Elections 2010 Siri si Siri: Pamoja na kauli za kujiamini - CCM wamejiandaa na kuukosa Urais

Liko wazi, no doubt, KUNA MTU YUKO WIZARA YA MAMBO YA NDANI AMBAYE YUKO CCM, AMENIPIGIA SIMU AKANIAMBIA NIKIENDA KUPIGA KURA NITAFUTE NA WENZANGU WA KUTOSHA TUKAMPE SLAA, SIJAAMINI MACHO YANGU,

CHADEMA FOR LIFE
 
Ni taarifa za kutia moyo hizi....

Na sikumbuki kama CCM wamewahi kuulizwa kama watakubalina na matokeo ....
...vilikuwa vinaulizwa vyama vingine tu...

Lakini jibu hapa sasa liko wazi...wamejiandaa kuukosa urais...

Ni Mtizamo unaoonyesha ukomavu wa kisiasa !
 
Kama CCM wapo tayari kwa kushindwa au kushinda, nini cha ajabu kitakacho wafanya wote walio against CCM kukubali kushindwa au kushinda.

Mimi ni muumini wa mabadiriko na naombea mageuzi halisi yatokee. Lakini Opposition parties wasipo shinda bado naami impact yao katika uendeshaji wa serikali ijayo utakuwa ni mkubwa sana. Mambo mendi ya uendeshaji serikali unaweza kubadirika sana. Margin ya ushindi kwa Kikwete (kama atashinda) itakuwa chini ya ile ya mwaka 2005....hii pekee ni itakuwa ni mafanikio makubwa kwani walikuwa hawaachi kutamba kuwa watashinda kwa kishindo zaidi ya 2005.

Bravo wapenda mageuzi, bravo Dr. Slaa, bravo Prof. Lipumba.

Muamusho huu wa kutaka mageuzi ndio unaanza kwani kizazi kipya ndiyo kinaongezeka. Vijana wenye umri kati ya miaka 13 mpka 17 watakuwa wamefikia umri wa kupiga kura uchaguzi mkuu ujao na matarajio makubwa ni kuwa sehemu kuwa yao ni kutaka mageuzi sio kama akina Kingunge, malechela na wenzao ambao kasi ya kuendana na kila jambo la maisha itazidi kuisha zaidi na zaidi.

Tujipe moyo wapenda mageuzi wala tusikate tamaa.
 
Kwa kweli niwazi CCM Tunasubiri Kikwete aapishwe 2,ajabu nikwamba ndani ya bunge CCM Itakuwa na 90% ya umiliki,haya vip hao wababaishaji wataweza,wengi wa wagombea wa upinzani hawana wake,vip wataongoza TAIFA la wanandoa
 
Mpita Njia,

Unasema ikitokea? Ukweli ni kwamba Slaaa anashindwa kwasababu pembezoni mwa nchi hana wabunge wala madiwani wa kulinda kula zake.

Hakuna mabolozi wala watendaji wa vijiji wa kuwashawishi wananchi mpaka dakika za mwisho wakapige kura. Viti vya mjini Slaa atapata kura nyingi lakini sio vijijini.

Hii propaganda ya vijijini tumeshaizoea. Nimeshuudia mzee wa kijijini, ambako ukikosa gari la asubuhi subiri kesho, anasema siwezi mpa JK sababu amekataa kumwongeza mshahara mwanangu. Siku hizi vijiji kibao kuna TV/Simu na updated kama mjini vile. Thus hili swala la vijijini ni propaganda tu CCM. Tumeizoea na wala haitukatishi tamaa.
 
Kanipigia aunt yangu toka tabora,yeye ni msimamizi wa uchaguzi ktk kata na ni kada wa ccm.jina lake ni la ukoo wa waziri mkuu mstaafu ambaye mwaka huu amepigwa chini kura za maoni pale kanda ya katikati.kaniuliza 'unakuja kupiga kura? nikamwambia niko njiani nakuja.'unampigia nani? nikamwambia 'dr slaa.Skuamini nlichokiskia,ameshangilia na kuniambia'big up aunt,tunataka mabadiliko.AMIZING!!!!!!!


duh! amizing
 
Jamani hii ya Slaa ni Tsunami! Mwamko wa watanzania toka kila kona ya nchi, hii si bure, kuna nguvu ya Maulana!, baadhi ya madiwani, wajumbe wa CCM, kwa midomo yao wana nishuhudia kwamba kampeni za CCM wanafanya kama ajira yao, lakini kura kwa Dr. wa ukweli.

Ndani ya chama wengi pia wanahasira ya "chama cha kifamilia" let us keep our finger crossed!

Hata mimi nakuhakikishia kuwa wengi wa wanaccm watapiga kura zao kwa dr wa ukweli, tuendelee wanamaombi
 
Ni habari ya kutia moyo!! Ana uzito gani ndani ya sisiemu?

Mnajidanganya, bila shaka hamjaijua sisiemu. Hivi mlishawahi kuona timu inacheza mpira ikifungwa halafu mashibiki wa timu iliyoshinda wanakatazwa kushangilia? ULIZA watu waliosoma maazengo. mechi ikipigwa kati ya Mazengo na Dodoma secondary.
Hiki ndo chama tawala. kitatawala milele.
 
Kwa kweli niwazi CCM Tunasubiri Kikwete aapishwe 2,ajabu nikwamba ndani ya bunge CCM Itakuwa na 90% ya umiliki,haya vip hao wababaishaji wataweza,wengi wa wagombea wa upinzani hawana wake,vip wataongoza TAIFA la wanandoa

Huku sasa ni kukosa hoja, jadili hoja mkubwa acha pumba!
 
Hivi slaa ataoa kwanza au ataapishwa kwanza? Bei ya sementi ikiwa elfu tano chips mayai itabakia 1500? Au huu ni usanii kama mwingene tena huu umepita mipaka? Great thinkers mpo?

Ukukosea kabisa kuchagua jina la SOKOMOKO maana inavyoonekana wewe ni sokomoko wa ukweli
 

Similar Discussions

0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom