Siri ya Magufuli kuogopa kuigusa IPTL ambayo inalipwa milioni 400 kwa siku na TANESCO

Ndiyo. Sioni sababu ya kulalama humu wakati kuna waliotoroka ccm na kutuambia ukweli wakati wa kampeni ili tuihukumu kwenye sanduku la kura. Na wapiga kura walinogewa na ladha ya chumvi ya sh. 300 na T-shirt na vijikofia wakapuuzia na kuwabeba wezi walewale kwa mara nyingine. Wacha watumalize kabisa huenda tutapata wazo la pamoja tutakapokuwa ndani ya kontena tukipekekwa china kuchomwa mishkaki na soseji.
usilaumu mkuu,swala la kupiga kura ni hatua ya kwanza lakini hatua ya pili nani atatangwazwa mshindi ni kitendawili hukumbuki Rais mstaafu alivyosema kwamba sizihitaji kura za wafanyakazi wewe unahisi alikuwa anamaanisha nini? huku Afrika kupiga kura ni kutimiza wajibu tu, lakini kimsingi haina maana,wewe unafikiri unapoambiwa kura ni haki yako unayaamini hayo maneno? kura haki yako nani kakuambia?
 
ilo suala kwa sasa liko jikoni magufuli analichambua ila wewe mtoa post unatudanganya kwa kusema kuwa tz inawalipa milioni 400 kwa siku huo ni uongo iyo ishu alishaizungumzia zitto kabwe ukiyaka kujua ni sh ngapi tz hulipa ingia kwenye website ya zito utaikuta hiyo na baada ya MJP kujua hilo alisema huo mkataba ni feki lazima aufuatilie ila nyie jueni kuwa vitu ambavyo vimeshapigwa mikataba huwa haivunjwi haraka haraka kama vile unavyouvunja muwa rais kaingia hata mwaka hujapita mnataka afanye kila kitu kwa mda mmoja vitu kama hivyo haviwezekani mkataba siku zote ukiuona upo tofauti ni lazima sheria zifuatwe tena huchukua mda sio tu kama unakurupuka usingizini jueni pia kuna kiongozi alioongoza nchi miaka kumi lakini hajafanya kama alivyofanya raisi wa sasa kwa mda mfupi kuleta maendeleo mkitaka kufanya mambo ili watu watambue ni lazima mzichambue kwanza alafu ndio mziweke hewani watu wengi nchini hawajui hata democrasia hufuata upepo tu wawe wanadanganywa au ukweli kwao wanaamini tu ukweli msiwe mnamkashifu rais wetu mnatakiwa pia mpime kazi alizozifanya kwa wananchi wake ndio muweze kukoment wadau yangu ni hayo tu
 
Hapo ni pagumu sana wandugu zangu, eneo hilo liko ki-internarional law, haiwezekani kuligusa japo siku ile anafungua kinyerezi alionesha wazi kuwa yeye kama rais hawezi kuendelea kuilipa iptl; nadhani bado pengine mkuu wa nchi anatafakari aanzeje na amalizeje hii ghasia; mikataba ya utata ni mingi sana kwenye nchi; hebu angalia GGM na Tsh 3 inayolipwa kwa taifa; nenda acia formerly Buzwagi, ni yaleyale cheki mwadui hapo hata vyombo vya habari huwa hazigusi kabisa yaani hata ukimuuliza mwanafunzi wa kodato cha nne usije shangaa endapo atakwambia hajui kama kuna almas tz maana hata serikali yenyewe wala bunge hawaongeleagi kabisa juu ya hili.

Mie nilimwelewa Rais Magufuli aliposema wazee ndo wametufikisha (wametusababishia hali mbaya na udumavu wa kiuchumi nchini). Mie nitaendea kuamini kuwa hata Rais mwenyewe hafurahii kabisa uwepo wa iptl na mikataba yote yenye utata. Ninaamini kuwa endapo Rais ataamua kuisambalatisha mikataba kama hiyo itabidi akae chini na wazee wa kazi ikiwemo na tiss na maofisa wa juu wa kampuni husika kucheza mchezo fulani hivi na baadaye kujakuonekana kampuni imevunja masharti ya mkataba na hivyo imepoteza uhalali wa kuendelea kufanya kazi zake. Wamarekani na nchi kubwa duniani wanaishi
kwa style hizi ikitokea tu wakapoteza imani na wewe huku wakijua fika mkataba wako unakuruhusu kufanya kile ufanyacho ndo hapo utazipenda tu idara za usalama wa mataifa haya yaani hawapotezi mda, watakuchezeshea technique za kiudundi kisha ikajikuta eti umevunja masharti ya mkataba nakwahiyo biashara au kazi siyo halali tena hivyo unatakiwa kuondoka nchini.

Bado Makufuli anayo nafasi ya kuvunja mikataba yote tata ila kunakazi kubwa ya lufanya na hapo ndipo ninamwelewa anaposema tumuombee kwa MUNGU, mimi nitamwombea kwelikweli maana majipu mengine yako sehemu mbaya sana ukigusa tu laweza kuondoka na uchumi wote wa taifa.

Serikali inaweza pia kuwaomba haya makampuni kufanya review/changes za terms za mikataba iliyosainiwa na serikali na haya makampuni huko nyuma, kwa kigezo cha kutonufaika kwa upande mmoja (yaani sisi Tanzania kama nchi). Hii inakubalika kisheria na inawezekana. Siamini kama makampuni yote yatakataa kurekebisha terms ikiwa hili suala litazungumzwa kirafiki. Hili litashindikana ikiwa tu wahusika katika serikali zilizosaini hii mikataba huko nyuma wana maslahi binafsi kwenye hii mikataba na hawataki marekebisho yeyote yafanyike. Kumbuka wakati mwingine kikulacho kinguoni mwako.
 
Hapo kuna mawili, ama kuna kitu anasubiri kikae sawa halafu awasombee wote na mahakama ya mafisadi au tangu apigwe chini kwenye kesi ya samaki aliowakamata laivu anaogopa hizo issue kubwa kubwa.
 
Hapo kuna mawili, ama kuna kitu anasubiri kikae sawa halafu awasombee wote ktk mahakama ya mafisadi au tangu apigwe chini kwenye kesi ya samaki aliyowakamata wachina wakivua samaki laivu anaogopa hizo issue kubwa kubwa.
 
Ili kufahamu ni kwa namna gani serikali ya awamu ya tano inakubalika, waruhusu CHADEMA wafanye hata mkutano mmoja tu wa hadhara.
 
"Wastaafu wangu, nitawalinda kwa nguvu zangu zote. Msiwe na hofu laleni usingizi mzito. Wadharauni wanaowasema vibaya kwani tumewazoea". Kwa kauli hii mnategemea mikataba ya aina ya IPTL itaguswa? Hapa ni mazingaombwe tu na mkizidi kujiuliza mtaishia kuambiwa ni miradi inayohusu ulinzi na usalama wa nchi kama ile ya meremeta na tangold. Mpoooo!!!!!
Umenikumbusha mbali. Hiv hii mahakama ya mafisadi imkute au mtuumiwa awaunganishe ktk kesi hawa wastaafu hii kauri ya huyu msema ovyo itahadhiri vipi mwenendo wa mahakama hiyo ?
 
Back
Top Bottom