Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 33,474
- 39,987
Pamoja na uhuru wa Rais kuteua kutoka mapendekezo ya makundi, ni sahihi kuhoji kwa nini ateue chaguo la tatu na siyo la kwanza na la pili.
Naelewa tume haina kauli ya mwisho juu ya katiba, lakini wakiishaandika draft na kuacha mengine, inakua vigumu kuyaondoa. Serikali inafanya makosa kujaribu kudhibiti mchakato huu maana hakuna serikali ya milele mahali popote. Katiba ikiwa mbaya wajue itatumika kuwakandamiza wao watakapokuwa wapinzani.
Mkuu wangu, haya ni matokeo ya kukubali CCM iendeshe mchakato wa Katiba Mpya kitu ambacho hakijawahi kuwa ajenda yao wala ilani yao. CDM na wale waliokubali Rais awe na nguvu alizonazo kwa kweli hawana haki ya kulalamika sasa. Ama waamue kushirikie na kupokea kitakacholetwa mezani au wakatae mapema kabla mchakato wenyewe haujaiva. Kwa mfano, kwanini walikubali sheria ambayo Rais anateua hadi mwenyekiti wa tume; kwanini asingeteua hao wajumbe wa tume na wao watakapokutana baada ya kuapishwa ndio wangechagua uongozi wao kutoka miongoni mwao?