Siri nje kujisalimisha kwa anayedaiwa kumteka Dr. Ulimboka

Huu ni mchezo wa kitoto sana, na kwa Tanzania tusivyokua na akili tutaliamini na hili na tutaliacha lipite hivi hivi!!
Mkuu nchi imeshabadilika. Nimeona watu walivyoipokea taarifa ya Kova ukizingatia kuwa wengi walikuwa wanaangalia TV wakati Lissu anasoma hotuba yake bungeni. Hata mtu wa kijiweni huwezi kumdanganya kwa hili.
 
To me, this story is like Crucifiction of Jesus Christ of which million of silly/ignorant christians believe in Today. It was made and it really works even today. Had it been Crucifixion, that could sound somehow and lead to pure salvation.

And to my intellectual point of view this Crucifiction of Dr. Ulimboka story will work out right. Big up Kova and your intelligency team.
 
Yule mkenya anayedaiwa kumteka Dr. Ulimboka na kisha kujisalimisha kwa mchungaji Gwajima hakwenda kutubu. Katika mahojiano kati ya mtangazaji Rita Chiwalo na mmojawapo wa wachungaji wa kanisa la Ufufuo na Uzima (anaitwa Gwandu Mwangasa) , mtu huyo alifika jana kanisani hapo na kukutana na baadhi ya wachungaji akitaka apelekwe kuonana na mchungaji Gwajima. Wachungaji hao walikataa katakata kumruhusu mtu huyo mpaka pale atakapowaeleza sababu hasa ya kutaka kuonana na Mchungaji wao mkuu. Ndio mkenya yule alipodai kuwa anajambo la kumweleza mchungaji Gwajima kwa vile ndiye aliyemteka Dr. Ulimboka.

Baada ya kusikia hivyo wachungaji wale walistuka na kuamua kumkagua simu yake na kukuta ujumbe unaosema "nimefika lakini bado najaribu kuwazoea." Ni ujumbe huu ndio uliopelekea wachungaji wale kumtilia mashaka mtu yule na kumwona si wa kawaida hivyoo kuamua kumripoti polisi. Pia mtu huyu hakwenda kanisani pale kutubu zaidi ya kujitambulisha tu kuwa ndiye mtekaji. Ndipo wachungaji wale wakaona suala lile si la kikanisa tena bali la polisi.

Katika hatua nyingine mchungaji huyo ametoa onyo dhidi ya watu wanaofanya usanii makanisani kwa lengo la kufanikisha mipango ya makundi fulani. Ameonya dhidi ya dhihaka zinazofanywa katika nyumba za ibada kwa malengo binafsi na kuwa wanaofanya hivyo wanachuma laana. Amesisitiza kuwa ule ujumbe wa simu unaashiria mtu yule alikuwa na ajenda ya siri.

Ssource: WAPO radio FM.

My take... You be a judge!

Very funny.
Jambazi!!!!!
Jambazi wote wanaenda after big jobs. Sasa Dr. Uli alikuwa big job wa nini?
As far as i can tell u big deal wa Dr. Uli at the time ni bief la kuwa kiongozi wa mgomo wa madaktari, na opposing side ni Sirikali. So if you connect the dots utaona basi huo ujambazi una husisha sirikali.
Au basi labda Dr. Uli alikuwa na tu billions siku hiyo (ina motivate majambazi kukufuata).
Jambazi haamki tu na kwenda kuua for no reason.

Nje ya hapo this is very cheap for even an average tanzanian ku absorb. Kova come up with something more tangible!!!
By the way tunajua 100% the government is involved, but at least kuwa kama msomi kwenye cover up yako.
 
Hakuna kitu kama hicho kwa maoni yangu siamini kwa sababu zifuatazo
1. Mkenya afike nchini na kujua msitu wa pande kuwa kunafaa kutupa mtuyaani maficho ya mauaji.
2. Afike tu na kujua kanisa la kawe? kwa nini ameacha mengine mengi ya kilokole hapo kati kwa nini kwa huyo mchungaji? naye huyo mchungaji kala dili na wahsika.
3. Katika mazungumzo ya ulomboka angesema kuwa wabaya wake walikuwa na lafudhi za kikenya kwani ni tofauti sana na ya ki tz. TUSIDANGANYANE KABISA. WATAFUTE MBINU NYINGINE.
 
Hivi ni nani anaweza kuniambia KAKOBE yuko wapi? mbona hasikiki, iko siku nitawaeleza picha yote. Kuhusu huyu jamaa ni mbinu chafu tena za kishetani zinazotumiwa na viongozi majua kwa kushirikiana na viongozi wa dini wasiowaminifu ili kuficha ukweli. Watu wangapi wametajwa kwenye hili suala, hata mgonjwa mwenyewe amemtaja mmoja wa polisi hao lakini hakuna hata aliyehojiwa hadi ikulu wapo wametajwa kwa majina , hakuna kilichofanyika, suala la mwanza la mh, Kiwia aliwaona kwa macho yake na namba za magari zikatabuliwa lakini hakuna kilichofanyika. Leo hii wanaleta upuuzi wa kiwendawazimu namna hii, wasubiri siku zinzkuja tutapiga hata makaburi yao kama watakuwa wamekufa.

..Mkuu usiwa-attack watumishi wa Mungu, tubakie tu kwenye Mada kuu.
Mie nasema, Kova yuko under the remote control, anaelekezwa mini cha kufanya 'do this...dont do this...'
kwani umesahau ile kasi ya Mizengo alivyoanza?
 
Kama hii ndivyo ilivyokuwa then 'usalama wa taifa' unasikitisha sana.......

This is too low jamani.....khaaaaa

Yule mkenya anayedaiwa kumteka Dr. Ulimboka na kisha kujisalimisha kwa mchungaji Gwajima hakwenda kutubu. Katika mahojiano kati ya mtangazaji Rita Chiwalo na mmojawapo wa wachungaji wa kanisa la Ufufuo na Uzima (anaitwa Gwandu Mwangasa) , mtu huyo alifika jana kanisani hapo na kukutana na baadhi ya wachungaji akitaka apelekwe kuonana na mchungaji Gwajima. Wachungaji hao walikataa katakata kumruhusu mtu huyo mpaka pale atakapowaeleza sababu hasa ya kutaka kuonana na Mchungaji wao mkuu. Ndio mkenya yule alipodai kuwa anajambo la kumweleza mchungaji Gwajima kwa vile ndiye aliyemteka Dr. Ulimboka.

Baada ya kusikia hivyo wachungaji wale walistuka na kuamua kumkagua simu yake na kukuta ujumbe unaosema "nimefika lakini bado najaribu kuwazoea." Ni ujumbe huu ndio uliopelekea wachungaji wale kumtilia mashaka mtu yule na kumwona si wa kawaida hivyoo kuamua kumripoti polisi. Pia mtu huyu hakwenda kanisani pale kutubu zaidi ya kujitambulisha tu kuwa ndiye mtekaji. Ndipo wachungaji wale wakaona suala lile si la kikanisa tena bali la polisi.

Katika hatua nyingine mchungaji huyo ametoa onyo dhidi ya watu wanaofanya usanii makanisani kwa lengo la kufanikisha mipango ya makundi fulani. Ameonya dhidi ya dhihaka zinazofanywa katika nyumba za ibada kwa malengo binafsi na kuwa wanaofanya hivyo wanachuma laana. Amesisitiza kuwa ule ujumbe wa simu unaashiria mtu yule alikuwa na ajenda ya siri.

Ssource: WAPO radio FM.

My take... You be a judge!
 
Mkuu nakupa big up sana Hebu tujiulize hivi kweli kijana mkenya ateke mtu kazi imalizike iwe kwa mafanikioa ama la walikuwa na sababu gani ya kumwacha hapa Tanzania? Pili je yeye kama ni jasusi kweli kazi yake haikufanikiwa walishindwa kumdhibiti hadi amwache eti aende kwenye maungamo? Haya sasa limekuja hili kwammba hakwenda kutubu bali kufanya uhalifu mwingine na sasa this time anamshirikisha hadi Gwajima, swali la msingi je huyu Gwajima alikuwa na interest gani na ulimboka?

hivi kunashida gani sisi wenye akili tukiona kama vile inatengenezwa fiction ground ambayo wataalaam wa criminal minds and investigation tunaweza kusoma kwamba kijana huyu siyo muhusika kwenye hili bali wanamtengenezea platform ili kuhadaa wenye akili? uzuri ni kwamba Ulimboka can tell us kama ndiye aliye muona ama la.

Jamani kinachotokea hapa siyo kwamba havipo vipo kabisa na TISS wanauwezo wa kutengeneza platform kwa kutumia records za most crimanals ili kusadikikisha watanzania wakijua kuwa sisi ni mambumbu. wasiunderestimate we can even do surveillance though GIS and see what happened and who were present at scene. tumeona GIS ikitumika kwenye criminal detection sehem nyingi ulimwenguni and now tunaowataalam wa GIS hata kama ni kwa kuchangia wengne tupo tayari we have to stop this foolish.

GIS = Geographical Information System

GPS = Global Positioning System

Tofauti za teknolojia hizi ni kwamba:

1. GIS inahusika zaidi na upimaji ramani (ingawa hata GPS inahusika) na survey, kwa mifumo ya maji, barabara, n.k.

2. GPS inahusika zaidi na ACTUAL LOCATION kwa kutumia GPS=enabled device. Inasadikiwa kwamba kila mobile phone inaweza kuonekana kwenye mitambo ya satellite inayotumia GPS, kwa hiyo, iwapo wana-usalama wanataka kujua mtu fulani yuko wapi, wakipata namba ya simu yake, wanaweza kumwona mahali alipo. Hapa ndipo "monitoring and surveilance" vinaweza kufanya kazi ya kumtafuta mtu yeyote.

TIP: Kama unataka usionekane (off the grid) kwa muda fulani, fanya yafuatayo.

1. Fungua simu yako. Toa betri.

2. Toa SIM card, weka pembeni.

3. Fanya shughuli zako kisha ukimaliza, rudisha SIM card na betri.

Usidanganyike. Hata kama simu yako imezimwa, na kila kitu (betri na SIM card) vimo ndani yake, wana-usalama WANAWEZA KUKUONA kupitia satellite kwa urahisi mkubwa.

Ndugu yangu "manshiroo" nadhani umenielewa. Katika hicho unachokizungumzia, GIS haina uhusiano wowote ule na criminal investigations. Teknolojia inayotumika ulimwenguni ni GPS. Hata kama simu yako sio GPS-enabled, BADO wanausalama wanaweza kuiona. Uwezo huo wanao.
 
yaani uliona wapi mtu anakuja kuombewa wewe unachukua simu yake kuipekua duh kichefu chefu cha mwaka!
usijifanye huijui Tz mkuu, hujasikia/kuona tangazo ambalo linasema "wanafunzi 5000 waliomaliza sekondari hawajui kuandika majina yao pamoja na kujumulisha"?.
Sasa unadhani hao wanafunzi wamejizaa??? ...si wametokana na sisi wenyewe?? Sasa ni tangia lini mgomba ukazaa kiazi!?
 
Mie mwenyewe niliposikia kwenye taarifa nikajichekea moyoni na kuona changa la macho la hali ya juu. Nafikiri ni muda muafaka kwa jeshi letu la polisi kutuma watumishi wake Mossad/KGB/CIA wakapigwe brashi. Kwenye msafara wasiwaache Kova na Mwema.
 
yaani uliona wapi mtu anakuja kuombewa wewe unachukua simu yake kuipekua duh kichefu chefu cha mwaka!

sasa na wewe unataka kuwa kama kova?!!! mbona taarifa inasema alikuwa hajaanza kuombewa na baada ya yeye kusema anahusika na utekwaji wa ilimboka ndipo hapo hao watu aliowakuta hapo kanisani walimtilia shaka na katika harakati hizo ndipo walipkekuwa simu....mbona ni kitu kidogo tu..ningekuona una akili kama ungeuliza ilikuwaje akawapa simu yake, mazingira yapi yalipelekea hadi akatoa simu na wao hao watu wakaipekua....
 
GIS = Geographical Information System

GPS = Global Positioning System

Tofauti za teknolojia hizi ni kwamba:

1. GIS inahusika zaidi na upimaji ramani (ingawa hata GPS inahusika) na survey, kwa mifumo ya maji, barabara, n.k.

2. GPS inahusika zaidi na ACTUAL LOCATION kwa kutumia GPS=enabled device. Inasadikiwa kwamba kila mobile phone inaweza kuonekana kwenye mitambo ya satellite inayotumia GPS, kwa hiyo, iwapo wana-usalama wanataka kujua mtu fulani yuko wapi, wakipata namba ya simu yake, wanaweza kumwona mahali alipo. Hapa ndipo "monitoring and surveilance" vinaweza kufanya kazi ya kumtafuta mtu yeyote.

TIP: Kama unataka usionekane (off the grid) kwa muda fulani, fanya yafuatayo.

1. Fungua simu yako. Toa betri.

2. Toa SIM card, weka pembeni.

3. Fanya shughuli zako kisha ukimaliza, rudisha SIM card na betri.

Usidanganyike. Hata kama simu yako imezimwa, na kila kitu (betri na SIM card) vimo ndani yake, wana-usalama WANAWEZA KUKUONA kupitia satellite kwa urahisi mkubwa.

Ndugu yangu "manshiroo" nadhani umenielewa. Katika hicho unachokizungumzia, GIS haina uhusiano wowote ule na criminal investigations. Teknolojia inayotumika ulimwenguni ni GPS. Hata kama simu yako sio GPS-enabled, BADO wanausalama wanaweza kuiona. Uwezo huo wanao.

hivi kumbe eeh ngoja kwanza nirudi nikapige nyanga yangu moja najua nitaipata tu halafu nikuprovie kwamba inaweza ama la lakin pia call it wereva ila si posibility ya kufanya criminal investigation hiyo kwa kutumia satellite ipo? basi twaweza kufanya kukata mzizi wa fitina.

ngoja nimtafute mwl kijana Charles.......... sijui kasharudi toka china i think anaweza kunifundisha vizuri hizi tofauti. lakin mkuu nikupongeze tu manake miye shule ya GIS mbona ilinishinda best niliklia kwa B ma plain nake sijui yanaitwa arch view mara sijui arch GIS mara sijui GPS kwangu mimi niliona ni ushetani tu lol. BUT Dr Joel Nobert alijitahd sana na marehem Dr Kimaro (RIP)
 
Hakuna shaka kuwa huu ni usanii. Kinachonisikitisha zaidi ni kuwa kwa jinsi movie hii ilivyochorwa inaonekana kwa kiasi kikubwa kanisa husika lilihusishwa na njama hizi? Kwanini waripoti polisi haraka haraka hivyo? Kwani huyu lagai angetubu tu nakuishia kuwa muumini mzuri mipango ya polisi ingefanikiwa kivipi? Kwa hiyo hapa mpango ulikuwa umepangwa kupitia kanisa hili. Nakumbuka jina la Gwajima limetajwa mara nyingi tu hapa JF kujihusisha na serikali. Hii hatari.
 
Changa la macho, ile sms waloikuta kwenye simu yake huyo anayejiita mkenya inaonekana ilikuwa ni movie fulani kwamba 'nimefika najaribu kuwazoea'.
1.Huenda wameitengeneza wapelelezi wa sakata hili lililofanywa na wendawazimu walomjeruhi Dr Ulimboka

2. Kama kweli ni jambazi sijaona kama wamemtumia vizuri huyo anayejiita jambazi pamoja na maneno yake ya kwenye simu yake ku trace ni nani alikuwa akiwasiliana nae (Je ni watekaji wenzake au ni hawa wanaohisiwa kuwa ni wahusika wa ishu ya Dr. Uli.
 
Ni kanisa katoliki tu ambalo waumini wake uenda kutubu kwa Padri. Makanisa mengine hawana utaratibu huo. Inakuwaje jambazi anaenda kutubu kwa mchungaji. Kama jambazi sugu, kwa nini aliendelea kukaa nchini wakati anajua ameshafanya uhalifu.
Kweli Kova unawafanya Watanzania wajinga kweli
 
Ingekuwa rahisi ku-conceal identity ya huyu "mkenya mtekaji" na kutangaza kuwa "kuna mtuhumiwa tunamshikilia ambaye anahusishwa utekaji na kujeruhi vibaya Dr Ulimboka na upelelezi unaendelea"...!

Otherwise, kama wana-Usalama (TISS & Police Force) wetu ndiyo wako hivi katika kupanga tukio hili wajisafishe basi hili ni JANGA KUBWA SANA kitaifa...!
 
Wana JF,heri sisi tuna ufahamu wa kujua haya mambo kwamba si kweli hii report lakin nimejaribu kupita uswahilini na kuwasikiliza wanavyozungumzia hii issu ya kukamatwa kwa mkenya feki yani wanaamini kabisa kwamba ni kweli daaaa yani kova anawadanganya watz wasio na upeo kiasi hiki?
 
Usanii-taka kati ya vyombo vya dini na vyombo vya dola:
Onyesho la Kwanza
- Mgomo umeanza, siku chache baadae Dr. Ulimboka atekwa na kupelekwa Chaka la Mauti
- Vyombo vya dola vyahusishwa na wanaharakati wanadai uchunguzi huru, baadhi ya wabunge wataka suala lijadiliwe bungeni.
- Serikali yakataa katakata, Liwalo na Liwe,yaunda tume na kuwajumuisha washukiwa bila ya kuwashirikia wenye madai.
- Mhe. Raisi atoa hotuba ya maandishi akiwa uhamishoni na kutoa fatwa juu ya waliogoma, wakati kesi iko mahakamani.

Onyesho la Pilli
- Viongozi wa dini wakutana na madaktari waliogoma, wawataka wagomaji kuomba radhi
- BAKWATA wajitoa mazungumzo na wanataka kuwashitaki wagomaji.
........
........
........
- Zaidi ya wiki mbili zimepita, si tume huru wala intelijensia bado hawajui nani alihusika kwa hivyo hajakamatwa mtu yeyote.
- Baada ya siku 17 tangu kutekwa kwa Dr. Ulimboka, Jambazi Sugu, Mkenya, ajisalimisha kwa chombo cha dini [kile kile kilichowataka madaktari waombe radhi] yeye ndie aliyemteka Ulimboka na kumpeleka kule kule Chaka la Mauti ambalo nyuma walipelekwa wengine na kuuwawa huko.

Drama itaendelea wiki ijayo
 
Back
Top Bottom