sio dhambi kutaka kuongoza chama au nchi

Crucifix

JF-Expert Member
Feb 20, 2011
1,651
588
Demokrasia imeshuka kwa % kubwa sana Tanzania. Kumekuwapo na mambo yasiyofaa na ya kinafiki kama vile kumwachia rais aliyepo madarakani amalizie kipindi chake cha miaka 10! Au mwenyekiti wa chama kumpisha rais mteule ambaye kabla hakuwa mwenyekiti wa chama. Wanaotangaza nia za kugombea vyeo katika vyama vyao wasemwa kwa kupanga mapinduzi, wanafukuzwa ama kuwekwa kitako na wazee ili wasirudie tena. Iweje mtu ukitaka uongozi, kiongozi aliyepo anasema unadhoofisha chama? Hebu tuache visanduku vya kura viamue nani wanafaa kuongoza vyama vilivyopo na nchi yetu; kwa kuwa sio dhambi kutaka kuongoza chama au nchi.
 
Back
Top Bottom