Elections 2010 Siri ya Mshahara wa Rais na Marupurupu ya Rais Wastaafu...

Aliyeamua kufanya siri mshahara huo ni Mkapa baada ya kuuongeza mshahara huo na marupurupu mara tu alipoingia madarakani hakutaka Watanzania tuujue.

Bubu nakubaliana na wewe kabisa kwa hili kwani nakumbuka mshahara wa mzee Ruksa umewahi kuandikwa gazetini a month or 2 kabla ya kumaliza kipindi chake na ilikuwa kilo nne (400,000) kama nakumbuka vizuri.
 
Macinkus,
Kama ungeweza ku-scan na kuipost angalau some few pages ingesaidia sana kama kaushahidi wa uliyosema ili mjadala upanuke zaidi.

natayarisha scan ya kurasa za ofisi ya rais kwa miaka mitatu tofauti na kuibandika hapa.

macinkus
 
Macinkus,
Kama ungeweza ku-scan na kuipost angalau some few pages ingesaidia sana kama kaushahidi wa uliyosema ili mjadala upanuke zaidi.

nipatie email yako nikutumie ukurasa moja wa hicho kitabu cha mishahara nk. ukipenda unaweza kuiweka jamvini.

macinkus
 
Nakubaliana na hoja hizi.

Mishahara ya viongozi ni Kodi ya Wananchi wa aina zote. Haipaswi kuwa siri. Mishahara ni malipo kwa shughuli zilizofanyika. Kazi inaweza kupimika kwa vipimo na vigezo vinavyoweza kuwekwa na kukubalika. Iwapo na mshahara utajulikana kuna uwezekano wa kupima kama Mshahara huo unastahili kwa uwajibikiji unaohusika.

Nakumbuka nilipoingia Bungeni Mshahara wa Rais bado haukuwa siri, sielewi ni kitu gani kimetokea. Mabadiliko hayo yalitokea pamoja na kubadili pia mfumo wa uandikaji wa Vitabu vyetu vya Bajet yaani Volumes 11 hadi lV. Kwa mfumo wa sasa ambao kimsingi umefumba sana, si rahisi hata kwa Wabunge kuisimamia Serikali kama inavyotakiwa na Katiba Ibara ya 63(3).

Majadiliano haya yanatupanua wote wenye nia njema na nchi hii na ninahakika pressure itajijenga kutumia mfumo wa Bajet ulio wazi zaidi. Tukaze mwendo kudai mabadiliko mengi kuelekea Transparency katika nchi yetu. Nina hakika wote wanaofuatilia masuala ya Bunge wakati Bunge likikaa kama Kamati ya Matumizi wanaona kinachofanyika hakina tofauti na mchezo wa kuigiza.

Watanzania ni haki yenu kupata hizi Taarifa, ni wajibu wenu kuzidai. Waliobahatika kufika Zambia, Mauritius, India wanafahamu mfumo wa Bajet ulivyo 'simple' lakini very Transparent wenye kuruhusu Bunge kwa niaba ya Wananchi kusimamia.

Mathalan, Safari za Rais zinajulikana ni ngapi za mwaka, zikitokea za ziada, zinaelezwa ni zipi na kwanini ili kupata idhini ya Bunge kwa fedha zilizotumika ambazo hazikuidhinishwa na Bunge. Kwetu ukiomba hiyo ni sawa na uhaini. Ukiuliza safari za Mawaziri au kiongozi yeyote wa Serikali na hasa ukitaka ku 'tie up' safari hizo na tija inayoambatana nayo unatazamwa kama mhaini. Kuna mafungu tunayaidhinisha kwa Mabilioni bila maelezo lakini mafungu mengine hata ya Shs 2,000,000 yameonyeshwa.

Kuna swala linafungwa fungwa hasa kuhusu masuala yanayohusu majeshi yetu. Ni dhahiri kabisa hakuna mzalendo yeyote anayetaka masuala ya mikakati ya ulinzi wa nchi au ya usalama wa nchi kujadiliwa hadharani. Lakini masuala ya matumizi ya kawaida ya fedha hata kama ni jeshi au chombo chochote cha usalama hata siku moja hayatakiwi kuwa siri, kwa sababu uwizi/ubadhirifu,ufisadi yanaweza kutokea kwa kisingizio cha Ulinzi na Usalama wa nchi kumbe hoja hapa ni uhalalishaji tu wa Ufisadi mkubwa. Watanzania tunahitaji kuwa macho katika kulinda rasilimali zetu.

Fedha zinazoidhinishwa na hivyo kukusanywa kutoka kodi zetu ni nyingi sana. Ni lazima tuwe wakali katika kuzilinda ipasavyo, alimradi tunafuata taratibu za kawaida za Transparency. Tuko mbali sana na lengo hili. Kwamba hatukufuka leo haina maana kuwa hatutafika na au tusipige hatua ya kwanza kuelekea huko. Inahitaji moyo.
 
Nyinyi, Bunge la Tanzania, mmempa Raisi nguvu ambazo hata Mola hana.

Mmeandika sheria inayosema "Rais asilipe kodi."

Mmeandika sheria inayosema mtu hashitaki, hashitakiwi kama Raisi hapendi, kwa kupitia nguvu alizonazo juu ya DPP. Yani Raisi anaweza kuruhusu uvunjaji sheria.

Hata Mungu hajajiruhusu kuruhusu dhambi.

Raisi wa Tanzania ana nguvu wanasheria wanaziita "plenary powers." Anaweza kufanya lolote lile na huwezi kumuuliza, hata mshahara wake ni nini.

Tushukuru Mungu hajaja Dikteta muua watu hapa, kwa sababu sheria za Tanzania zingemrahisishia. Yani tuko primed, tumewiva kwa mazingira hayo ya Kidikteta japo hayajaja. Tushukuru Nyerere, Mwinyi, Mkapa na Kikwete wamekuwa binadamu katika hilo. Kuna siku litakuja jitu hapa lita abuse hizi sheria.

Sio lita abuse, litatumia, hizi sheria, litaanzisha unduli hapa.

Bunge lenu lina hatia kuandika hizi sheria.

Ni wapi duniani Raisi halipi kodi?
 
..sheria ya mafao ya viongozi wakuu wastaafu ilipitishwa wakati Salim Ahmed Salim akiwa Waziri Mkuu.

..tena walielekeza kwamba mafao hayo yatawahusisha Rashidi Kawawa na Cleopa Msuya ambao wali-serve kabla ya sheria kupitishwa.

..nadhani ilikuja kurekebishwa tena wakati wa Ben Nkapa na Frederick Sumaye.

Dr.Slaa,

..taifa linatumia fedha nyingi sana kuhudumia safari za viongozi wakuu, pamoja na mawaziri.

..bajeti ya misafara ya viongozi wakuu iko chini ya wizara ya mambo ya nje.

..nakumbuka wakati Sumaye akiwa waziri mkuu wabunge walimsumbua sana kutokana na matumizi ya sh mill 500 kwa safari ya USA.

..hakuna mbunge aliyehoji misafara ya Mkapa ambayo kwa kweli ilikuwa mingi na mikubwa kuliko ule wa Sumaye.

..sijui kama ulikuwa ni uoga wa kumkabili Mkapa, au kitu kingine, kilichosababisha hali ile.

..hata suala la ufisadi wabunge na waandishi walikuwa wakimuandama Sumaye kwa kashfa ya shamba la eka 7 kibwaigwa na kumstahi Mkapa huku akijizawadia mgodi wa Kiwira.

..i am seeing the same trend sasa hivi. imefika mahala tuache kuoneana aibu.
 
Ya nini tuandikie wino wakati mate yapo.......I mean mate wakati wino upo...
Pale utumishi yuko mama mmoja anaitwa mama"....". Anaweza kwenda kuchungulia na kutuambia Specific figure, sio tunagesigesi tu hapa. Maana ni lazima utakuwa umeandikwa mahali. I'll get back to you......

Bado twakusubilia ndugu..
 
Wakoloni walipo ondoka Tanganyika, walituachia kitabu kilichoitwa Staff List. Kilikuwa kinachapishwa mara mbili kwa mwaka na wizara ya Utumishi. Nilicho nacho cha mwish kuchapishwa ni cha 1972. Maafisa wote wa serkiali walikuwa wanaandikwa kwenye kitabu hiki. Taarifa zifuatazo zilikuwamo: mshahara, tarehe ya kuzaliwa, ya kuajiriwa, elimu, mahali alipo, jinsia, hali ya ndoa nk. Sijui kulitokea nini baada ya hapo, kwani sijakiona tena kitabu hicho tangu kufariki kwa ofisa aliyekuwa anashughulikia uchapishaji wake (marehemu Hussein Haji). Ukurasa wa Ikulu wa mwaka 1972 kwa mfano, unasomeka ifuatavyo:

Basic Salary Appointment Name BirthDate Station Date of Appointment Remarks
Per annum marital status
48,000 President m Mwl J.K.Nyerere D’salaam 9.12.62
M.A. LLD (Edin.) 1922

56,000 1st VP mSheikh A.A.Kaarume Zanzibar 27.4.64
48,000 Minister m A.Jumbe Zanzibar 27.4.64
of State
48,000 Minister of m Sheikh A.M.Mwinyi D’salaam 6.11.70
State
50,000 Princ Sec m D.A Nkembo B.A. D’salaam 13.3.56
(Lond) 28.6.30
Orodha hii ilikuwa nik kwa wizara zote.Wakati huo kulikuwa hakuna watumish hewa.

Macinkus

Imepinda, Nyerere hakusoma M.A LLD (Edin) alisoma Economics and History.
Halafu Makerere alisomea stashahada au shahada?

The wikipedia page needs some editing, wanasema Nyerere alikuwa Mtanzania wa kwanza kusoma katika a British University, kwanza Tanzania haikuwapo, halafu hata kama unaongelea Tanzania ya leo kuna mzee wao kina Mwapachu alisoma Uingereza miaka ya 1920's.

http://en.wikipedia.org/wiki/Julius_Nyerere
 
Only in Africa......na ndio Miafrika Ilivyo.....

Inakuwaje hatujui mshahara wa raisi? It doesn't make sense na sijasikia libunge hata limoja lililopendekeza muswada kubadili hiyo "sheria" inayosemwa ya mshahara wa raisi kuwa siri au misheria mingine ya kijinga kijinga......

FMES said it best: viongozi wetu ni reflection yetu sisi wenyewe. Miviongozi mijinga na mianainchi na yenyewe mijinga vile vile. And I emphatically stand by my statement.
 
Nyinyi, Bunge la Tanzania, mmempa Raisi nguvu ambazo hata Mola hana.

Mmeandika sheria inayosema "Rais asilipe kodi."

Mmeandika sheria inayosema mtu hashitaki, hashitakiwi kama Raisi hapendi, kwa kupitia nguvu alizonazo juu ya DPP. Yani Raisi anaweza kuruhusu uvunjaji sheria.

Hata Mungu hajajiruhusu kuruhusu dhambi.

Raisi wa Tanzania ana nguvu wanasheria wanaziita "plenary powers." Anaweza kufanya lolote lile na huwezi kumuuliza, hata mshahara wake ni nini.

Tushukuru Mungu hajaja Dikteta muua watu hapa, kwa sababu sheria za Tanzania zingemrahisishia. Yani tuko primed, tumewiva kwa mazingira hayo ya Kidikteta japo hayajaja. Tushukuru Nyerere, Mwinyi, Mkapa na Kikwete wamekuwa binadamu katika hilo. Kuna siku litakuja jitu hapa lita abuse hizi sheria.
Sio lita abuse, litatumia, hizi sheria, litaanzisha unduli hapa.

Bunge lenu lina hatia kuandika hizi sheria.

Ni wapi duniani Raisi halipi kodi?

Kuhani naona unasahau Mwembechai, Zanzibar, BOT, EPA, Meremeta etc etc.

Si ndiyo uvunjaji wa sheria wenyewe huu ambao watu wana cite presidential privileges kuwa protect marais na marais wastaafu?

Tena mpaka wengine wanasema waliogopa kuondoa "heshima ya serikali"? Walisema jiheshimu utaheshimika, mtu asiyejiheshimu, mwizi, mlafi, muuaji hafai kuheshimiwa na kupewa perks zote hizi.
 
Wait a minute...Nina kaswali hapa...Hiyo pension ambayo amelipwa Mkapa na ambayo inazidi hata mshahara wa Kikwete wa miaka miwili amechukuwa lini?(24 months=2 yrs)

Naomba tuanzie na hapo kwasababu hiyo ni kiji allowance tu bado asilimia 50 ambayo ni nusu ya mshara aliokuwa akiupokea pamoja na kwamba mshahara wake una fikia aslimia 80 ya mshahara wa JK!

HII NI KUFURU!
Mkapa also received a winding-up allowance of a sum equal to the amount that would be received as salary in 24 months by incumbent President Kikwete.

The current Political Service Retirement Benefits Act, passed by the National Assembly in 2000, spells out a generous package of retirement perks for the former president, including an annual pension granted monthly of a sum equal to 80 per cent of the salary of incumbent President Jakaya Kikwete.

Furthermore, after leaving public office, he was entitled to receive a gratuity of a sum equal to 50 per cent of the total sum received by himself as salaries during his entire ten-year tenure as head of state from 1995.

Makubwa!
 
Pamoja na mambo mengi ambayo ni kero kwa sababu serikali haiyaweki wazi, mshahara wa rais unapaswa kuwa wazi, may be hata wale wanaokimbilia ikulu wataacha.
 
Mkapa pia aliomba na kupewa travelling allowance ya $10 million. One million for every year he was in office.
 
Wakoloni walipo ondoka Tanganyika, walituachia kitabu kilichoitwa Staff List. Kilikuwa kinachapishwa mara mbili kwa mwaka na wizara ya Utumishi. Nilicho nacho cha mwish kuchapishwa ni cha 1972. Maafisa wote wa serkiali walikuwa wanaandikwa kwenye kitabu hiki. Taarifa zifuatazo zilikuwamo: mshahara, tarehe ya kuzaliwa, ya kuajiriwa, elimu, mahali alipo, jinsia, hali ya ndoa nk. Sijui kulitokea nini baada ya hapo, kwani sijakiona tena kitabu hicho tangu kufariki kwa ofisa aliyekuwa anashughulikia uchapishaji wake (marehemu Hussein Haji). Ukurasa wa Ikulu wa mwaka 1972 kwa mfano, unasomeka ifuatavyo:

Basic Salary Appointment Name BirthDate Station Date of Appointment Remarks
Per annum marital status
48,000 President m Mwl J.K.Nyerere D’salaam 9.12.62
M.A. LLD (Edin.) 1922
56,000 1st VP mSheikh A.A.Kaarume Zanzibar 27.4.64
48,000 Minister m A.Jumbe Zanzibar 27.4.64
of State
48,000 Minister of m Sheikh A.M.Mwinyi D’salaam 6.11.70
State
50,000 Princ Sec m D.A Nkembo B.A. D’salaam 13.3.56
(Lond) 28.6.30
Orodha hii ilikuwa nik kwa wizara zote.Wakati huo kulikuwa hakuna watumish hewa.

Macinkus

..wazee mtu aliyekuwa akilipwa shilingi 50,000 mwaka 1970.....zilikuwa pesa nyingi sana...nyumba ya kawaida ya room 3 mwaka 1970 iliweza kujengwa kwa shilingi 25,000 tu...nyumba ya namna hiyo leo inaweza kujengwa kwa milioni 15...naongelea nyumba za mwananchi wa kawaida...

kwa kifupi mshahara wa 50,000 mwaka 1970 ..leo unatakiwa usipungue milioni 30 kwa mwezi...that is if you use simple arithmetic...kwani miaka hiyo mfanyakazi msomi wa kawaida unapokea tsh 2,000..na pesa inatosha kabisa kutunza familia ya watu wanne na kusaidia ndugu kijijini ...na still ukifika mwisho wa mwezi mishahara inakutana..unaweza kubakiwa na shilingi hadi 500..ukawena banki!!!
 
Imepinda, Nyerere hakusoma M.A LLD (Edin) alisoma Economics and History.
Halafu Makerere alisomea stashahada au shahada?

The wikipedia page needs some editing, wanasema Nyerere alikuwa Mtanzania wa kwanza kusoma katika a British University, kwanza Tanzania haikuwapo, halafu hata kama unaongelea Tanzania ya leo kuna mzee wao kina Mwapachu alisoma Uingereza miaka ya 1920's.

http://en.wikipedia.org/wiki/Julius_Nyerere

sijui kama tuiamini wikipedia au rekodi ya utumishi rasmi ya serikali ambayo unaweza kuiona kwenye kiambatanisho cha thread "utumishi wa umma -mishahara" ambayo imo humu leo. tafadhali iangalie ina rekodi tangu 1964.
macinkus
 
Haya mafao mbona ya kawaida tu kama mtu angekuwa mwadilifu? Tatizo la huyo mzee ni kukosa uadilifu. Nyie mnataka Rais mstaafu akauze karanga ili aishi au aingie jikoni kujipikia? Give me a break! No country in the world will fail to give these to its ex-President.

He has to deliver to his/her own people at least. Kuna watu Tanzania hii hawako affected na chochote ukianzia bajeti ya nchi mpaka hao wawakilishi wenyewe. Coz they dont feel their presence no more except for a certain class of people. You got that.
 
Mimi nafikiri hamna tatizo kwenye marupurupu ya rais kama yeye binafsi anajieshimu na kulitumikia taifa kwa uhadilifu mgogoro unakuja pale ambapo anakuwa fisadi wa mali za umma halafu akistaafu aendelee kulipwa mapesa kibao kwa jina la marupurupu ambayo alitakiwa kulipwa rais mwadirifu.
 
Bora hao mpresida wajue kwamba tunatafuta mishahara yao bado. Hata hivyo najua ni kuubwaa saanaaaaaaaaaa.

Sujui kwa nini wafanye tena business hujo ikulu na kujichotea mathusand of million dollars
 
Nijuaavyo, wakati mwinyi anaondoka mshahara pamoja na marupu rupu ya raisi kwa mwezi ilikuwa Milioni 30. Sina hakika kama kuna mabadiliko yalifanywa wakati wa mkapa
 
Back
Top Bottom