Siogopi kufa: Filikunjombe!

Katika hatua nyingine, Mbunge wa Ludewa, Deo Filikunjombe, ameapa kuwa yuko tayari kufa kwa ajili ya kutetea Watanzania wanyonge na kwamba haogopi vitisho uchwara vinavyotolewa na baadhi ya watu.

Alisema kamwe hawezi kukaa kimya akitazama namna Watanzania wanavyoporwa haki zao na viongozi wachache wenye uroho wa madaraka.

“Hatuwezi kufumbia macho wizi huu unaoliangamiza taifa kwa hofu kuwa ni chama changu. Ubunge wangu ni kwa manufaa ya Wana Ludewa na Watanzania wote, hivyo, wanaonishambulia wao ndio maadui wa CCM na Watanzania,” alisema mbunge huyo.

Alipuuza madai kuwa hatua yake ya kuungana na wapinzani katika suala la kutia saini kura ya kutokuwa na imani na waziri mkuu ni hatua za kukihama chama chake.

Huku ndiko kufa kishujaa
 
kama kweli ameamua kuwafia wananchi wa Ludewa, basi na awe wa kwanza kuuza suti zake, anunue mitumba ya kuvaa yeye, watoto wake, na wananchi wake. PUMBAVU! Ninyi wanasiasa kiama chenu ki karibu sana, mnaruka angani kila siku hali kuwa majirani zenu kapuku! Ilikuwaje mkapiga hatua ya mia, hali kuwa jirani yako ana moja? Wote wezi tu! Eti mnajiita wakombozi....PUMBAVU. CHE GUEVARA alisema hivi ...i am not a liberator, liberators do not exist. The people liberate themselves .....
 
Nani ambaye hatakufa katika dunia hii!!! Tusiogope kusimamia haki kwa kuhofia kufa/kuuwawa!
 
Mtoto wa mjini issue ni kwamba CAG karipoti ubadhirifu wa kutisha wa watendaji wa serikali, asilimia kubwa yawabunge wamepiga kelele mpaka mapovu yakawa yanawatoka! lakini ukweli uko palepale je hiyo ndiyo solution? baadhi ya ripoti za kamati za bunge zimependekeza mawaziri husika wawajibike, mawaziri wamegoma! silaha pekee kwa mujini wa kanuni za bunge ni kumbana waziri mkuu ikitegemewa kwamba atawasiliana na Rais ili mawaziri hao wawajibishwe. Zitto akaamua kuchukua hatua badala ya kulalamika tu lakini cha ajabu wabunge wooote wa CCM waliokuwa wanatokwa na mapuvu wakanywea except hao wachache ambao ni very courageous!! sasa wewe ulikuwa unataka afanye nn zaidi? ww ungekuwa na uthubutu huo??

huyu jamaa anafikiria 2015, usishangae 2014 akahamia cdm akagombania ubunge 2015 kwa ticket ya cdm, wabunge wengi ni ma hypocrites. Its always about them them and them and never their people..sasa huyu badala ya kutueleza nini atafanya kuhakikisha viongozi wanawajibishwa kila siku anasema yuko tayari kufa, well kufa atakufa tu siku moja hata asipokua tayari, acheni siasa za ajabu ajabu, watanzania wameamka sasa hivi mambo ya kuibiwa mchana kweupe na maneno yenu sasa hivi hamuambulii kitu
 
Akina Anna Kilango, Ole sendeka wako wapi tuliwasifu sana JF baadaye tunaanza kuwatukana.

Twende taratibu kumwaga sifa nyingi mbele hatukujui
u
AGREED. Very well said mkuu. That's has been a recycling case at JF. Kwa kweli mi huyu jamaa sijaona, ni afadhali ya Godfrey Zambi
 
OLE MILYA, DEO FILIKUJOMBE NA WAPAMBANAJI WAPYA WENGINEO:
KUMBUKENI SISI WANANCHI TUTAWAVISHENI TAJI BAADA YA KAZI YA UKOMBOZI WA MTANZANIA ENYI WENYE KUSTAHILI ZAIDI

Ni wajibu tena ni haki yetu sisi 'Nguvu ya Umma' kuwalinda kwa ukamilifu masaa 24 wale Wapambanaji woote wanaotumiwa vitisho kwa sababu tu ya kupigania HAKI, HESHMA NA UTU wa kila Mtanzania bila kujali tofauti za itikadi za kichama.

Mpambanaji Deo, uwe na amani kwa WaTanzania wote tunatambua kwaamba juhudi zako hazi UNAFIKI ndani yake hata chembe. Hivi karibuni WaTnzania tutfikia malengo yetu mkuu ya ukombozi na hivyo kila mtu kupigwa butwaa kwamba ala kumbe inawezekana?

Endelea kusimamia kidete KILE UNACHOKIAMINI na wala usitetereke msimaamo kila kukicha kama huyu dogo January Makamba.

Baada ya kazi wananchi tutawavisheni taji wenye kustahili zaidi. Utaifa Mbeeeeeele kma tai, itikadi za kisiasa nyuma!!

Katika hatua nyingine, Mbunge wa Ludewa, Deo Filikunjombe, ameapa kuwa yuko tayari kufa kwa ajili ya kutetea Watanzania wanyonge na kwamba haogopi vitisho uchwara vinavyotolewa na baadhi ya watu.

Alisema kamwe hawezi kukaa kimya akitazama namna Watanzania wanavyoporwa haki zao na viongozi wachache wenye uroho wa madaraka.

“Hatuwezi kufumbia macho wizi huu unaoliangamiza taifa kwa hofu kuwa ni chama changu. Ubunge wangu ni kwa manufaa ya Wana Ludewa na Watanzania wote, hivyo, wanaonishambulia wao ndio maadui wa CCM na Watanzania,” alisema mbunge huyo.

Alipuuza madai kuwa hatua yake ya kuungana na wapinzani katika suala la kutia saini kura ya kutokuwa na imani na waziri mkuu ni hatua za kukihama chama chake.
 
Hao mawaziri kama watafukuzwa kazi,watafukuzwa na Ikulu. Sasa . Filikunjombe atauawa na nani? Mbona tunaongea maneno bila mpangilio?
Mnafiki mkubwa huyo. Alipokuwa jeshi la polisi kama msaidizi wa Mahiiita ji atuambie aliyoyafanya. Atoke CCM kama alivyojitoa MPENDA zoo.
 
Huyu Filikunjombe naye siyo msafi kihivyo. Alipewa rushwa na TCRA ili kuisafisha kutokana na hesabu zake zilizokuwa zimejaa ufisadi. Anyamaze kimya kabisaaa

Hii ni spin ya wanamagamba; kama Filikunjombe alipewa rushwa na TCRA na wewe unajua na ushahidi unao kwanini hukumshitaki kwa vyombo husika unangoja mpaka anapowashika pabaya ndio unaanza kulalama?
 
Hata DAUDI BALALI alisema haogopi kufa lakini amekufa, vivyo hivyo HORICE KOLIMBA

Siku yako ya kufa ikifika imefika hakuna mjadala; kama ingekuwa hawa magamba ndio wanaamua nani afe basi saa hizi Mwakyembe angekwisha kuwa "past tense" lakini kwavile hawa magamba hawashiki ufunguo wa ahela basi jamaa ndio maana anaendelea kujenga barabara huko Arusha!!
 
Huu ni upuuzi, Mbona wewe Una Wadogo wako kijijini Hawana Hata chupi? Mbona huwanunulii.

kama kweli ameamua kuwafia wananchi wa Ludewa, basi na awe wa kwanza kuuza suti zake, anunue mitumba ya kuvaa yeye, watoto wake, na wananchi wake. PUMBAVU! Ninyi wanasiasa kiama chenu ki karibu sana, mnaruka angani kila siku hali kuwa majirani zenu kapuku! Ilikuwaje mkapiga hatua ya mia, hali kuwa jirani yako ana moja? Wote wezi tu! Eti mnajiita wakombozi....PUMBAVU. CHE GUEVARA alisema hivi ...i am not a liberator, liberators do not exist. The people liberate themselves .....
 
Ahmada Umelewa.....
Mtu mwerevu siku zote atapigania mantiki, na si mfumo, kwasababu mantiki hubadilisha mfumo, lakini si mfumo kwa mantiki. Ipi ni mantiki ya maisha zaidi ya furaha? Unaona nini? Mimi, wewe na yeye ndio wajibu wetu katika UTU. Mantiki ya maisha ni kama hatua, usipige ya pili kabla ya jirani yako hajaifikia moja. Unataka kuvua nguo hadharani kwa kuwa mimi nimevua? Mantiki je? Pigania hilo hadi kifo chako, na si kuongozwa na hisia.
 
huku CCM sijui huyu malaika mtoa roho ni mwanachama wa CCM maana hata Magufuli alipotoka pale Upendo Hospital alipokuwa amepumzishwa alitamka maneno haya.."HAWANIWEZI NG'OOO"
 
Sema tena sijasikia....huogopi kufanywa nini????????????

Ungekuwa jirani na Pinda angekuchapa kofi la kukosa uwajibikaji wa pamoja (collective responsibility).
Wewe kweli mama porojo lakini chunga magamba noma!!!! unaweza chunwa kama kiti moto
 
Back
Top Bottom