Siri ya Shule za Seminari kufaulisha wanafunzi ni ipi?

Jamani naomba mwenye uelewa wa kwa nini Seminari za kidini (dini zote) wanafunzi wake hufaulu sana kwenye mitihani ya kitaifa? (CSEE & ACSEE) nimefuatilia matokeo yao kwa muda mrefu, naona ni watu ambao tunapaswa kujifunza toka kwao.

** Viongozi wetu wa dini hebu tupeni siri ya mafanikio.
Waalimu wa seminary wapo 'committed'.
 
Ushidani miongoni mwa wanafunzi. Walimu ambao wapo committed pia inachangia lakini kila kitu kinaanzia kwa wanafunzi. Wewe kama unamiliki shule jaribu kuwa tia morali wanafunzi ili wapende wanachokifanya. Vingine sasa vinafuatia kama mazingira etc.
 
Binafsi napata ukakasi kusema shule "inafaulisha" au "kufelisha" wanafunzi. Sababu ni kwamba kauli kama hizi zinaondoa nafasi ya mwanafunzi mwenyewe katika kufanikiwa au kutofanikiwa kwake.

Nionavyo mimi, wanafunzi wengi wa shule za seminari (hata hivyo sio zote) wanafanya vizuri kwa sababu ya nidhamu na juhudi binafsi za mwanafunzi, motisha na uwajibikaji wa walimu, pamoja na mazingira tulivu yanayomtanguliza Mungu.

Ni katika shule za dini (hasa seminari) na shule chache za binafsi ndiko mambo haya yote yanaingiliana na kutengeneza mchanganyiko mzuri (well blessed to make a homogenous mixture).

Gharama za kufanya hivyo ni kubwa sana (si pesa tu). Tukiona inafaa na tutaweza kuhusu tunaweza kujiiga.
 
Wanafanya mchujo wamaana laiti kama shule zakata zingefanya mchujo weny sifa wasingezidi 10
 
Unauliza Swali Ambalo Jibu Lake Lipo Wazi!!!
Hizo SEMINAR hazina lolote Bali Ubora Wao Mkubwa Upo KWENYE KUIBA MITIHANI tu!!
Mbona Wengine Walitoka na 1 Form4, cha Ajabu Ndani Ya Advance Walipojileta Government Tuliwasokota Vibaya.
Ni wizi wa Mitihani tu hao, Hawana lolote Mkuu.
 
Unauliza Swali Ambalo Jibu Lake Lipo Wazi!!!
Hizo SEMINAR hazina lolote Bali Ubora Wao Mkubwa Upo KWENYE KUIBA MITIHANI tu!!
Mbona Wengine Walitoka na 1 Form4, cha Ajabu Ndani Ya Advance Walipojileta Government Tuliwasokota Vibaya.
Ni wizi wa Mitihani tu hao, Hawana lolote Mkuu.
Uwe unakuja na ushahidi tu.
 
Sometime huwa wanafanya kagumashi ya paper JARIBU kufuatilia utagundua kipimo kizuri kawatafute vyuo vikuu kama wataendelea kufanya vizuri jibu hakuna vyuo vikuu vingi unakomaa mwenyewe no spoon feeding au kutengewa mezani kama baadhi ya seminari nizijuazo Mimi wanafikia kuhonga hadi gari ili paper itoke out.
 
Tuchukue watoto waliofaulu shule ya kata ya kawaida tuwapeleke seminary tuone kama watafundishwa wapate one wote, siri ni wao kuchukua watoto wenye uwezo mkubwa baada ya kufanya usahili wao na kuwabaini, hivyo vingine vya nizamu ni vigezo vidogo mno
 
Hata ubungo Islamic ni seminary nao wanaiba mitihani, kwani wangapi hutoka na1 government school na advance government hufeli? Acha wivu seminary za kikristo hutoa gifted and talented students nyie kalieni kuwahimiza watoto kukariri 36, wakati sisi watoto wanakalili laws kwenye physics
 
Unauliza Swali Ambalo Jibu Lake Lipo Wazi!!!
Hizo SEMINAR hazina lolote Bali Ubora Wao Mkubwa Upo KWENYE KUIBA MITIHANI tu!!
Mbona Wengine Walitoka na 1 Form4, cha Ajabu Ndani Ya Advance Walipojileta Government Tuliwasokota Vibaya.
Ni wizi wa Mitihani tu hao, Hawana lolote Mkuu.
Nyie karirini juzuu 36 wenzenu wanafaulu, eti kuiba mtihani! Hata sisi Azania tuliibaga mitihani ya six na zero zilikuwa kibao, tambua hata mtihani ukivuja mwenye akili ndio atafaulu sababu anavijua
 
kinachofanya wanafunzi wa seminari na ma-sister za kikatoliki kufaulisha ni;
1.Mtihani wa interview wa kuingilia kidato cha kwanza ambayo huwawezesha kuchagua ma-generous.
2.Sheria na utaratibu mzima wa shule husika.(kila kitu kufanyika kwa ratiba)mdogo wangu aliyekuwa akisoma st.franscis alienda kusoma muda wa kusali na alifukuzwa shule pamoja na wazazi kwenda kuomba mshamaha wale ma-sister waligoma katakata.
3.Hawapokei watoto wanaohamia.walioanza nao ndio wanaendelea nao bila kusahau mchujo wa hali ya juu passmark ni 60 mf. shule ya Bethel mafinga.(kwa shule zetu za kayumba mtu akipata wastani wa 60 yaaani huyo ni kipanga lol)kwa shule ya bethel ukimpeleka tution mtoto wako wakati wa likizo na sister akapata ubuyu ndio basi mwanao anafukuzwa shule haijalishi ana akili kiasi gani
4.Shule za seminari hawapo kibiashara. kuna mwaka seminary ya mafinga,wanafunzi kidato cha nne waligoma.walifukuzwa wote! mwaka huo hapakufanyika mtihani wa kidato cha nne.huwezi amin wanafunzi wale wengi wao wakaenda shule ya jeshi ,kawawa. kwa mwaka ule ile shule walipanda sana rank ya kufaulisha kitaifa. lol
5.wao husoma o'level kwa miaka 5 ukijumlisha na PRE-FORM ONE pia wana misingi mizuri ya lugha ya kiingereza.
6. wengi wao hulazimishwa kusoma somo la bible-knowladge ambao hupata grade A ambayo huwapandisha division. na kufanya ufaulu wa shule kuwa mkubwa.
NAOMBA KUWAKILISHA. SAMAHANI KWA MWANDIKO MCHAFU. WASALAM.
 
Back
Top Bottom