Recta
JF-Expert Member
- Dec 8, 2006
- 855
- 38
Recta I wish wewe ndie ungekuwa mgombea maana unajua kuchambua fikra na mahitaji ya wananchi wako. Umezungumza jambo moja kubwa na la msingi kuwa kampeni si wakati wa kumtafuta aliye bora ila ubora wa mgombea unatakiwa uonekane toka mwanzo nyakati za nyuma. Kwa hili nakuunga mkono lakini piaukazungumzia kuwa kampeni ni sehemu ya kufanyia ushawishi ili mgombea auzike kwa wapiga kura ni kweli kabisa lakini wasitake tuwanunue kwa uongo wao ila kwa facts zao. Unajua kujua kuongea sio kujua kutenda ingawa kuna maana kubwa sana unapojua kuongea na kujua kutenda pia
Pia nashukuru kwa kujaribu kuona baadhi ya ahadi za wagombea niliowachambua hapo juu kuwa ni za uongo na uzandiki wa hali ya juu.
Mwisho niseme kuwa tunahitaji kiongozi mwanamapinduzi mwenye itikadi ambayo hata wananchi wenyewe wataiona kama kulamba sumu vile lakini matokeo yake baadaye yawe ya kusherehekea na siyo kiongozi ambaye maneno yake na misimamo yake ni kama kulamba asali lakini matokeo yake yawe kilio na kusaga meno.
Kuambiwa elimu bure kila siku sio jambo la kushangilia tunataka serikali ambayo itahahakikisha kuwa wananchi wanaweza kutumia akili zao na rasilimali zilizopo kama vile madini, misitu, ardhi na nyinginezo kujikwamua kimaisha ikiwa ni pamoja na kusomesha watoto wao kwa kulipa karo ya shule. Leo hii siwezi kushangilia elimu ya bure kwa sababu ina maana tutaendelea kuibiwa na viongozi wachache kwa sababu hiyo hiyo.
Nashukuru sana Mokoyo kwa maelezo yako na heshima uliyonipa hadi kudhani kuwa ningefaa kuwa mmoja wa wagombea. Nashukuru kama nilichokiandika kimekushawishi kwa kiasi chochote kuona ukweli wa jinsi ambavyo taifa hili linalosuasua kwenda mbele, linavyohitaji juhudi na maarifa ya kila mmoja wetu kulikwamua katika kisiki ambapo limegota.
Mkuu, naamini kuwa kuwezesha waTanzania mmoja mmoja ni hatua ya juu na ya muhimu kabisa katika kujenga Taifa linalojitegemea. Wananchi wakiweza kushiriki katika kila nyanja ya uchumi wa nchi yao, ni dhahiri kuwa Taifa litanufaika kwa kiasi kikubwa sana, na umasikini wetu utakuwa historia. Ni kweli kabisa hayo unayosema.
Kwa upande mwingine, naamini tuko nyuma sana katika kuondoa ujinga na umasikini nchini (tukiweka pembeni maradhi na rushwa). Hatua ya kwanza ni lazima ichukuliwe ili wananchi waweze kushiriki constructively katika kujiletea maendeleo yao kwa ufanisi mkubwa. Hatua hiyo ndugu yangu ni kuhakikisha kuwa wananchi kwa asilimia kubwa iwezekanavyo wanakuwa na afya njema wakati wote, na wanaepuka magonjwa yanayoweza kuepukwa (kama, Malaria, kipindipindu na mengine ya aibu). Ni aibu kuwa na jamii ambayo watoto wanaozaliwa wanakuwa katika hatari ya kufa wangali wachanga. Ni aibu kuwa asimilia ya wakina mama wanaokufa wakijifungua bado ni kubwa na ya kutisha katika nchi yenye uhuru unaokaribia miaka Hamsini. Hii hali inabidi serikali ipambane nayo kwa kila hali.
Ili tuweze kusimamia na kufaidika vyema na rasilimali zetu, ni lazima tuwe na jamii ambayo imeelimika vya kutosha na hapo ndipo wengine wanaweza kuwategemea wao kuelimika na kuwa huru kiuchumi. Wachina walifanya hivyo, na ndio siri ya maendeleo yao ya sasa na miaka mingi ijayo. Hatua ya kwanza ya kuhakikisha kuwa jamii ya Tanzania inapata elimu ya kutosha, ni lazima ichukuliwe na serikali kwakuwa uchumi wa nchi kwa sasa uko mikononi mwa serikali inayotawala. Hili likiwezekana, nchi itakuwa salama na yenye heshima na maendeleo zaidi.
Mkuu wangu, nakuomba niendelee kukushawishi upige kura mwaka huu kwa uhuru na haki yako ili uweze kuona mabadiliko au maendeleo unayohitaji. Ni imani yangu kuwa, kama hatutashiriki kwa wingi kupiga kura, uwezekano mkubwa wa kuongozwa na tusiotaka watuongoze.