Siri nzito ya Zombe na Bageni

Hii hukumu bado naendelea kuiona ni ya ajabu.. Sielewi pamoja na maelezo ya shahidi lakini anaekutwa na hatia ni mmoja tu.. Hakuna hata accomplice aliekutwa na hatia jamani..? Wanasheria waliomo humu naomba wanisaidie kunielewesha labda ntaelewa..
 
Kosa lililofanywa hapa ni shtaka alilofunguliwa zombe, nafikiri waliamua kumsaidia , maana wanajua hakuwa eneo la tukio, sio rahisi kupatikana na hatia ya mauaji, wangetaka atiwe hatiani wangemfungulia shtaka la kuficha wahalifu tokea mwanzo na hoja zao wangezipeleka huko, hakika angetiwa hatiani, lakini kwa kwenda mbali zaidi wangeweza kufuatilia mazungumzo aliyokuwa nayafanya bageni kwa simu.
 
Watu ambao wangekutwa na hatia moja kwa moja ni yule aliyetoa amri na alitekeleza. hao wengine wangeshtakiwa kwa makosa ya kuficha mauaji, aliyetelezwa alitoroka na hadi leo hajapatikana, nao ni utata mtupu.
 
Ongeeni sheria na yote yale lakini hawa watu wasio na hatia kuuawa kinyama vile huenda damu yao ikavifuata hadi vitukuu vya waliofanya hayo. Bora hao askari walio confess laana itaishia kwao na wameweka nafsi zao huru!
 
msitu wa pande ni pale ilipo law school kwa sasa ambapo lilikua poli kuanzia stend ile mpya mawasiliano hostel mpya zinazojengwa za udsm kwa kifupi lile lilikua eneo la posta na simu enzi izo mpaka huku mkapa foundation

Brother, heshima mbele.....msitu hupo nje ya mji na hupo chini ya hifadhi ya misitu tembelea hapa TFCG, Misitu Yetu Project: Pande Game Reserve kwa taarifa zaidi.
 
isije ikawa zuga....maana moja ya watu ambao hawaamin kama Balali alikufa ni mm....sasa asje akasafir kwenda kuish huko vietnam af tunaambiwa kanyongwaa....tuoneshwe LIVE
Balali huwezi kumfananisha nahuyu mNUKA VUMBI lazima atatumbukia kwenye kitanzi tu Believe me...na Jana ndio picha yake ya mwisho kitaa ataishi ngome hadi siku walume wakiamu kumaliza kazi wapuuzi hawa wanatia watu umaskini na uKIWA wa lazima sababu ya Tamaa ya pesa
 
Hii hukumu bado naendelea kuiona ni ya ajabu.. Sielewi pamoja na maelezo ya shahidi lakini anaekutwa na hatia ni mmoja tu.. Hakuna hata accomplice aliekutwa na hatia jamani..? Wanasheria waliomo humu naomba wanisaidie kunielewesha labda ntaelewa..
Ndugu yangu Sheria ni Fani yakucheza na Maneno so Inategemea unajipangaje ukiwa Mahakamani na ujue KESI yakuua hadi utiewe Hatiani kuna vitu Vingi wanazingatia
 
Kosa lililofanywa hapa ni shtaka alilofunguliwa zombe, nafikiri waliamua kumsaidia , maana wanajua hakuwa eneo la tukio, sio rahisi kupatikana na hatia ya mauaji, wangetaka atiwe hatiani wangemfungulia shtaka la kuficha wahalifu tokea mwanzo na hoja zao wangezipeleka huko, hakika angetiwa hatiani, lakini kwa kwenda mbali zaidi wangeweza kufuatilia mazungumzo aliyokuwa nayafanya bageni kwa simu.
Ndio maana nimemwambia jamaa humu Fani ya Sheria nikucheza na Maneno inategemea kesi umeipangaje
 
Hivi million 5 zinakushawishi kuua watu??? I'm very confused!!
Shangaa hapo!

Na mbona hawajawahi kusema hao waliokuwa wanasema majambazi (wafanyabiashara ya madini) walikuwa na kiasi gani cha fedha au madini yenye thamani ya shilingi ngapi?!
Kina Zombe walitakiwa pia kuadhibiwa kwa kupora pesa/madini ya hao wafanyabiashara kwa kifupi wao kama polisi ndio waligeuka majambazi na wauaji!
 
Watoto wa waliouawa hao kina Chigumbi ndio kwanza walikuwa wamewasili Form One 08/01/2006 baada ya siku chache parade tukaambiwa hicho kisa
Walilia sana
Maskini jamani. i hope Mungu amewasimamia wako vizuri sasa. yaani nimetokwa machozi jamani. yaani uskie baba yako kauwawa! duh, ni miongoni mwa vitu vitakavyobaki vichwani mwao for as long as they live
 
haw
shetani wa kwanza ndio nani?
a ni miongoni mwa walioishi kama malaika, sasa acha wajue shetani anaishije.....tena asinyongwe haraka, akae kwanza huko kifungoni with no contact from outside world alafu akidhani keshazoea hiyo hali ndo apewe tarehe ya kunyongwa, hiyo tarehe iwe ni a year later just to torture him more
 
Back
Top Bottom