Siri ya kujinyonga diwani kata mlangali yafichuka

Praff

Senior Member
Mar 9, 2012
139
12
Kutokana na message alizoziacha hayati diwani wa kata ya mlangali ludewa, na message hiyo kusomwa na mwendesha mazishi, mh. Huyo aliamua kujinyonga baada ya kutapeliwa sh. Mil 81 na mganga mmoja wa kienyeji mzaliwa wa mlangali (maarufu kama MSABE) anayeishi dar, mganga huyo aligoma kulipa katakata. Sh mil 41 kati ya hizo ni mali ya saccos mlangali na zilizobaki ni mali ya familia. Mazishi ya diwani huyo yalihudhuriwa na maelfu ya watu kutoka sehemu mbalimbali. Hii ni ishara kwamba Kacheche alipendwa na wengi. Hata hivyo imekuwa ni gumzo kwa baadhi ya watu ambao waliweka fedha kwenye saccos hiyo. Diwani huyo alikuwa ni meneja wa saccos hiyo.
 
angeongea na JK kisha waingie mkataba wa kurudisha kidogo kidogo kama ilivyokuwa EPA
 
pesa chama hakina tena, kilichobaki ni kucheza upatu tuu

sangoma kiboko bana
 
Kweli dunia tunapita!Sangoma kama katajwa jina nadhani kaishakwea pipa!
 
Tusiwe tunadharau mauaji kirahisi hivyo; je wamechunguza na kuona kweli huyo jamaa kajinyonga mwenyewe? Yaani hakuna kuhusika kwa mtu mwingine?

hata kama Wahehe wana tabia ya kujinyonga, ni vizuri kufanya uchunguzi mpaka kujiridhisha kweli kwamba hakuna foul play.
 
Kwa nini asimtaje jina wakati ndie aliyesababisha hayo yote?
 
Kajinyonga kajiua, inatisha na kusikitisha huwezi amini kiongozi wa juu kuchukua hela za wenzako na kuzichezea kamari lazima ujimalize kwa njia yoyote maana hata akimaliza udiwani hatalipwa hivyo
 
Back
Top Bottom