Sipendi Dharau!

Jpinduzi

Senior Member
Feb 26, 2011
136
68
Heshima mbele kwanza!Week Iliopita nilikuwa natoka mahala,sasa kuna duka moja maarufu sana mitaa yetu tunayoishi sasa nikaingia hapo dukani kabla hata sijauliza kitu nachotaka simu yangu ikaita basi ikabidi niongee na simu kwanza na muuza duka akanisubiria ghafla akaja baba mmoja akaulizia neti iliyokuwa imetundikwa nje 6x6, jibu nililo sikia kutoka kwa muuza duka alisema haiuzwi.Nilipo maliza kuongea na simu nikamuuliza kweli hio net hauzwi?alichojibu kwamba mweshimiwa huoni na mtu mwenyewe?hanauwezo na hiyo neti?ataiwangia tu hapa!
Kusema ukweli nilishindwa la kufanya mtu mwenyewe alishaondoka hata pakumpata ili nimuulize kweli hanauwezo wa kuinunua au la ilishindikana kwani alikuwa ameshajichanganya kwenye kundi la watu kibao ambapo si rahisi kumpata.​
 
Miswahili ndivyo ilivyo.Wanga asifanye usiku aje kufanya machana?
 
wewe aliku attend vizuri?

Kwangu mimi haikuwa tatizo,alinihudumia mizuri tu!Ila mambo ya kudharau baadhi ya watu kwa muonekano au mavazi sio vizuri kwani watu wengine kazi zao haziruhusu kupendeza!yaan nature ya kazi hairuhu hivyo!Inawezekana yule baba ametoka kazini anaelekea kwake huwezi jua!
 
Wauza mitumba kwani hujawaona?...Hasa wale wanaotundika nguo za bei kali na viatu, ukienda pale utakuta anaanza kwa kukuangalia juu hadi chini, ndipo anakupa bei!
Akikuona michosho wala hakuangalii hata sura, anakujibu huku anamtext mpenzi!
 
Hii thread imenigusa sana. Huwa sipendi kabisa dharau. Kama ingekuwa mimi ndio wewe, baada ya majibu hayo ningemwambia apeleke ujinga wake chooni na nisinge nunua tena bidhaa yeyote kwake. Mpuuzi kabisa huyo jamaa!
 
Wauza mitumba kwani hujawaona?...Hasa wale wanaotundika nguo za bei kali na viatu, ukienda pale utakuta anaanza kwa kukuangalia juu hadi chini, ndipo anakupa bei!
Akikuona michosho wala hakuangalii hata sura, anakujibu huku anamtext mpenzi!

Mi mtu akinifanyio hivyo natoka naingia duka la jirani alafu nikitoka na mifuko yangu najipitisha hapo dukani kwake abaki macho yanamng'aa. Dharau ni kitu kibaya sana.
 
Unajua wenye maduka wanashindwa kuelewa pesa haisemi mfukoni!!! Kuna watu ile ni vunga yao lakini wapo full loaded, yaani full mavumba.
 
Mi mtu akinifanyio hivyo natoka naingia duka la jirani alafu nikitoka na mifuko yangu najipitisha hapo dukani kwake abaki macho yanamng'aa. Dharau ni kitu kibaya sana.

Kweli dawa ya nyodo ni nyodo.
 
Wauza mitumba kwani hujawaona?...Hasa wale wanaotundika nguo za bei kali na viatu, ukienda pale utakuta anaanza kwa kukuangalia juu hadi chini, ndipo anakupa bei!
Akikuona michosho wala hakuangalii hata sura, anakujibu huku anamtext mpenzi!

hiyo inaonekana ni tabia yako
 
Wenye biashara wanawajua wabaya wao, usikute amemshtukia na chuma ulete yake ndio kaamua kumpa shit kimtindo.
 
Back
Top Bottom