Sinza: Wenye magari kaeni chonjo na kibaka huyu kwani anawaibia sana

LEGE

JF-Expert Member
Oct 14, 2011
5,123
9,167
Wana jf mnao ishi sinza au pita sinza njia ya sinza makaburini ambayo inakatisha na kwenda kutokea njia iendayo ubungo. Kuna kibaka mmoja anawaliza sana mchana kweupe na siyo siri anameki sana hera.Kibaka huyo kaweka kabendera kekundu katikati ya bara bara kuna sehem bara bara imeharibika kuna shimo kufanya mwenye gari yeyote apitae hapo lazima apunguze mwendo na magari hayawezi kabisa kupishana hivyo anatumia mwanya huo kuomba fedha kwa madereva na kujifanya ya kutengenezea shimo hilo.

Source mim mwenyewe namwona hapa kila siku ndiyo mchezo wake.
Kama huamin pita ili upate ushahidi.
 
dawa ni kupita na kumwagia upupu,kama polisi hawamchukilii hatua asubiri kidogo utasikia
 
niliogopa kweli, kumbe anaomba omba tu? si kibaka huyo mwacheni kabuni kamradi kake, atakuwa anaomba tanroad wasipitie kurekebisha hilo shimo ili aendelee kutengeneza ela
 
Baba_Enock alikwisha acha kutembelea maeneo ya Sinza siku nyingi - Sinza imekuwa kama Tandale na Mwananyamala! Better Manzese au Mabibo kuliko Sinza!
 
Kwahiyo wadau mnashauri aachwe siyo mbona huwa yakiwakuta mkakutana na wajanja na wakawaliza huwa mnalalama???

Nyie mnao mtetea kama siyo kibaka ni omba omba hamjaelewa vizuri huyu jamaa anajifanya anarekebisha hili shimo daily kwa hiyo huwa anasimamisha magari hapa na kuwataka wachangie fedha kwaajiri ya urekebishaji wa shimo hilo.

Kwa wanaume haina shida sana kwa wanawake ndiyo huwa kero kwao.
 
acha upumbavu wewe. hawa watu wapo dar nzima na ni hali ya kawaida tu tulishazoea. barabara nyingi dar zina mashimo so wale vijana kwa kuwa hawana kazi wanashinda pale mchana kutwa wakijitolea kuziba lile shimo. wakisha maliza wakati huo ndo na nyie mnatoka makazini, wanawaombeni 100 ya kuvuta sigara, uwape usiwape hawakufanyi kitu wala kukulaumu. sasa kuwapa hiyo mia ndo unaona ishu sana wakati wamekusaidia gari yako isiharibike? tumieni akili kufikili
 
Sio asavali ya huyo 'kibaka' kuliko nyie mnaojaza paDM za uwongo huko maofisini halafu mnakuwa wagumu kweli kugawana umaskini hata hizo miamia..mibongo bana kwaunafik na kukosa priority.
 
wewe haujaona vibaka. nenda kiburugwa au hata tandika tu ukutane na mafisi wakupige roba za mbao mchana halafu urudi hapa useme yule jamaa kibaka. Mia
 
Wana jf mnao ishi sinza au pita sinza njia ya sinza makaburini ambayo inakatisha na kwenda kutokea njia iendayo ubungo. Kuna kibaka mmoja anawaliza sana mchana kweupe na siyo siri anameki sana hera.Kibaka huyo kaweka kabendera kekundu katikati ya bara bara kuna sehem bara bara imeharibika kuna shimo kufanya mwenye gari yeyote apitae hapo lazima apunguze mwendo na magari hayawezi kabisa kupishana hivyo anatumia mwanya huo kuomba fedha kwa madereva na kujifanya ya kutengenezea shimo hilo.

Source mim mwenyewe namwona hapa kila siku ndiyo mchezo wake.
Kama huamin pita ili upate ushahidi.

Lege,
Hii habari yako ina upungufu mkubwa. Kwa tafsiri ya wengi, huyo jamaa siyo kibaka ama kama tuna tafsiri tofauti ya Kibaka. Lakini umekwenda mbali zaidi kusema watu wajihadhari wakati hujaandika kuna madhara gani watumiaji wa hiyo barabara wanapata. Tatizo la barabara za Dar linajulikana, na utendaji mbovu wa halmashauri zetu siyo siri tena, sidhani kama kuna ubaya iwapo kuna mtu ametumia mwanya huo kupata ridhiki wakati hanyang'anyi wala kukulazimisha utoe hiyo hela. Zaidi kwa mwenye gari, hasa magari madogo, ni rahisi zaidi kumpa shilingi mia mbil aendelee kutengeneza kuliko gharama inayoweza kutokea kutokana na gari kupita kwenye mashimo kama mahandaki. Hivi kuna ubaya kama anatengeneza hela nyingi ambayo anapewa kwa hiyari ya mtoaji? Na hela nyingi ni kiasi gani? Mkuu naona umetumia hisia zaidi.
 
Sasa hapo ukibaka uko wapi? Huyu amejiajiri hapo. Mbona hakuibii unapatia mwenye, isitoshe huwa hakuna kiwango maalum, mara nyingi wanapewa chenji au kama ukiguswa sana unatoa 1,000/=. Na usipompatia hakufanyi kitu, maana barabara sio yake. Kama unaona ameshinda hapo tangu asubuhi na shimo bado halijazibwa, punguza mwendo kama ulivyofanya asbh pita tu bila kumpatia hiyo chenji, maana hawa ukizozana nao waweza kupiga gari jiwe halafu wahamie sehemu ingine.
 
Natafuta Nyumba ya kupanga ya familia,angalau vyumba 3 hadi 4,maeneo ya Kijitonyama au Sinza,iwe na fenci na packing,piga number 0689300002,bei laki 2.5 hadi 3.5
 
Mleta hoja anakwepa sema ukweli.Pale sinza makabulini kuna wezi wa magari.
Pale kuna ukumbi wa mwika,pembeni kuna vibaaaa vimefuatana na kuangalia makabulini,Ndg WE ROGWA KAPAKI PALE GARI au unakwenda pale baa kuna msosi mzuri au makaburini kuzika na jamaa wanakuona we ni mgeni maeneo yale,Ndg dk 5 ni nyingi gari inakuwa inatembea kuelekea wanakokujua,
Taadhari kwa wale wapenda sifa na magari kujidai sinza utalitafuta gari mfukoni.
 
Natafuta Nyumba ya kupanga ya familia,angalau vyumba 3 hadi 4,maeneo ya Kijitonyama au Sinza,iwe na fenci na packing,piga number 0689300002,bei laki 2.5 hadi 3.5

kama unataka nyumba ipo mwenge 0762 615195.
Ina vyumba 3 sebure 1,choo na bafu,jiko na daining.
Kama utahitaji nitwangie.
 
Sijaielewa hii habari kabisa kweli waalimu wanaosahihisha mitihani yetu huwa wana kazi kubwa sana kujua mwanafunzi anaelezea kitu gani
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom