Siri nyingine ya Ngeleja: Wamarekani tayari wanachimba Uranium Tunduru kisiri siri?

Tatizo naloliona kwa watanzania walio wengi ni kwamba wako obsessed mno na hiyo uranium but for a fact liganga, mchuchuma ndiyo haswaa kunaweza kufanyika serious mining ya kututoa watanzania. Coal na iron ore deposit ya pale ina thamani kuliko proven reserves zote za gold Tanzania ukichanganya na ile iliyochimbwa na kuuzwa pia.Wakuu Niger kuna uranium ya kufa mtu na imeanza kuchimbwa miaka kibao, vipi wamefaidika nini ulifanya comparison say hata na Equatorial Guinea au Angola. Kuna uranium kibao Namibiana imeanza kuchimbwa siku nyiingi. Ukija South Africa ya kumwaga, lakini hata siku moja SA wakiwa wanazungumzia mining industry hawaifikirii hata kuifikiria. There's huge deposits of uranium in Australia na inachimbwa miaka kibao. LAKINI "THE MOTHER OF ALL MINING INDUSTRY NI COAL NA IRON ORE".Wawekezaji wa coal wameliona hilo na wanajua watanzania tunapuuzia na hatujui kitu kuhusu coal, si inaitwa mkaa, hivyo hapa tutapigwa bao balaaaa!!!! Lakini kama tungekuwa taifa serious coal mining ndiyo tungeikazania kwa sasa.
Nyambala tutakuwaje serious wakati wewe unaonyesha udhaifu mkubwa kwa kubeza uranium, dhahabu nk eti coal na iron ore ndio itatutoa, kama tumeshindwa dhahabu ambayo ingetutoa kama tungeisimamia vizuri tutawezaje coal na iron ore. Kwataarifa tu ni kwamba huko serikalini wengi kama sio wote wana mawazo ya kijinga kama yako na ndio maana rasilimali zetu hazitunufaishi kitu ila zinamnufaisha mwekezaji, huo ni 'ukilaza' ndugu yangu
 
Unapoongelea thamani ya uranium unapaswa uwe na credible sources! mwaka jana uranium (yellow cakes) price iligonga $140 per pound! Japokuwa thamani yake huwa inapanda na kushuka yaani si stable speculation zinadai bei ya uranium itaendelea kupaa kutokana na mahitaji ya Uchina! Na ndio maana makampuni mengi yanakuja kufanya exploration! Kwa sasa 1 pound ni $ 53 Market price!

Naungana na Nyambala, Hakuna kampuni inayochimba Uranium hapa Tanzania. Kuna kampuni nyingi zinafanya Uranium Exploration. Uranium haina thamani sana kama watu wengi wanavyo fikiria. bei ya Julai 11, 2011 ya U3O8 ni 53.75USD per Pound.
 
Jana mbunge wa viti maalim (CHADEMA) Naomi Amy Kaihula kasema kuwa kuna kampuni ya Kimarekani inachomba Uranium kisirisiri (clandestinely) katika wilaya ya Tunduru .

Alisema kaona kwa macho yake uchimbaji ukiwa unaendelea. Sasa cha kujiuliza mbona hili hatuna habari nalo? Mkataba wake ulisainiwa lini? environmental impact assessment ilifanywa na nani? Mkataba una worth how much? serikali inapata kiasi gani?

Lakini sitoshangaa kusikia kama huu ulikuwa ni mchongo wa BILIONEA Jairo na dumber mwenzie Ngeleja.

Why keep it secret? kwa nini wananchi hawajulishwi kinachoeendelea ndani ya maeneo yao? Hivi law & order iki break katika mazingira haya serikali itajibu nini?

Habari ndio hiyo

Sina Uhakika kama uko sahihi hapo nilipo highlight.... Unajua wengine huwa hata drilling huwa wanaita Uchimbaji....

Nadhani huyo Mbunge alliona diamond drill rigs.....
 
Kibatani cha THANKS kirudishwe please!Hata mimi nipo kwenye tasnia ya migodi,ulichokiongea wewe na alichokiongea Nyambala ni sahihi kabisa.Toka mwaka jana nimekuwa nawafuatilia hao jamaa wa MANTRA kwa ukaribu sana...ukweli ni kwamba bado hawajaanza kuchimba!Wanachokifanya kwa sasa ni uchimbaji mdogo kwa ajili ya tafiti za kimaabara na pengine uchimbaji wa kufanya "levelling" kwa ajili ya kuandaa maeneo ambayo watakuja kuweka plant zao mbali mbali.Ikumbukwe wataweka plant kama tatu pale,main plant ya ku-process uranium,acid plant na electricity plant coz umeme wetu ndio hivyo tena.Nawasilisha.
Mbona sasa mnazunguka mbuyu? Huo uwekezaji ni siri au? Mbunge angejibiwa na waziri kwamba hakuna mkataba wa uchimbaji au upo wenye maslahi kadha wa kadha, huwezi kuandaa maeneo ya kufunga mitambo kabla hujaingia mikataba, kimsingi hapa ndipo serikali inapokera wananchi wake na utakuta mikataba yenyewe ni ya kinyonyaji
 
Naungana na Nyambala, Hakuna kampuni inayochimba Uranium hapa Tanzania. Kuna kampuni nyingi zinafanya Uranium Exploration. Uranium haina thamani sana kama watu wengi wanavyo fikiria. bei ya Julai 11, 2011 ya U3O8 ni 53.75USD per Pound.

Hatumaanishi iwe sawa na dhahabu.....kumbuka ni millions of tonnes zitachimbwa.....pipa la mafuta ghafi ni $100 maana yake lita ni $0.5 na bado mafuta ni pasua kichwa
 
Ofcourse acha wachimbe.. na hakuna haja ya kumlaumu Ngeleja na wizara yake.

Laumu majuha zaidi ya milioni nne walioirudisha CCM madarakani kwenye uchaguzi wa mwaka jana. Biblia inasema utavuna ulichopanda, na ndo kinachotokea sasa hivi.


Ama kweli umenena. Hapo kwenye red ni noma. Natamani makada wa CCM hata akina Shellukindo wangeisoma hii comment.
 
Nguvu ya umma itumike kumwajibisha ngereja, this man should step down. Madini yanaibiwa, hakuna umeme nchini, anatumia mbinuchafu ya kuhonga viongozi wa serikali kulinda masilahi ya Mafisadi. Barua ya jana iliyosomwa Bungeni ni uthibitisho tosha kabisa kumfukuza kazi Ngereja kwa sababu alikuwa anajua deal lote.

Nakubaliana na wewe kwa asilimia mia.
 
Mkuu hiyo uranium haina thamani kiasi hicho mpaka kampuni ya nje ya nchi irisk kuja kuchimba kisirisiri na after all lazima uelewe kuna masuala ya grade per ton. Jmani watanzania tunahitaji tuelimike kuhusu haya mambo sasa kama hata mbunge anaweza kuongea hii (kama ni kweli) basi tuna tatizo kubwa!!!!!! Uchimbaji industrialized si sawa na "uchoji" (uchimbaji wa sululu).Uranuim yenye thamani kubwa ni ile enriched ambayo hata kuna baadhi ya nchi zilizoendelea kama Australia, Canada still wanauza raw (not enriched). Sasa mtu eti kwenda Tunduru ambako hata umeme hakuna, barabara ya lami hakuna, maji hakuna, reli hakuna halafu ikafanyika hiyo mining ya uranium is just a HOAX.
Hata kama uranium yetu haina thamani, chetu chetu. Watanzania mnaponzwa kwa kudharau yaliyo madogo huku ndo yanawaumiza, pole sana kaka makubwa hatutoyaweza.
 
Mkuu hiyo uranium haina thamani kiasi hicho mpaka kampuni ya nje ya nchi irisk kuja kuchimba kisirisiri na after all lazima uelewe kuna masuala ya grade per ton. Jmani watanzania tunahitaji tuelimike kuhusu haya mambo sasa kama hata mbunge anaweza kuongea hii (kama ni kweli) basi tuna tatizo kubwa!!!!!! Uchimbaji industrialized si sawa na "uchoji" (uchimbaji wa sululu).

Uranuim yenye thamani kubwa ni ile enriched ambayo hata kuna baadhi ya nchi zilizoendelea kama Australia, Canada still wanauza raw (not enriched). Sasa mtu eti kwenda Tunduru ambako hata umeme hakuna, barabara ya lami hakuna, maji hakuna, reli hakuna halafu ikafanyika hiyo mining ya uranium is just a HOAX.

Tupe ukweli mbadala. Uranium huko inajulikana hata kabla ya uhuru. Na miaka ya sabini walikuwepo warusi. Unachosema ni kupotosha focus kuwa kuna shughuli zinaendelea. Bahati mbaya you are not convincing by a logical arguement.
 
Mkuu, utafiti maana yake wanachimba samples kutumia drills only. Utafiti unaweka wazi so manay things before establishing the mine. Wanatambua pattern ya mali, concentration, and how will they be extracting. Haya ni baadhi tu ya mambo wanayoyafanya kabla ya kujenga mgodi, kumuka pia, setting out, plan ya mgodi pia inaletwa na informations from exploration.

Explorations pia inaongeza thamani ya eneo, maana kila results zinapoletwa na kuthibitishwa ndivyo thamani ya kampuni ya utafiti inavyoongezeka na kudetermine meadi utakuwaje. Tusiruke ruke tu bila kijua tunafanya nini bana!!!

Hakuna mgodi huko, ni utafiti tu....

Utafiti wa nini tena jamani nchi hii watu wakija toka huko Ujerumani wanajua wapi kuna Mafuta wapi kuna Madini mbona hawaendi kufanya research Baharini kati ya Tanganyika na zanzibar si ndio kuna mafuta wakachukuwe sample basi. ni Uongo mtu we have everything ni kuchimba na hawa viongozi wetu wanataka kutu rubuni wakidhani nasi ni mazuzu tuuu. Me nilisona GESECO (Geita Secondary) pale in 1993 hakukuja watu kufanya research ni kuna Gold kule makampuni yakija ni kuchimba sasa wewe leo waniambia kuna cha research ulisha wai ona wapi ndio yale yale kila baada ya miaka mitano ati kampuni jina lingine hakuna faida mitambo ile yote yafanya nini sasa si wafunge warudi zao.
 
tatizo kubwa linalosumbua nchi hii ni kutokua n
i kutokua na viongozi wazalendo,ambao wanaipenda nchi yao nawanajali mustakabari wa nchii hii kwa vizazi vijavyo,suala la uchimbaji wa madini ya uranium lililo ibuliwa na mbunge ni swala nyeti na lilipaswa kutolewa majibu na waziri husika na si kukaa kimya,kwa nchi na viongozi makini tuhuma kama hizi zinapojitokeza na waziri akashindwa kutoa maelezo makini kujibu hoja inabidi ajiuzulu awapishe viongozi wazalendo wfanye kazi.pamoja tunajenga taifa.
 
mkuu hiyo uranium haina thamani kiasi hicho mpaka kampuni ya nje ya nchi irisk kuja kuchimba kisirisiri na after all lazima uelewe kuna masuala ya grade per ton. Jmani watanzania tunahitaji tuelimike kuhusu haya mambo sasa kama hata mbunge anaweza kuongea hii (kama ni kweli) basi tuna tatizo kubwa!!!!!! Uchimbaji industrialized si sawa na "uchoji" (uchimbaji wa sululu). Uranuim yenye thamani kubwa ni ile enriched ambayo hata kuna baadhi ya nchi zilizoendelea kama australia, canada still wanauza raw (not enriched). Sasa mtu eti kwenda tunduru ambako hata umeme hakuna, barabara ya lami hakuna, maji hakuna, reli hakuna halafu ikafanyika hiyo mining ya uranium is just a hoax.
madini ya uranium yanatengeneza mabomu ya nuclear na ni madini ya thamani sana
 
Napenda Kujau Ngeleja kabla ya kuwa mbunge na kuwa waziri alikuwa akifanya kazi kwa nani, Company ya nani, Rostam, JK, EL, au Serikalini?

Najaribu kuja Uzalendo wake umeegemea wapi?
 
Mkuu you got me wrong, nachomaanisha hiyo habari ni ya uongo period.


Sidhani kama hii habari ni ya uongo kama unavyotaka tuamini. Hii kitu imesemwa Bungeni na kwa utaratibu wa kawaida kama Mbunge angekuwa amesema uongo kingemlipukia!!! Sikusikia mtu akimwambia huyo mbunge kwamba amesema uongo. Ninaanza kuwa na wasiwasi na post zako hapa JF, kwa maana ya kwamba upo kazini labda!!!! Just kupinga na ku-neutralize hoja!!!!

Tiba
 
Mkuu ni lini processing plant ilijengwa huko Tunduru kwa ajili ya uchimbaji huo? All in all nachokiona ni kwamba watanzania wengi tumeaminishwa kwamba hiyo uranium ina thamani kubwa mno pengine kuliko madiniyeyote yale kiasi kwamba humu kuna thread kwamba Hillary Clinton alikuja bongo kwa sababu hiyo, Bush naye ni sababu hiyohiyo, kuna sijui wamarekani gani basi ilimradi ni habari za kijiwenijiwerni tu. Sasa na hii eti kuna wamarekani wanachimba huko Tunduru. Kuna watu walidiriki hata kusema kwamba migodi yote ya uranium inamilikiwa na wamarekani na kwamba mtu mwingine huruhusiwi. Cha ajabu kampuni kama Mantra ziko kwenye stock exchange!!!! Mgodi mkubwa wa uranium - Olympic dam, Australia wala si wa wamarekani.

Nachosikitika zaidi pia ni kwamba hizi sauti, na malalmiko yalistahili kuelekezwa kule Liganga mchuchuma. Kule hatujui hiyo kampuni ya kichina mkataba wake ukoje? Ukubwa waeneo watakalo dili nalo,Tutafaidikaje na hata details ndogo ndogo tu kama kujua wataanza lini mradi wenyewe haijulikani. Wakati huohuo hiyo kampuni Sichuan Hongda haijawahi kufanya hiyo shughuli, haina uzoefu na Coal pia chuma. Ule ni mradi mkubwa kuliko yote Afrika mashariki na kati lakini ni kama haupo. Ila hizi uranium projects ambazo zote combined haziwezi kufikia thamani ya investment ya Bulyanhulu zinatuchechetua na kuwa sensitized mpaka tunapoteza focus!!!!!

​Hii kampuni nimejaribu kuitafuta online, yaani haina hata website!!! Zaidi ya links zenye habari mbalimbali kuhusu kampuni hiyo!!
 
kama mkuu wake alishaolewa unategemea nini kwa yeye wala ngereja anatekeleza ndoa ya mkuu wake na USA
 
kila mbuzi atakula kwa urefu wa kamba yake.... Ivo malalamiko hayaasaidii cha msingi jitaidi kamba yako iwe ndefu


Jana mbunge wa viti maalim (CHADEMA) Naomi Amy Kaihula kasema kuwa kuna kampuni ya Kimarekani inachomba Uranium kisirisiri (clandestinely) katika wilaya ya Tunduru .

Alisema kaona kwa macho yake uchimbaji ukiwa unaendelea. Sasa cha kujiuliza mbona hili hatuna habari nalo? Mkataba wake ulisainiwa lini? environmental impact assessment ilifanywa na nani? Mkataba una worth how much? serikali inapata kiasi gani?

Lakini sitoshangaa kusikia kama huu ulikuwa ni mchongo wa BILIONEA Jairo na dumber mwenzie Ngeleja.

Why keep it secret? kwa nini wananchi hawajulishwi kinachoeendelea ndani ya maeneo yao? Hivi law & order iki break katika mazingira haya serikali itajibu nini?

Habari ndio hiyo
 
madini ya uranium yanatengeneza mabomu ya nuclear na ni madini ya thamani sana

Mkuu kwanza unapaswa uilewe sentensi kiujumla "hiyo uranium haina thamani kiasi hicho mpaka kampuni ya nje ya nchi irisk kuja kuchimba kisirisiri" halafu baada ya hapo ufahamu kuwa matumizi makubwa ya uranium ni kuzalisha umeme, na hata bei yake kwa sasa inakuwa kubwa kwa sababu China imewekeza kwa kiasi kikubwa sana kwenye nuclear power station. Bei ya Uranium kwa pound moja, ambayo ukirouind ni kama nusu kilo ni $53 kwa sasa dhahabu yenye uzito huo wa 1 pound ambayo ni almost 12 Troy Ounces kwa bei ya sasa ya 1oz = $1600 ni sawa na $19,200. Sasa sijui huo uthamani sana wa uranium uko wapi. Tujaribu kuwa tunafanya utafiti kidogo badala ya kutumia mihemko kufikiri!
 
Sidhani kama hii habari ni ya uongo kama unavyotaka tuamini. Hii kitu imesemwa Bungeni na kwa utaratibu wa kawaida kama Mbunge angekuwa amesema uongo kingemlipukia!!! Sikusikia mtu akimwambia huyo mbunge kwamba amesema uongo. Ninaanza kuwa na wasiwasi na post zako hapa JF, kwa maana ya kwamba upo kazini labda!!!! Just kupinga na ku-neutralize hoja!!!!

Tiba

Hata wa CCM?
 
Hata kama uranium yetu haina thamani, chetu chetu. Watanzania mnaponzwa kwa kudharau yaliyo madogo huku ndo yanawaumiza, pole sana kaka makubwa hatutoyaweza.

Jamani eeh! sijasema haina thamani nilichosema "hiyo uranium haina thamani kiasi hicho mpaka kampuni ya nje ya nchi irisk kuja kuchimba kisirisiri"
 
Back
Top Bottom