewa tafsiri yake ni kuwa hakulelewakatika misingi na tamaduni za kibena ama atakuwa anatoka kwenye ukoo wa wachawi,wavivu ,wakorofi,wagomvi na mwisho atakuwa anatoka kwenye ukoo usio na heshima ,kwa alivyo Makinda si rahisi kuolewa enzi zetu ukitaka kuoa ukionyesha nyumba Wazee watakujibu kibena ''Khakha si vwakutolwa aho have.vwakali,vwahavi ,ama vwagata.''tafsiri yake ni kuwa hao si wakuolewa hao ni wakali,wachawi,ama wavivu kufikiri hao.

Kha kha yote hayo yanamhusu? So sad
 
Vipi mkuu unataka kutangaza uchumba ili uvifaidi vijisenti vya bajeti ya bunge? Huyu mama navyomjua hana mme wala mchumba na enzi zake wakati anasoma UD alikuwa kicheche wa kutupwa.

Wabunge wafukuzia posho wameanza kuona Bungeni pa chungu, kwani za Jairo hazipatikani, posho za vikao nazo zinapigiwa kelele. Wengi wa zamani watapakimbioa kwani walikuwa wanatumikia matumbo yao na siyo wananchi!
 
Kwani huyo Filikunjombe mnayemsifia amefanya nini cha pekee?
huyo Filikudzombe,kimsingi hata kwa bure hatakiwi Ludewa,mkoa mpya wa Njombe umepatikana.Mbunge wa magharibi yeye amejikatalia kuwa wananchi hawakumchagua bali NEC.Bibi yeye hakuchaguliwa kabisa bali ujanja ujanja alifanikiwa kupenye baada ya rafu kali.Mbunge wa Njombe kaskazini ni balaa la jimbo hata darasa la pili hakumaliza.Sasa kweli mkoa huu unaweza kupiga hatua?Makete nako hali mbaya mbunge wao ni mtalii.Nampenda kagame aje agombe ubunge kupitia CHADEMA Njombe kaskazini na kusini yote yaunganishwe.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom