Siri ya Shule za Seminari kufaulisha wanafunzi ni ipi?

Michewen

JF-Expert Member
Jun 27, 2012
24,553
32,175
Jamani naomba mwenye uelewa wa kwa nini Seminari za kidini (dini zote) wanafunzi wake hufaulu sana kwenye mitihani ya kitaifa? (CSEE & ACSEE) nimefuatilia matokeo yao kwa muda mrefu, naona ni watu ambao tunapaswa kujifunza toka kwao.

** Viongozi wetu wa dini hebu tupeni siri ya mafanikio.
 
MAVAZI gani hayo mkuu? unajua saa nyingine hizi zinazoitwa seminari (kuna za ukweli na Uchwara). Uchwara mara nyingi huangukia pua kwenye matokeo ya fom4 na fom 6. Kwa mfano ile JUNIOR SEMINARI pale MORO au AGAPE SEMINARI - Marangu zipo hoi sana.
NB: Nyingine jazia nikiandika zote hapa nitaonekana mchonganishi, na mwezi wa toba huu.
 
1. Mazingira mazuri ya ufundishaji na ujifunzaji
2. Social welfare ziko vizuri
3. Time management (na hapa ndipo taasisi nyingi za umma zinapochemka kila mtu anaunda sub-time table yake)
4. Uongozi mzuri na mahusiano mazuri baina ya watumishi, watawala na wanafunzi jambo linalojenga ari ya kujituma miongoni mwao.
5. Nidhamu ya hali ya juu kwa msaada wa Mungu (kwa imani zao); shule za umma zimekuwa hazina mkazo katika mambo ya elimu ya dini ambayo huwafanya wanafunzi kuwa na hofu ya Mungu na kuwa na nidhamu.
6. Maslahi mazur kwa watumishi
7. Mchujo kutoka darasa moja kwenda jingine; hii huwafanya kuwaondoa slow learner na kubaki na wale "golden one". Lakin katika shule za umma wote slow learners na fast learners hulazimika kubaki na hakuna kumrudisha nyuma darasa hata kama uwezo wake unaonekana hauridhishi (na hapa ndipo kosa kubwa lilipo)
 
Ni ukweli usiofichika kuwa taasisi za kanisa tajwa zimejipambanua kwa huduma bora na kuzalisha wataalamu katika fani za UONGOZI, ELIMU na AFYA. Hii ni mifano tu ya taasisi hizo.
1. Seminari zote za katoliki
2. Vyuo vya Udaktari na Uuguzi (Bugando, Ifakara n.k)
3. Vyuo Vikuu ...SAUT n.k.
Asanteni sana Kanisa katoliki kwa kutupa kilicho bora kabisa.
 
Jamani naomba mwenye uelewa wa kwa nini Seminari za kidini (dini zote) wanafunzi wake hufaulu sana kwenye mitihani ya kitaifa? (CSEE & ACSEE) nimefuatilia matokeo yao kwa muda mrefu, naona ni watu ambao tunapaswa kujifunza toka kwao.

** Viongozi wetu wa dini hebu tupeni siri ya mafanikio.
Ukiacha sababu zilizotajwa na wachangiaji wengine, shule za seminari zinafanya vizuri kwa sababu moja kubwa tuu ya kuchagua wanafunzi bora kupitia interview, mara nyingi shule hizi hazichukui vilaza kwa kuogopa kuchafua jina la shule wakati wa matokeo, laiti zingechukua wanafunzi wa uwezo wa kawaida naamini zisingeweza kuongoza mara nyingi hivyo.
 
Usilojua usiku wa Giza fuatalien vzr sio kubuni kuna ya kapetin ndo maana huyu mwenye div one akienda govnmnt anazingua vby.
 
Back
Top Bottom