mchemsho
JF-Expert Member
- Jun 8, 2011
- 3,212
- 867
Inawezekana kuna mambo ya kishirikina ndani yaki, lastime kuna waliokuwa wanasema yule kiongozi wa Mwenge at last lazima anakufa sijui kama lina ukweli hili.
Kuna wazee fulani pale Kilimanjaro maeneo ya Kiboriloni(kwa sasa hawapo tena) walikuwa wakisikia mwenge unakuja Moshi walikuwa wanaondoka maeneo ya hapo wanaenda huko milimani suala ni kwamba wasiuone tu huo mwenge mpaka utakapoondoka na wanasema walikuwa wakiamini kwamba ukiuona Mwenge unaweza kupata nuksi, balaa, mikosi na vilevile kuna mambo makubwa ya kishirikina yanafanyika.
Sisi vijana wa leo tujiulize Mwenge una faida gani kwa mwananchi na nchi wa/ya Tanzania?
unachosema mkuu acheche kina ukweli, nakumbuka 2007 nilikuwa najitolea kufundisha shule flani kijijini kwetu, mwenge ukaja kuzindua jengo la bweni la wasichana, nilipewa assignment ya kuandaa ndoo ya mchanga na kuupeleka staff room, baada ya mwenge kufika ulioelekwa ofisini kisha ukazungukwa na wanajeshi, then ulizimwa halafu wakamwaga majivu na(mchanga?) kwenye mfuko, kisha wakaweka tena mchanga kidogo kutoka kwenye ile ndoo kwenye ule mwenge, ukawashwa shuguli za uzinduzi zikaendelea. nilipouliza hakuna aliyenipa jibu zaidi ya kusema kuwa baada ya kuhitimisha mbio za mwenge mchanga ule na majivu yale yaliyokusanywa nchi nzima huwekwa kwenye chombo kimoja na kusemewa vineno hv, then hutupwa baharini, ati ili kudumisha muungano...