Siri ya SHEIN

normal_DSC_1224.JPG


Makamu wa Rais Dk Ali Mohamed Shein akiangalia Bidhaa za aina mbali mbali za futari wakati alipotembelea katika soko la Kawe Dar es salaam kufuatia ziara yake ya kuangalia bei za bidhaa hizo katika masoko yaliyomo ndani ya Wilaya ya kinondoni ambapo bei za bidhaa hizi zimepanda kwa kiwango kikubwa kulinganisha na bei za awali.
 

Unaua JK mtu mbaya sana

huyu jamaa bwana kapewa role ya ajabu kweli kweli

naamini haya usama wa taifa haupati naye taabu

akienda kazini kule anakuta tayari ana mkasi wake

akitoka kazini ni msikitini au kenda nunua Nyama au Nazi

kisha Huyooo home
 
normal_DSC_0479.JPG


Makamu wa Rais Dk Ali Mohamed Shein akikata utepe kuashiria ufunguzi rasmi maonesho ya 14 ya kimataifa ya kilimo yanayofanyika Mkoani Arusha leo kuli ni Waziri wa Kilimo na Chakula Mh Steven Wasira.
 
SHEIN FOR PRESIDENT

si mla rushwa

hana makuu

ni mpole

msomi

hachanganyi kazi na masuala ya serikali

huyu ananikumbusha mzee IDRISSA ABDUL WAKIL

 
Brazameni yaani mtundu kama nini!

Hizi picha zinanikumbusha mbali kweli!

VP ila kweli ni Mswalihina na sii mla rushwa!
 
Wakti mwingine ni vizuri tukawa na utani na tunacheka, inasaidia kiafya.

Hii ni budi mheshimiwa VP aelewe.
 
brazameni
kwikwi kwi !
nimecheka kweli mpaka mbavu zinaniuma kwa hiyo kazi ya makamu ni kufungua na kukagua au...
 
SHEIN FOR PRESIDENT

si mla rushwa

hana makuu

ni mpole

msomi

hachanganyi kazi na masuala ya serikali

huyu ananikumbusha mzee IDRISSA ABDUL WAKIL


Kweli kabisa, Kikwete amwachie Shein nchi sasa kwa hiyo miaka miwili na nusu iliyobakia.
 
yaani tangu wiki iliyopita sijacheka kama nilivyocheka leo hadi mishipa ya masikio inauma, uso umenipauka na nywele zinanyonyoka!

Angalau yeye anafungua vitu halafu anaishia zake kwenda kufungua kingine, kinachofuata baada ya hapo lwao!
 
Priceless..mwacheni mzee wa watu amalize muda wake ale pension yake ...kwa kweli nimecheka sana leo
 
ndio maana silali bila kupitia hapa JF. Nimecheka mpaka machozi yamenitoka. Kwamba akiingia ofisini anakuta mkasi wake upo mezani, anaubeba huyooo anaingia kwenye misele.....kwi kwi kwi! JF nimeamini ni kila kitu. Kumbe mtu anaangaliwa weee, baadae watu wanakuja na posti yake.
 
Wakti mwingine ni vizuri tukawa na utani na tunacheka, inasaidia kiafya.

Hii ni budi mheshimiwa VP aelewe.

wewe unasema UTANI? mzee hu si utani hata kidogo jamaa ana mikati mitatu mmoja uko ofisini na miwili iko kwenye gari lake sasa sijui wataka nini tena !

hapa hakuna utani hata kidogo

kuina jamaa aliniambia kuwa katika wafanyakazi wa serikali wanao enjoy basi ni wale uslama wa Taifa wa VP

Jamaa kwanza ukienda kumfuata ofisini hana yale mambo yatu ya kupeana vimemo vya kazi...yuko very open atakuambia ukiwa na mambo BINAFSI wewe njoo nyumbani

matokeo yake watu huwa hawamfuati ofisni kisa? Hutopata ukitakacho...kama ni kazi atakuambia subiri magazeti kisha fuate taratibu yaani procedures za hiyo kazi sasa tofauti na wenzie akina Maghufuli na Karamagi wao kutoa vimemo kwenda Human Resources ni norm

Pili atakaa ofisini mpaka saa nne hivi kisha Huyoooooo o course bila kusahau MKASI wake mara utamwona yuko YOMBO DOVYA anakagua mbuzi mara mchana utamwona KITUNDA mara jioni utamwona MBAGALA reli anakata utepe tuuu


Tatu huyu mtu hana majivuno na gharama yake kubwa ni mswala wake tuuu mkewe kama mjuavyo ni nadra sana kumwona kwenye picha na husikii mkewe kaenda Korea sijui kwenye magongamano ya wainjilisti kama mkewe JK na wala husikii kama mkewe ana uswahiba na ROSTAM kama mkewe bwamkubwa


Nne, Huyu jamaa anaishi maisha very modest, kwanza jamaa yuko kwenye swaumu almost the whole week kasoro Ijumaa sasa hata yale mambo ya kula kula ovyo hana suti zake ni zile zile yaani kusema ukweli kama atakuwa na binti umri wa kuoa basi mie niko tayari kwenda kupeleka posa maana huyu ndio ukisikia FATHER IN LAW ndio huyu bwana


Tano akishswali tu saa mbili usiku ni KITANDANI for very simple reason: Wale jamaa liaowaambia wakiwa na mambo yao binafsi wamfuate nyumbani nao wanamjua jamaa ni BOARER na hupati chochote..contrary to Muungwana ambaye kulechelewa kulala ni wajibu kwani atakutana na watu wee kisha kuna hilo suala la kutanzamayaliyojiri JF


Sita, huyu bwana ni msomi lakini hana mijivuno na narudia kusema huyu ananikumbusha MZEE IDRISSA ABDUL WAKIL


Halafu mnauliza eti viongozi waadilifu wako wapi...huyo hapo tunaye and we should not make a mistake this is our guy
 
Brazameni.. stop!!! yaani nimeingia hapa nimeikwepa kwepa hii thread ili nipate msosi kwanza.. sasa nimeiangalia hizo sababu zako nimecheka hadi nimepelewa... maana unaweza kuua maana sababu zinaingia akilini!

Halafu nikiangalia na hizo picha ninaamini unasema kweli. Sasa mwenzio mbavu sina maana nimecheka hadi kibasikweli changu kimepinduka nikabingirika huku miwayawaya ya kompyuta imenizunguka!!

shemeji yenu mdogo kuniona akafikiri nataka kujiua!! sasa.. ni kasheshe!! ananiuliza kumetokea nini Tanzania?...
 
Back
Top Bottom