Siri nzito ya Kikwete, Karamagi yaibuliwa

Ndio nini sasa....? Hebu zungumza ueleweke bana...sio kila mtu anajua kila methali, msemo, misamiati, n.k....

Hey how come you don't understand? Its a Bantu thing afterall! Bantu boy once you get tired of monkeying around JF, get in touch with the embassy in DC. My business organization wants to make use of your clowning talent. This could potentially translate into a multibillion dollar "bizniss" in Bongo.
 
Dada yangu Mwafrika wa Kike,

Najua ungetamani sana tume hii ya rais, ije na majina ya watu!!! hili nadhani itabidi usubiri tume nyingine itakayouundwa na washirika wako labda. (tehe tehe tehhh)

Walioweza sikiliza Hotuba ya Rais wa Jamhuri kabla ya kuhaririwa wakati akilizungumzia hili suala la madini nadhani watakuwa wamemuelewa kama nilivyoelewa mimi, uhariri wa vyombo vya habari na perception ya mtu binafsi anavyotaka kulichukulia jambo ndivyo vitu ambavyo vinafanya hili jambo lionekane kana kwamba unahitaji elimu ya wana anga za juu ili kulielewa!

Labda nitoe mfano, wa Tume ya Warioba, kazi yake ilikuwa kuonyesha mianya kwenye jamii na kupendekeza namna ya kuiziba, ingawa pia ikawa na mifano michache ya watu waliozidi kuimaliza nchi kwa rushwa zilizokidhiri lakini nia na madhumuni yake ilikuwa rushwa ikoje kwenye jamii na namna gani ya kupigana nayo!!!

Ambayo kwa maoni yangu sheria zilizofuata zilizingatia kwa kiasi hata kama sio kwa ukamilifu taarifa ile ya tume ya warioba.


Tume ya madini iliyoundwa haina tofauti sana kwenye outcome zake na Tume ya Warioba, kwamba ni mifumo, sheria zinabadilishwe vipi tufaidike,,, nadhani AOB ya tume ndio inaweza taja waliokubuhu kukwepa hata sheria zilizopo, hizi hutolewa kama mifano. kwa ajili ya sheria ijayo kuzipa mianya hiyo.

Haya Ndio nilisema kuanzia siku ya kwanza - nikiwa mmoja wa watu waliopondea hii tume, kamati, usanii, au whatever the name lile utasema. Ninajua tofauti ya tume na kamati ya bunge, na kama unakumbuka watu walivyozidi ubishi hapa Mwanakijiji aliweka tofauti hizo hapa na ubishi ukaisha.

Kwa msingi wa uliyosema, Alichounda Kikwete ni kama tu vyote vilivyopita ukianzia Waryoba na mpaka tume itakayoundwa in the future kuhusu namna ya kuunda tume nzuri za kurekebisha mambo ambayo kamati ilikuwa inachunguza kwa nini tume ya kwanza haikupendekeza hayo kwenye kamati ya.... Confusing.....

Huu ni upotevu wa muda na pesa kidogo zilizosalia baada ya wizi mkuu uliofanyika BOT na upotevu wa mabilioni unaondelea sasa hivi chini ya serikali ya Kikwete.
 
Can we wait for results before we jump in conclusion? Give me a brake! Tusiwe wapinzani kwa kila kitu, first tuwape kamati muda, kisha tuangalie nini kitafanyika. Kuanza kuconclude kwamba nothing will be done is not fair.
 
Peter Machunde ni business partner wa Karamagi.Wana kampuni inaitwa Vertex Securities na ofisi zao ziko Ohio Street kwenye jengo la ubalozi wa Zambia.Pia Karamagi ana kampuni nyingine inaitwa Smart Finance,inaendeshwa na mama mmoja wa kirusi,ambaye inasemekana alimpora mtu,hawa wanatoa mikopo kwa wafanyakazi wa serikali.
 
Can we wait for results before we jump in conclusion? Give me a brake! Tusiwe wapinzani kwa kila kitu, first tuwape kamati muda, kisha tuangalie nini kitafanyika. Kuanza kuconclude kwamba nothing will be done is not fair.

Haya mambo ya kuamulia watu cha kusema yanawezekana china au ccm pekee. Wananchi wengine wana haki na wajibu wa kuhoji kile ambacho serikali zao zinafanya kwa niaba yao.
 
Can we wait for results before we jump in conclusion? Give me a brake! Tusiwe wapinzani kwa kila kitu, first tuwape kamati muda, kisha tuangalie nini kitafanyika. Kuanza kuconclude kwamba nothing will be done is not fair.


tatizo siyo results... tatizo ni mchakato wa kufikia matokeo yale. Ndio maana wale ambao tumewahi kukaa kwenye kiti cha nyuma kwenye maabara ya Kemia na tukaanza "kukoroga koroga" kwenye zile burners mwisho tulijikuta tunawasha moto kwa kuchanganya makemikali yasiyotakiwa. Ndio maana katika maabara kuna utaratibu wa kufanya utafiti, utaratibu unaoamua nini kinahitajika, nini kinafanyika mwanzo, na nini kinawekwa kwa kiasi gani na kwa muda gani.

Mtindo huo wa kuangalia process nzima upo kwenye hesabu pia; wale ambao tulikuwa tunapenda hesabu kidogo kulikuwa na furaha pale unapofanya hesabu za Proof ambapo siyo jibu ambalo ni muhimu zaidi bali kuweza kukokotoa na kuonesha umeweza vipi kufikia jibu hilo. Ni kwa sababu hiyo utaona kuwa waliopata maksi za juu siyo tu walipata jibu sahihi bali walionesha mtiririko mzima wa hesabu kufikia jibu hilo.

Sasa ili kuweza kuwa na matokeo ya uhakika na yasiyo na uharibifu basi the process matters not just the results. Vinginevyo tutafika mwisho na kuhoji kama matokeo ni sahihi. Kwa mantiki hiyo basi suala siyo matokeo ya kamati na ya kuwa tusubiri ndiyo tuhukumu. Kwangu mimi naamini process nzima ya kazi ya Kamati isiwe na makosa au na kuonekana makosa. Hivyo, kabla hatujaletewa matokeo tuhakikishiwe kuwa the process itself is credible. So far, the inherent conflict of interests renders the whole process to be a mere illusion of the first kind!
 
Acha dharau we dada. Umejuaje kama mi ni bwa mdogo...usitake kuanzisha zali na mimi hapa....oohoooooo...we kama hujui jibu lake funga domo
 
Bwana Mdogo Tulia...OOOH!!Haya mambo Makubwa Acha kimbelembele kama Mkojo wahasubuhi..
 
Tume? timu? ni kwa masilahi ya nani?
Nani anajua kuwa David Tarimo kutoka kampuni la PWC NI TAX CONSULTANT WA BARRIK?
Alianzia kule resolute, n.k.

Maigizo, ila Zitto hana budi kuwa ndani ili tuweze kujua toka jikoni nini kinaendelea na hakuna sababu ya Zitto kujitoa so far.
 
Tume? timu? ni kwa masilahi ya nani?
Nani anajua kuwa David Tarimo kutoka kampuni la PWC NI TAX CONSULTANT WA BARRIK?
Alianzia kule resolute, n.k.
.

Kwa taarifa yako uhusiano wake na Barick, akiutumia kwa masilah ya upande wa nchi yetu, it is a big plus to us!
 
Kilitime,
kama kweli Tarimo ni Tax Consultant wa Barrick na kama kuna michezo michafu wanafanya basi uwekano mkubwa ni yeye ndiye atakuwa anawafundisha. Katika hali kama hiyo si rahisi mtu huyo akafanya kazi kwa maslahi ya taifa.

ktk mazingira ambayo Tarimo ni mtuhumiwa kunatakiwa kuwa na incentive ya yeye kuwasaliti watuhimiwa wenzake--barick. personally siioni!!
 
Siri nzito ya Kikwete, Karamagi yaibuliwa

na Ratifa Baranyikwa
Tanzania Daima


IMEBAINIKA kuwa, wajumbe wa kamati iliyoundwa na Rais Jakaya Kikwete, kupitia mikataba ya madini, wana sifa zenye kila dalili ya shaka kuwemo katika kamati hiyo.

Kwamba baadhi ya wajumbe hao, walihusika katika utiaji saini mkataba wa Buzwagi na mmoja wa wajumbe wa kamati ni rafiki mkubwa wa Waziri wa Nishati na Madini, Nazir Karamagi, ni jambo linalotia shaka kuhusu kuteuliwa kwao katika kamati hiyo.

Hayo yalibainishwa jana katika kongamano la wanavyuo la kuadhimisha Siku ya Wanafunzi Duniani, lililohudhuriwa na wasomi wa kada mbalimbali, wakiwemo madaktari, wanasheria, wahadhiri wa vyuo vikuu, wanaharakati na wanasiasa wa kambi ya upinzani.

Kongomano hilo lilifanyika katika Ukumbi wa DDC mkabala na Mlimani City, karibu na kilipo Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, sehemu ya Mlimani.

Wachangiaji wengi katika mdahalo huo, walieleza kuwa kamati hiyo iliyoundwa na Rais Kikwete ni kiini macho cha kuwaghilibu Watanzania, ili wasiendelee kuhoji kuhusu utata unaodaiwa kuwepo kwenye mikataba ya madini, kwa vile wajumbe wa kamati hiyo wote hawana sifa za kuunda kamati hiyo.

Wa kwanza kuelezea udhaifu wa kamati hiyo, alikuwa Katibu Mkuu wa CHADEMA, Dk. Wilibroad Slaa, ambaye alidai kwamba, mmoja wa wajumbe wa kamati hiyo ni swahiba mkubwa wa Waziri Karamagi ambaye hawezi kumtia matatani rafiki yake (Karamagi).

Dk. Slaa alimtaja mjumbe huyo kuwa ni Peter Machunde, kutoka Soko la Hisa Dar es Salaam (DSE), ambaye mwaka jana alialikwa bungeni na Karamagi na akatambulishwa mbele ya Bunge kuwa ni rafiki yake.

Akizungumza kwa kujiamini, Dk. Slaa aliyenukuu kitabu cha kumbukumbu za Bunge (Hansard) cha Agosti 7, mwaka 2006, alisema hata kualikwa kwa Machunde bungeni kuna kila dalili za shaka kuwa alikuja kufanya moja ya kazi za Karamagi.

“Mwaka huo, Karamagi akiwa Waziri wa Viwanda na Biashara, alimtambulisha bungeni Machunde kama rafiki yake, leo hii anatambulishwa kwenye kamati ya akina Zitto.

“Hawa watu walikuja kufanya nini bungeni? Tunafuatilia walikuja kufanya nini… hatutaki kamati kiinimacho, kamati hii haitokani na Zitto peke yake, mwishoni mwa wiki ijayo tutatoa taarifa nyingine juu ya hiyo kamati na ndiyo maana tunasema hakuna wa kumfunga paka kengele kwa sababu wote wanafahamiana,” alisema Dk. Slaa.

Mwanasheria Tundu Lissu, ambaye aliposimama kuzungumza alishangiliwa na mamia ya washiriki wa kongamano hilo, alisema haungi mkono kuwepo kwa kamati hiyo na haikupaswa kuwepo, huku akiwachambua wajumbe wake, mmoja baada ya mwingine.

“Tuna historia ya ‘ku-miss use’ hizi kamati, inapaswa tujiulize hii kamati ya Zitto ni ya nini wakati kuna kamati nyingine tano zinazohusu masuala ya madini zilishaundwa na zimewasilisha ripoti zao, lakini hazijawekwa wazi mpaka leo na hatujui nini ripoti hizo zimependekeza?” alisema.

Lissu aliitaja kamati ya kwanza kuwa iliundwa mwaka 2001 chini ya uenyekiti wa Jenerali Mboma, ambayo ilikamilisha kazi yake, lakini mpaka leo ripoti yake haijawekwa hadharani.

Alisema mwaka 2002 kamati nyingine iliundwa na mwenyekiti wake alikuwa Brigedia Mang’enya, ambayo ilitoa ripoti yake kimya kimya mwaka 2003 na haijulikani nayo ilipendekeza kitu gani.

“Kamati ya tatu iliyoundwa ni ile iliyoongozwa na aliyekuwa Katibu Mkuu Wizara ya Nishati na Madini mwaka 1994-1995, Dk. Jonas Kipokola. Mmoja wa wajumbe wake kwa sasa anaonekana tena kwenye Kamati ya Zitto… Maria Kejo alikuwepo kwenye kamati hii… ripoti haijatolewa,” alisema Lisu huku akionekana kusikitika.

Lissu, katika madai yake alimuelezea Kejo kuwa ndiye aliyehusika kusaini mkataba mbovu wa IPTL, hivyo kuteuliwa kwake katika kamati hiyo, kunaonyesha jinsi Rais Kikwete alivyofanya uteuzi wenye shaka.

“Maria Kejo, miaka ya 1994/95 alijibadilisha jina akijiita Maria Ndosi, miaka ya hivi karibuni ameanza tena kujiita Maria Kejo, huyu ndiye aliyehusika kusaini mkataba wa IPTL, hii ipo kwenye ripoti ya Transparence International ya IPTL, na kwamba zipo kumbukumbu zinazoonyesha kuwa alihusika kuwashawishi baadhi ya viongozi kuchukua rushwa ili mkataba huo usainiwe.

Mjumbe mwingine aliyetajwa na Lissu kuwa hafai kuwa kamati hiyo, ni Mwenyekiti wa Chama cha United Democratic (UDP), John Momose Cheyo, kwa vile alikuwa mpiga debe mkubwa wa kusainiwa kwa IPTL.

Akizungumza kuhusu ushiriki wa Zitto katika kamati hiyo, alisema bila kuingia kiundani kuwa, uteuzi wake hauna maana kwa sababu hana cha kufanya katika kamati hiyo iliyojaa tuhuma nzito za rushwa.

Lissu pia alimgusa Machunde akidai kuwa ni hatari kuwa katika kamati hiyo kwa vile kuna ushahidi wa kualikwa kwake bungeni na Karamagi kwa ajili ya kushawishi baadhi wa wabunge wasilivalie njuga suala la Richmond.

Mwingine aliyetajwa katika orodha hiyo ya kutofaa kuwa katika kamati hiyo ni Salome Makange, Mwanasheria wa Wizara ya Nishati na Madini anayedaiwa na Lissu kuwa si muadilifu na kwamba ni mmoja wa watu waliohusika kusaini mkataba wa Buzwagi.

“Mkataba wa Buzwagi au wowote ule ni lazima usainiwe na mwanasheria wa wizara, leo wapo kwenye kamati… Mark Bomani (Jaji) ambaye ni Mweyekiti wa Kamati hiyo, historia inaonyesha kuwa ni mwana CCM na Harrison Mwakyembe hajawahi kusema chochote kuhusu madini. Tume inakwenda kufanya nini, haina ‘term of reference?” alihoji Lissu.

Alisema mbali na wajumbe wa kamati hiyo kutokuwa na sifa, hata muundo wa kamati yenyewe hauna nguvu za kutosha za kufanya kazi kwa uhuru na uwazi.

Alisema kama Rais Kikwete ana nia ya dhati ya kuunda kamati ya kupitia mikataba ya madini, anapaswa kuunda kamati teule ya Bunge ambayo ina mamlaka na nguvu kisheria za kumuita mtu yeyote na kumhoji.

“Kamati ya Bunge ina nguvu, kwenye kamati hii unaweza kumuita Karamagi na ukamwambia lete mikataba, akikataa unamfunga, Kamati ya Rais haina ‘judicial power’, mimi naona rais anajitakasa tu kwa wananchi,” alisema Lissu.

Naye Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Kabwe Zitto, alisisitiza msimamo wake kuwa amekubali uteuzi huo na kwamba atahakikisha anaweka maslahi ya taifa mbele.

Alisema sekta ya madini inaonyesha kuwa sekta inayokuwa, lakini mchango wake kwa pato la taifa hauongezeki.

Baadhi ya watu wengine mashuhuri waliozungumza katika mdahalo huo na kuunga mkono kuwepo kwa shaka dhidi ya wajumbe wa kamati hiyo, ni Profesa Mwesiga Baregu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, ambaye pia alisisitiza mshikamano wa wasomi na kutumia usomi wao ili kuleta maendeleo.

Wengine ni mwanahabari mkongwe, Makwaiya wa Kuhenga, Mbunge wa Viti Maalum (CHADEMA) na Waziri Kivuli wa Elimu ya Juu, Susan Lyimo na Dk. Azaveli Lwaitama wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, ambao wote walisisitiza nguvu ya pamoja katika kuleta mapambano ya kifikra.

Rais Kikwete alitangaza kamati hiyo hivi karibuni na itaongozwa na Mwanasheria Mkuu mstaafu, Jaji Mark Bomani.

Wengine kwenye kamati hiyo itakayofanya kazi kwa miezi mitatu ni Mbunge wa Bariadi Mashariki (UDP), John Cheyo, Dk. Harrison Mwakyembe (CCM) ambaye ni Mbunge wa Kyela, Ezekiel Maige kutoka Jimbo la Msalala (CCM), Peter Machunde wa Soko la Hisa la Dar es Salaam, David Tarimo wa PriceWater Coopers na Maria Kejo wa Wizara ya Sheria na Katiba.

Pia wamo Mwanasheria wa Wizara ya Nishati na Madini, Salome Makange, Mugisha Kamugisha kutoka Wizara ya Fedha na Edward Kihundwa, ambaye ni Mkurugenzi Msaidizi, Idara ya Makazi, Wizara ya Ardhi na Maendeleo ya Makazi.

yan yatafichuka mengi kabla hawajaiacha hii dunia, yaliyo fanyika gizan yatafunuliwa nuruni!
 
In any committee what you expect is check and balance. What i believe Zitto is obligated to provide check and balance to this committee, his job will be to analyze all facts provided, and consult other mambers concern the facts .

What i don't understand is why Upinzani rise ant-trust for this committee which includes different people. Zitto is our red flag, if any non sense happen i believe Zitto will rise his red flag. That is check and balance. Nothing will be published if there is no agreements between members, unless otherwise CCM wamnunue Zitto which is possible due to Tanzanian works ethics.

Nikwasababu upinzani hatutaki tena kubuluzwa na watu ambao hata shule hawakwenda au kama wameenda hawakuelimika, wamekuwa na tabia za kitapeli miaka zaidi ya 50 sasa bado tukubali uhuni huu wa ccm, katu haiwezekani labda kwako
 
Mauzauza Tanzania ni mahala pake.

Nasikia Karamagi anafanya juu chini kurudi mjengoni
Nadhani siyo kupitia jimbo lake la zamani Bukoba Vijijini... Na wala si Kilosa, kule Kilosa kawanyang'anya wakaazi wa Changarawe maeneo ya kulima...!
 
Back
Top Bottom