siri imefichuka.sasa afanyeje?

Mi wanawake waongo adhabu yao ni talaka tu pale pale uhusiano unakufa moja kwa moja kwa nini anidanganye mi siku zote ni mkweli na hii inanisababishia kukosa mashori.
yah man....
 
Hivi sie midume wadau mnajua tunamatatizo yetu ya ajabu sana.....kwani alivyoenda kutoa mahari amuoe anataka kutuambie WASINGEZAA WATOTO NDANI YA NDOA YAO???...kama alikuwa anataka kumwoa ili wazae naye watoto basi ANATAKIWA ASHANGILIE...maana mama ameonyesha uwepo wa uzazi..na hasa zaidi mbegu bora inayozaa wawili-wawili....

Matatizo yetu midume yanaanzia hapa.....UKIMWOA MWANAMKE NA HANA UZAZI....UGOMVI MANYANYASO MATUSI KERO TALAKA .......ndani ndio hapakaliki tenaaa.....

kijana aambiwe kuwa AMAPATA MKE BORA na atangaze ndoa fastaaaaaa....ZAENI MKAONGEZEKE MKAIJAZE DUNIA....au asichopenda yeye ni kutoambiwa mapema kuwa nimeshazaa watoto???.....ni muda tuu...inawezekana jamaa aliharakisha ndoa...wangekaa uchumba kwa miaka say mi3-mi5 angeambiwa tuuu....
NI MAONI YANGU TU WADAU
 
kijana aambiwe kuwa AMAPATA MKE BORA na atangaze ndoa fastaaaaaa....
nani anajali?
ishu sio kuzaa arifu....ishu hapo ni udanganyifu......msichana hakuwa mkweli kipindi chote cha uchumba wao.....
 
Hivi sie midume wadau mnajua tunamatatizo yetu ya ajabu sana.....kwani alivyoenda kutoa mahari amuoe anataka kutuambie WASINGEZAA WATOTO NDANI YA NDOA YAO???...kama alikuwa anataka kumwoa ili wazae naye watoto basi ANATAKIWA ASHANGILIE...maana mama ameonyesha uwepo wa uzazi..na hasa zaidi mbegu bora inayozaa wawili-wawili....

Matatizo yetu midume yanaanzia hapa.....UKIMWOA MWANAMKE NA HANA UZAZI....UGOMVI MANYANYASO MATUSI KERO TALAKA .......ndani ndio hapakaliki tenaaa.....

kijana aambiwe kuwa AMAPATA MKE BORA na atangaze ndoa fastaaaaaa....ZAENI MKAONGEZEKE MKAIJAZE DUNIA....au asichopenda yeye ni kutoambiwa mapema kuwa nimeshazaa watoto???.....ni muda tuu...inawezekana jamaa aliharakisha ndoa...wangekaa uchumba kwa miaka say mi3-mi5 angeambiwa tuuu....
NI MAONI YANGU TU WADAU

Wewe hujaelewa somo, juu tumeongelea sana kuhusu ukweli kuliko watoto. Huyu mwanamke ni muongo wa kutupwa, tena zaidi ya hapo ni mjinga.Huwezi kuficha kitu ambacho hakifichiki.Kuendelea kukaa naye ni kutafuta matatizo.Watu mara nyingine huingia katika ndoa wakijua kuwa mume/mke ni bomu, halafu baadaye waje watuletee matatizo makubwa zaidi wakati washaoana na kuzaa watoto.

No tears, kama anataka kuoa aoe lakini asiseme hakuonywa.
 
Yaani watu wengine siwaelewi...kama una mtoto its best to say it mapema sana, ikiwa mwenzako anafeel they cant love your baggage as well akajiondoa mapema...on the other hand kama he/she is okay they get used to the idea mapema pia. vitu vingine vyaweza kufichika ila mtoto jamani????? hili jambo is both ways kama mjamaa pia ana m/watoto from the past its good to let your mate know. sasa kikilipukia kama cha huyu mdada utaanzia wapi???? mmmm kali sana hii!!
 
Wakuu mie nadhani hili jambo halina ujumla, Kikubwa zaidi ni MAPENZI its no question kwamba mwanamke si mwaminifu kabisa na wote tunajua uaminifu ni nguzo kuuu kwenye mahusiano yaliyo thabiti.huyo mwanamke alitakiwa amwambie ukweli jamaa na amwachie jamaa aamue na sio kumficha kwa kisingizio eti angejua angemkacha, ila tusisahau pia Love conquers all, kwenye mapenzi kila kitu kinawezekana hata ambavyo vinaonekana haviwezekani vinawezekana , so swala hapa ni kiasi gani jamaa anampenda huyo mwanamke, je! anampenda sana kiasi kwamba anaweza kumsamehe hiyo deceit? au hawezi kumsamehe?. Kama anaweza kumsamehe na yuko tayari kubeba hiyo resposibility ya watoto mie naona aendelee nae, ukizingatia watu huwa wanabadilika for better na hy mwanamke anaweza kubadilika, na pia inadepend alimficha kuhusu watoto kwenye mazingira yapi?.
Kama anaona hawezi kumsamehe kwa kweli asijilazimishe he better call off the wedding plan na achukue hamsini zake. coz hata akimuoa hiyo ndoa itakuwa ya maumivu na majuto.
SO MWISHO WA SIKU ANAYEWEZA KUAMUA NI YEYE COZ NI YEYE ANAYEWEZA KUPIMA MAPENZI YAKE NA HIYO DECEIT YA HUYO MWANAMKE
 
There is love and there is what is termed as being a "doormat".

Accepting this is more like being a doormat. I mean I could even defend the woman if she had kept her secret until the last minute prior to the trip ya ukweni, sasa kumuacha jamaa mpaka anafika kwa wazazi bila kumuambia sio tu kukosa uaminifu na uadilifu, bali ni kukosa upendo na heshima pia.

If this guy goes through with this even this woman will lose the little respect she may still have for him.
 
Wanawake ni balaa sana ila hayo yapo jamani......ukiwa ndani ya penzi jiandae kwa lolote usijiachie...
 
Kumwacha mwanamke sio sahihi kwani ni vyema mwanaume akapata ufumbuzi kwa nini mwanamke hakumwambia mapema kama yeye alishajaliwa watoto miaka ya nyuma. Inawezekana mwanamke aliogopa kupoteza penzi lakini hata hivyo bado mwanamke ana makosa ilikuwa ni vizuri kumjulisha mapema mpenzi wake kwani kuzaa kabla ya kuolewa si dhambi. Pili mwanamke kama angeendelea kufanya siri ni kwamba upendo wake kwa watoto wake ungepungua kwani asingekuwa huru kuwa nao angekuwa anawanyima watoto haki yao. Sio kila kosa solution ni kuachana bado wanayo nafasi ya kushauriana na kurekebisha makosa kama hayo kabla ya ndoa. Tusimhukumu mwanamke labda alikuwa na nia njema tu.
 
Humu tumekuwa tukisisitiza umuhimu wa ukweli kwenye mahusiano. Siri yoyote kwenye mahusiano hatimaye hufumka na kuja nje. Kuficha siri si kukosa uaminifu tu, ni ujinga vile vile. Kusema kweli kama mimi ndo huyo mwanaume, huu ndo mwisho wa ndoa. Anaweza kuendelea kumega tu, wakati akiangaza huku na kule. Ila ndoa na huyu dada will prove problematic.

Inawezekana kwa huyu dada hiki alikiona ni kitu cha kawaida kiasi kwamba hakutarajia mwanaume ashangae au afanye lolote. Na hapa ndo nasema ni ujinga vile vile.
 
Jamaa amekuwa aki date demu kwa mda wa mwaka mzima.na ni mengi wameongea na ikafika tym ya kwenda kwa wazazi wa msichana kujitambulisha.walipofika tu,watoto wawili mapacha umri miaka minne walikuja mbio wakiita mummy.jamaa roho ilikuja mdomoni na kwa hasira akamuuliza mchumba mtarajiwa mbona hukunieleza kwamba ulizaa?kwa kweli jamaa alikuwa amempenda huyo msichana na sasa yuko kwa njia panda.asaidiweje??

naomba kuuliza maswali mawili;

...kilichomkasirisha nini baada ya hao watoto kumwita huyo dada Mummy?

...sababu gani zinazomuweka jamaa njia panda?
 
Kuzaa isiwe ishu sana kwa jamaa.Kutokuambiwa ukweli awali kunaweza kuwa kumechangiwa na jamaa kmwenyewe.Hatuna uhakika jamaa ameshakuwa mkweli kwa binti kiasi gani.Yawezekana ndivyo walivyoleana, nikimaanisha kuwa kuna mambo mengi hawajawa wazi kwa pande zote.

Jamaa aendelee nae kama anaona bado mapenzi yapo.

Vilevile tusihukumu sana mabiti wanaozaa kabla ya ndoa.Hizo mimba hawazipati kwa kulamba Azam ice cream ni sisi wanaume tunahusika.Hebu tujiulize wana forum wanaume, wale mabinti tuliowahi kuwa na affair nao tukawapiga chini pengine wakiwa wajawazito wako wapi? pengine mmoja wao ndiye huyo kakutana na jamaa na anatamani jamaa amuoe.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom