Sio mimi mwalimu, ni kinara huyo

PhD

JF-Expert Member
Jul 15, 2009
4,599
3,673
kwa wale wanaosikiliza Tangazo la Malaria haikubaliki, utasikia vitoto viwili vikipiga story wakati mwalimu anafundisha , mwalimu anapogundua na kuwaita mbele kamoja kanasema, sio mimi mwalimu ni kinara huyo, inanikumbusha shule za msingi za vijiji jinsi tulivyokuwa tunasemeana kwa walimu.
 
Unanikumbusha darasa la kwanza baada tu ya kujua kusoma na kuandia basi nikaandika barua kwenda kwa msichana kuomba urafiki- dogo mwenzangu dawati moja akanisemea kwa mwalimu "Mwalimu ameandika barua ya MATUSI" ilikuwa noma - ikabidi nipite mbele ya darasa niisome "kwako dada mpenzi salaam sana ama baada ya salaam mimi mzima wa afya hofu na mashaka ni juu yako tu wewe uliye mbali na upeo wa machao yangu. (wakati yule dada tunasoma darasa moja). Madhumuni ya barua hii ......usiku silali nakuota wewe dada uliye mzuri naomba UNIKUBALI"

Nilivyomaliza kuisoma, wote tukapita mbele mimi na mamsapu tukachapwa fimbo tatu tatu, kwa kuwa nilikuwa kipanga nikasitisha kumwonyesha hesabu yule dogo mpaka alipotubu.

Yule dogo ndiye aliyekuwa anaandika wapiga kelele, alikuwa mnoko ingawa hakuwa monitor.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom