Wote wanafaa, kwa amoni yangu uteuzi huu ni mwanzo mzuri, tumwombe Mungu tufikie huko tunakotarajia" Katiba Muafaka'
Mimi hii tume naipa only 40%. Ni watu wachache ninaowaamini. 1. Salim Ahmed Salim. 2. Prof Baregu 3. Dr sengondo.nashangaa watanzania wengi kuishabikia tume hii aliyoiunda JK, siikandii na nakiri kuwa ina watu makini lakini tatizo langu linakuja kwenye uwakilishi wa makundi mbalimbali kama sheria inavyojipambanua. kama sikosei tume inaundwa 80% na wanasiasa na viongozi wastaafu kwa nini? wafanyakazi kma walipakodi wakubwa wa nchi hii wanawakilishwa na nani? vijana je? ebu tuangalie kundi lingine wazee uwakilishi wao upo wapi? au watasema kwa sababu akina butiku, warioba, ramadhani ni wazee wanatosha! hapana tunataka mzee yule anayejua jinsi wenzake wanavyosotea dawa pale mwananyamala hospitali na mwisho wa siku wanaambia wakanunue wakati tayari walishapewa msamaha watibiwe bure. wakulima je? vipi makundi ya dini?. jamani nchi hii siyo ya wanasiasa na viongozi wasitaafu na waliopo kwenye system. rais kajitahidi lakini azingatie uwakilishi wa makundi
Ukijua siri zao utajua kama maoni unayotoa yatazingatiwa au yataachwa kwa maagizo ya serikali. Kwa mfano kuna huyu Humphrey Polepole ambaye ameingia kama mwakilishi wa asasi za kiraia. Huyu mkutano wa kupendekeza jina lake kule Dodoma ulivurugika, pamoja kusaidiwa na Ikulu baada ya ya mkutano wake na Kikwete bado alishika nafasi ya tatu. Mapendekezo ya asasi za kiraia wa kwanza alikuwa John Ulanga, wa pili Profesa Ruth Meena wa TGNP lakini Kikwete amewaacha wote akamchukua huyu.
Msimamo wake unajulikana kabla kwa kuwa mara zote alivyozungumza na vyombo vya habari kuhusu muswada mbovu wa sheria ya katiba uliokataliwa na asasi za kiraia yeye alitofautiana na wenzake na kuunga mkono. Uchaguzi ule wa Dodoma tulishuhudia NGO zenye utii kwa serikali zikieleza kuwa haziwataki wanasheria kama Wakili Harold Sungusia wa LHRC kwenye tume ya katiba kwa kuwa atakwenda kupingana na serikali. Hivyo wakataka Kikwete amchague Polepole kutoka TYC ili NGO ambazo zimekuwa zikichochea wananchi nchini kuhusu katiba zisipate uwakilishi wenye nguvu ndani ya tume.
PM
Duh huyo Polepole kumbe ndio yule dogo wa Azania!? aisee...
PM kala kona kama yule ndugu yetu Hutaki Unaacha?paparazi muwazi karudi kundini kumwaga cheche
Wote wanafaa watanganyika na wazanzibar
wapeni nafasi
acheni majungu
Tango,
Kwani wakristo na wayahudi ni moja?
Mbona nyerere alifukuza Wa israel akakata mahusiano ya ki diplomasia? Hapo utasemaje?
Nyerere aliwafukuza Wayahudi au israel? Mbona unachanganya habari?