Sio ishu ya sura, ni kazi!

dreamcatcher

Member
Jan 13, 2011
10
0
Nikiwaangalia kwa makini wasoma habari wa wenzetu, nabaini tofauti kubwa mno na hawa wa kwetu hapa nyumbani. Inanisikitisha mno ndugu zangu, kuwa tofauti hii hutuweka sisi kama jamii kwa ujumla (ni wazi kuwa wao ndio wanaotuwakilisha sisi sote machoni mwa dunia nzima inayowatazama) katika hali ya kufanana na majuha, wasiojua wala kulielewa wanachokifanya!

Inakuaje pale ambapo msoma habari aliyetunukiwa vyeti vya habari, kushindwa kutamka neno "Rio-de-janeiro"?

Eti anasoma kama vile yupo chekechea! "Ri- rio da... de jeNAIro"! eh! jamani??? je, hakuwa na muda wa kujiandaa? hakupitia hata script zake kabla ya kukaa pale na kuuza sura badala ya kusoma habari?

Ukimwacha huyo, wenzake wote hawana nafuu. Wanaosema eti "kipindi hichi!" hawakusoma somo la kiswahili hawa? au hawakuwepo katika somo la ngeli? au ndio "fasheni" mpya?Mwingine kaandika gazetini ukurasa wa kwanza herufi kuuubwa na zilizokolezwa "MGAWO WA UMEME".

Haya basi, tusiwalaumu sana wao... ila, jamani, editor alikuwa wapi? na director? na wote wanaohusika na mchakato wote wa kutoa kitu presentable kwa jamii?

Hii ni TBC jamani! network kubwa mno kwetu sisi! Tunarushwa hadi kwenye Dstv!

Akh! angalieni wenzetu jamani... angalieni content na quality ya Nation Tv (na hio sio tv ya taifa huko kwa wenzetu). Utaona aibu bwana. Ha ha haaaaaaaa! nacheka manake naona na kwenye EAC tumo... he he heeeeee! i wish and hope that we can epuka kushika mkia jamani!

Nafikiri, labda tumeweka fikira zetu zote kwwenye muonekano wa nje... Wasoma habari warembo, wamejipodoa, wanang'ara na kuvutia machoni, meza zao zinapendeza na backdrop ndio usiseme! ah! Inauma sana...
 
Hiyo ndo bongo!Kazi kuuza sura tu!Mkuu wa nchi mwenyewe msanii...unategemea nini kutoka kwa waliopo chini yake!
 
wauza nyago tuu! wote wa mipasho kwahiyo maneno ya kiswahiliswahili ndo wanayaweza,vibondez
 
umenichekesha kweli
mtu kapiga dededede kibao hahaha
kisa baba yake anajuana na mkubwa
 
Back
Top Bottom