Siri kashfa ya EPA hadharani

Candid Scope

JF-Expert Member
Nov 8, 2010
11,883
6,884
• Mnyika amwandikia barua Spika kutaka ufafanuzi

WAKATI utata wa sh bilioni 135 zilizoibwa katika Benki Kuu ya Tanzania (BoT), kupitia Akaunti ya Madeni ya Nje (EPA), unaendelea kuligubika taifa, imebainika kuwa serikali imeamua kulibeba deni hilo na kuliingiza katika deni la taifa. Chini ya utaratibu huo, serikali italilipa deni hilo kwa riba na hadi deni hilo litakapo iva, serikali italazimika kulipa sh bilioni 230 badala ya sh bilioni 137.7 zilizoibwa na wajanja.

Hali hiyo imebainishwa katika taarifa ya Mkaguzi na Mdhibiti wa Hesabu za Serikali (CAG) katika ripoti yake ya fedha za Serikali Kuu kwa mwaka ulioishia Juni 30 2009, fungu 22 kuhusu deni la taifa na matumizi mengine ya taifa.

Kwa mujibu wa ripoti hiyo, serikali imebadilisha deni katika Akaunti ya Malipo ya Nje (EPA) la sh bilioni 137.7 kuwa dhamana ya serikali zitakazolipwa kwa riba ya kiwango cha sh bilioni 11.50 katika kipindi cha miaka 20 kilichopitishwa . Kwa hali hiyo, deni lote ambalo linapaswa kulipwa na serikali kwa riba litafikia sh bilioni 230, hivyo kulifanya taifa kubeba deni la EPA.


Hatua hiyo ambayo inazidisha mzigo wa madeni kwa serikali, imemfanya Mbunge wa Ubungo, John Mnyika, kumwandikia barua Spika wa Bunge, Anne Makinda akitaka ufafanuzi juu ya wizi wa EPA, kupitia Kampuni ya Kagoda.

"Mheshimiwa Spika, haya yanafanyika bila Bunge lako kushirikishwa kwa ukamilifu ikiwemo kutaarifiwa makampuni ambayo yamerejesha fedha za EPA, kiasi kilichorejeshwa kwa kila kampuni na orodha ya makampuni ambayo hayajarejesha pamoja na wamiliki wake, mojawapo ya makampuni hayo ikiwa ni Kagoda," alisema Mnyika.


Kabla ya kufikia uamuzi wa kulibeba deni hilo, serikali iliunda tume ya watu watatu kuchunguza na kubaini wezi wa fedha hizo na kuzirejesha bila kufikishwa mahakamani. Hata hivyo taarifa ya tume hiyo iliyoongozwa na Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini (IGP), Said Mwema, imebaki kuwa siri, kwani haijulikani watuhumiwa gani wamerejesha, kiasi cha pesa kilichopatika na kiasi cha fedha kilichobaki mikononi mwa watuhumiwa wengine.


Uchunguzi uliofanywa na Tanzania Daima kuhusiana na hatua hiyo ya serikali kuingiza fedha za wizi wa EPA katika deni la taifa, ndio uliosababisha Mbunge wa Ubungo, John Mnyika, kuuliza swali bungeni.

Mnyika akiuliza swali la nyongeza juzi, alitaka kujua uchunguzi wa wizi wa fedha za EPA kupitia Kampuni ya Kagoda, umefikia wapi. Lakini wakati akijibu swali hilo, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (Utawala Bora), Mathias Chikawe, alijibu kwa kifupi sana kwamba serikali bado inaendelea na uchunguzi wa tuhuma dhidi ya kampuni hiyo.


Hata hivyo uchunguzi zaidi uliofanywa na gazeti hili, umebaini kuwa Mnyika amemwandikia barua Spika wa Bunge, Anne Makinda, akieleza kutoridhishwa kwake na majibu ya Waziri Chikawe kuhusu uchunguzi juu ya Kampuni ya Kagoda ilivyohusika na wizi wa fedha za EPA.

"Utakumbuka kwamba katika mkutano wa tatu wa Bunge, kikao cha kwanza, Aprili 5 mwaka huu, niliuliza swali la nyongeza kutokana na swali la msingi namba nne kwa Ofisi ya Rais (Utawala Bora).

"Katika swali hilo nilihoji serikali itoe kauli kuhusu hatua zilizochukuliwa kuhusiana na Kampuni ya Kagoda Agricultural Limited na kukumbusha kwamba serikali imekuwa ikitoa ahadi za mara kwa mara bungeni kuwa uchunguzi unaendelea kwa kushirikiana na vyombo vya kimataifa. Niliuliza ni lini uchunguzi huo utakamilika? "Katika majibu yake, waziri alitoa jibu fupi kwamba uchunguzi bado unaendelea, bila kutoa majibu ya ukamilifu kama Kanuni za Kudumu za Bunge (Toleo la 2007) kifungu 46 (1), kinavyohitaji," alisema.


Mnyika alisema kwa ajili hiyo, anaomba kuwasilisha maelezo yafuatayo bungeni kwa mujibu wa kanuni ya 50 na ya 28 ili kuitaka serikali kutoa majibu ya ukamilifu kwa kuwa miaka takriban mitatu imepita toka uchunguzi husika uanze. Ikumbukwe kwamba Kagoda inatuhumiwa kuchota jumla ya dola za Marekani 30,732,658.82 (sh 40 bilioni) katika Akanuti ya Madeni ya Nje (EPA), ndani ya BoT. Fedha hizi na nyingine zipatazo sh bil. 73 zilichotwa katika kipindi cha kuelekea Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2005.


Serikali imekuwa ikitoa kauli za kujichanganya kuhusu ufisadi wa Kagoda. Mathalani Septemba 15, 2006, Waziri wa Fedha wakati huo, Zakia Meghji, aliwaandikia wakaguzi wa hesabu wa Kampuni ya Deloitte & Touche ya Afrika Kusini akisema, fedha za Kagoda zilitumika kwa "kazi za usalama wa taifa." Nyaraka mbalimbali, zinaonyesha kuwa cheti cha usajili wa Kagoda Na. 54040 kilichotolewa na Ofisi ya Wakala wa Usajili wa Leseni za Biashara na Makampuni (BRELA), kinaonyesha Kagoda ilisajiliwa Septemba 29, 2005 na waliohusika kuisajili wanatajwa kwa majina. Hadi sasa siri za ufisadi wa kampuni hiyo na kampuni nyingine zilizohusika na wizi wa fedha za EPA zimebaki kwa Rais Jakaya Kikwete, Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP), Said Mwema, Mkurugezi wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU), Edward Hoseah na Johnson Mwanyika, ambao walikuwa wajumbe wa Kamati Maalumu ya Rais ya kufuatilia walioiba benki.



Tanzania Daima
 
haya mambo haya muda si mrefu Bongo kutanuka tene sio kidogo kutanuka mpaka watu watashangaa

Rais wa burundi aliwahi kusema Bongo haina amani bali watu hawajui na ndo wanaanza kujua yaani sipati picha
 
Hawa mpaka siku tukiwa na Katiba mpya itakayoondoa madaraka ya Rais tutawakamata wote hawa!
 
Unajua Spika naye inawezekana alipata Mgao wa hayo Mabilioni ,naye si amepandikizwa na CCM na Mafisadi kwa kiinimacho cha kuweka spika Mwanamke? Tutarajie kusikia Majibu yake ya Mkato,nyodo na Mbwembwe kama ambavyo huwa anamjibu Tundu Lisu hasa utasikia ''kanuni..namba...ya Bunge inanipa mamlaka kama spika kuamua serikali ijibu au isijibu"....nk Spika Naye Kibaraka tu wa Mafisadi
 
Hadi sasa siri za ufisadi wa kampuni hiyo na kampuni nyingine zilizohusika na wizi wa fedha za EPA zimebaki kwa Rais Jakaya Kikwete, Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP), Said Mwema, Mkurugezi wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU), Edward Hoseah na Johnson Mwanyika, ambao walikuwa wajumbe wa Kamati Maalumu ya Rais ya kufuatilia walioiba benki.

Kwa hiyo waliunda kamati ya kufuatilia wizi ili majibu wabaki nayo wao? kwa hiyo wamekula pesa za vikao na majibu hawatoi, na wanaendelea kuchunguza nini wakati wezi wanajulikana, dr slaa si alisha watajia, au wanapotezea ili mwishowe tusahau haya bwana. wanjanja wao
 
Unajua Spika naye inawezekana alipata Mgao wa hayo Mabilioni ,naye si amepandikizwa na CCM na Mafisadi kwa kiinimacho cha kuweka spika Mwanamke? Tutarajie kusikia Majibu yake ya Mkato,nyodo na Mbwembwe kama ambavyo huwa anamjibu Tundu Lisu hasa utasikia ''kanuni..namba...ya Bunge inanipa mamlaka kama spika kuamua serikali ijibu au isijibu"....nk Spika Naye Kibaraka tu wa Mafisadi
Murha mbuya! Nu umutulutumbi oree ghose ni iyake??
 
Chadema ongeza kasi, shindilia zaidi. Naona kama Chadema wanawachapa ccm makonde kushoto na kulia wakisindikiza na mateke nyuma huku wananchi wakizomea

Je ccm wanaweza kujinasua?
 
Ccm wameshazoea wizi hao, CDM kazeni buti mpaka 2watiririshe, wanajifanya wanajivua gamba huko Dodoma, hawajui kama kansa inakaa kwenye damu...? Mwisho wenu utafika tu, mtajificha kama mwenzenu wa Ivory Coast, Pambaf nyie, pesa zetu mnafanya mitaji...!
 
sasa kama kamati ilipewa fedha kufanya uchunguzi na mwisho igome kutoa report hadharani huu si ufisadi mwingine huu?kulikuwa na haja gani ya kutangazia umma kumeundwa kamati ya kufatilia huo wizi?au ndio janja ya kufanya watu watulie na kusahamu madudu ya serekali yao?mwisho wa huu usanii ni lini jamani?na huyo aliepelekewa hiyo report kwann asije hadharani na kusomea wananchi matokeo??na kama uchunguzi unaendelea kwann pia wasitoe sehemu ya matokeo yaliyo tayari????
 
CCM inafikiri matatizo haya yaliyosababishwa na serikali ya ccm mojawapo ikiwa ni kashfa ya EPA itasuluhishwa kwa kupata wajumbe wapya wa kamati kuu nk
 
Back
Top Bottom