Siri nzito yafichuka CHADEMA

......what do you think that CDM(a reasonable party) can do under this socio-political crisis!!!!
 
Kwanza kabisa inabidi hawa chadema wachunguzwe hizi fedha za kampeni inayoanza mapema hivi wanazitoa wapi? kikijulikana chanzo chao cha fedha, mchezo utakuwa umekwisha. Kuna mengi yamejificha.

Ni kama zile za uamsho mkuu eti....???!!
 
... Mgeta, hii ndio siri nzito - my foot!! Siri ya mwizi wa twiga za Tanzania kuhamishia Uarabuni utauandikia lini??

Mkuu nilikuwa nimeiona hii thread nilipo ona ni ndeefu nikasema ngoja nile nitulie niisome, kweli itafika mahala tutaacha kusoma magazeti
 
Kwanza kabisa inabidi hawa chadema wachunguzwe hizi fedha za kampeni inayoanza mapema hivi wanazitoa wapi? kikijulikana chanzo chao cha fedha, mchezo utakuwa umekwisha. Kuna mengi yamejificha.

Masikini zomba!
 
hii kweli siri nimesoma zaidi ya mara 5 na sipati kitu duuh hizi shule za kayumba aaaah!
 
Mashaka Mgeta | Nipashe Jumapili | 3rd June 2012

Maandamano na mikutano ya hadhara inayofanywa na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), imebainika kuwa ni sehemu ya mikakati yake inayolenga kuibua chuki za wananchi na kukiangusha Chama Cha Mapinduzi (CCM) katika Uchaguzi Mkuu ujao.

Vyanzo vya habari ndani vya Chadema ambavyo havikutaka kutajwa majina yao, vimelieleza NIPASHE Jumapili kuwa, chama hicho kilifanya tathmini na kubaini kasoro zilizochangia kushindwa katika Uchaguzi Mkuu wa 2010.

Miongoni mwa kasoro hizo, ni ari ndogo iliyojitokeza kwa wananchi kulinda kura za wagombea urais na ubunge kupitia Chadema.
“Ili wananchi wawe tayari kuona umuhimu wa kulinda kura za chama cha siasa, inabidi wawachukie watawala, sasa tunachokifanya ni kueleza upungufu wa chama tawala ili wananchi waamke, waichukie CCM,” kilieleza chanzo hicho.

Hata hivyo, akihutubia mkutano wa hadhara kwenye uwanja wa Mahakama jana, Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe, pamoja na mambo mengine alisema chama hicho kitaendelea kuwachochea wananchi kuiasi CCM na kukiunga mkono chama chake.

Mbowe alisema, “wanasema Mbowe ni mchochezi, wanasema Chadema inapandikiza chuki, mimi na chama changu tutaendelea kuuhamasisha umma kuondokana na woga, wawachukie watawala walioshindwa kuwaletea maendeleo.”

Chadema imekuwa na utaratibu wa kuandaa maandamano na mikutano ya hadhara kupitia kile kinachojulikana kama operesheni maalum, mathalani kwa sasa ikijulikana kama Operesheni Okoa Kusini.

KUCHUKUA MFUMO WA CCM

Kwa upande mwingine, mkakati uliobuniwa na kuzinduliwa na Chadema, ukijulikana kama Vuguvugu la Mabadiliko (M4C) umetajwa kama wenye lengo la kukisimika chama hicho hadi kwenye ngazi ya ubalozi, kama ilivyo kwa CCM.

Kupitia M4C Chadema inajikita kwa ‘kuvuna’ wanachama na kusimika uongozi katika ngazi tofauti kuanzia mabalozi, matawi, kata, jimbo, wilaya, mkoa hatimaye taifa.

Tayari Chadema kwa kutambua umuhimu wa kukiweka chama katika ngazi ya msingi (ubalozi), kimetumia ibara ya 7.1.1 ya Katiba yake kimeweka tarehe ya kufanyika uchaguzi nchi nzima.

Mbali na ngazi ya ubalozi, Chadema imetumia ibara ya 7.1.3 kutangaza uchaguzi wa chama hicho ngazi ya tawi, ambapo awali kilionekana kutokuwepo katika maeneo mengi ya nchi.

“Tunapoingia ndani ya jamii kufikia ngazi za msingi, tawi na kata, tutajihakikishia kuichukua nchi kwa urahisi zaidi,” kilieleza chanzo hicho.

Chadema imetoa maelezo ya taratibu za uendeshaji wa uchaguzi ndani ya chama hicho kwa ngazi za msingi na matawi, kikitumia ibara ya 11-1 ya chama hicho na kuzisambaza nchi nzima.

Mkurugenzi wa Kampeni na Uchaguzi wa Chadema, Msafiri Mtemelwa, alithibitisha kuchapishwa kwa maelezo hayo na kwamba yatafanikisha chaguzi hizo kufanyika kwa mujibu wa Katiba.

Maelezo hayo yanataja Septemba Mosi hadi Oktoba 5, mwaka huu kuwa siku za uchaguzi ngazi za msingi wakati ule wa matawi utafanyika kati ya Desemba 5 hadi Januari 8, mwaka ujao.

Chaguzi nyingine na ngazi zake kwenye mabano zitafanyika Februari 8 hadi Machi 14, mwaka ujao (kata), Aprili 14 hadi Mei 23, mwaka ujao (jimbo), Juni 23 hadi Julai Mosi, 2013 (wilaya) na Agosti 2 hadi Septemba 11 mwakani (mkoa).

Chaguzi zote hizo zitafanyika zikihusisha pia mabaraza tofauti ya Chadema, lile la vijana (Bavicha), wanawake (Bawacha) na Wazee.
Chanzo kimeeleza kuwa kupatikana kwa uongozi katika ngazi hizo kutaiwezesha Chadema kuwa na mtandao utakaohusika katika kulinda nafasi za wagombea uwenyekiti wa mitaa, vitongoji na vijiji, udiwani, ubunge na urais.

Mwenyekiti wa serikali ya kijiji cha Mwembe Mmoja (CCM) mkoani Mtwara , Abdallah Suleiman Mnyalu, alisema kazi za kisiasa hususani kukutana na kuzungumza na wananchi, zitaiathiri CCM katika chaguzi zijazo.

Alipotakiwa na NIPASHE Jumapili atoe maoni yake kuhusu athari za Chadema katika ngazi za msingi kwenye jamii, Mnyalu alisema chama hicho kinafanya kazi zilizopaswa kufanywa na CCM, lakini chama hicho tawala kimelala.

“Wenzetu hawa wanapita na kukutana na wananchi, lakini sisi wenye dola hatufanyi hivyo mpaka ufike Uchaguzi Mkuu,” alisema.

Mnyalu alisema pia kuwa vitendo vya unyanyasaji vinavyofanywa na viongozi wa serikali katika ngazi za msingi vimechochea chuki ya wananchi kwa chama tawala, hivyo kutoa mwanya kwa wapinzani hususani Chadema kuungwa mkono.

MATUMIZI YA MTANDAO WA MAWASILIANO

Imebainika kuwa Chadema imejizatiti kutumia njia mbalimbali kuwafikia wapiga kura, wakiwemo wasiojitokeza na kushiriki shughuli za kisiasa hadharani.

Kupitia mkakati huo, imeelezwa kuwa chama hicho kitatumia njia ya mitandao ya kijamii iliyopo kwenye mawasiliano ya kisasa, kupenyeza kampeni na hoja zake.

MKAKATI WA KUJIENEZA

Kikiwa katika Operesheni Okoa Kusini inayoendelea kwenye mikoa ya Lindi na Mtwara, Chadema kinawatumia viongozi na makada wake kufika maeneo ya vitongoji, vijiji na kata ambapo wanazungumza na wananchi, kufungua matawi na kusimika uongozi wa muda.

Jana, Chadema kilichoanza ziara zake mkoani Mtwara Mei 27, mwaka huu, kimeingia mkoani Lindi ambapo kitafanya mikutano ya hadhara na kufungua matawi yake hadi Juni 9, mwaka huu kitakapofanya mkutano wa hadhara mjini Lindi.


Yanibidi nitafute KAMUSI inawezekana SIRI ina maana zaidi ya moja, ntarudi muheshimiwa!!!
 
Mm, bado hii ni siri, akiiweka wazi itakuwa si siri tena. Huyu mwandishi alitaka kujaza tu gazeti ili litoke. Kwani huwezi kutoa gazeti ukurasa mmoja ukiwa empty?
 
kaka ulitaka kusema siri au serikali au siasa kwa sababu nimeishia kuwa kama wasomaji wenzangu sijapata ona siri mm au nisome tena na tena
 
Kwanza kabisa inabidi hawa chadema wachunguzwe hizi fedha za kampeni inayoanza mapema hivi wanazitoa wapi? kikijulikana chanzo chao cha fedha, mchezo utakuwa umekwisha. Kuna mengi yamejificha.

tunatoa sana michango mkuu, umezoea uwizi wa magamba!
 
Back
Top Bottom