Siri nje kujisalimisha kwa anayedaiwa kumteka Dr. Ulimboka

tatizo la kazi ya upolisi wanaoifanya ni failures. ushahidi ni jinsi walivyofoji vyeti vya form 4 ili wajiunge na jeshi hilo. viazi vingi sana mle.
 
Kova uko wapi?

Anaandaa maigizo mengine! Huu sasa ushakuwa us*ge! Yaani hata mtoto wa miaka 7 mwenye akili nzuri hawezi amini wanachofanya hawa polisi!

Kweli naanza kuamini maneno ya jamaa yangu aliyesema polisi sasa ni ya wale walioshindwa kielimu kwingine kote! Wanashindwa hata kudanganya kiakili? Shame on you Kova and your boys!
 
Kwanin asipigwe picha then docta Uli athibitishe kama ni kati ya wale aliowaona wakimteka...??!!
 
Huyo jamaa mkenya wala
sio muhusika wa tukio nahisi. Tokea lini muhusika akaenda kujisalimisha
kiulaini namna hiyo?. Huu ni mchezo ambao Usalama wa Taifa wamepanga
kuucheza kwa nia ya kuficha kilichotokea na wahusika halisi wa
tukio.

Yaani ndgu yangu inasikitisha mno jinsi uwt wanavyofanya kazi za kijinga kabisa!
Na angalia kila hatua wanakosea, yule anaedaiwa mkenya kumbe walikuwa wanamwongoza wenyewe kina jack zocka!
Mungu anazidi kuwaumbua!
 
Nilimsikia Kova ITV akisema Mkenya huyo kasema kuna mkono wa Serikali,lakini kova alikuwa akiongea kama mtu aliyekuwa akibabaika!kazi ipo.
 
Nashindwa kuelewa.. Inakuaje mtu uliye juu katika ngazi UOFISA. Tena Kanda Maalum..
Uliyetokea kukubalika na Kuheshimika kwa Wananchi na Kuwa sehemu ya Imamni yao kwako,
Unageuka MBUMBUMBU NA MCHANGA katika kufikiri kiasi hiki..
KOVA!!!! Kamanda ambaye ulijizolea Sifa kubwa kwa Operesheni zako za ukweli... Lakini sasa UMEKUBALI KUNUNULIWA KIRAHISI KIASI HIKI?

SASA!!!!
Tambua umekua miongoni mwa WALAANIWA ktk Taifa hili..
Tambua kuwa umekua Watanzania wa leo ni si wale wa MIAKA ILEEE ya 60.... WANAJUA UIGIZAJI HUU UNAOUFANYA.....
Aibu yako HII...
 
ficha upumbavu wako wewe ***** wapi walioripoti ccm imeusika uzuri jamaa kaenda kanisan kujisalimisha we unaleta maswala ya kijinga jinga hapa serikal aina dini.jitaid uonekane umesoma we pimbi ,jitu zima njaa zinakufanya unajirudisha utoto kumbuka unategemewa na jamaa zako usiuze u2 wako 2cheep fku


@bydefault
Mkuu taratibu nadhani hukumsoma vzr, post yake ameiweka kiutani kidogo.

Hakustahili karipio kali kiasi hicho hata kama alimaanisha alichoandika.

Uwe na amani..
 
Nashindwa kuelewa.. Inakuaje mtu uliye juu katika ngazi UOFISA. Tena Kanda Maalum..
Uliyetokea kukubalika na Kuheshimika kwa Wananchi na Kuwa sehemu ya Imamni yao kwako,
Unageuka MBUMBUMBU NA MCHANGA katika kufikiri kiasi hiki..
KOVA!!!! Kamanda ambaye ulijizolea Sifa kubwa kwa Operesheni zako za ukweli... Lakini sasa UMEKUBALI KUNUNULIWA KIRAHISI KIASI HIKI?

SASA!!!!
Tambua umekua miongoni mwa WALAANIWA ktk Taifa hili..
Tambua kuwa umekua Watanzania wa leo ni si wale wa MIAKA ILEEE ya 60.... WANAJUA UIGIZAJI HUU UNAOUFANYA.....
Aibu yako HII...


kama unakumbuka kun member mmoja liweka riport humu juu ya njma za polis..na akadai kuwa kova ameambia ahakikishe anaisfisha serikali...ile riport sijui iko wapi ...kama kuna mtu anayo aitupie hapa maana kova kwa asilimi 92 amepita mle mle kwenye ile report....
 
mimi nilifikiri limeenda kudai malipo ya kazi.
kwa nini lisiende kutubu kenya,huko hakuna makanisa?
jamani uongo mwingine jaribuni kuuvalisha hata sweta,kwa nini lipelekwe mahakamani haraka?mbona wale wa mtalii wengine bado wanatafutwa na upelelezi unaendelea?
ulimboka kasema walikuwa kama wanne hakuna sababu ya kufanya upelelezi kwanza na kujua hao watatu ni kina nani kabla ya kukimbilia mahakamani?
huyo mkenya aliyetesa raia mliyeapa kumlinda kwa nini msimng'oe meno na kucha hadi aseme alikuwa na nani?
au na nyie ni polisi wa kenya mliyeapa kulinda raia wa kenya anayetesa na kuumiza mtanzania?

kova kazi unayo.
 
Balozi wa Kenya uko wapi uraia wa nchi yako unachakachuliwa na Kova? kwamba Wakenya ndo makatili sana?? Mbona Lisu alishataja orodha jana ambayo sijasikia kupelekwa mahakamani?
 
Kinachoniudhi ni jinsi akili za watanzania zinavyofanywa kuwa viza kila na siku na vyombo vya usalama. Polisi waliwezaje kumfikisha huyo mtu mahakamani with story kama hiyo, inanikumbusha yuke Dumisani Dube, aliyemgonga marehemu Sokoine. Huu mchezo wa kuua watu haujaanza juzi, umeanza siku nyingi na wanapandikizwa watu wa kutoka nje, huyu mkenya kapandikizwa kama alivyopandikizwa Dumisani Dube aliyetokea ANC ya South Africa

Tangu lini jambazi, mwenye kikundi cha ujambazi, anayejihusisha na silaha, ajisalimishe kwa tukio kama la Ulimboka ambaye wala hajafa.Kama ni jambazi sugu, amefanya mangapi makubwa kabla, why atubu kwa hili tukio moja tu. Kama ni kujisalimisha, aliacha makanisa mangapi hadi aende hilo? mbona hakwenda polisi? Polisi sio vyema kuwafanya watanzania viazi kiasi hicho, it is shameful kwa nchi kama Tanzania kuwa na jeshi la polisi lenye kuwafanya watanzania wapumbavu

Yaani hili suala litazidi kulidhalilisha jeshi la police, Tiss na serikali kwa ujumla wake.

Serikali ilikuwa ipo katika kujipanga jinsi ya kuwadanganya wananchi juu ya suala la Ulimboka na njia zote zilizokuwa evaluated hazikuwa na matunda au positive results kwa wananchi.

Hamadi amejitokeza mjinga huyo mmoja serikali, tiss na police wakaona ni loopwhole ya kutokea katika suala ambalo tayari wananchi wanaamini ni serikali inahusika.

Kuthibitisha uongo wa Kova jiulizeni maswali haya,

1.0 Professional criminala hawezi kutomjua boss wake ipasavyo kwani vizuri. Hii ni dhana ambayo Kova alishindwa kabisa khisafisha serikali mpaka kufikia kusema hajui kama ni mserikali au laaaah.

2.0 Hajasema ameingia nchini lini, passport yake ni feki au kweli??? Je walikuja tu kwa ajili ya Dr. Ulimboka au walikuwa na 50 zao ndiyo hiyo jamaa anayefahamu wakenya wahalifu akampa kazi?????

3.0 Inawezekana Kova akatumia hii ili kuzima tuhuma za akina Mnyika na Dr. Slaa kujadiliwa kuwa system ilitaka kuwadhuru kwa kuanzisha jambo lingine litakalo draw tension kubwa kwa wananchi.
 
ERASTO SYL Tangu jana nilikuwa nataabika akilini kuwaza ni majambazi sugu wangapi wanakwenda makanisani kufanya confession na kisha kuwa waumini wazuri tu wa makanissa bila taarifa zao kuripotiwa polisi. Why this time!
Pastor Mwansasu alikuwa Criminal wa kutumia Machine gun, lakini alizisalimisha kwenye counter ya polisi Mbeya baada ya Kutubu, Record ipo. Pastor Lusekelo aliacha U-Gangster na madawa baada ya kutubu Record ipo Iringa. Pastor Mwiru huyu alikuwa 'Super' Maana alikuwa na Skeleton Master-Key zenye uwezo wa kufungua mageti yote. Baada ya kutumikia kifungo akatubu na amekabidhi zana zote kwa Polisi Nairobi Record ipo,
Vipi huyu Kanyanga...isiwachanganye sana hii
 
That is a problem of being clever among the fools! Sasa hawa ndiyo thinkers na planners wa TISS na Polisi. Tangu utotoni baba yangu alikuwa akinionya nisijiunge na chombo chochote cha kijeshi/usalama kwasababu ukiwa askari unasalimishi akili yako kwa mtawala, yaani unampa UBONGO wako yeye anakuwekea UBUYU ndani ya kichwa chako. Matokeo yake unakuwa below IQ, na kama mtawala naturally yuko below IQ.Hii inaonyesha nikiasi gani aliyetunga jambo hili alivyo na UBUYU badala ya ubongo ndani ya kichwa chake na kuonyesha jinsi vyombo vya usalama vilivyo jaa watu walio below IQ!.
 
halafu mi najua kuwa watu hasa wakristo wakatoliki ndo huwa wanaenda kutubu kwa padre au askofu...sasa hivi hawa walokole nao huwa wanaenda kutubu kwa mchungaji au wao huwa wanashuhudia hadharani!!!
 
Yule mkenya anayedaiwa kumteka Dr. Ulimboka na kisha kujisalimisha kwa mchungaji Gwajima hakwenda kutubu. Katika mahojiano kati ya mtangazaji Rita Chiwalo na mmojawapo wa wachungaji wa kanisa la Ufufuo na Uzima (anaitwa Gwandu Mwangasa) , mtu huyo alifika jana kanisani hapo na kukutana na baadhi ya wachungaji akitaka apelekwe kuonana na mchungaji Gwajima. Wachungaji hao walikataa katakata kumruhusu mtu huyo mpaka pale atakapowaeleza sababu hasa ya kutaka kuonana na Mchungaji wao mkuu. Ndio mkenya yule alipodai kuwa anajambo la kumweleza mchungaji Gwajima kwa vile ndiye aliyemteka Dr. Ulimboka.

Baada ya kusikia hivyo wachungaji wale walistuka na kuamua kumkagua simu yake na kukuta ujumbe unaosema "nimefika lakini bado najaribu kuwazoea." Ni ujumbe huu ndio uliopelekea wachungaji wale kumtilia mashaka mtu yule na kumwona si wa kawaida hivyoo kuamua kumripoti polisi. Pia mtu huyu hakwenda kanisani pale kutubu zaidi ya kujitambulisha tu kuwa ndiye mtekaji. Ndipo wachungaji wale wakaona suala lile si la kikanisa tena bali la polisi.

Katika hatua nyingine mchungaji huyo ametoa onyo dhidi ya watu wanaofanya usanii makanisani kwa lengo la kufanikisha mipango ya makundi fulani. Ameonya dhidi ya dhihaka zinazofanywa katika nyumba za ibada kwa malengo binafsi na kuwa wanaofanya hivyo wanachuma laana. Amesisitiza kuwa ule ujumbe wa simu unaashiria mtu yule alikuwa na ajenda ya siri.

Ssource: WAPO radio FM.

My take... You be a judge!

Namwamini sana Mchungaji Gwajima, naomba kwa hili aombe sana Mungu alifunue wazi maana Serikali wanataka kucheza mchezo mchafu na kumchafua Mtumishi wa Mungu tunayemwamini, asije fikiri serikali inampenda bali ni kwamba wanataka kumwiingiza kwenye chuki fulani dhidi ya wananchi..Mchungaji Gwajima namshauri kuwa huu ni muda muafaka kwake kuonyesha kuwa Mungu hashiriki uhalifu, afanye maombi hawa wahalifu waumbuke mara moja na serikali yao..Naamini sana ktk maombi na nguvu ya Mungu
 
ficha upumbavu wako wewe ***** wapi walioripoti ccm imeusika uzuri jamaa kaenda kanisan kujisalimisha we unaleta maswala ya kijinga jinga hapa serikal aina dini.jitaid uonekane umesoma we pimbi ,jitu zima njaa zinakufanya unajirudisha utoto kumbuka unategemewa na jamaa zako usiuze u2 wako 2cheep fku

Aiseeeeeeeeeee,yaani nyie ccm na polisi wenu plus your weak government mtatukana sana mwaka huu,the issue ni kwamba ccm na serikali yake walitaka kumuua dk.ulimboka, full stop. njoo utukane tena
 
Back
Top Bottom